Showing posts with label masikio. Show all posts
Showing posts with label masikio. Show all posts

Tatizo la Masikio Kupoteza Usikivu,Chanzo,Dalili na Tiba yake,Afyaclass Forum •

Tatizo la Masikio Kupoteza Usikivu,Chanzo,Dalili na Tiba yake,

Tatizo la Kupoteza Usikivu kwa Mtu huweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo Uzee(Umri mkubwa) Pamoja na mtu kukaa kwenye mazingira ya makelele mengi makubwa kwa muda mrefu,

Sababu zingine kama vile masikio kuwa na Nta kupita kiasi(excessive earwax), pia huweza kupunguza usikivu wa masikio kwa Muda.

Wakati mwingine kulingana na chanzo cha tatizo hili huwa vigumu kwa masikio kurudisha usikivu wake kama Mwanzo,ila tiba ikasaidia tu kupunguza baadhi ya madhara,

Soma zaidi hapa chini....!!!!

DALILI ZA TATIZO HILI LA MASIKIO KUPOTEZA USIKIVU WAKE NI PAMOJA NA;

- Mtu kuanza kupata shida ya kuelewa maneno kutoka kwa watu wengine hasa wakiongea mazingira yenye kelele au watu wengi

- Mtu kuanza kuongea kwa Sauti kubwa sana, bila kujua anaongea kwa sauti kubwa zaidi kwa wengine

- Kuomba mara kwa mara watu wengine kuongea taratibu ila kwa Sauti kubwa ili usikie vizuri

- Kuhitaji Sauti ya TV au REDIO kuwa Juu Zaidi ili usikie vizuri

- Kuhitaji Sauti ya Simu Kuwa Juu zaidi ili uweze kusikia vizuri wakati wa mazungumzo n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?

mara nyingi tatizo la Masikio kupoteza usikivu wake hutokana na;

1. kuharibiwa kwa sehemu ya ndani ya sikio(inner ear), Na hii husababishwa na sababu mbali mbali kama vile; Uzee(umri mkubwa), mtu kukaa kwenye mazingira yenye makelele mengi makubwa kwa muda mrefu n.k,

Vitu hivi huweza kusababisha shida kwenye vinyweleo au Nerve cells kwenye eneo la cochlea,

Kumbuka vinyweleo hivi au Nerve cells hizi ndyo hutuma taarifa(sound signals) kwenda kwenye Ubongo, Hivo baada ya kuharibiwa haziwezi tena kufanya kazi vizuri hivo tatizo la upotevu wa usikivu hutokea.

2. Kujengwa kwa Nta taratibu ndani ya sikio(Earwax), Nta ikizidi huweza kuziba ear canal na kuzuia upitishwaji wa Mawimbi ya Sauti,

Hivo kuondoa uchafu huu(Nta/earwax) huweza kurudisha usikivu wa sikio lako.

3. Maambukizi ya Sikio, masikio kushambuliwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama bacteria,fangasi,virusi n.k huweza kuleta tatizo la masikio kupoteza usikivu wake

4. Kuwa na shida ya kimaumbile kwenye mfupa eneo la sikio(abnormal bone growths), hii hutokea tangu ukiwa tumboni

5. Uwepo wa tatizo la Uvimbe ndani ya sikio, hasa sehemu ya nje au katikati ya sikio(outer or middle ear),

Hii pia huweza kusababisha masikio kupoteza usikivu wake.

6. Kupatwa na Tatizo la Kupasuka NGOMA ya SIKIO(Ruptured eardrum),

Makelele mengi,Sauti kubwa sana, mabadilikio ya gafla ya Presha,kuingiza kitu chenye ncha kali sikioni,maambukizi ya magonjwa n.k,

Vyote hivi huweza kusababisha tatizo la Ngoma ya Sikio kupasuka,kisha Mtu kupoteza Usikivu wake. N.K

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA KUPATA TATIZO LA KUPOTEZA USIKIVU MASIKIONI

- kuwa na Umri Mkubwa(Uzee)

- Kufanya kazi kwenye mazingira yenye makelele mengi na makubwa mara kwa mara,

Au kukaa kwenye mazingira yenye makelele zaidi kila mara,makelele ya mziki mkubwa, makelele ya milipuko mikubwa ya mabomu,vyuma kugongwa sana n.k

- Kuwa na Mtu mwenye tatizo hili ndani ya Familia yako(heredity)

- Matumizi ya baadhi ya Dawa hovio pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya,mfano dawa kama; gentamicin, sildenafil (Viagra) au dawa jamii ya chemotherapy drugs, huweza kuharibu sehemu ya ndani ya sikio(inner ear).

Kutumia Dose kubwa za aspirin au dawa zingine za maumivu(pain relievers), Dawa za Malaria(antimalarial drugs) N.k

- Kupatwa na magonjwa ambayo husababisha Homa kali(high fever), kama vile meningitis n.k, huweza kuharibu eneo la cochlea ndani ya sikio."

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUPOTEZA USIKIVU

Zipo tiba mbali mbali kulingana na chanzo husika,ila kwa Ujumla,tiba huweza kuhusisha;

- Kuondoa uchafu au Nta zinazoziba masikio(Removing wax blockage).

- Upasuaji kwa baadhi ya matatizo

- Kutumia Dawa za kutibu infections mbali mbali

- Kutumia vifaa vya kuongeza Usikivu(Hearing aids). N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Chanzo cha Sikio kutoa Usaha au Maji MajiAfyaclass Forum •

 Chanzo cha Sikio kutoa Usaha au Maji Maji

• • • • • •

TATIZO LA KUTOKA USAHA AU MAJIMAJI MASIKIONI (OTORRHEA) chanzo chake

Tatizo la kutokwa na usaha au maji maji sikioni ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Otorrhea ni tatizo ambalo huweza kumpata mtu yoyote bila kujali umri wake wala jinsia yake.

Shida hii huweza kuanzia sehemu ya ndani ya sikio yaani Inner Ear, sehemu ya katikati ya sikio yaani Middle Ear na hata sehemu ya Nje ya sikio yaani Outer Ear.

DALILI ZA TATIZO HILI

- Mtu mwenye shida hii kwanza kabsa utaonekana usaha ndani ya sikio au maji maji yakitoka ndani ya sikio

- Sikio kuanza kutosikia vizuri au kuziba

- Wengine hupata maumivu ndani ya sikio

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA USAHA AU MAJI MAJI SIKIONI

Zipo baadhi ya Sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili la kutokwa na usaha au maji maji sikioni, na sababu hizo ni kama vile;

- Kupatwa na shida ya maambukizi ya Fangasi za masikioni ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Otomycosis

- Kupatwa na maambukizi ya Ugonjwa wa Tuberculosis(TB) ndani ya sikio

- Pia Mgonjwa wa Virusi vya ukimwi huweza kupatwa na shida hii ya kutokwa na usaha au maji maji masikioni

- Kupata tatizo la Kansa ya sikio ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Neoplasm

- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria N.K ambayo huathiri ngoma ya sikio,sehemu ya katikati ya sikio pamoja na sehemu ya Nje ya sikio lako

- Ngoma ya Sikio kupasuka

- Kuchomwa na kitu chochote chenye ncha kali sikioni au Kuingiwa na kitu chochote sikioni kama vile; punje ya mahindi,maharage,mdudu, Kijiwe N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Maambukizi kwenye Sikio la mtoto,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Forum •

Maambukizi kwenye Sikio la mtoto,chanzo,dalili na Tiba

Maambukizi kwenye Sikio hutokea wakati Vimea vya magonjwa kama vile Virus au bacteria wanaposhambulia sehemu ya kati kwenye sikio(middle ear) ambapo kwa kitaalam maambukizi haya hujulikana kama Otitis media.

Mara nyingi maambukizi kwenye Sikio huambatana na maumivu ya sikio,uchafu kutoka n.k, na kwa baadhi ya watoto tatizo hili hupona lenyewe.

Kwanini Watoto hupata maambukizi kwenye Sikio kwa urahisi zaidi kuliko watu wazima?

Watoto hupata maambukizi ya sikio mara nyingi zaidi kuliko watu wazima kwa sababu:

1. Sehemu ya sikio inayojulikana kama eustachian tubes haifanyi kazi sawa na watu wazima, hali ambayo husababisha maji kukusanyika nyuma ya ngoma ya Sikio(eardrum).

2. Kinga yao ya mwili bado haina uwezo wa kupambana na vimelea vya magonjwa vyakutosha

3. Wana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa kutoka kwa watoto wengine.

Dalili za Maambukizi kwenye Sikio

Dalili za Maambukizi kwenye Sikio ni pamoja na;

  • Kupata maumivu ya Sikio
  • Kukosa hamu ya chakula
  • Kupata shida ya Usingizi
  • Kupata shida ya Kusikia au kutokusikia vizuri kwenye sikio lililoathiriwa
  • Kuhisi hali ya Uzito,pressure au kujaa ndani ya Sikio lako
  • Kutokwa na usaha au uchafu sikioni,uchafu ambao huweza kuwa na rangi ya njano,brown au nyeupe n.k

USHAURI: Usiweke chochote kwenye mfereji wa sikio ikiwa una uchafu au maji kutoka kwenye sikio lako, Kitu chochote kinachogusa ngoma ya sikio iliyopasuka kinaweza kusababisha uharibifu zaidi.

Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio

Bakteria na virusi husababisha maambukizi kwenye sikio. Mara nyingi, maambukizi ya sikio huanza baada ya baridi au maambukizi mengine ya njia ya juu ya kupumua. Vijidudu huingia kwenye sikio lako la kati kupitia bomba la eustachian (eustachian tube).

Mara tu Virusi au bakteria wanapoingia ndani ya sikio wanaweza kusababisha mrija wa eustachian kuvimba. kuvimba huku kunaweza kusababisha mrija kuziba, na hivyo kusababisha kutokufanya kazi vizuri na maji maji kwenye sikio lako la kati kupata maambukizi.

Vitu hivi huongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye sikio

• Umri: Watoto wachanga na watoto wadogo (kati ya miezi 6 na miaka 2) wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya sikio.

• Family history: Kupata maambukizi ya sikio kunaweza kuwa tatizo ndani ya familia yako

• Mafua: Kuwa na mafua huongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio. Watoto walio katika vituo vya kulelea watoto wachanga na katika vikundi wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa au kupata maambukizi kwenye masikio kwa sababu wana uwezekano mkubwa wa kuwa karibu na watoto walio na mafua au magonjwa mengine ya kupumua ambayo ni yakuambukiza.

• Magonjwa ya muda mrefu(Chronic illnesses): Magonjwa ya muda mrefu ikiwemo magonjwa ambayo husababisha upungufu wa kinga mwilini pamoja na magonjwa sugu ya kupumua (kama vile cystic fibrosis na pumu au Asthma), yanaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio.

• Sababu zingine ambazo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio ni pamoja na;

  • Uvutaji wa Sigara
  • Kuwa kwenye mazingira ya moshi
  • Uchafuzi wa hali ya hewa
  • Uchafu wa mwili n.k

Madhara ya Maambukizi ya Sikio kwa Mtoto

Madhara ya Maambukizi ya Sikio ni pamoja na;

- Kupoteza uwezo wa kusikia

- Mtoto kuchelewa kuongea, Fahamu ili mtoto ajifunze Lugha na kuendelea kuongea anahitaji kusikia, hivo endapo maambukizi ya sikio yataathiri uwezo wa mtoto kusikia, hata kuongea pia inaweza kuwa tatizo kwake.

- Kupasuka kwa ngoma ya Sikio,Takriban asilimia 5% hadi 10% ya watoto walio na maambukizi ya sikio hupasuka kidogo kwenye ngoma ya sikio. Mara nyingi, mpasuko huu hupona wenyewe. Ikiwa sivyo, mtoto wako anaweza kuhitaji upasuaji.

- kusambaza maambukizi zaidi, Maambukizi yasiyotibiwa au maambukizi yasiyopona yenyewe yanaweza kuenea.

Maambukizi haya yanaweza kuenea kwenye mfupa nyuma ya sikio lako (mastoiditis). Mara kwa mara, maambukizi yanaweza kuenea kwenye utando unaozunguka ubongo wako na uti wa mgongo (meninji) na kusababisha homa ya uti wa mgongo(meningitis).

Matibabu ya Maambukizi ya Sikio

Matibabu yanategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:

Umri wa mtoto wako.

Ukali wa maambukizi.

Asili ya maambukizi (maambukizi ya mara ya kwanza, yanayoendelea au ya kurudia).

Ikiwa maji yanabaki kwenye sikio la kati kwa muda mrefu.n.k

Mara nyingi, maambukizi ya sikio hupona bila matibabu. Mtoa huduma wako anaweza kufuatilia hali ya mtoto wako ili kuona kama inaimarika kabla ya kuagiza matibabu. Mtoto wako anaweza kuhitaji dawa za kuua vimelea vya magonjwa au upasuaji kwa maambukizi ambayo hayatoki. Wakati huo huo, dawa za maumivu zinaweza kusaidia kwenye dalili kama vile maumivu ya sikio.

Dawa za maumivu ambazo huweza kutumika ni pamoja na;

  • acetaminophen (Tylenol®)
  • ibuprofen (Advil®, Motrin®)

Kamwe Usimpe mtoto aspirini. Aspirini inaweza kusababisha hali ya kutishia maisha inayoitwa Reye’s syndrome.

Zingatia haya ili kuzuia maambukizi ya sikio kwa Mtoto

- Hakikisha unamkinga mtoto na magonjwa yanayoathiri mfumo wa hewa(respiratory illnesses) ikiwemo mafua.

- Epuka kabsa uvutaji wa Sigara au kukaa kwenye mazingira yenye moshi wa Sigara

- Hakikisha unamnyonyesha mtoto wako kwa kipindi cha miezi sita bila kumchanganyia na kitu chochote, bila kusahau kuendelea kunyonyesha hadi miaka 2 au zaidi hata baada ya kuanza kumpa na vitu vingine.

Maziwa ya mama hutoa kinga ya kutosha kwa mtoto,Antibodies kwenye maziwa ya mama hupambana na virusi na bakteria wanaosababisha maambukizi.

- Hakikisha mtoto anapata chanjo zote muhimu anazotakiwa kupewa. n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Tatizo la SIKIO AU MASIKIO KUZIBA,chanzo,Dalili na TibaAfyaclass Forum •

 Tatizo la SIKIO AU MASIKIO KUZIBA,chanzo,Dalili na Tiba

• • • • • •

FAHAMU KWA KINA TATIZO LA KUZIBA KWA SIKIO KUTOKANA NA NTA PAMOJA NA CHANZO CHAKE

Moja ya vyanzo vikubwa vya tatizo la kuziba kwa sikio ni NTA. Maana ya NTA, Hapa tunazungumzia kuhusu vitu vyenye asili ya umaji umaji pamoja na mnato ambavyo hupatikana ndani ya sikio.

Kazi ya NTA sikioni ni pamoja na Ulinzi wa sikio juu ya vitu vinavyoingia,ambapo NTA huweza kunata, kushikilia pamoja na kuzuia kitu kisipite ndani ya sikio Kwa haraka,Mfano wale wadudu wadogo wadogo ambao hupenda kuingia ndani ya sikio huweza kunaswa hapa. Lakini pia nta husaidia katika kusafisha sikio, pamoja na kulainisha Sikio.

SABABU ZA NTA KUZIBA SIKIO NI PAMOJA NA;

- Uwepo wa Nta kupita kiasi sikioni huweza kusababisha tatizo la Sikio kuziba, Lakini hali hii huweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo mashambulizi ya magonjwa mbalimbali ndani ya sikio.

- Kuwa na tabia ya kupenda kutumia pamba katika kusafisha masikio, Pamba zingine huweza kunaswa na NTA hivo kupelekea hali ya Sikio kuziba

- Kutumia mara kwa mara carotenoids

-  Hali ya kimaumbile ya mtu ambapo mtu huzaliwa na udhaifu flani ndani ya sikio

DALILI ZA TATIZO LA SIKIO KUZIBA KUTOKANA NA NTA NI PAMOJA NA;

1. Kuanza kupata hali ya kukohoa mara kwa mara

2. Kuanza kutoa harufu mbaya sikioni

3. Kuwa na maumivu ya sikio

4. Sikio kuanza kutoa Uchafu

5. Kupata hali ya muwasho ndani ya Sikio

6. Kuhisi hali ya uzito wa sikio

7. Kusikia kelele kama za kengele masikioni

8. Sikio kupoteza uwezo wake wa Kusikia

MADHARA YA KUZIBA KWA SIKIO KUTOKANAKO NA NTA.

1. Sikio kupoteza uwezo wake wa kusikia

2. Miwasho ya mara kwa mara sikioni hasa hasa kwenye Mlango wa kuingilia Ndani

3. Kero ya kusikia kengele masikioni kila mara

4. Ngoma ya sikio kupatwa na hatari ya kutoboka

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matitiAfyaclass Forum •

Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, tarehe 8 Machi ,2024

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza lengo likiwa ni kuwafikia wananchi ambao wanashindwa kufika hospitali kwa sababu mbalimbali.

huduma hii ambayo inaratibiwa na Wanawake wa Bugando ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inafanyika kwa siku tatu mfululizo, tarehe 04 – 06, Machi 2024 katika maeneo ya Bujingwa Shule ya Sekondari, Buswelu round about na Mabatini.

Akizungumzia huduma hii, Mwenyekiti wa Wanawake Bugando Bi. Eunice Kitula amesema

“wanawake wa Bugando kwa kutambua kuwa jamii hususani wanawake wanakabiliwa na magonjwa mbalimbal ikiwemo kansa ya mlango wa kizazi na Kansa ya matiti na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuna utaratibu wa kuchunguza afya zetu mara kwa mara, hali hii imetusukuma kuendesha huduma hii ili kubaini changamoto zozote za kiafya mapema na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzitibu na kutoa ushauri wa kitaalamu na ndicho tunachokifanya ” amesema Bi. Eunice Kitula na kuwakaribisha wananchi kujitokeza na kutumia fursa hii adhimu.

Kwa upande wake mtaalamu wa uoni Idara ya Macho Bw. Justice Daffa ametanabaisha kuwa sehemu kubwa kubwa ya wagonjwa waliowaona wana tatizo la uoni hafifu unaotokana na kurithi na wengine wachache umetokana na kujiumiza na vitu mbalimbali ikiwemo vijiti au peni. Bw. Daffa amesiaitiza Wazazi na Walimu kushirikiana kutambua tatizo la uoni hafifu mapema na kalipatia ufumbuzi mapema ili kuepukana na upofu unaoweza kuzuilika na kuongeza kuwa ni rahisi Mwalimu kugundua tatizo la uoni kwa kumwangalia Mwanafunzi kushindwa kuona ubaoni akiwa mbali au akiwa karibu.
@wizara_afyatz
@kanisa_katolikitz
@dr.fabian_massaga

Huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani
ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD