TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA UGUMBAAfyaclass Bongo Social •

UGUMBA

• • • • • •

TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA UGUMBA

.

Kwa hivi sasa moja ya matatizo makubwa yanayosumbua ndoa nyingi ni watu au wanandoa kukosa watoto, Zipo baadhi ya tabia ambavyo huweza kuwa chanzo kikubwa cha tatizo la Ugumba kwa watu.


TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA UGUMBA NI PAMOJA NA;


- Matumizi ya pombe kupindukia/kupita kiasi au kuwa Mlevi


- Kuwa na tabia ya kuvuta sigara mara kwa mara


- Kuwa na tabia ya kutoa mimba mara kwa mara hapo nyuma


-  Kuwa na maambukizi sugu ambayo hayatibiwi kwa asilimia kubwa, Mfano maambukizi ya fangasi,UTI au maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke ambapo kwa kitaalam hujulikana kama pelvic Inflammatory disease au PID


- Mwanaume anayefanya kazi kwenye mazingira ya joto sana na kwa mda mrefu huwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la kuzalisha mbegu chache na zenye uwezo mdogo wa kulirutubisha Yai ambapo kwa kitaalam  hali hii hujulikana kama Low Sperm count


- Kuwa na tabia ya kujichua au kufanya punyeto


- Matumizi ya dawa hovio bila kuzingatia mashariti kutoka kwa wataalam wa afya


- Kupendelea kula vyakula kama chips huweza kumuathiri mwanaume katika uzazi wake, ikiwa ni pamoja na nguvu za kiume pamoja na uwezo wa kuzalisha mbegu bora kwa kiwango kinachotakiwa.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWAAfyaclass Bongo Social •

MPASUKO

• • • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWA


Tatizo hili huweza kumpata mtu wa umri wowote (mtoto,kijana na hata mzee), lakini pia tatizo la mpasuko wa mfereji wa haja kubwa huweza kutokea kwa mtu wa Jinsia yoyote yaani Mwanaume au mwanamke.


CHANZO CHA TATIZO LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;


1. Mtu kushiriki mapenzi kinyume na maumbile


2. Kupatwa na tatizo la Choo kigumu ambalo huchukua mda mrefu


3. Kujisaidia kwa kujilazimisha na kwa kutumia nguvu nyingi


4. Mtu kuwa na shida ya kuharisha kwa mda mrefu


5. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya zinaa ikiwemo ugonjwa wa kaswende


6. Kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi


7. Kupatwa na shida ya saratani ya Njia ya haja kumbwa ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Rectal Cancer


8. Kupatwa na magonjwa ambayo huhusisha miwasho mingi pamoja na kuvimba kwa eneo hili,ikiwemo pamoja na tatizo la kushambuliwa na Fangasi kwa muda mrefu


9. Kupatwa na ajali ambayo huweza kuhusisha kuchanika kwa maeneo haya


DALILI ZA TATIZO LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;


- Mtu kuhisi maumivu makali wakati wa kujisaidia


- Kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu


- Nguo ya ndani kuwa na damu au matone tone ya damu baada ya kuivua



MATIBABU YA TATIZO LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWA


✓ Matibabu ya tatizo hili hutegemea sana chanzo chake,mfano; kama tatizo limetokana na mgonjwa kushambuliwa na magonjwa mbali mbali basi atapewa dawa za kudhibiti magonjwa hayo, kama shida imetokana na kujisaidia choo kigumu basi mgonjwa atapewa dawa za kulainisha choo N.K



✓ Lakini kwa ujumla wake baadhi ya matibabu huhusisha matumizi ya;


 Zinc oxide ambazo ni Cream kwa ajili ya kupaka eneo la tatizo, Nitroglycerin, botox N.K


Lakini kama tatizo litakuwa kubwa zaidi basi njia salama kuliko zote ni Upasuaji.


MADHARA YA TATIZO HILI LA MPASUKO WA MFEREJI WA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kupatwa na maumivu makali wakati wa kujisaidia


- Mgonjwa kukosa amani  na furaha kabsa wakati akihisi haja kubwa


- Mgonjwa kupata maumivu makali wakati akishiriki tendo la ndoa


- Kutokwa na damu kwenye kinyesi


- Mgonjwa kuchafua Nguo ya ndani kwa damu au matone ya damu


- Mgonjwa kupata shida wakati wa kutembea




KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

MADHARA YA MATUMIZI YA ASALI KWA MTOTO MDOGOAfyaclass Bongo Social •


ASALI KWA MTOTO 

• • • • •

MADHARA YA MATUMIZI YA ASALI KWA MTOTO MDOGO


Watu wengi hawafahamu kwamba mtoto mdogo hatakiwi kupewa asali kabsa, kuna madhara ambayo huweza kumpata mtoto mdogo kama akiwa anapewa asali mara kwa mara.


ATHARI YA ASALI KWA MTOTO MDOGO


Kwa watoto ambao wana umri wa chini ya Mwaka Mmoja, huweza kupata madhara wakitumia asali mara kwa mara kutokana na uwepo wa bacteria aina ya Clostridium botulinum kwenye asali.


Clostridium botulinum ni bacteria ambao huweza kuwepo ndani ya asali, endapo mtoto mdogo atapewa asali bacteria hawa huweza kupenya moja kwa moja na kuzalisha sumu kali ambayo hufyonzwa katika utumbo wa mtoto na kusababisha tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama Infant Botulism.


Tatizo hili la Infant botulism huambatana na dalili mbali mbali.


• Dalili ya kwanza kabsa ni mtoto kupata choo kigumu,kupata shida wakati wa kujisaidia au kukosa kabsa choo.


•Mwili wa mtoto kukosa nguvu kabsa na kuwa dhaifu


• Mtoto kupoteza kabsa hamu ya kunyonya au kula kitu chochote


• Mtoto akilia sauti hutoka kidgo sana au hulia kama mtu ambaye amechoka sana na hana nguvu kabsa


• Uwepo wa mtoto kucheza, au movement kwa ujumla hupungua sana


• Mtoto kukosa kabsa nguvu ya kunyonya maziwa ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Poor sucking


• Ngozi ya mtoto kuanza kuwa  kavu sana na kubadilika rangi


• Uwezo wa mtoto kutoa mkojo kupungua kwa kiasi kikubwa au kupatwa na tatizo la urinary retention

 
• Uwezo wa umeng'enyaji wa chakula cha mtoto tumboni kupungua kwa kiasi kikubwa


• Mapigo ya moyo kwa mtoto kuanza kubadilika



Hayo ndyo baadhi ya madhara ya matumizi ya asili kwa mtoto mdogo, hivo basi ni wito wangu kwa wazazi au walezi wa watoto kuacha kabsa tabia ya kuwapa watoto wadogo asali kwani ni hatari sana kwa afya zao.



Mbali na madhara ambayo nimekwisha yataja hapo juu katika makala hii, Mtoto pia huweza kupoteza maisha kabsa kutokana na madhara ya sumu kali ambayo huzalishwa na bacteria hawa aina ya Clostridium botulinum.

.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

ORODHA YA MAGONJWA YANAYOWASUMBUA SANA WATU KWA HIVI SASAAfyaclass Bongo Social •

 MAGONJWA

• • • • • •

ORODHA YA MAGONJWA YANAYOWASUMBUA SANA WATU KWA HIVI SASA


Japo orodha hii haikuzingatia idadi ya watu wanaougua au hatari ya ugonjwa,hivo hizi ni namba tu haimaanishi kwamba namba moja basi ndyo ugonjwa hatari hapana, dhumuni la makala hii ni kukuonyesha tu baadhi ya magonjwa ambayo huwapata sana watu kwa hivi sasa.


1. Ugonjwa wa Kisukari


2. Ugonjwa wa Presha au shinikizo la Damu


3. Tatizo la Vidonda vya tumbo


4. Ugonjwa wa saratani au kansa mbali mbali kama vile;

  • Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake
  • Saratani ya matiti
  • Saratani ya damu
  • Saratani ya utumbo mkumbwa
  • Saratani ya koo
  • Saratani ya mifupa
  • Saratani ya ini
  • Saratani ya Ngozi
  • Saratani ya tumbo
  • Saratani ya tezi dume
  • Saratani ya mapafu
  • N.K


5. Tatizo la Bawasiri


6. Magonjwa ya Moyo ikiwemo yale yanayohusisha moyo kuwa mkubwa pamoja na mishipa ya damu kuziba


7. Magonjwa ya zinaa ikiwemo Kisonono,kaswende pamoja na ugonjwa wa UKIMWI


8. Magonjwa yanayohusisha mfumo wa hewa na upumuaji kama Pneumonia,Korona N.K


9. Ugonjwa wa asthma au Pumu


10. Tatizo la kuwa na uvimbe katika sehemu mbali mbali za mwili,ikiwemo pamoja na uvimbe wa Kizazi pamoja na mirija ya uzazi kuziba kwa wanawake


11. Ugonjwa wa Fangasi za aina mbali mbali kama vile; Fangasi wa sehemu za siri,Fangasi wa kwenye ngozi,Fangasi wa miguuni, Fangasi wa kwenye Damu N.K


12. Ugonjwa wa UTI, ambapo kirefu chake ni Urinary track infection na maana yake ni maambukizi yanayotokea katika mfumo wa Mkojo ikiwemo katika njia ya mkojo,kibofu cha Mkojo,Figo N.K


13. Ugonjwa wa PID Kwa wanawake, ambapo kirefu chake ni pelvic inflammatory disease na maana yake ni maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke


14. Tatizo la Mvurugiko wa vichocheo vya mwili ambapo kwa kitaalam hujulikana kama hormone imbalance


15. Magonjwa yote yanayohusu mtu kuishiwa na damu ikiwemo lile la sickle cell


16. Magonjwa ya Figo


17. Tatizo au ugonjwa wa Homa ya Ini


18. Ugonjwa wa presha ya macho ambao  kwa kitaalam hujulikana kama Glaucoma


19. Ugonjwa wa Gauti


20. Matatizo ya hedhi kwa Wanawake


21. Ugonjwa wa Tezi Dume


22. Ugonjwa Kiharusi au kwa kitaalam hujulikana kama STROKE


23. Ugonjwa wa kifua kikuu maarufu kama TB


24. Tatizo la mwanaume kuwa na mbegu za kiume chache ambapo kwa kitaalam hujulikana kama low sperm count


25. Ugonjwa wa Malaria


26. Tatizo la homa ya Uti wa Mgongo


27. Tatizo la utapiamlo kwa baadhi ya watoto


28. Ugonjwa wa kifafa hasa kifafa kinachotokea wakati wa ujauzito au kifafa cha mimba


29. Matatizo au magonjwa ya akili pamoja na kuchanganyikiwa


30. Magonjwa yote yanayohusisha miguu ambapo kwa asilimia kubwa huwapata wazee



N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO KWA MAMA MJAMZITOAfyaclass Bongo Social •

 MSONGO WA MAWAZO

• • • • •

MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO KWA MAMA MJAMZITO


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia hali ya Msongo wa Mawazo kwa mama Mjamzito, na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;


- Mama mjamzito kupigwa au kujeruhiwa katika ajali mbali mbali


- Ujauzito wake kukataliwa na mtu aliyempa huo ujauzito


- Au changamoto mbali mbali katika maisha yake ya mahusiano


- Mama mjamzito kufukuzwa kazi


- Mama mjamzito kutengana na mume wake


- Mama mjamzito kufiwa na mtu wake wa karibu kama baba,mama,mume N.K


- Pia changamoto mbali mbali za kiuchumi kama vile kukosa pesa kabsa za matunzo, Kukosa pesa kwa ajili ya chakula N.K


MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO KWA MAMA MJAMZITO


Tafiti mbali mbali za wataalam wa afya zinasema kwamba,Msongo wa Mawazo ambao mama mjamzito huwa nao, huweza kusababisha athari mbali mbali zikiwemo zile zinazotokea wakati wa uumbaji wa mtoto, na wakati mwingine hata watoto kuzaliwa na ulemavu flani katika mwili.


Athari za mama mjamzito kuwa na msongo wa mawazo au kwa kitaalam tunaita Severe depression, huweza kutokea kabla,wakati na baada ya mtoto kuzaliwa.


• Ujauzito huweza kutoka wenyewe kama mama mjamzito akiwa na hali ya msongo wa mawazo kupita kiasi.


• Mama huweza kujifungua mtoto mwenye ulemavu flani kama vile tatizo la Midomo Sungura ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Cleft lip and cleft palate au kuzaa mtoto mwenye shida ya Mgongo wazi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama spinal bifida.


• Kama Msongo wa mawazo utaendelea hata baada ya mama kujifungua, huweza kupelekea madhara makubwa zaidi hata kufikia hatua ya kutoa uhai wa mtoto aliyezaliwa au mama kujiua mwenyewe.


DALILI ZA MAMA MJAMZITO MWENYE MSONGO WA MAWAZO NI PAMOJA NA;


- Mama mjamzito kufanya kazi moja kwa masaa mengi,Mfano; Mama mjamzito huweza kufagia eneo dogo tu lakini kwa masaa mengi anafanya kazi hyo hyo moja tu


- Mama mjamzito kuanza kuongea mwenyewe mara kwa mara,hyo ni dalili pia ya msongo wa mawazo


- Mama mjamzito kuanza kuongelea mambo yanayohusu kujiua mwenyewe au kuua mtoto aliyetumboni au atakayezaliwa


- Mama mjamzito kuanza kuomba msamaha kila mara kwa watu,hata kama kitu alichokifanya sio kosa kabsa katika hali ya kawaida


- Mama mjamzito kukosa usingizi kabsa na wakati mwingine akilala anaweweseka sana usku


KUMBUKA; Ukiona mtu unayekaa naye ana dalili kama hizi msaidie mapema kwa kumpeleka kwa wataalam wa afya ili kuepusha madhara makubwa ambayo huwe za kutokea hapo baadae.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

TATIZO LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI KWA MWEZIAfyaclass Bongo Social •

HEDHI

• • • • • •

TATIZO LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI KWA MWEZI


Moja ya vitu ambavyo mwanamke hutakiwa kuvizingatia sana ni kuhusu mzunguko wake wa hedhi, Mzunguko wa hedhi huweza kumpa mwanamke kila aina ya ishara hata pale akiwa ni mgonjwa,kupitia mzunguko wa hedhi mwanamke anaweza kujua ana tatizo flani.


Mizunguko ya hedhi ipo tofauti kwa wanawake mbali mbali, Lakini kuna migawanyiko mikuu mitatu kwa kuangalia mda wa mzunguko wa hedhi yaani; 


(i) Kuna mzunguko wa hedhi mfupi mfano; siku 21


(ii) Kuna Mzunguko wa hedhi wa wastani au kawaida wa siku 28


(iii) Na kuna Mzunguko wa hedhi mrefu mfano; siku 35


Lakini kuna mizunguko ya aina mbili kwa kuangalia mabadiliko ya mzunguko wa hedhi yaani; 


(i) Kuna mzunguko usio badilika badilika au kwa kitaalam hujulikana kama REGULAR MENSTRUAL CYLCE


(ii) Na kuna mzunguko unaobadilika badilika yaani kwa kitaalam hujulikana kama IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE


SABABU ZA MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI AU ZAIDI NDANI YA MWEZI MMOJA NI PAMOJA NA;


1. Kuwa na tatizo la Mvurugiko wa vichocheo mwilini ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hormone imbalance.


2. Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango ambazo zina vichocheo kama progestrone na estrogen Mfano,Sindano,au vipandikizi(Vijiti).


3. Mwanamke kubadilisha mazingira au hali ya hewa,Mfano; kutoka sehemu moja ambayo amekaa kwa mda mrefu na kwenda sehemu nyingine ambayo hajawahi kukaa kabsa.


4. Mwanamke Kuwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi


5. Mwanamke kufanya kazi ngumu kupita kiasi


6. Pia mwanamke akifanya sana mazoezi ya mwili kupita kiasi huweza kupatwa na tatizo hili


Kuna baadhi ya wanawake hupata period mara mbili au zaidi kwa mwezi ambayo huambatana na maumivu makali sana ya tumbo hadi wengine kufikia hatua ya kulazwa kabsa hosptal.



KUMBUKA; Ukiona shida hii ni vizuri kukutana na wataalam wa afya ili kujua chanzo cha tatizo lako kwani hata magonjwa hatari kama uvimbe kwenye kizazi huweza kuwa na dalili kama hizi pia,hivo usipuuzie tatizo hili.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

MATITI YA MWANAMKE KUKOSA UWIANOAfyaclass Bongo Social •

 MATITI

• • • • •

MATITI YA MWANAMKE KUKOSA UWIANO


Wakina mama wengi ambao hunyonyesha hupatwa sana na hali hii ya matiti kutofautiana ukubwa au size. Hali hii sio tatizo kwa mama anayenyonyesha kwani ni kiashiria kwamba mtoto anapenda kunyonya titi flani zaidi ya lingine.


Huna haja ya kuwa na wasi wasi ila cha msingi ni mtoto anyonye na kushiba vizuri maziwa ya mama yake. Lakini endapo hali hii unaiyona ni kero kwako, basi wakati unamnyonyesha mtoto,anza na titi dogo  na hakikisha unalitumia mara mbili zaidi ya lile kubwa.


VIPO VIASHIRIA VYA HATARI KATIKA TITI LAKO AMBAVYO NI PAMOJA NA;


1. Titi moja kuwa kubwa kuliko lingine wakati wewe hunyonyeshi


2. Chuchu ya titi lako kutoa usaha au Damu,hii sio ishara nzuri,ni mojawapo ya dalili za magonjwa kama saratani ya matiti N.K


3. Kuwa na vitu ndani ya titi ambavyo ukivishika vipo mithili ya punje ya mchele au harage


4. Kuwepo kwa ugumu ndani ya titi au maeneo ya kwapani


5. Kuwa na tatizo la michubuko pamoja na vidonda kwenye titi lako


6. Kupata maumivu ya titi yanayoendana sambamba na joto la mwili kupanda au kuwa na homa.


KUMBUKA,moja ya saratani ambazo huwasumbua wanawake wengi ni pamoja na saratani ya matiti,hivo jenga tabia ya kujichunguza mwenyewe mara kwa mara, na kugundua mabadiliko yoyote yanayoweza kutokea ndani ya titi lako kwa jumla wake.


Mbali na tatizo la Saratani ya matiti,pia titi huweza kukumbwa na tatizo la kuvimba kwa tezi ndani ya titi pamoja na titi kushambuliwa na magonjwa mengine.


Kumbuka haya kwa mama anayenyonyesha;


- Fanya usafi wa mikono yako kabla ya kumshika mtoto


- Hakikisha umeosha au kusafisha titi lako kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto


- Unyonyeshaji hutakiwa kwa kipindi cha miezi sita bila mtoto kuchanganyiwa maziwa ya mama na vyakula vingine


- Baada ya kipindi cha miezi sita ya maziwa ya mama pekee,anza kumchanganyia mtoto maziwa ya mama na vyakula vingine ila usiache kumnyonyesha mpaka afikishe umri wa miaka miwili au mitatu ukiweza.


NB; Maziwa ya mama ni kinga tosha kwa mtoto hasa hasa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni,ambapo kinga ya mtoto dhidi ya magonjwa ipo chini sana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA Afyaclass Bongo Social •

 SURUALI ZA KUBANA

• • • • • •

MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA 


Watu wengi wamekuwa wakivaa suruali za kubana sana hasa hasa wakina dada,bila kujua pia uvaaji wa suruali za kubana sana una madhara kiafya.


Swala la kuvaa suruali za kubana sana mapaja kwa wadada au wanawake imekuwa fashion kwa watu wengi, na huku baadhi yao wakifikia hatua ya kutokuwa na Nguo nyingine zaidi ya suruali tu.


YAPI NI MADHARA YA KUVAA SURUALI ZA KUBANA SANA?


- Wataalam wa afya wanasema uvaaji wa suruali za kubana sana mapaja ya mtumiaji kwa muda mrefu husababisha tatizo la kukandamiza mshipa wa fahamu ambao hupita eneo la mapajani ambao kwa kitaalam hujulikana kama Lateral femoral cutaneous nerve.


Madhara ya Mgandamizo huu wa mshipa wa fahamu unaopita kwenye eneo la paja la Mtu ni kupata ganzi pamoja na kupata tatizo la kuhisi kuchomwa chomwa kwenye eneo la paja  ambapo tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Tingling thigh syndrome au Meralgia paresthetica.



USHAURI


• Wataalam wa afya wanapendekeza mtu kuvaa nguo ambazo haziubani sana mwili wake ikiwa ni pamoja na kuacha kabsa tabia ya kuvaa suruali za kubana sana mapaja pamoja na kuvaa viatu virefu sana kwa Muda mrefu.


Kwa kudokeza tu kwa ufupi Madhara ya Uvaaji wa Viatu virefu ni pamoja na;


- kupata maumivu makali ya kiuno na mgongo


- kupata maumivu ya miguu kwenye joint


- kudondoka


- Kupata tatizo la misuli ya mwili kukaza


N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

DAWA YA FANGASI UKENIAfyaclass Bongo Social •

 FANGASI UKENI

• • • • •

DAWA YA FANGASI UKENI


Zipo dawa nyingi ambazo hutumika katika matibabu ya Fangasi ukeni,huku zingine zikiwa za asili na zingine za hospital. Lakini kwa upande wangu nitaelezea baadhi ya dawa za hospital zinazotumika kutibu tatizo la Fangasi ukeni.


NB; Fangasi jamii ya Candida albicans ndiyo hushambulia sana sehemu za siri za mwanamke.


DALILI ZA FANGASI UKENI NI PAMOJA NA;


1. Mwanamke kupata miwasho sehemu za siri ikiwa ni pamoja na eneo la ngozi kati ya njia ya haja kubwa na sehemu za siri


2. Mwanamke kutokwa na uchafu wenye rangi kama maziwa,ambao huambatana na harufu mbaya ukeni


3. Sehemu za siri kuwa na michubuko pamoja na vidonda kwenye mashavu na ngozi ya ukeni


4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu


5. Kupata maumivu wakati wa tendo la Ndoa


MADHARA YA FANGASI WA UKENI NI PAMOJA NA;


- Mwanamke kunuka au kutoa sehemu zake za siri


- Mwanamke kutokwa na uchafu mithili ya maziwa Mgando


- Mwanamke kuwa mkavu na Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa


- Sehemu za siri za mwanamke kuwa na michubuko pamoja na vidonda


- Kukosa raha ya tendo la Ndoa


- Kukerwa na miwasho sehemu za siri hata ukiwa mbele za watu


- Fangasi sugu huweza kukusababishia hata tatizo la kutokushika mimba



DAWA YA FANGASI UKENI


• Baadhi ya Dawa ambazo hutumika hospitalini kutibu fangasi wa ukeni ni Pamoja na Clotrimazole ambapo kuna Cream ya kupaka sehemu za siri pamoja na ile ya vidonge vya kudumbukiza ukeni,ambapo vinaweza kuwa vitatu au sita, Na mwanamke hudumbukiza kimoja kimoja kila akilala mpaka amalize dose.


Tazama kwenye picha hapa chini kuona mfano wa Clotrimazole Cream ya kupaka


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

DALILI ZA UGONJWA WA UTI(MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA N.K) NAAfyaclass Bongo Social •

 UTI

• • • • •

DALILI ZA UGONJWA WA UTI(MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA N.K)


Ugonjwa wa Uti huonyesha dalili mbali mbali kulingana na Jinsia ya Mtu(mwanamke au mwanaume),pamoja na kulingana na hali ya mtu Mfano; Mama Mjamzito N.K.


DALILI KUBWA ZA UGONJWA WA UTI NI PAMOJA NA;


1. Kupata maumivu wakati wa kukojoa


2. Kuhisi hali ya Mkojo kuchoma wakati wa kukojoa


3. Kuhisi hali ya Kukojoa mara kwa mara


4. Kupata maumivu makali ya tumbo hasa hasa upande wa kushoto au chini ya kitovu


5. Kutoa mkojo ambao umebadilika rangi


6. Kuhisi hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika


7. Kupata maumivu ya viungo,joint pamoja na misuli ya mwili


8. Kuhisi uchovu wa mwili usio wa kawaida


9. Joto la mwili kupanda au kuwa na homa


10. Kutoa mkojo wenye harufu kali na wakati mwingine kutoa mkojo uliochanganyika na Damu


11. Mgonjwa kukosa hamu ya kula


12. Kupata maumivu makali ya kichwa


13. Kupatwa na maumivu makali ya kiuno pamoja na Mgongo


14. Kwa mwanaume,maambukizi ya UTI huweza kupelekea kuwa na hali ya ukavu ukeni pamoja na maumivu wakati wa tendo la ndoa


WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA UTI


- Wanawake zaidi ya Wanaume


- Wajawazito


- Wanaoshare vyoo na watu wengi Mfano maeneo yote yenye public toilets kama Stend,Sokoni, Gesti N.K


- Walevi


MATIBABU YA UGONJWA WA UTI


Zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kutibu tatizo la UTI zikiwemo za hosptal na zingine za asili. Miongoni mwa dawa za hosptal zinazotumika kutibu ugonjwa wa Uti ni pamoja na Ciproflaxin, Azuma(azthromycin), Amoxicilin N.K


Kumbuka mama mjamzito hatakiwi kutumia dawa kali kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa UTI,ili kuepusha madhara ambayo huweza kutokea kwake na kwa mtoto aliyetumboni,Ndyo maana mara nyingi mama mjamzito akiwa na tatizo la UTI hupewa Amoxicilin.


MADHARA YA UGONJWA WA UTI NI PAMOJA NA;


- Maumivu makali ya tumbo


- Maumivu wakati wa tendo la ndoa


- Kukojoa damu


- Ukavu wa sehemu za siri za mwanamke


- Matatizo ya Figo


N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







0 Comment

TATIZO LA DEGEDEGE,MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKEAfyaclass Bongo Social •

 DEGEDEGE

• • • • • •

TATIZO LA DEGEDEGE,MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE


Hili ni tatizo ambalo linahusisha hali ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kutingishwa au kutetemeshwa, tatizo hili huleta hali ya kukakamaa kwa misuli ya mwili wa binadamu.


Tatizo la degedege huweza kumpata mtu wa umri wowote ule,japo kuna makundi ya watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Dege dege.


MAKUNDI AMBAYO YAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;


-  Watoto wadogo


- Mama wajawazito


- Wenye magonjwa yanayosababisha mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye Damu


- Wenye matatizo la kuishiwa na pumzi,kushindwa kupumua na kukosa hewa ya Oxygen


- Ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wanaopata tatizo hili


- Mwanamke ambaye aliwahi kupata tatizo la degedege kwenye ujauzito uliopita


- Mtu ambaye alishawah kupata tatizo la degedege angalau mara moja kwenye maisha yake


- Vijana


CHANZO CHA TATIZO LA DEGEDEGE


Tatizo la degedege kwa asilimia kubwa husababishwa na ubongo wa mtu kushambuliwa na baadhi ya magonjwa au kuwa na tatizo la kushindwa kufanya kazi vizuri ambapo hupelekea upungufu wa vichocheo vya Sukari kwenye damu yaani kwa kitaalam Hypoglycemia pamoja na kuwa na upungufu wa hewa ya oxygen kwenye Damu yaani kwa kitaalam hypoxia. 


Hata hivo tatizo la dege dege huweza kuhusishwa na magonjwa yanayoshambulia Uti wa Mgongo kama Vile homa ya Uti wa mgongo  pamoja na Magonjwa mengine kama MALARIA.


DALILI ZA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;


• Misuli ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kukakamaa


• Hali ya kupinda shingo na kurudisha kichwa nyuma


• Hali la mwili kutetemeka au kutingishwa


• Hali ya kutoa mapovu Mdomoni


• Kupata shida ya upumuaji


• Kupatwa na shida ya macho kugeukia kwa nyuma na kuonekana weupe wa jicho tu huku weusi wa jicho ukipotea


• Kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo pamoja na haja kubwa


• Kuwa na shida ya kupoteza kumbukumbu


• Mgonjwa kupoteza Fahamu kabsa



MATIBABU YA TATIZO LA DEGEDEGE


Matibabu ya tatizo la degedege hutegemea chanzo cha tatizo hili, Mfano; endapo tatizo la degedege limesababishwa na magonjwa ya Uti wa mgongo kama homa ya uti wa mgongo au magonjwa mengine kama Malaria,vivyo hivyo matibabu yatakuwa ni ya kutibu Malaria pamoja na homa ya Uti wa mgongo.


Endapo Mgonjwa ana dalili zozote za Degedege ni vizuri kuwahishwa hospital haraka kwa ajili ya vipimo na kuanza matibabu kamili.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

JE KUTOA JASHO LENYE RANGI HUASHIRIA UWEPO WA TATIZO GANI?Afyaclass Bongo Social •

 JASHO LA RANGI

• • • • •

JE KUTOA JASHO LENYE RANGI HUASHIRIA UWEPO WA TATIZO GANI?



Katika hali ya kawaida, kwa binadamu mwenye afya bora hutakiwa kutoa jasho ambalo halina rangi yoyote au wengine hupenda kusema nyeupe,japo rangi ya jasho la kawaida sio nyeupe bali tunasema jasho halina rangi yoyote.


Kwa tafsiri nyingine tunaweza kusema kwa hali ya kawaida jasho la mtu linatakiwa kufanana kama maji yalivyo,endapo Litakuwa na rangi ya tofauti na maji yalivyo linaashiria kuna shida kiafya.


Uwepo wa tatizo la Chromhidrosis humfanya mtu kutoa jasho lenye rangi mbali mbali maeneo ya kwapani na Usoni.


NB; Mtu mwenye tatizo hili la Chromhidrosis huweza kutoa jasho lenye rangi mbali mbali kama vile;

 

 ✓ Jasho lenye rangi nyekundu


 ✓ Jasho lenye rangi ya Njano


 ✓ Jasho lenye rangi ya kijani


  ✓ Jasho lenye rangi ya blue


  ✓ Jasho lenye rangi nyeusi



Ni mara chache sana tatizo hili kutokea kwa watu, hata wewe msomaji hapa unaweza kushangaa kama kuna tatizo kama hili la mtu kutoa jasho lenye rangi, ila ukweli ni kwamba tatizo hili lipo.


CHANZO CHA MTU KUTOA JASHO LENYE RANGI  AU CHANZO CHA TATIZO LA CHROMHIDROSIS


- Tatizo hili la kutoa jasho lenye rangi mbali mbali kwenye makwapa au uso wa mtu hutokana na uzalishaji wa kiwango kikubwa cha Pigment zinazojulikana kama Lipofuscin kwenye tezi la Jasho, ambazo ndyo huleta rangi kwenye jasho. Endapo tezi la jasho litazalisha pigment za Lipofuscin kwa wingi sana jasho la mtu litatoka likiwa na Rangi.


Kumbuka jasho hili hutoka wakati Mtu akifanya kazi Ngumu, akitembea sana, jua kali N.K kama ilivyo visababishi vya jasho la kawaida,tofauti yake ni rangi tu.


JE WEWE USHAWAHI KUONA MTU ANATOA JASHO LA RANGI?


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

TATIZO LA KIUNGULIA KWA MAMA MJAMZITOAfyaclass Bongo Social •

 KIUNGULIA KWA MAMA MJAMZITO

• • • • •

TATIZO LA KIUNGULIA KWA MAMA MJAMZITO


Moja ya tatizo ambalo humsumbua sana Mama mjamzito ni pamoja na kuwa na hali ya kiungulia cha mara kwa mara, hali hii humnyima au kumkosesha raha kabsa mama mjamzito.


CHANZO CHA TATIZO LA KIUNGULIA KWA MAMA MJAMZITO


- Sababu kubwa ya mama mjamzito kupatwa na Kiungulia ni kutokana na mabadiliko ya vichocheo vya mwili ambayo hutokea kipindi cha Ujauzito, na mabadiliko hayo huhusisha vichocheo mbali mbali kama Progesterone, Estrogen na Relaxin.


i). Hali hii ya mabadiliko ya vichocheo vya Progesterone  huhusisha uzalishaji wa kiwango kikubwa cha Progestrone,ambapo matokeo yake husababisha utembeaji wa chakula pamoja na kufyonzwa kwake kwenda taratibu sana.


ii). Uzalishaji wa kiwango kikubwa cha kichocheo aina ya Relaxin husababisha kulegea kwa misuli ya njia ya chakula, kutanuka kwa Njia ya chakula, pamoja na ring inayofungua na kufunga wakati chakula kinaingia tumboni kulegea, hivo kupelekea chakula kilichopo tumboni kurudi na kupanda juu, hapa ndipo mama mjamzito hupata kiungulia kikali kwani chakula pamoja na acid iliyopo tumboni hurudi na kupanda juu. 


MJAMZITO FANYA HAYA ILI KUPUNGUZA HALI YA KIUNGULIA


• Epuka tabia ya kula vyakula vingi kwa wakati mmoja


• Jitahidi kunywa maji mengi kwa siku nzima


• Epuka kula vyakula vyenye mafuta sana


• Epuka kula vyakula vyenye mchanganyiko wa viungo vingi


• Punguza ulaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha acid


• Jitahidi kuweka kitu kama mto wakati wa kulala na kuepuka kulala chini kabsa ili kupunguza uwezakano wa acid iliyopo tumboni kurudi na kupanda juu


• Epuka matumizi ya Sigara na Pombe kipindi cha Ujauzito, kwani mbali na madhara mengine ambayo huweza kumpata mtoto na mama,Pombe na sigara huweza kuchangia hali ya kiungulia


• Hakikisha huwi na tatizo la Uzito uliopita kiasi,hivo jitahidi kuweka sawa uzito wako wa mwili


• Epuka kuwa na Msongo wa mawazo au Stress nyingi wakati wa Ujauzito


• Epuka tabia ya kulala hapo hapo mara tu baada ya kula chakula


• Epuka kuvaa nguo zinazobana tumbo lako pamoja na kiuno chako


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

UKURUTU KWENYE MWILI,NGOZI,AU KWENYE KORODANI NA UKENIAfyaclass Bongo Social •

 UKURUTU

• • • • •

UKURUTU KWENYE MWILI,NGOZI,AU KWENYE KORODANI NA UKENI


Tatizo hili la Ukurutu huweza kuwapata watu wa Jinsia zote(mwanaume&mwanamke) lakini pia na watu wa umri wowote ikiwemo watoto wadogo,vijana na hata wazee.


Ukurutu huu huweza kutokea maeneo mbali mbali katika mwili wa binadamu kama vile; ukurutu kwenye Ngozi ya mwili mzima au maeneo mbali mbali kama vile kwenye mikono,miguu,makalioni,mgongoni,shingoni,kwenye ngozi ya korodani za mwanaume, eneo la katikati ya sehemu ya haja kubwa ma sehemu za siri,au maeneo ya kwenye ngozi ya uke kwa wanawake.


CHANZO CHA TATIZO LA UKURUTU NI NINI?


Wataalam wa afya wanasema hakuna sababu ya moja kwa moja ya mtu kupatwa na tatizo hili la Ukurutu ila Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuwa na shida hii ya ukurutu mwilini, na sababu hizo ni kama;


- Kuwa na allegery ya baadhi ya vitu, kama vile baadhi ya vyakula,Nyama, Sabuni,madawa au baadhi ya vitu vyenye kemikali ambazo una allergy nazo.


- Mabadiliko ya vichocheo mwilini, hii huhusishwa zaidi katika kipindi cha ujauzito ambapo baadhi ya wanawake wajawazito hupatwa na tatizo hili la ukurutu wa Ngozi na miwasho mwilini pindi wakiwa wajawazito.


- Mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Virusi au Bacteria aina ya Staphlococcus aureus.


- Kusumbuliwa na tatizo la Fangasi, Wapo fangasi wanaoshambulia kwenye Ngozi na pia wapo fangasi wa kwenye Damu, Jamii hii ya fangasi wa kwenye Ngozi na kwenye Damu huweza kusababisha tatizo la Ukurutu na miwasho kwenye Ngozi.


- Mabadiliko ya hali ya hewa katika mazingira,Hapa tunazungumzia hali ya joto na jua kali pamoja na hali ya baridi kali,watafiti wanasema kuna baadhi ya watu hupatwa na hali ya ukurutu kwenye ngozi kipindi cha joto na jua kali,huku wengine wakipatwa na ukurutu kwenye ngozi kipindi cha baridi kali.


- Matumizi ya baadhi ya dawa au vipodozi vya Ngozi huweza kuleta reaction kwenye Ngozi na kusababisha tatizo hili la Ukurutu.


DALILI ZA TATIZO LA UKURUTU MWILINI


1. Kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili huanza kupatwa na upele kwenye Ngozi ya kichwani pamoja na mashavuni,huku upele huo ukiambatana na miwasho.


2. Kwa watoto wenye umri wa Zaidi ya miaka miwili hadi umri wa kubalehe,huanza kupata upele maeneo mbali mbali ya mwili kama vile kwenye miguu, magotini, shingoni au kwenye viganga vya mikomo.


3. Kwa watu wazima huanza kupata upele kwenye maeneo yote ya mikunjo,kama mikunjo ya magotini,viwiko vya mikono, maeneo ya ngozi ya shingoni N.K


4. Ngozi ya mwili kutoa vitu vyeupe mithili ya unga unaopukutika.


5. Kupatwa na miwasho kwenye Ngozi ya mwili hasa hasa maeneo yote ambayo yana upele upele.


NJIA MBALI MBALI ZA KUTIBU TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Hakikisha unapaka mafuta vizuri Ngozi yako ya mwili ikiwemo maeneo yote yenye ukurutu


✓ Hakikisha hutumii vitu vyote ambavyo unaona vinakuletea hiyo allergy,kama chakula,sabuni,dawa,vipodozi vya ngozi N.K


✓ Epuka kuvaa Nguo za jamii ya mpira


✓ Hakikisha unapata matibabu sahihi ya Fangasi Kama una tatizo lolote la Fangasi Mfano; Fangasi wa kwenye Ngozi,Fangasi wa kwenye Damu N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

TATIZO LA KUPATWA NA KIZUNGUZUNGU,CHANZO CHAKE NA MATIBABU YAKEAfyaclass Bongo Social •

 KIZUNGUZUNGU

• • • • •

TATIZO LA KUPATWA NA KIZUNGUZUNGU,CHANZO CHAKE NA MATIBABU YAKE


Tatizo hili linawapata watu wengi, na wengine hata kufikia hatua ya kupata madhara mbali mbali kama kuanguka au kudondokea sehemu za hatari zaidi kama kwenye moto,Barabarani, N.K, hata kufikia hatua ya watu kupoteza kabsa maisha.


ZIPO SABABU MBALI MBALI ZA MTU KUPATWA NA HALI YA KIZUNGUZUNGU


Na miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;


1. Kuwa na tatizo la Shinikizo la Damu au kuwa na Ugonjwa wa Presha


2. Kuwa na tatizo la Magonjwa mbali mbali ya moyo,ikiwemo pamoja na tatizo la mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba,moyo kuwa mkubwa N.K


3. Kuwa na matatizo ya Ugonjwa wa kisukari


4. Kuumwa Ugonjwa wa Malaria huweza pia kukusababishia hali ya kizunguzungu kikali


5. Kuwa na shida au matatizo mbali mbali yanayohusu masikio huweza kusababisha hali ya kizunguzungu kwa mhusika. Sehemu ya ndani kabsa ya sikio ina viungo ambavyo huhusika na kuleta hali ya usawa au BALANCE katika mwili,endapo pakitokea shida ndipo mtu hushindwa kubalance mwili wake na kuona hali ya kizunzungu.


6. Kuwa na shida ya Ongezeko la damu Kupita kiasi mwilini huweza kusababisha kizunguzungu kikali


7. Pia ifahamike kwamba matumizi ya baadhi ya dawa huweza kumsababishia mhusika kizunguzungu kikali


8. Kutokuwa na Mzunguko mzuri wa Damu katika mwili


9. Lakini pia damu kupungua sana mwilini huweza kusababisha hali ya kupepesuka na kizunguzungu kikali kwa mtu,wengine hata kuishiwa kabsa na nguvu na kudondoka chini


10. Pia endapo mtu kapata ajali ambayo imehusisha kugongwa Kichwa,au kuvuja Damu sana huweza kupata kizunguzungu kikali na hata kudondoka chini


MATIBABU AU VITU VYA KUFANYA KWA MTU MWENYE SHIDA YA KIZUNGUZUNGU.


- Kwanza kabsa matibabu ya Shida hii ya kizunguzungu yataanzia pale ambapo tumegundua chanzo chake ni nini. Lakini mgonjwa akifika hospital atafanyiwa vipimo mbali mbali kulingana na historia ya tatizo lake kama vile; vipimo vya wingi wa damu,Kipimo cha Presha, kipimo cha Sukari,Magonjwa ya moyo, kipimo cha Malaria N.K


Na ndipo chanzo cha tatizo huanza kutibiwa hapo hapo baada ya vipimo.


MADHARA YA KIZUNGUZUNGU NI PAMOJA NA;


• Kudondoka au kuanduka Chini


• Kuumia au kupata majeraha baada ya kudondoka


• Kupoteza Maisha



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

FAHAMU KUHUSU MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWAAfyaclass Bongo Social •

UCHUNGUZI KWA MTOTO

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWA


Kwa kawaida mtoto anapozaliwa tu anatakiwa kulia, kama asipolia wataalam wa afya wanasema Kuna tatizo, Lakini baada ya mtoto kuzaliwa hata kama amelia,uchunguzi wa kina hufanyika kwa kitaalam tunasema Newborn Examination.


Vitu vingi sana hufanyiwa uchunguzi ili kuangalia kama kuna tatizo lolote kwa mtoto au mtoto yupo sawa ili asijekupata madhara baada ya kuzaliwa,anavyoendelea kukua na hata anapokuwa mtu mzima.


 MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWA NI PAMOJA NA;


1. Kwanza kabsa kuhakikisha mtoto amelia mara tu baada ya Kuzaliwa,hilo ndyo jambo la kwanza kabsa ambalo hufanyika.


2. Baada ya kitovu cha mtoto kukatwa na kufungwa vizuri,bado uchunguzi wake utaendelea ili kuhakikisha hakuna damu,au kitu chochote cha tofauti kama usaha kinachotoka kwenye kitovu cha mtoto.


Kumbuka; Hairuhusiwi kuweka kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto,zile imani za kuweka vitu kama mavi ya ng'ombe kwenye kitovu cha mtoto,ni kuhatarisha tu afya ya mtoto na kumpelekea kupata magonjwa wala hakuna cha zaidi.


3. Macho ya mtoto huchunguzwa,kama kuna dalili zozote za magonjwa kama macho kutoa usaha,N.K. Ingawaje hata kama hakuna dalili za magonjwa kama kaswende au kisonono,bado mtoto atawekewa dawa ya macho ili kumkinga na magonjwa haya.


4. Pua ya mtoto huchunguzwa,kwamba ina matundu mawili kama watu wengine kwa ajili ya kuvuta na kutoa hewa kwa urahisi zaidi.


5. Masikio ya mtoto huchunguzwa na kuangalia kama yanatoa uchafu wowote mfano; Usaha N.K.


6. Sehemu za siri za mtoto huchunguzwa kwa ukaribu zaidi ikiwemo tundu la kutolea Mkojo kama lipo, na kama lipo je lipo sehemu sahihi au lipo sehemu nyingine?,na kama mtoto ni wa kiume,wataalam wa afya huhakikisha korodani zimeshuka kama kawaida.


Kwani endapo mtoto amezaliwa na korodani zipo kwa ndani na hazijashushwa katika hali yake ya kawaida, huweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto hapo baadae,Mfano uwezo wa kutengeneza mbegu utaathirika na mtoto kushindwa kumpa mwanamke mimba.


Kumbuka; Korodani kuwa nje au kushuka au kuning'inia,hiii imewekwa kabsa sio bahati mbaya, Lengo ni ili korodani ziwe na joto ambalo litasaidia katika kutengeneza mbegu pamoja na afya ya begu,na joto hili huwa tofauti kidogo na joto la mwili mzima,ndyo maana korodani zinashuka na kuning'inia kwa Nje kidogo.


7. Sehemu ya Haja kubwa ya mtoto huchunguzwa na kuhakikisha sehemu hiyo ipo na mtoto anaweza kujisaidia vizuri. 


➡️ KUMBUKA; wapo watoto ambao huzaliwa na sehemu ya haja Kubwa au Sehemu ya haja Ndogo haipo au Imeziba,hivo baada ya tatizo hili kugundulika mtoto hufanyiwa upasuaji mapema na kutibu tatizo hili, Ndyo maana Mama wa mtoto anatakiwa ahakikishe mtoto baada ya kuzaliwa anakojoa vizuri na anajisaidia haja kubwa vizuri.


Kama mtoto anajisaidia kwa shida au hajisaidii kabsa(haja kubwa na haja ndogo) mama wa mtoto hutakiwa kutoa taarifa mapema kwa wataalam wa afya.


8. Joto la mwili la mtoto huendelea kuchunguzwa na kuhakikisha halipandi au mtoto hawi na Homa,Kwani homa ni moja ya dalili za hatari kwa mtoto.


9. Pia kunyonya kwa mtoto huendelea kuchunguzwa,kwani ni lazima mtoto awe ananyonya Vizuri kwa ajili ya afya yake. 


Kumbuka;  Maziwa ya mama sio lishe tu kwa mtoto bali ni Kinga na Tiba pia Kwa mtoto mdogo, Kinga ya mtoto mdogo dhidi ya magonjwa hutegemea pia maziwa ya mama yake.


10. Baada ya uchunguzi wa kina kwa mtoto,hakikisha pia mtoto wako anaanza kupata Chanjo za magonjwa mbali mbali,Kama vile chanjo ya Kumkinga na ugonjwa wa kifua kikuu au  kwa kitaalam hujulikana kama BCG ambazo huanza kutolewa mara tu baada ya mtoto kuzaliwa.


NB; HAKIKISHA UNAHUDHURIA KLINIKI ZOTE ZA MTOTO WAKO,KWA AJILI YA AFYA BORA NA UKUAJI BORA KWAKE.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

MAMBO YAKUFANYA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA FANGASIAfyaclass Bongo Social •

 FANGASI

• • • • •

MAMBO YAKUFANYA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA FANGASI


Watu wengi hawajui kwamba Fangasi huweza kushambulia maeneo mengi sana katika mwili wa binadamu, Wengi wao hujua fangasi wa Miguuni tu. Fangasi huweza kushambulia maeneo mbali mbali katika mwili wa Binadamu kama Ifuatavyo;


✓ Kuna Fangasi wa kwenye Damu


✓ Kuna Fangasi wa miguuni pamoja na vidole vyake


✓ Kuna fangasi wa kwenye Viganja vya mikono pamoja na vidole vyake


✓ Kuna Fangasi wa Sehemu za siri za mwanamke na mwanaume


✓ Kuna Fangasi wa mdomoni


✓ Kuna Fangasi wa kwenye Ulimi


✓ kuna Fangasi wa kwenye koo


N.K


• Soma: Chanzo cha Tatizo la Kwikwi na Tiba yake


MAMBO YAKUFANYA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA FANGASI NI PAMOJA NA;


• Epuka kuvaa Viatu vibichi au vyenye majimaji au Soksi Mbichi,hii itakusaidia kujikinga na Fangasi wa Miguuni.


• Epuka kuvaa Nguo za ndani Mbichi au zenye unyevu unyevu hii itakusaidia kujikinga na Fangasi wa Sehemu za Siri.


• Zingatia usafi wa mwili hasa hasa sehemu za siri, hii itakusaidia sana usipate Fangasi mara kwa mara Mfano; Kwa mama mjamzito ambaye kinga ya mwili imeshuka kwa sababu ya Ujauzito huwa katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa kwa Urahisi kama vile FANGASI wa Ukeni na UTI.


• Epuka kushiriki mapenzi Kwa Njia Ya Mdomo na mtu mwenye tatizo hili la Fangasi, au epuka kubusiana(kissing) hasa hasa na yule ambaye anasumbuliwa na Fangasi wa ulimi na Mdomoni.


• Epuka matumizi ya dawa hovio,kwani dawa zingine huweza kushusha kinga ya mwili na kukupelekea kushambuliwa na Magonjwa kama Fangasi kwa urahisi.


• Epuka matumizi ya dawa au sabuni zenye kemikali ambazo huweza kubadilisha hali ya ndani ya uke,ikiwemo hali ya acid,kuleta ukavu,na kusababisha mwanamke kupata fangasi wa ukeni kwa urahisi.


KUMBUKA; Fangasi huweza kuonyesha dalili tofauti tofauti kulingana na eneo la mashambulizi ya Fangasi hao. 


• Soma: Chanzo cha Tatizo la Kwikwi na Tiba yake


DALILI HIZO ZA TATIZO LA FANGASI NI PAMOJA NA;


- Kupatwa na miwasho sana sehemu za Siri pamoja na maeneo mengine ambapo fangasi wameshambulia kama vile Miguuni na kwenye Vidole


- Ngozi ya sehemu za siri kuzunguka mashavu ya uke,pamoja na ngozi ya korodani kubadilika rangi na kuwa Nyekundu


- Kupata michubuko maeneo ya sehemu za siri na sehemu zingine ambazo fangasi wameshambulia kama kwenye mikono na miguuni


- Kutokwa na uchafu kama maziwa mgando ukeni


- Sauti kubadilika na kuanza kukwaruza hasa hasa kwa mgonjwa mwenye Fangasi wa kooni


- Mgonjwa wa fangasi kooni hupata shida ya kula au kumeza kitu chochote


MATIBABU YA UGONJWA WA FANGASI


Matibabu ya Fangasi hutegemea sana na eneo ambalo fangasi wameshambulia,hivo matibabu ya Fangasi huhusisha dawa mbali mbali kama vile; Clotrimazole Cream,au Clotrimazole ya tubu za kuweka ukeni.


• Soma: Chanzo cha Tatizo la Kwikwi na Tiba yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUPANGA UZAZIAfyaclass Bongo Social •

 UZAZI

• • • • • •

VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUPANGA UZAZI


Kuna mambo mengi unatakiwa kuyafaham na kuzingatia katika swala zima la kupanga Uzazi. Na ifahamike tu kwamba swala la kupanga uzazi lisiwe la Mwanamke peke yake,Uzazi bora huhusisha watu wawili yaani Mume na Mke katika Familia.


VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUPANGA UZAZI NI PAMOJA NA;


1. Muda sahihi wa kupata watoto, hapa tunazungumzia umri(Interval) kati ya mtoto na mtoto, Wataalam wa afya wanashauri umri sahihi wa kupata watoto ambao ni mzuri kiafya uwe kuanzia miaka 2 au 3 kati ya mtoto na mtoto.


Hii huwapata watoto nafasi ya kupata muda wa kutosha wa kunyonya,Lishe N.K,hivo watoto huwa na afya bora zaidi na kuwa na Kinga ya kutosha dhidi ya Magonjwa mbali mbali ambayo huwasumbua sana watoto hasa wenye umri wa chini ya Miaka 5.


2. Kuzingatia sana katika kuchagua Njia sahihi kwenu,ambayo haitawaletea madhara au kuwasababisha mkapata watoto mapema au mkachelewa sana.


Mfano; Njia kama kalenda sio sahihi sana Kwa mtu ambaye Mzunguko wake unabadilika badilika yaani kwa kitaalam tunaita IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE hivo huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kupata Mimba bila yeye kupanga.


Lakini pia Njia ya Uzazi wa Mpango aina ya Sindano,Huweza kuchelewesha sana Mwanamke kubeba mimba pale atakapohitaji kubeba,Hivo kusababisha mwanamke kukaa mda mrefu sana bila kupata Mtoto.


3. Kuzingatia kanuni za unyonyeshaji bora kwa watoto wote, ikiwemo ile ya kutowachanganyia watoto chakula na maziwa kabla ya kumaliza miezi 6, Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama peke yake bila kuchanganyiwa na kitu kingine chochote kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzoni yaani kwa kitaalam hujulikana kama EXCLUSIVE BREASTFEEDING.


Na unyonyeshaji bora ni ule ambao unaenda hadi mtoto afikishe miaka miwili au mitatu ukiweza,huku akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama pamoja na kuchanganyiwa na vitu vigingine baada ya miez sita ya mwanzoni.


4. Shirika la Afya Duniani yaani WHO linashauri idadi ya watoto katika familia liwe hadi Watano,ili kuhakikisha afya bora kwao, lakini na kwa Mama Pia.


KUMBUKA; Vitu vingine ambavyo ni vya muhimu vya kuzingatia katika kupanga uzazi ni pamoja na;


- Kuendelea kujitunza na kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na magonjwa mengine mbali mbali ambayo huweza kuwa hatari kwa wazazi wote wawili pamoja na mtoto aliye tumboni. Mfano wa magonjwa hatari ni kama; UKIMWI,KASWENDE pamoja na KISONONO.


- Kuendelea kudumisha hali ya usafi wa mwili pamoja na Mazingira ili kutokukaribisha magonjwa kama vile; Malaria,UTI,FANGASI,PID N.K ambayo yote haya huweza kuwa hatari kubwa kipindi cha Ujauzito.


- Kuepuka matumizi ya dawa hovio bila kufata maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMOAfyaclass Bongo Social •

 UKIMWI

• • • • • •

DALILI ZA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMO


UKIMWI Ni ugonjwa wa upungufu wa Kinga Mwilini yaani kwa kitaalam huitwa ACQUIRED IMMUNODEFICIENCY SYNDROME(AIDS) ambao husababishwa na Virusi(virusi vya ukimwi(VVU)) wanaojulikana kwa kitaalam kama HUMAN IMMUNODEFICIENCY VIRUS au kwa kifupi HIV. Mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi huweza kuonyesha dalili mbali mbali ila makala ya leo inagusia kuhusu dalili za ugonjwa wa ukimwi kwenye Ulimi.


DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMO NI PAMOJA NA; 


1. Mdomo wa mgonjwa wa ukimwi huweza kupata hali ya kukauka sana na kuwa mkavu mara kwa mara.


2. Kutokana na kukosekana kwa uzalishaji mzuri wa mate,meno ya mgonjwa wa ukimwi huweza kuwa katika hatari ya kuoza kwani mojawapo ya kazi ya mate ni pamoja na ulinzi wa meno.


3. Kupatwa na tatizo la kuwa na vidonda mdomoni,kwenye Ulimi na maeneo ya kuzunguka kwenye lips, Vidonda hivo huwa mithili ya Duara ambavyo huweza kutokea kwa nje au ndani ya mdomo pamoja na Ulimi.


4. Kushambuliwa na Fangasi wa Mdomoni mara kwa mara ambao kwa kitaalam hujulikana kama thrush au  Candidiasis.


5. Kupatwa na Vidonda vinavyoambatana na homa mara kwa mara, japo tatizo hili huweza kupotea kabsa baada ya mgonjwa kuwa kwemnye dawa za ARV's.



6. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba Fizi za meno ambazo huambatana na maumivu hasa wakati wa kula kitu.


7. Ngozi ya fizi za meno kuwa na madoa doa yenye rangi kama ya Dhambarau.


8. Kuota vitu kama nywele au vikamba kamba kwenye Ulimi wa Mgonjwa.


9.Ngozi ya juu ya mdomo kuwa na mabaka mabaka ya rangi nyeupe.


Soma: Ugonjwa wa Ukimwi,chanzo,dalili na Tiba


KUMBUKA; Moja ya sehemu za kwanza kuonyesha dalili za Ugonjwa wa Ukimwi pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni pamoja na MDOMO NA ULIMI.

Hivo ukiona dalili hizi nenda hosiptal mapema kwa ajili ya Vipimo na uchunguzi zaidi.


NJIA AMBAZO MTU HUWEZA KUPATA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI NI PAMOJA NA;


- Kushare vifaa vyenye Ncha kali kama sindano na Nyembe


- Kupewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi


- Kufanya Ngono zembe


- Kufanya mapenzi kinyume na maumbile


N.K


Soma: Ugonjwa wa Ukimwi,Chanzo,Dalili na Tiba


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD