Showing posts with label tatizo la vichwa vikubwa. Show all posts
Showing posts with label tatizo la vichwa vikubwa. Show all posts

WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bureAfyaclass Forum •

DAR ES SALAAM; WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bure katika kambi maalum itakayofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Kambi maalum ya upasuaji huo Itafanyika kwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itafanyika Aprili 20 na ya pili mwezi Mei.

Akizungumza leo Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji MOI, Dk Lemeri Mchome amesema wamekuja na mkakati ambao utahakikisha huduma hiyo inawafikia watoto wengi ambao hawajaipata.

“Tumepanga kufanya kambi ya upasuaji tarehe 20 Aprili na Mei, itatanguliwa na kliniki kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa watoto na kuwapanga kwa ajili ya kambi,” amesema.

Amesema MOI kwa kushirikiana na wadau wanafanya huduma hiyo, wakiwemo chama cha wazazi wenye watoto hao na MO Dewji Foundation.

“Kwa niaba ya Watanzania tunawashukuru kwa kuamua kuwasaidia watoto waliopata changamoto, tumeona kwa sasa watoto wapate huduma wote wengine wanakuja na kushindwa kupata matibabu kwa ajili ya fedha tuko na timu nzima kuhakikisha huduma endelevu na jumuishi,”ameeleza.

Mwakilishi wa MO Dewji Foundation, Amina Ramadhani amesema wamepanga kusaidia watoto hao kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

“Kuanzi vipimo na gharama za upasuaji na kufuatilia baada ya huduma na tutawasaidi watoto hawa kwa kipindi cha mwaka tutafatilia hapa MOI na kutoa gharama zote wapate huduma.

Amesema ili kufanikisha hilo watasaidiana kuleta watoto kutoka mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga huku wazazi wakipewa nauli na malazi kwa kushirikiana na ASBATH.

“Kuna watoto ambao wanatoka mikoani kama 25 hivi na wazazi wao hawana uwezo wa kuja, watawezeshwa ili waweze kufika wataandaliwa makazi na ASBATH na tutawasaidia kupata chakula.

Aidha MKurugenzi wa Chama cha Wazazi wa Wwatoto Wenye ulemavu wa Kichwa kikubwa na Mgongo wazi(ASBATH), Suma Mwaipopo amewashukuru wote kwa ushirikiano kwa ajili ya kambi na kuwasihi wazazi kutoka mikoa yote wasikose kwa faida yao.

WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa
upasuaji bure
0 Comment

Fahamu ukweli, hatari na matibabu ya Vichwa vikubwaAfyaclass Forum •

Fahamu ukweli, hatari na matibabu ya Vichwa vikubwa

Kichwa kikubwa ni ugonjwa wa watoto wachanga wa kutanuka chemba za maji za kichwani na hivyo kupeleka muonekano wa kichwa kuwa mkubwa. Ugonjwa huu ni matokeo ya kuzalishwa kwa maji mengi kichwani ama kuziba kwa njia za kupitisha/kufyonzwa maji hayo.

Hutokana na sababu za kinasaba, hivyo mtoto kuzaliwa na kichwa kikubwa. Aina hii huambatana na matatizo mengine kama vile mgongo wazi (SPINE BIFIDA) na mguu kifundo (TALIPES). Sababu nyingine ni maambukizi ya mishipa ya fahamu pindi mtoto anapozaliwa au mara tuu baada ya kuzaliwa.

Ukweli kuhusu kichwa kikubwa 

  • Asilimia 50 ya watoto wa kichwa kikubwa huwa na changamoto ya ukuaji.
  • Kuanza matibabu mapema baada ya mtoto kuzaliwa hupunguza changamoto hizi za ukuaji.

Vihatarishi vyake

  • Ukosefu wa virutubisho (vitamins) aina ya folic acid wakati wa ujauzito.
  • Unywaji holela wa baadhi ya dawa za hospitali wakati wa ujauzito.
  • Ajali, hususani kwa watu wazima
  • BAADHI YA WATU WALIOZIDI MIAKA 60 (NORMAL PRESSURE HYDROCEPHALUS)

Dalili zake

Kwa watoto wachanga chini ya umri wa mwaka 1

  • Kulialia hovyo
  • Kushindwa kunyonya au kula vizuri.
  • Kuchelewa kukaza shingo
  • Kuvimba/kujaa utosi

Kwa watoto wakubwa na WATU WAZIMA

  • Kichwa kuuma
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Matatizo ya kuona, kutembea, balance
  • Macho kuzama chini kamaa jua linalokuchwa

Matibabu yake

  • Kuwekewa mirija maalum ya kutoa maji (shunt)
  • Njia ya kisasa ya matundu (ETV)

Via:DR JUMA MAGOGO

>> Soma Zaidi tatizo la vichwa vikubwa au mtoto kuzaliwa na Kichwa kikubwa

>>Soma Zaidi kuhusu Faida za Vidonge vya Kuongeza Damu

>>Soma Zaidi tatizo la mgongo wazi (SPINE BIFIDA) 

Fahamu ukweli, hatari na matibabu ya Vichwa vikubwa
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD