Showing posts with label magonjwa ya Zinaa. Show all posts
Showing posts with label magonjwa ya Zinaa. Show all posts

Magonjwa ya Zinaa na dalili zakeAfyaclass Forum •

Magonjwa ya Zinaa na dalili zake

Magonjwa ya Zinaa ni yale magonjwa yote ambayo huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa Mtu mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Magonjwa hayo husababishwa na maambukizi ya Viini mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Parasite au Virusi

Kuna Magonjwa Mengi ya Zinaa ila katika Makala hii ntaeleza Magonjwa Makuu Manne(4);

  1. Ugonjwa wa Kisonono
  2. Ugonjwa wa Kaswende
  3. Ugonjwa wa Chlamydia
  4. Pamoja na Trichomoniasis

1. Ugonjwa wa Kisonono

Ugonjwa wa Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na Bacteria ambaye kwa kitaalam hujulikana kama Neisseria gonorrhoeae, Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Zipo Dalili mbali mbali za Ugonjwa huu wa Kisonono ikiwemo;
  • Mwanaume Kutokwa na usaha sehemu za Siri,kwenye uume
  • Mwanamke kutokwa na ute ute ambayo umechanganyika na usaha ukeni n.k

2. Ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa ambapo Chanzo chake ni maambukizi ya bakteria aitwaye Treponema pallidum,

Bakteria hawa huingia mwilini kupitia mikato,michubuko au mikwaruzo kwenye ngozi,kidonda au kupitia utando wa ndani wenye unyevunyevu au maji maji n.k.

Zipo Dalili mbali mbali za Ugonjwa wa Kaswende ambazo zimegawanyika kulingana na hatua au Stage ya Ugonjwa huu;

Ugonjwa wa kaswende umegawanyika kwenye hatua kuu Nne yaani; 

  • primary,
  • secondary,
  • latent/hidden
  • Pamoja na tertiary,

Kwenye hatua mbili za mwanzo(primary na secondary) kaswende huambukiza zaidi, kwenye hidden au latent stage kaswende hubaki kuwa active lakini mgonjwa anaweza asionyeshe dalili zozote, na kwenye Tertiary Stage hapa ugonjwa huleta madhara zaidi kwenye afya.

(1).Primary syphilis

Hapa huhusisha wiki 3 mpaka 4 toka Mgonjwa kuambukizwa bacteria wanaosababisha Kaswende,Na dalili zinazoanza kuonekana ni kama kidonda kidogo sana ambacho hata hakina maumivu yoyote kwa kitaalam huitwa chancre,

Kidonda hiki kidogo hakina maumivu yoyote ila kinakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuambukiza, Mtu anaweza hata asijue kwamba ana kijidonda hiki(chancre),

Na kinatokea sehemu ambapo bacteria wemeingilia Mwilini kama vile Mdomoni,Sehemu za Siri au kwenye njia ya haja kubwa.

Wastani kidonda huweza kuonekana wiki 3 baada ya kuambukizwa, lakini huweza kuchukua siku 10 mpaka 90 kuonekana, na Wakati mwingine Mtu huweza kuwa na dalili Moja tu ya Kuvimba kwa tezi za Lymph( yaani Swollen lymph nodes).

Na mtu mwingine huweza kuambukizwa kwa kugusana na kijidonda hicho(Direct contact) hasa wakati wa kufanya mapenzi.

(2).Secondary syphilis

Katika hatua hii Ngozi inaweza kuwa na vipele au Rashes, ambavyo huacha vimadoa doa au alama kwenye ngozi,maumivu ya koo au mtu kuwa na sore throat,n.k

Rashes hizi kwenye ngozi haziwashi na mara nyingi huonekana kwenye viganja vya mikono pamoja na kwenye miguu kwa chini(sole), japo pia zinaweza kuonekana maeneo mengine.

Na watu wengine wanaweza wasijue mpaka zinaisha zenyewe.

Dalili zingine kwenye secondary syphilis ni pamoja na;

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuvimba kwa lymph nodes

- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

- Kupata Homa

- Uzito wa mwili kushuka au kupungua

- Nywele kunyonyoka(hair loss)

- Maumivu kwenye joints n.k

KUMBUKA;Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa makini kwa Mgonjwa mwenye shida hii,maana tafiti nyingi zinaonyesha ugonjwa wa kaswende unaweza kuwa na dalili ambazo hufanana kabsa na magonjwa mengine au Nonspecific symptoms, hali ambayo inaweza kuwa ngumu hata mtu kujua kama ana tatizo hili.

(3).Latent syphilis

Hatua ya tatu ya ugonjwa wa kaswende inajulikana kama latent au hidden, stage.

Dalili zote zilizoonekana kwenye hatua ya kwanza na ya pili zinapotea, hivo hakuna dalili yoyote inaonekana kwenye stage hii ndyo maana ya kupewa jina la hidden au latent stage.

Japokuwa dalili zimepotea ila Bacteria bado wapo mwilini na wakati mwingine huweza kuchukua muda kabla ya kwenda stage ya nne(tertiary stage of syphilis).

(4).Tertiary syphilis

Baadhi ya tafiti zinaonyesha ni asilimia 14% mpaka 40% ya watu wenye ugonjwa wa kaswende hufika stage hii,

Hatua hii ya ugonjwa wa kaswende inaweza kuchukua Muda mrefu sana hata miaka mpaka mtu kuingia kwenye stage hii toka siku ya kwanza ya maambukizi(initial infection).

Na madhara yake kwenye stage hii ni makubwa sana hata kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

3. Ugonjwa wa Chlamydia

Chlamydia ni Ugonjwa wa Zinaa ambao husababishwa na kuenezwa na bakteria aitwaye Chlamydia trachomatis, na unaweza kuambukizwa kwa njia ya kufanya tendo la ndoa.

Dalili za Ugonjwa wa Chlamydia ni pamoja na:

  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na Uchafu ukeni
  • Kutokwa na Uchafu kwenye Uume
  • Kupata maumivu ukeni wakati wa tendo
  • Kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuvuja damu ukeni baada ya tendo
  • Kupata maumivu ya Korodani n.k

Kumbuka; Dalili hizi pia huweza kuingiliana na magonjwa mengine.

 4. Trichomoniasis

Ugonjwa huu wa Trikomonasi hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS ambavyo pia huweza kuvipata kwa njia ya kujamiiana.

DALILI ZA UGONJWA WA TRIKOMONASI NI PAMOJA NA HIZI;

(a) Kwa Wanawake

1. Mgonjwa kupata miwasho sehemu za siri, ambapo hupata miwasho maeneo ya kuzunguka ukeni ikiwemo pamoja na ngozi ya mashavu ya uke.

2. Kutokwa na uchafu sehemu za siri  wenye rangi kama njano,nyeupe au Kijani kwa mwanamke

3. Mwanamke kuvuja damu sehemu za siri

4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu pamoja na kuvimba

5. Kuhisi hali kama ya kuungua sehemu za siri mara kwa mara

6. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

7.Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa

8. Kupata hisia za mkojo mara kwa mara ndani ya mda mfupi n.k.

(b). Kwa Wanaume

1. Mgonjwa kupata miwasho sana sehemu za siri, kwenye Njia ya Mkojo ikiwemo eneo la kitundu kidogo cha mkojo kwenye uume

2. Kutokwa na uchafu kwenye Njia ya mkojo

3. Kuhisi hali ya kuchomwa au kuungua baada ya mwanaume kutoa mbegu za kiume au baada ya mwanaume kumwaga shahawa akifanya mapenzi

4. Kuhisi hali ya kuungua au kuchomwa wakati wa kukojoa

5. Kupata hisia za kukojoa mara kwa mara ndani ya mda mfupi n.k.

Kumbuka; Dalili hizi pia huweza kuingiliana na magonjwa mengine.

Je,Una Matatizo haya na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende,chanzo chake(Syphilis)Afyaclass Forum •

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende,chanzo chake(Syphilis)

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa ambao hutokana na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kwa jina la Treponema pallidum,

Unaweza kupata ugonjwa wa Kaswende kupitia mgusano(direct contact) kwenye michubuko au vidonda ambavyo tayari vimeathiriwa na bacteria hawa, michubuko au vidonda hivi huweza kuwepo maeneo kama vile;

- Mdomoni

- Kwenye Uume

- Kwenye Uke

- Sehemu ya haja kubwa n.k

Asilimia 99% ya maambukizi haya ya kaswende,watu huyapata wakati wakifanya mapenzi au tendo la ndoa.

KUMBUKA; Watoto wanaweza kupata ugonjwa wa kaswende kama mama zao wenye ugonjwa huu hawakutibiwa,hii hujulikana kama congenital syphilis.

HUWEZI KUPATA KASWENDE KWA;

- Kushare vyoo

- Kushare vijiko au vyombo vya kula

- Kuvaa nguo za mtu mwingine n.k

Na hii ni kwa sababu bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kaswende hawawezi kuishi kwa Muda mrefu nje ya mwili wako.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA UGONJWA HUU WA KASWENDE

• Wanaofanya mapenzi bila kinga/Condom(Ngono zembe)

• Wenye wapenzi wengi(multiple sexual partners)

• Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao

•Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile

• Wenye maambukizi ya UKIMWI

• Wenye wapenzi ambao tayari wana ugonjwa huu wa kaswende

DALILI ZA UGONJWA WA KASWENDE NI ZIPI?

Ugonjwa huu wa kaswende umegawanyika kwenye hatua Nne yaani;

- primary,secondary,latent na tertiary,

Kwenye hatua mbili za mwanzo(primary na secondary) kaswende huambukiza zaidi, kwenye hidden au latent stage kaswende hubaki kuwa active lakini mgonjwa anaweza asionyeshe dalili zozote, na kwenye Tertiary Stage hapa ugonjwa huleta madhara zaidi kwenye afya.

(1).Primary syphilis

Hapa huhusisha wiki 3 mpaka 4 toka Mgonjwa kuambukizwa bacteria wanaosababisha Kaswende,

Hapa dalili zinaanza kuonekana kama kidonda kidogo sana ambacho hata hakina maumivu yoyote kwa kitaalam huitwa chancre,

Kidonda hiki kidogo hakina maumivu yoyote ila kinakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuambukiza, Mtu anaweza hata asijue kwamba ana kijidonda hiki(chancre),

Na kinatokea sehemu ambapo bacteria wemeingilia Mwilini kama vile Mdomoni,Sehemu za Siri au kwenye njia ya haja kubwa.

Wastani kidonda huweza kuonekana wiki 3 baada ya kuambukizwa, lakini huweza kuchukua siku 10 mpaka 90 kuonekana, na Wakati mwingine Mtu huweza kuwa na dalili Moja tu ya Kuvimba kwa tezi la Lymph(Swollen lymph nodes).

Na mtu mwingine huweza kuambukizwa kwa kugusana na kijidonda hicho(Direct contact) hasa wakati wa kufanya mapenzi.

(2).Secondary syphilis

Katika hatua hii Ngozi inaweza kuwa na Rashes,maumivu ya koo au mtu kuwa na sore throat,

Rashes hizi kwenye ngozi haziwashi na mara nyingi huonekana kwenye viganja vya mikono pamoja na kwenye miguu kwa chini(sole), japo pia zinaweza kuonekana maeneo mengine.

Na watu wengine wanaweza wasijue mpaka zinaisha zenyewe.

Dalili zingine kwenye secondary syphilis ni pamoja na;

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuvimba kwa lymph nodes

- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

- Kupata Homa

- Uzito wa mwili kushuka au kupungua

- Nywele kunyonyoka(hair loss)

- Maumivu kwenye joints n.k

KUMBUKA;Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa makini kwa Mgonjwa mwenye shida hii,maana tafiti nyingi zinaonyesha ugonjwa wa kaswende unaweza kuwa na dalili ambazo hufanana kabsa na magonjwa mengine au Nonspecific symptoms, hali ambayo inaweza kuwa ngumu hata mtu kujua kama ana tatizo hili.

(3).Latent syphilis

Hatua ya tatu ya ugonjwa wa kaswende inajulikana kama latent au hidden, stage.

Dalili zote zilizoonekana kwenye hatua ya kwanza na ya pili zinapotea, hivo hakuna dalili yoyote inaonekana kwenye stage hii ndyo maana ya kupewa jina la hidden au latent stage.

Japokuwa dalili zimepotea ila Bacteria bado wapo mwilini na wakati mwingine huweza kuchukua muda kabla ya kwenda stage ya nne(tertiary stage of syphilis).

(4).Tertiary syphilis

Baadhi ya tafiti zinaonyesha ni asilimia 14% mpaka 40% ya watu wenye ugonjwa wa kaswende hufika stage hii,

Hatua hii ya ugonjwa wa kaswende inaweza kuchukua Muda mrefu sana(miaka) mpaka mtu kuingia kwenye stage hii toka siku ya kwanza ya maambukizi(initial infection).

Na madhara yake kwenye stage hii ni makubwa sana hata kuhatarisha maisha ya mgonjwa,

BAADHI YA MADHARA KWENYE HATUA HII YA UGONJWA WA KASWENDE NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kuwa kipofu au kutopoteza uwezo wa kuona(blindness)

- Mgonjwa kupoteza uwezo wa kusikia

- Kuathiriwa afya ya akili, kuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu n.k

- Kuharibiwa kwa soft tissue pamoja na mifupa

- Kupatwa na matatizo kwenye mfumo wa fahamu(neurosyphilis), ambapo bacteria wa kaswende hushambulia ubongo pamoja na uti wa mgongo.

- matatizo kama kiharusi(stroke), meningitis n.k

- Kupatwa na matatizo la Moyo n.k

KWA UPANDE WA MTOTO ALIYEZALIWA NA UGONJWA WA KASWENDE(congenital syphilis) ANAWEZA KUWA NA DALILI HIZI;

1. Kuchelewa hatua zake za ukuaji, kama kukaa,kusimama,kuongea n.k

2. Kuwa na dalili za kifafa au degedege

3. Kuwa na rashes kwenye ngozi

4. Kupandisha Homa

5. Ngozi na sehemu zingine kuwa na manjano(jaundice)

6. Kuwa na dalili za kuishiwa na damu(anemia)

7.Kuwa na vidonda ambazo vinaambukiza zaidi(infectious sores)n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA KASWENDE

Moja ya tiba kubwa kwa ugonjwa wa kaswende kwa mama mjamzito na watu wengine ni pamoja na kupewa dawa ya Penicillin ambapo hutolewa kwa mfumo wa sindano(Penicillin Injection).

Lakini kwa mtu mwenye allergy na Penicillin huweza kupewa antibiotics zingine ikiwemo;doxycycline,ceftriaxone n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamuAfyaclass Forum •

Kaswende ni ugonjwa gani,

Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana. Huu ni ugonjwa wa Zinaa.#Soma hapa Orodha mpya ya magonjwa ya Zonaa

Ugonjwa huu huanza kama kidonda ambacho mara nyingi hakina maumivu na kawaida huonekana kwenye sehemu za siri, puru au mdomo. Kaswende huenea kutoka kwa mtu hadi mtu kwa kugusana moja kwa moja na vidonda hivi. Pia inaweza kupitishwa kwa mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua na wakati mwingine kwa njia ya kunyonyesha.

Baada ya maambukizo kutokea, bakteria wa kaswende wanaweza kukaa kwenye mwili kwa miaka mingi bila kusababisha dalili. Lakini maambukizi yanaweza kuwa hai tena. Bila matibabu, kaswende inaweza kuharibu moyo, ubongo au viungo vingine. Inaweza kuhatarisha maisha pia.

Ugonjwa wa Kaswende ukiwa kwenye hatua za mwanzo unaweza kuponywa, wakati mwingine kwa Sindano moja tu ya dawa inayoitwa penicillin.

Ndiyo maana ni muhimu kupata uchunguzi wa afya mara tu unapoona dalili zozote za kaswende. Wajawazito wote wanapaswa kupimwa kaswende katika uchunguzi wao wa kwanza wa ujauzito pia.

Dalili Za Ugonjwa wa Kaswende

Kaswende hukua kwa hatua, Na Dalili zake hutofautiana kwa kila hatua(Stages). Lakini hatua hizi zinaweza kuingiliana,na dalili zake zikawa hazina mpangilio uliosawa. Unaweza kuambukizwa na bakteria wa kaswende bila kugundua dalili zozote kwa miaka.

Soma Zaidi hapa kuhusu Dalili za Ugonjwa wa Kaswende kwenye Kila hatua(Stages);

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende,chanzo chake(Syphilis)

Ugonjwa huu wa Kaswende huweza kusababisha Uharibufu wa;

  • Ubongo
  • Nerves
  • Macho
  • Moyo
  • Mishipa ya Damu(Blood vessels).
  • Ini
  • Mifupa na joints.

Matatizo haya yanaweza kutokea miaka mingi baada ya maambukizi ya awali, ambayo hayajatibiwa.

Kaswende inayoenea
Katika hatua yoyote ile, na ambayo haijatibiwa inaweza kuathiri ubongo, uti wa mgongo, macho na sehemu nyingine za mwili. Hii inaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya au hata kutishia maisha.

Kaswende ya kuzaliwa nayo(Congenital Syphilis)
Wajawazito walio na kaswende wanaweza kupitisha ugonjwa huo kwa watoto wao. Watoto ambao hawajazaliwa wanaweza kuambukizwa kupitia kiungo ambacho hutoa virutubisho na oksijeni ndani ya tumbo, kinachoitwa placenta. Maambukizi pia yanaweza kutokea wakati wa kuzaliwa.

Watoto wachanga walio na kaswende ya kuzaliwa wanaweza wasiwe na dalili. Lakini bila matibabu ya haraka, watoto wengine wanaweza kupata:

– Vidonda na upele kwenye ngozi.

– Homa.

– Ngozi na macho kubadilika rangi na kuwa manjano, hali inayoitwa kwa kitaalam jaundice

– Seli nyekundu za damu kuwa pungufu, kuwa na tatizo la upungufu wa damu au hali inayoitwa anemia.

– Kuvimba kwa wengu na ini.

– Kupiga chafya au kuwa na shida inayoitwa rhinitis.

– Mabadiliko ya mifupa.n.k

Dalili za baadaye zinaweza kujumuisha kuwa na shida ya ukiziwi, matatizo ya meno na pua, hali ambayo daraja la pua huanguka.n.k

Watoto walio na kaswende pia wanaweza kuzaliwa mapema sana. Wanaweza kufa wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa. Au wanaweza kufa baada ya kuzaliwa.

Chanzo cha Ugonjwa wa Kaswende

Chanzo cha kaswende ni bakteria aitwaye Treponema pallidum. Njia ya kawaida ya kaswende kuenea ni kwa kugusa kidonda cha mtu aliyeambukizwa wakati wa kujamiiana kwa uke, mdomo au Njia ya haja kubwa.

Bakteria huingia mwilini kupitia mikato,michubuko au mikwaruzo kwenye ngozi au kwenye utando wa ndani wenye unyevu wa baadhi ya sehemu za mwili.

Hatari ya kupata Kaswende

Hatari ya kupata kaswende ni kubwa ikiwa:

– Unafanya ngono bila kinga.

– Kufanya ngono na zaidi ya mpenzi mmoja.

– UnaIshi na VVU, virusi vinavyosababisha UKIMWI na haupo kwenye Tiba

– Uwezekano wa kupata kaswende pia ni mkubwa kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume.n.k

Matatizo/Madhara;
Bila matibabu, kaswende inaweza kusababisha uharibifu katika mwili wote. Kaswende pia huongeza hatari ya kuambukizwa VVU na inaweza kusababisha matatizo wakati wa ujauzito. Matibabu yanaweza kusaidia kuzuia uharibifu huu. Lakini hayawezi kurekebisha au kubadilisha uharibifu ambao tayari umetokea.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu
0 Comment

Hii ndyo Orodha mpya ya magonjwa ya zinaa kwa SasaAfyaclass Forum •

Hii ndyo Orodha mpya ya magonjwa ya zinaa kwa Sasa.

Magonjwa ya zinaa

Magonjwa ya Zinaa ni yale magonjwa yote ambayo huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kufanya mapenzi.

Magonjwa haya unaweza kuyapata kwa njia kama vile;

  • Vaginal sex
  • oral sex
  • au anal sex.
  • Pia huweza kusambazwa kupitia ngozi kugusana
  •  kuenea kwa kugusana kwa karibu sana kimwili kama vile kupapasana,ingawa hii ni mara chache.

Magonjwa ya Zinaa huweza kuenezwa baada ya mtu kupata maambukizi ya Viini mbali mbali vya magonjwa kama vile;

  • Bacteria
  • Fangasi
  • Virusi
  • Parasite n.k

Orodha ya magonjwa ya zinaa

Hii ndyo orodha ya magonjwa ya Zinaa kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa-CDC, pamoja na Shirika la Afya Duniani(WHO);

1. Bacterial Vaginosis

Maambukizi ya bacteria ukeni, Soma Zaidi ugonjwa huu wa Bacterial Vaginosis hapa.

2. Ugonjwa wa Chlamydia

Ugonjwa wa chlamydia kwa jina lingine hujulikana kama Ugonjwa wa pangusa, Soma Zaidi hapa ugonjwa huu wa Chlamydia.

3. Ugonjwa wa Kisonono(Gonorrhea)

Soma hapa Ugonjwa huu wa kisonono,dalili,matibabu.

4. Ugonjwa wa homa ya Ini(Hepatitis)

Pia virusi wa ugonjwa huu unaweza kuwapata wakati wa kufanya mapenzi

Soma Zaidi hapa, Ugonjwa wa hepatitis

5. Maambukizi ya Herpes

Genital herpes pia ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa,lakini watu wengi wenye maambukizi haya hawajui kama wanayo.

6. Ukimwi,VVU(HIV/AIDS)

Watu walio na magonjwa ya zinaa wana uwezekano mkubwa wa kupata pia virusi vya Ukimwi(VVU), ikilinganishwa na watu ambao hawana magonjwa ya zinaa.

Soma Zaidi hapa,Ukimwi pamoja na dalili zake

7. Maambukizi ya Virusi wanaojulikana kama Human Papillomavirus (HPV)

Soma Zaidi hapa kuhusu kirusi hiki cha HPV na Madhara yake

8. Mycoplasma genitalium (Mgen)

Mycoplamsa genitalium, au Mgen ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambayo mtu huweza kupata dawa jamii ya antibiotics akatumia na kupona.

9. Ugonjwa wa Kaswende(Syphilis)

Kaswende pia ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambayo huwapata watu wengi Zaidi,

Soma Zaidi hapa ugonjwa wa Kaswende,chanzo,dalili na Tiba.

10. Maambukizi ya Trichomoniasis

Soma Zaidi hapa tatizo hili la trichomoniasis 

11. Kwa Mujibu wa CDC, magonjwa haya pia yaliwekwa kwenye Orodha yao ya magonjwa ya Zinaa;

  • Maambukizi ya bacteria kwenye Via vya Uzazi(PID)
  • Chancroid,
  • scabies n.k.

Soma Zaidi hapa:

1. Jinsi ya kujikinga na magonjwa ya Zinaa

2. Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya Zinaa

3. Dalili za magonjwa ya Zinaa

4. Matibabu ya magonjwa ya Zinaa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Hii ndyo Orodha mpya ya magonjwa ya zinaa kwa Sasa
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD