Showing posts with label ugonjwa wa sukari. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa sukari. Show all posts

Jinsi ya Kupunguza Hatari ya Kupata KisukariAfyaclass Forum •

 Jinsi ya Kupunguza Hatari ya Kupata Kisukari

Kisukari ni ugonjwa hatari ambao unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya yako. Kwa bahati mbaya, idadi ya watu wanaougua kisukari inaongezeka kila mwaka, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kuzuia ugonjwa huu mapema kabla ya kujitokeza.

Pata picha tu Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la afya Duniani(WHO)

Idadi ya watu wenye Ugonjwa wa Kisukari(diabetes) Duniani iliongezeka kutoka Million108 mwaka1980 mpaka kufikia Watu million 422  kwa mwaka 2014, Je kama Idadi inaongezeka kila mwaka leo hali Ipoje?

Pia ugonjwa huu wa Kisukari ni chanzo kikubwa cha matatizo mengine kama vile;

  • Upofu wa macho(blindness),
  • Tatizo la Figo kushindwa kufanya kazi(kidney failure),
  • Shambulio la moyo(heart attacks),
  • Tatizo la kiharusi(stroke)
  • Pamoja na Tatizo la watu Kukatwa MIGUU

• Soma zaidi hapa,Dalili za Ugonjwa wa Kisukari 

Kuna hatua kadhaa za kufuata ili kupunguza hatari ya kupata kisukari, na makala hii itakusaidia kujifunza jinsi ya kufanya hivyo.

1.Kula vyakula sahihi

Vyakula vyenye kiwango cha juu cha sukari, wanga, na mafuta yasiyofaa ni hatari kwa afya yako na vinaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari.

Kwa hiyo, ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi, kama vile matunda, mboga mboga za majani, protini, na wanga unaochujwa.

2. Fanya Mazoezi ya mara kwa mara

Mazoezi ya mara kwa mara yanasaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari,

Jaribu kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kwa siku, angalau siku tano kwa wiki.

Mfano wa mazoezi haya ni pamoja na

  • Mazoezi ya kutembea,
  • kukimbia,
  • kuogelea,
  • Kuendesha baiskeli,
  • Pamoja na yoga.

3. Punguza Unene wa mwili

Unene wa mwili ni hatari kwa afya yako na inaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari. Kwa hiyo, ni muhimu kupunguza uzito wako kwa kupitia lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara.

4. Tumia Maji ya kutosha

Unywaji wa maji wa kutosha ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari. Jaribu kunywa angalau lita 2.5 ya maji kwa siku.

5. Punguza Matumizi ya Pombe


Hitimisho:

Kupunguza hatari ya kupata kisukari ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kuepuka madhara makubwa ya ugonjwa huo.

Kwa kuzingatia lishe bora, mazoezi ya mara kwa mara, unywaji wa maji wa kutosha, na kupunguza matumizi ya pombe, unaweza kupunguza hatari kwako ya kupata kisukari.

Ni muhimu kufuata hatua hizi kama njia ya kudumu ili kuhakikisha afya yako na kuepuka hatari ya kupata kisukari.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Serikali yatumia bilioni 346.4 kutibu wagonjwa wa kisukari na tezi dumeAfyaclass Forum •

Serikali yatumia bilioni 346.4 kutibu wagonjwa wa kisukari na tezi dume

Na WAF – Dodoma

Serikali imesema kuwa gharama ya kutibu wagonjwa wa Sukari kwa mwaka ni shilingi bilioni 300, na gharama za kutibu wagonjwa wote wa tezi dume ni shilingi bilioni 46.42 hivyo kupelekea jumla ya gharama za matibabu kwa magonjwa haya mawili kufikia shilingi bilioni 346.42.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali namba 98 kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Igalula, Mhe. Venant Daud aliyeuliza Je, Serikali haioni haja ya kutoa msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wa sukari na tezi dume nchini.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa gharama za matibabu ya magonjwa hayo mawili ni kubwa sana wakati bajeti ya dawa lna vifaa tiba kwa mwaka ni shilingi bilioni 200.

“Ikitokea huduma ya matibabu kwa magonjwa haya mawili kutolewa bure kutasababisha huduma nyingine katika nchi kusimama”. Amesema Dkt. Mollel.

Aidha, amesema Serikali inasisitiza utekelezaji wa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, ya kutoa huduma ya Msamaha kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia huduma za afya hata hivyo, wenye uwezo wa kulipia wataendelea kuchangia.

Dkt. Mollel ameongeza kuwa mwaka 2022/2023 gharama ya msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wa sukari na saratani ya tezi dume ilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 70.4

Vile vile Dkt. Mollel amesisitiza viongozi wa Mamlaka za mikoa na Serikali za mitaa kusimamia sekta ya afya kikamilifu ili kuleta ubora wa huduma ili kutekelza azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kila Mtanzania kupata huduma bora za afya.

Serikali yatumia bilioni 346.4 kutibu wagonjwa wa kisukari na tezi dume
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD