Showing posts with label magonjwa ya ngozi. Show all posts
Showing posts with label magonjwa ya ngozi. Show all posts

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamuAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamu



Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo chanzo chake ni utitiri mdogo sana yaani tiny burrowing mite ambao hujulikana kama Sarcoptes scabiei.  Mtu hupata muwasho sana kwenye eneo ambalo utitiri huo umechimba.

Na wakati mwingine hali huwa mbaya Zaidi nyakati za Usiku ambapo Utitiri huu huhitaji kuchimba Zaidi.

Scabies inaambukiza na inaweza kuenea haraka kupitia mawasiliano ya karibu ya mtu na mtu katika familia, kikundi cha watoto, darasa la shule, nyumba ya uuguzi au gereza n.k. Kwa sababu upele huenea kwa urahisi, wahudumu wa afya mara nyingi hupendekeza kutibu familia nzima au watu wowote wa karibu.”

SCABIES: Makala 

Scabies, ni ugonjwa wa ngozi unaohusishwa na kuwasha na madoa madogo mekundu kwenye ngozi, yanayosababishwa na utitiri wa kuwasha(itchy mite).

Aina ya Utitiri huu yaani tiny burrowing mite hujulikana kwa kitaalam kama Sarcoptes scabiei.

Dalili za Scabies

DALILI ZA UGONJWA WA SCABIES NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata muwasho sana kwenye ngozi yake, na sana sana muwasho huu huzidi sana wakati wa usiku

– Kuanza kupata upele kwenye ngozi

– Ngozi kuanza kuwa na madoa doa mekundu

– Na maeneo ya ngozi ambayo huweza kuathiriwa zaidi ni pamoja na;

• Kati kati ya vidole

• Eneo la kwapani

• Kuzunguka kiuno

• Kwenye mikono

• Chini ya miguu kwenye sole

• Kuzunguka maziwa au matiti

• Kwenye sehemu za siri za Mwanaume(Around the male genital area)

• Eneo la matakoni

• Kwenye magoti

• Na kwa upande wa watoto wadogo, sana sana hutokea kwenye kichwa(Scalp), viganja vya mikono pamoja na miguuni.

MATIBABU YA SCABIES

– Zipo njia mbali mbali za kutibu Ugonjwa huu wa Scabies pamoja na vitu vya kuzingatia na kufanya ukiwa nyumbani, ikiwemo swala la usafi wa mwili pamoja nguo zako,

Na kwa upande wa tiba huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo za kunywa au Cream za kupaka n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siriAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume na Mwanamke, na katika Makala hii tumechambua baadhi,

Kuwasha na maumivu ni dalili za mara kwa mara ikuwa una Ugonjwa wa ngozi. Dalili Nyingi hazina madhara lakini dalili hizi zinaweza kuashiria hali ya kutatanisha zaidi ambayo ingehitaji Msaada wa mapema.

Maambukizi ya mara kwa mara ni kama vile ya  Fangasi(candida),Masundosundo au warts, magonjwa ya ngozi kama vile pumu ya ngozi/ eczema au psoriasis.

Kuna pia hali zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuathiri ngozi ya sehemu za Siri kama vile ugonjwa wa sclerosis au lichen planus n.k. Uvimbe na matuta yanaweza kutokea. Saratani za ngozi zinaweza kutokea n.k

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Baadhi ya Magonjwa ambayo huweza Kuathiri ngozi ya Sehemu za Siri ni pamoja na;

1. Fangasi sehemu Za Siri,Candida (thrush)

Ugonjwa wa Fangasi sehemu za Siri ni miongoni mwa magonjwa ambayo kwa kiasi kikubwa hushambulia ngozi ya Sehemu za Siri, Na moja ya dalili kubwa ni Mtu kupata muwasho sehemu za Siri.

#SOMA Zaidi hapa Fangasi sehemu za Siri kwa Mwanaume na Mwanamke

2. Maambukizi ya Genital herpes

Ugonjwa huu husababisha malengelenge kwenye sehemu za siri,unaweza kujitokeza na kundi la malengelenge madogo na/au vidonda. Vidonda vinaweza kuonekana kwenye vulva, ngozi ya matako,ngozi ya perianal au ngozi kwenye mapaja ya juu. Kawaida huweza kudumu kwa wiki kadhaa.

#Soma Zaidi hapa kuhusu Genital herpes

3. Masundosundo au Genital warts pamoja na molluscum contagiosum

Genital warts husababishwa na kirusi kinachojulikana kama human papillomavirus (HPV).

Tatizo hili pia huweza kuathiri ngozi ya Sehemu Za Siri.

#SOMA Zaidi hapa kuhusu Genital warts

Molluscum contagiosum haya ni maambukizi ya ngozi ambayo husababishwa na kirusi kinachoitwa pox virus, na inatoa vipele vidogo vya rangi ya ngozi kwenye ngozi.  Unaweza kupata kwa kugusana, ngozi kwa ngozi eneo la sehemu za siri,ambapo hii ni sehemu ya kawaida ya maambukizi.

4. Saratani ya Ngozi,

Pia Saratani ya ngozi huweza kuathiri eneo la ngozi ya Sehemu za Siri, hapa tunazungumzia Saratani kama vile melanoma skin cancer.

5. Magonjwa mengine ya ngozi ni pamoja na;

  • Psoriasis
    Psoriasis ni ugonjwa sugu wa uchochezi kwenye ngozi ambao huathiri karibu 2% ya idadi ya watu. Psoriasis isiyo ya kawaida inaweza kuathiri ngozi kwenye sehemu ya kinena, uke, mikunjo ya paja, Vulva, ngozi ya perianal, na matako.
  • Lichen sclerosus
    Lichen sclerosus ni ugonjwa sugu wa ngozi ambao unaweza kuathiri ngozi ya sehemu za siri. Unaweza kusababisha uwekundu au michubuko, mabaka meupe, kupoteza kwa usanifu wa kawaida wa uke na kubana kwa mlango wa uke.  Dalili ni pamoja na kuwasha,maumivu wakati wa kujamiiana n.k.  Sababu ya lichen sclerosus haijulikani lakini wakati mwingine inahusishwa na hali nyingine za autoimmune kama vile ugonjwa wa tezi.
  • Lichen planus
    Lichen planus ya ngozi ni upele wa kawaida unaowasha ambao huelekea kuisha ndani ya wiki 2. Lichen planus ya vulva, hata hivyo, inaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi, na kwa baadhi ya wanawake inaweza kusababisha maumivu ya sehemu ya uke.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
0 Comment

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGOAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi yake ya Asili, na kukufanya uwe na mabaka mabaka.

Dalili za Ugonjwa wa Ngozi kuwa Nyeupe,Vitiligo

Dalili ya Ugonjwa huu wa Vitiligo ni pamoja na;

✓ Ngozi kuanza kupoteza rangi yake ya asili na kuwa na mabaka mabaka ambapo kwa asilimia kubwa, mara ya kwanza huanza kuonekana maeneo kama vile;

  • Mikononi
  • Usoni
  • Sehemu Za Siri
  • Na maeneo yote ya mwili karibu na tundu au uwazi

✓ Nywele kuwa nyeupe au kuwa kama Mvi kwenye maeneo ya Kichwani,Kope,nyusi,au Ndevu n.k

✓ Kupotea kwa rangi ya asili kwenye Tishu ambazo zinazunguka Mdomo,Lips za mdomo,Puani n.k

Ugonjwa wa Vitiligo unaweza kuanza kwenye Umri wowote ingawa mara nyingi huanza kabla ya Mtu kufikisha Umri wa miaka 30.

Chanzo cha Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa Vitiligo hutokea pale ambapo seli zinazozalisha rangi (melanocytes)  kufa au kuacha kabsa kuzalisha melanin — ambapo hii ndyo pigment inayoipa ngozi rangi,nywele pamoja na macho.

Vipande vinavyohusika vya ngozi huwa vyepesi au vyeupe. Haijulikani ni nini hasa husababisha seli hizi za rangi kushindwa kufanya kazi au kufa. Ingawa Inaweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo:

  1. Matatizo ya Mfumo wa Kinga ya Mwili (autoimmune condition)
  2. Matatizo ya Urithi,Family history (heredity)
  3. Matukio kama vile kuungua sana kwenye ngozi
  4. Kuumia sana au kupata majeraha makubwa ya Ngozi baada ya kugusana na baadhi ya Kemikali
  5. Msongo wa mawazo n.k

Kumbuka; Melanin ni natural pigment ambayo huipa ngozi rangi yake ya asili, na huzalishwa na Seli zinazojulikana kama  melanocytes.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Ugonjwa wa Vitiligo

– Kuwa na Mtu mwenye shida hii kwenye Familia yako

– Kuwa kwenye mazingira ya kugusa kemikali mara kwa mara,mfano phenol-containing chemicals,n.k

– Kupata matukio kama vile kuungua sana Ngozi, kupata majeraha makubwa ya ngozi n.k

– Kuwa na matatizo kwenye Mfumo wa kinga ya Mwili n.k

Fahamu Pia,Mtu mwenye Ugonjwa wa Vitiligo huweza kupata madhara mengine ikiwemo;

FAHAMU KWA KINA TATIZO AU UGONJWA WA VITILIGO (UGONJWA UNAOIFANYA NGOZI KUPOTEZA RANGI YAKE)

• • • • • •

Ni tatizo linaloifanya ngozi ipoteze rangi yake ya asili. Sehemu zinazopoteza rangi huongezeka ukubwa kadri siku zinavyozidi kwenda. Tatizo hili linaweza kuathiri pia nywele,pamoja na sehemu ya ndani ya kinywa

Siku zote rangi ya ngozi na nywele za binadamu huamuliwa na vichocheo vya melanin. Vitiligo hutokea baada ya sehemu (seli) zinazozalisha vichocheo ya melanin kufa,au vikiacha kufanya kazi. Kwa msingi huu,kufa au kuacha kufanya kazi kwa seli zinazozalisha melanin kunaweza kusababishwa na mambo matatu

1.Matatizo kwenye mfumo wa ulinzi wa mwili ambao huanza kuzishambulia seli zake wenyewe kama maadui (wavamizi),jambo ambalo kitaalamu huitwa Autoimune condition

2.Kurithi

3.Mzio (allergy),stress pamoja na mionzi mikali ya jua au ajali kubwa ya ngozi

Tatizo hili siyo la kurogwa wala kuambukizwa,na haliwezi kumpata mtu mwingine kwa kugusana au hata kushirikiana naye mambo kadhaa kwenye jamii,hivyo tusiwatenge na kuwanyanyapaa wagonjwa wa tatizo hili ambao hupitia kipindi kigumu sana cha masongo wa mawazo,kuungua vikali na mwanga wa jua pamoja na matatizo ya kuona na kusikia

Tatizo hili halina tiba ya kudumu,hata hivyo msaada wa matibabu hutolewa kulingana na umri,ukubwa wa tatizo,jinsi maisha ya mtu yalivyo athirika pamoja na kasi ya kukua kwa tatizo.

 Vyote hivi hulenga kuleta ahueni ya tatizo kwa mgonjwa pamoja na kuipunguza kasi ya kukua/kusambaa kwa tatizo hili.

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD