MAKOSA WANAYOFANYA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA PEDI(mambo yakuzingatia)Afyaclass Bongo Social •

PEDI

• • • • • •

MAKOSA WANAYOFANYA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA PEDI(mambo yakuzingatia)


Mada za usafi wa mwanamke ni pana sana siwezi kumaliza kusema kila kitu, hivyo leo nitajikita zaidi katika matumizi sahihi ya pedi na mambo ya kuzingatia kabla ya kununua pedi. Wadada wengi wamekuwa wakitumia pedi na kuziacha zikizagaa mitaani hali inayofanya nijiulize kama tu ameshindwa kujua sehemu sahihi ya kuhifahi au kutupa pedi aliyotumia yeye mwenyewe.


Yafuatayo ni makosa yanayofanywa katika uchaguzi na matumizi ya pedi kwa wanawake:

1. Kutonawa mikono kabla na baada ya kutumia pedi. Mikono hushika sehemu mbalimbali hivyo kuna uwezekano ikawa na vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa hiyo kushika pedi bila kunawa mikono kwa sabuni kunaweza kuhamisha vimelea hivyo kutoka mikononi na kwenda kwenye pedi inayotegemewa kuvaliwa.


2. Kutunza pedi bafuni au chuoni. Wadada wengi hupendelea kutunza pedi zao chooni/bafuni.


3.Kutoangalia muda wa matumizi wa pedi kabla ya kutumia au baada ya kuzihifadhi kwa muda mrefu hali inayopunguza kiwango cha ufanisi cha pedi sababu ya kuisha kwa muda wake wa matumizi.


4.Kununua pedi zinazouzwa kiholela kwa njia ya utangazaji na za bei rahisi (promotion) ambazo baadhi zimeonekana kutengenezwa kwa malighafi zilizo chini ya kiwango au kukaa kwa muda mrefu hivyo kuuzwa kwa bei rahisi ili zitoke na kutumika haraka kabla ya kuisha muda wake.


5.Kutumia pedi ambazo zipo katika majaribio maalum. Kama tunavyojua kuna kila aina za pedi mpya katika soko kwa kadri siku zinavyozidi kwenda na baadhi ya pedi huingizwa sokoni kinyemela pasipo tafiti za kutosha na bila hata kuthibishwa na mamlaka husika.


6.Kutumia pedi kwa muda mrefu. Wanawake wengi hususani katika nchi zinazoendelea huwa hawamudu kutumia pedi moja kwa muda wa masaa mawili kama inavyoshauriwa na wataalamu hivyo kujikuta katika hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa mkujo na njia za uzazi .


7.Kupendelea pedi zenye uwezo mkubwa wa kufyonza unyevunyevu ili ivaliwe muda mrefu pia ni tatizo sababu kwa kadri muda wa kuvaa pedi moja unapozidi kuongezeka na hatari za maambukizi ya magonjwa pia inazidi kuongozeka.


Je nini kifanyike ili kujikinga??? 


Wanawake wanashauriwa kufanya yafuatayo ili kuhakikisha usalama wa afya zao 

1. Kunawa mikono vizuri kwa sabuni kabla ya kugusa pedi ambayo unatarajia kuivaa na baada ya kuvaa kunawa tena mikono vizuri.


2. Kutohifadhi pedi bafuni au chuoni au sehemu yote yenye unyevunyevu na isiyo na mwanga wa kutosha ili kutotengeneza mazingira ya kukua kwa vimelea vya magonjwa ndani ya pedi.


3. Kuangalia kwa makini muda wa matumizi ya pedi kabla ya kununua au baada ya kutunza pedi kwa muda muda mrefu ili kuepuka kutumia pedi zilizopita muda wake wa matumizi.


4. Kuepuka kununua pedi zinazouzwa kiholela na zisizothibitishwa na TBS na mamlaka nyingine zenye dhamana ya kuangalia ubora wa pedi hizo. Mwanamke anatakiwa kuangalia nembo ya uthibitisho wa mamlaka hizo na kujiridhisha kuhusiana na usalama wa pedi hizo kabla hajanunua.


5. Kubadilisha pedi kila baada ya masaa mawili, kama tunavyojua damu ni moja wapo ya chakula kizuri sana kwa vimelea vya magonjwa kama bacteria ,unyevunyevu unaosababishwa na kuvaa pedi kwa muda mrefu pia unapelekea ustawi wa bacteria hao na joto ambalo lipo katika maumbile ya ndani ya mwanamke vikiungana kwa pamoja vinatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa bacteria , hivyo wanawake wanashauriwa kutovaa pedi hizo kwa muda usiozidi masaa mawili ili kuepuka mazingira hayo.


6. Kuchagua aina sahihi inayokutosha ina kuepuka pedi zinazobana sana kupita kiwango sababu zinaweza pia kukufanya usiwe huru na kutengeneza joto la ziada na michubuko katika maumbile ya mwanamke,hivyo mwanadada unashauriwa kutumia pedi itakayokukaa vizuri(isilegee sana wala kuachia sana)


7. Kwa wadada wanaotumia vitambaa badala ya pedi ni muhimu pia kuzingatia kanuni za kiafya na usafi kabla na baada ya kutumia vitambaa hivyo kama vile kuchagua kitambaa angavu ,kukiloweka na kukifua vizuri, kuanika kwenye sehemu yenye mwanga wa jua wa kutosha na upepo wa kutosha pasipo na unyevunyevu ,kupiga pasi kabla ujakihifadhi na kabla ya kutumia ili kuuwa vimelea vya magonjwa na kuvitunza sehemu nzuri ambayo haina unyevunyevu, penye hewa na mwanga wa kutosha na mwisho ni kubadilisha kitambaa hicho kila baada ya masaa mawili pamoja na kunawa mikono vizuri kabla na baada ya matumizi. 

Cc; @afyadarasa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

UGONJWA WA EDEMA(maana yake na chanzo chake)Afyaclass Bongo Social •

 EDEMA

• • • • •

UGONJWA WA EDEMA(maana yake na chanzo chake)


Ugonjwa wa Edema ni ugonjwa unaohusisha kuvimba kwa sehemu mbali mbali za mwili ikiwa ni pamoja na kuvimba Miguu au mikono.


CHANZO CHA UGONJWA WA EDEMA


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuvimba sehemu mbali mbali za mwili ikiwa ni pamoja na Miguu. Sababu hizo ni kama vile;


- Magonjwa ya figo, Mtu mwenye matatizo ya figo huweza kuvimba maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwa ni pamoja na Uso au miguu.


- Mtu mwenye tatizo kwenye Ini lake


- Mama Mjamzito huweza kuvimba miguu kwa asilimia kubwa


- Mtu ambaye amekaa kwa muda mrefu pasipo kutembea hasa ukiwa kwenye safari ndefu


- Mtu mwenye allegy na baadhi ya vitu kama vyakula aina ya nyama Flani N.K.Huweza kuvimba mwili baada ya kula vitu hivi


- Reaction inayotokana na dawa ambazo sio sahihi kwako

N.K


MATIBABU YA UGONJWA WA EDEMA


Matibabu ya tatizo hili hutegemea sana na chanzo chake, kama nilivyoeleza hapo juu kuhusu vyanzo mbali mbali. 

Hivo basi kama tatizo ni allegy mtu atapewa dawa za allegy mfano Cetrizine N.K


kama tatizo ni reaction ya dawa, magonjwa ya Figo,Ini N.K Basi tiba itahusu maeneo haya.





KWA USHAURI ZAIDI, ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







0 Comment

DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIAAfyaclass Bongo Social •

 MALARIA

• • • • •

DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIA


UTANGULIZI; UGONJWA WA MALARIA(chanzo chake,dalili na Tiba yake)


CHANZO CHAKE;


Ugonjwa wa malaria ni ugonjwa ambao husababishwa na Vimelea vya magonjwa ambavyo kitaalam hujulikana kama PLASMODIUM na kusambazwa kwenda kwa mtu na mbu jamii ya ANOPHELES.


Vimelea hivi vya Plasmodium vimewekwa katika makundi mbali mbali kama vile;


1. Plasmodium Oval


2. Plasmodium Vivax


3. Plasmodium Malariae


4. Pamoja na Plasmodium Falciparum


DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kupata hali ya kizunguzungu kikali


- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika


- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula


- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa


- Kupatwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara


- Kupata maumivu ya viungo,misuli pamoja na joint kwenye mwili wako


- Mwili wa mgonjwa kuchoka au kupata uchovu kupita kiasi


- Malaria kali huweza kusababisha mtu kuwa na dalili za kuchanganyikiwa, kuweweseka N.K


- Lakini pia malaria huweza kuleta shida ya upungufu wa damu mwilini, hivo mgonjwa huweza kupata dalili mbali mbali za upungufu wa damu mwilini kama vile;


 macho kubadilika rangi na kuwa meupe au paleness


Ngozi ya kwenye viganja vya mikono, lips za mdomo kuwa nyeupe au paleness


Kukosa nguvu,kizunguzungu N.K


MATIBABU YA UGONJWA WA MALARIA


- Dawa mbali mbali huweza kutumika kutibu ugonjwa wa malaria kama vile; Malaffin,ALU(maarufu kama Mseto), Quinine N.K


KUMBUKA; Dawa ya Sulfadoxine Pyrimethamine maarufu kama (SP) kutolewa kwa mama mjamzito kwa ajili ya kumkinga na Ugonjwa wa Malaria.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHAI YA KIJANI NA FAIDA ZAKE(maarufu kama Green tea)Afyaclass Bongo Social •

CHAI YA KIJANI

• • • • • •

CHAI YA KIJANI NA FAIDA ZAKE(maarufu kama Green tea)


Je ushawahi kusikia kuhusu chai ya Kijani?


Ni kweli kwamba kuna chai ya kijani ambayo maarufu hujulikana kwa jina la Green tea. Chai hii ni ya kijani kwa sababu ya aina ya majani yaliyotumika kuandaa chai hii.


Chai hii ina faida nyingi sana kwenye mwili wa mtumiaji,na katika makala hii nitagusia baadhi na kukuonyesha umuhimu wa chai ya kijani au Green tea.


- Chai hii ya Kijani au Green tea ina kiasi kidogo sana cha Caffeine ambacho huweza kuleta raha na msisimko wa tofauti sana kwenye mwili wa mtumiaji bila kusababisha madhara zaidi yatokanayo na utumiaji wa kiwango kikubwa cha Caffeine mwilini.


- Chai hii husaidia sana kwa wale watu ambao wana tatizo la uzito kupita kiasi, hivo kama una shida hii ya uzito mkubwa, chai hii inakufaa sana.


- Chai ya kijani husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba.


- Chai ya kijani au Green tea huleta afya ya mishipa ya damu


- Chai ya kijani husaidia kuboresha mzunguko mzima wa damu


- Chai ya kijani huimarisha afya ya seli hali za mwili


- Chai ya kijani husaidia kuboresha afya ya ubongo,pamoja na mfumo mzima wa akili ikiwa ni pamoja na kuleta utulivu mkubwa wa akili.


- Chai ya kijani husaidia kuimarisha uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa mtu.


N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MTOTO ANAANZA KUTAMBAA NA UMRI GANI?(au miaka mingapi?)Afyaclass Bongo Social •

 KUTAMBAA

• • • • •

MTOTO ANAANZA KUTAMBAA NA UMRI GANI?(au miaka mingapi?)


Swali ambalo wamama wengi hujiuliza hasa wale ambao ndyo mtoto wao wa kwanza, Wengi wao hawana uzoefu wowote hivo hujiuliza maswali mengi ikiwemo pamoja na hili, na wengi wao wakiwa na wasi wasi kwamba huenda watoto wao wana matatizo au shida yoyote.


Miongoni mwa maswali mengi ambayo wakina mama wengi waliojifungua hasa mimba za kwanza hujiuliza sana ni kama vile;


1. Hivi mtoto wangu ataanza kutambaa na umri gani?


2. Hivi mtoto wangu atatembea baada ya umri gani?


3. Hivi mtoto wangu ataanza kusimama baada ya muda gani?


4. Hivi mtoto wangu ataanza kuongea baada ya muda gani?

N.K


MTOTO ANAANZA KUTAMBAA NA UMRI GANI?


Jibu; Watoto wengi huanza kutambaa wakiwa na umri wa miezi 5 mpaka 10, huku wengi wao wakianza kutembea wakiwa na umri wa mwaka mmoja.


Japo wengine huweza kuwahi sana na wengine huweza kuchelewa sana kwa sababu mbali mbali,ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayosababisha udumavu wa mtoto.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

UGONJWA WA DEMENTIA(chanzo,dalili na tiba)Afyaclass Bongo Social •

 DEMENTIA

• • • • • •

UGONJWA WA DEMENTIA(chanzo,dalili na tiba)


Ugonjwa wa dementia ni ugonjwa unaohusisha kuharibika kwa seli hai za ubongo kutokana na mjumuisho wa magonjwa mengi ambayo husababisha mtu kupoteza uwezo wa kumbu kumbu kichwani,uwezo wa kufikiria,uwezo wa kutatua matatizo, uwezo wa kuongea N.K


Na miongoni mwa magonjwa makubwa ambayo husababisha Shida hii ya Dementia ni pamoja na Ugonjwa wa Alzheimer's, ugonjwa huu huchangia kwa wastani wa asilimia ya 60% mpaka 80%.


Sababu zingine ambazo huchangia kutokea kwa tatizo hili la Dementia ni pamoja na;


- Mtu kuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu (severe depression)


- Unywaji wa pombe kupita kiasi


- Madhara yatokanayo na matumizi ya baadhi ya dawa


- Upungufu au ukosefu wa vitamins Mwilini


- Matatizo yatokanayo na tezi aina ya Thyroid


DALILI ZA UGONJWA WA DEMENTIA NI PAMOJA NA;


- Mtu kupoteza uwezo wake wa kutunza kumbu kumbu kichwani


- Mtu kuwa na shida katika kuongea lugha yake


- Mtu kuwa na shida katika kufanya maamuzi yake


- Uwezo wa mtu katika kufikiria mambo huathirika kwa kiwango kikubwa


MATIBABU YA UGONJWA WA DEMENTIA


• Hakuna matibabu ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Dementia, ila kuna tiba juu ya kuthibithi dalili mbali mbali zinazojitokeza kwa Mgonjwa wa Dementia.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

SIRI USIYOIFAHAMU KUHUSU MAJI YA KUNYWAAfyaclass Bongo Social •

 MAJI YA KUNYWA

• • • • •

SIRI USIYOIFAHAMU KUHUSU MAJI YA KUNYWA


Mbali na faida lukuki ambazo zipo kwenye maji ya kunywa.Mwili wa binadamu kwa kiasi kikubwa umetawaliwa na sehemu ya maji.


Hata ubongo pia unahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana


Hapa utakubaliana na mimi kwamba,Maji ni uhai.


Lakini pia maji ndyo husaidia katika kupikia,kuosha vyombo,kufua,kuoga pamoja na matumizi mengine kama vile; Chooni N.K


Katika afya ya binadamu maji huchangia kwa asilimia kubwa sana kuliko kitu kingine chochote.


Fahamu hii; Utafiti unaonyesha kwamba, Ukinywa maji wastani wa Lita 2.5 kwa siku unapunguza uwezekano wa kupatwa na UTI kwa zaidi ya asilimia 50%.


Lakini pia hata kama una Uti,Maji yenyewe huweza kukusaidia wewe kupona kabsa UTI ambayo uko nayo.


Ndyo mana unashauriwa kutumia maji sana kwa siku angalau Lita 2.5 mpaka 3 kwa siku. Hii ni bora sana kwa afya ya mwili wako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

TATIZO LA MAPIGO YA MOYO KUWA CHINI AU KUPUNGUA(maarufu kama bradycardia)Afyaclass Bongo Social •

  BRADYCARDIA

• • • • •

TATIZO LA MAPIGO YA MOYO KUWA CHINI AU KUPUNGUA(maarufu kama bradycardia)


Katika hali ya kawaida endapo hakuna mabadiliko yoyote ndani ya moyo wako, hata moyo ukiendelea kudunda unaweza kusahau kabsa kama kuna moyo unadunda na kufanya kazi kila sekunde.


Lakini endapo kuna badiliko lolote mfano; mapigo ya moyo kuongezeka,moyo kwenda kasi sana au mapigo ya moyo kupungua sana,utaanza kuhisi mabadiliko makubwa kwenye mwili wako.


Katika makala hii tunazungumzia tatizo la mapigo ya moyo kupungua sana au kuwa kidogo,hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama bradycardia.


SABABU ZINAZOWEZA KUCHANGIA UWEPO WA TATIZO HILI LA BRADYCARDIA NI PAMOJA NA;


1. Misuli ya moyo kuchoka kufanya kazi kutokana na sababu ya kuzeeka au kuwa na  umri mkubwa


2. Kuharibika kwa tissu za moyo kutokana na hali ya uzee


3. Kuharibika kwa tissu za moyo kutokana na magonjwa mbali mbali ya moyo


4. Magonjwa ya moyo ambayo mtu huzaliwa nayo kwa kitaalam tunasema congenital heart diseases


5. Kuwa na tatizo la moyo kuvimba au kwa kitaalam tunaita myocarditis kutokana na maambukizi mbali mbali ya magonjwa


6. Kuwa na shida ya moyo kujaa maji


7. Kuwa na shida ya moyo kuwa mkubwa


8. Kuwa na tatizo la kuziba kwa mishipa ya moyo


10. Tatizo la tezi aina ya thyroid kufanya kazi chini ya kiwango yaani kwa kitaalam tunaita hypothyrodism


11. Kuwa na tatizo la moyo kufanya kazi chini ya kiwango kutokana na madhara ya operation iliyofanyika ya moyo


-

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAIDA ZA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMAAfyaclass Bongo Social •

  KUAMKA MAPEMA

• • • • •

FAIDA ZA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMA


Watu wengi hawajui kwamba kuna faida za kuamka asubuhi na mapema, huku wengine wakiamka tu mapema kwa sababu wana shuhuli nyingi ambazo huwafanya waamke asubuhi na mapema. 


Kuna faida nyingi katika mwili wa binadamu kwa mtu ambaye ana tabia ya kuamka mapema, na katika makala hii tumechambua baadhi ya faida hizo.


FAIDA ZA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMA


- Husaidia kuimarisha afya nzima ya Ubongo wako


- Huimarisha uwezo wa  kutunza kumbukumbu kwa mtu


- Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo ikiwa ni pamoja na kuzuia usipatwe na magonjwa mbali mbali ya moyo


- Husaidia katika kuimarisha mfumo mzima wa damu ikiwa ni pamoja na mzunguko wake


- Husaidia kupata muda mzuri wa kufanya mazoezi ya mwili kwa afya yako


- Husaidia katika kupanga mipango ya siku nzima



Pia wataalam wa afya hushauri upate muda wa kutosha wa kulala na kujipumzisha ndipo uamke mapema pia.


Kwani hata kuchelewa kulala sana na kukosa muda wa kutosha kulala huweza kuleta madhara mbali mbali kama vile; Kuathiri uwezo wa ubongo kufanya kazi, kudhoofika kwa mwili na N.K



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KUCHELEWA KULALA(na kukosa muda wa kutosha wa kulala)Afyaclass Bongo Social •

  KULALA

• • • • •

MADHARA YA KUCHELEWA KULALA(na kukosa muda wa kutosha wa kulala)


Katika hali ya kawaida, tips mbali mbali za afya hushauri mtu kupata muda wa kutosha wakupumzika pamoja na kulala kwani kuna umuhimu mkubwa wa kufanya hivo.


Zipo faida nyingi za mtu kupata muda wa kutosha wa kulala katika afya ya binadamu, na katika makala yetu tunachambua kuhusu madhara ya kuchelewa kulala au kukosa muda wa kutosha wa kulala.


MADHARA YA KUCHELEWA KULALA(na kukosa muda wa kutosha wa kulala)


- Hudhoofisha uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa mtu

- Huathiri afya nzima ya ubongo kwa mhusika

- Huleta hali ya mwili mzima kudhoofika

- Kushuka kwa kinga ya mwili,tafiti zinaonyesha watu ambao wanakosa muda wa kutosha wa kulala hupatwa na magonjwa ya mara kwa mara zaidi ya wale wanaopata muda wa kutosha wa kulala

- Hukuweka katika hatari za kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo


- Hukuweka katika hatari ya kupatwa na tatizo la kukosa kabsa usingizi yaani Insomnia pale unapohitaji kulala


- Huweza kuwa chanzo cha kupatwa na magonjwa mbali mbali ambayo huhusisha mfumo mzima wa damu ikiwa ni pamoja na kuathiri mzunguko mzima wa damu


-


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MATUMIZI YA FLAGYL KUZUIA MIMBA(ukweli wa mambo)Afyaclass Bongo Social •

 FLAGYL

• • • • •

MATUMIZI YA FLAGYL KUZUIA MIMBA


Je ni kweli kwamba ukitumia flagyl hupati mimba kama wengi wanavyofikiria?


Kuna watu wengi wanaambiana kwamba eti ukitumia flagyl kabla ya kufanya mapenzi basi unajikinga na kupata ujauzito hata ukiwa umeshiriki tendo la ndoa kwenye siku za hatari


TUANZIE HAPA JINSI YA BAADHI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO HUFANYA KAZI KUZUIA MIMBA


Tuangalie kwanza jinsi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinavyofanya kazi kuzuia mimba, halafu hapo baadae tuangalie na matumizi ya Flagyl kwenye mwili wa binadamu, mwisho tujibu swali letu.


- Moja ya vitu ambavyo njia za uzazi wa mpango hufanya ili kuzuia usipate mimba ni pamoja na;


1. Kuzuia au kupunguza kabsa uwezo wa mayai kutoka katika vifuko vyake yaani kwa kitaalam tunaita Ovulation, kitu ambacho hufanya kuwa vigumu sana kwa mbegu za kiume kukuta yai na kulirutubisha(mimba)


2.Kuongeza uzalishaji pamoja na uzito wa mucus kwenye mlango wa kizazi au tunaita Thickening of cervical mucus, kitu ambacho husaidia kukinga na kuzuia mbegu za kiume kupita kwenye mlango wa kizazi na kulifikia yai la mwanamke


3. Ngozi kwenye Ukuta ambapo mtoto huweza kujishikiza baada ya urutubishaji hufanywa kuwa nyembamba sana kiasi kwamba hata kama yai limerutubishwa ni vigumu sana kijusi kujishikiza hapo na mimba ikaendelea kukua


Soma: Mwanamke Kubeba Mimba baada ya Kujifungua


MATUMIZI YA FLAGYL PAMOJA NA KAZI ZAKE MWILINI


- Flagyl hutumika kutibu magonjwa au maambukizi yanayosababishwa na vimelea jamii ya parasite pamoja na bacteria mbali mbali kwenye mwili wako ikiwemo;


1. Maambukizi ya Giardia kwenye utumbo mdogo


2. Maambukizi ya amiba(amoeba) kwenye utumbo mkubwa


3. Maambukizi ya bacteria ambayo hujulikana kama Bacteria vaginosis, Trichomonas vaginal infections N.K


MAJIBU YA SWALI LETU


 Je matumizi ya flagyl huzuia mimba?


Majibu; Kutokana na jinsi ulivyoona mchakato wa kuzuia mimba ulivyo pamoja na kazi za Flagyl ulizoziona, ni dhahiri kwamba ni vitu viwili tofauti.


Hivo basi ukweli ni kwamba,matumizi ya Flagyl hayana uhusiano wowote na kukuzuia wewe usipate mimba. 


Hiyo ni dhana tu na imani potofu,


MADHARA YA KUTUMIA FLAGYL ILI KUZUIA MIMBA


Badala ya flagyl kukuzuia usipate mimba kama wengi wanavyodhani, inaweza kukusababishia madhara makubwa kwenye mwili wako hasa pale unapotumia kwa lengo la kuzuia mimba


Na madhara hayo ni kwamba, baada ya kutumia flagyl utapata mimba kama kawaida, na mwisho wa siku huweza kuathiri katika uumbaji wa mtoto, na kukupelekea wewe kuzaa mtoto mwenye matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ulemavu wa viungo


Soma: Mwanamke Kubeba Mimba baada ya Kujifungua


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

MADHARA YA KUTUMIA DAWA YA FLAGYL(METRONIDAZOLE) PAMOJA NA POMBE(athari zake)Afyaclass Bongo Social •

  FLAGYL

• • • • •

MADHARA YA KUTUMIA DAWA YA FLAGYL(METRONIDAZOLE) PAMOJA NA POMBE(athari zake)


Kwanza kabsa katika utangulizi wa makala hii,tuangalie matumizi mbali mbali ya dawa aina ya Flagyl au kwa jina lingine la kitaalam hujulikana kama Metronidazole


MATUMIZI YA FLAGYL PAMOJA NA KAZI ZAKE MWILINI


- Flagyl hutumika kutibu magonjwa au maambukizi yanayosababishwa na vimelea jamii ya parasite pamoja na bacteria mbali mbali kwenye mwili wako ikiwemo;


1. Maambukizi ya Giardia kwenye utumbo mdogo


2. Maambukizi ya amiba(amoeba) kwenye utumbo mkubwa


3. Maambukizi ya bacteria ambayo hujulikana kama Bacteria vaginosis, Trichomonas vaginal infections N.K


MADHARA YA KUCHANGANYA DAWA YA FLAGYL PAMOJA NA POMBE


Endapo upo kwenye dose ya flagyl(Metronidazole) huruhusiwi kutumia pombe kabsa,na endapo utachanganya vitu hivi viwili upo kwenye hatari ya kupatwa na madhara mbali mbali ikiwemo;


1. Kupatwa na shida ya viungo mbali mbali vya mwili kama figo pamoja na Ini


2. Kupatwa na tatizo la mapigo ya moyo kubadilika na kuanza kwenda mbio


3. Kupatwa na tatizo la kuishiwa pumzi na kushindwa kupumua kabsa,hali ambayo huweza kusababisha hata kupoteza maisha kabsa


4. Kupatwa na hali ya kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika


5. Kupatwa na kizunguzungu kikali hadi wengine kudondoka chini


6. Kupatwa na tatizo la maumivu makali ya kichwa


7. Joto la mwili kupanda gafla na kuhisi homa kali

N.K


Hivo basi ni hatari sana kuchanganya dawa ya Flagyl pamoja na pombe, epuka kabsa matumizi ya pombe ukiwa kwenye dose ya Flagyl kwani ni hatari kwa afya yako na maisha yako.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MATUMIZI YA DAWA ZA ASILI KUONGEZA UCHUNGU KWA MJAMZITO(madhara yake)Afyaclass Bongo Social •

  UJAUZITO

• • • • •

MATUMIZI YA DAWA ZA ASILI KUONGEZA UCHUNGU KWA MJAMZITO(madhara yake)


Zipo imani nyingi na zipo tamaduni mbali mbali za baadhi ya watu, kuhusu matumizi ya dawa za asili kwenye kuongeza uchungu kwa mama mjamzito.


Huku wengine wakiwa na imani kwamba mama mjamzito akitumia dawa hizo hujifungua kwa haraka zaidi.


Dawa hizo hutumiwa kwa njia mbali mbali huku zingine zikifichwa katika sehemu za siri za mwanamke,eti kwa lengo la kuongeza uchungu kwa mama huyu.


Je nini madhara yake?


Kuna vitu vingi vya kitaalam lazima uvifahamu kwa mama mjamzito kabla ya kufanya kitu chochote.


Vit hivo ni pamoja na hali ya mtoto aliyetumboni, mlalo wake, historia ya mama kwa mimba za nyuma, hali ya kondo la nyuma au placenta ikoje N.K


Endapo umetumia dawa hizo za asili kwa ajili ya kuongeza uchangu wakati mama ana matatizo mengine nini kitatokea?


Mfano; Huwezi ukamuongezea uchangu wa mama kujifungua kawaida wakati kondo lake la nyuma limeziba kabsa njia ya mtoto kupita, 


huwezi kumuongezea mama uchungu wa kuzaa kawaida wakati ana kovu au kidonda kikubwa cha operation za mimba za nyuma, matokeo yake ni kusababisha mtoto kufia tumboni,mtoto kuzaliwa na ulemavu, mama kupasuka kizazi,mama kufariki N.K


Na kwa bahati mbaya,asilimia kubwa ya watu ambao wanatumia dawa hizi,hata huo uchungu hauongezeki bali hata kusukuma tu mtoto wanashindwa.


KUMBUKA;Epuka matumizi ya dawa hovio kwa ajili ya afya yako na afya ya mtoto aliyetumboni.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAHAMU MADHARA YA RANGI(za ukutani,magari,michoro n.k)Afyaclass Bongo Social •

 RANGI ZA UKUTANI

• • • • • •

FAHAMU MADHARA YA RANGI(za ukutani,magari,michoro n.k)


Kama ilivyozoeleka kwenye masikio ya watu, kila kitu kina faida zake pamoja na hasara zake.


Hata rangi ambazo tumezoea kuziona zikipendezesha vitu mbali mbali,zina faida zake na hasara zake.


Hapa tunazungumzia rangi ambazo hupakwa kwenye vitu mbali mbali kama vile; rangi za magari, rangi za kuta za nyumba,rangi za michoro na picha mbali mbali, N.K


Tafiti za afya zinaonyesha kwamba ndani ya rangi hizo kuna kemikali mbali mbali ambazo huweza kuleta madhara mbali mbali katika mwili wa binadamu kama vile Saratani, Magonjwa ya vifua,mapafu, N.K


Hizi hapa ni baadhi ya kansa au Saratani ambazo huweza kuchangiwa na uwepo wa kemikali hizo kwenye rangi mbali mbali;


- Saratani ya damu


- Saratani ya mapafu


- Saratani ya koo


- Saratani ya kongosho


- Saratani ya mdomo


- Saratani ya kibofu


- Saratani ya Ngozi


NB; Hivo basi, kwa wewe ambaye unafanya kazi zozote zinazohusu rangi, unashauriwa kujikinga sana kwa kuvaa nguo za kufunika mwili wako wote kama vile Evarol, Kofia ngumu kichwani, boot miguuni pamoja na mask usoni ili kujikinga na kuingiwa na rangi hizi kwenye mwili wako.


Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba,afya yako ndyo mtaji wako wa kwanza.


-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UGONJWA WA APPENDIX AU KIDOLE TUMBO(chanzo,dalili na tiba yake)Afyaclass Bongo Social •

  APPENDIX

• • • •

UGONJWA WA APPENDIX AU KIDOLE TUMBO(chanzo,dalili na tiba yake)


Kwa kawaida,appendix au kidole tumbo ni sehemu ya muendelezo wa utumbo mkubwa au mpana mwishoni, ambapo huwa na kitu mithili ya kidole chako cha mwisho cha mkononi.


CHANZO CHA TATIZO LA APPENDIX


Kwa kawaida baada ya chakula kuyeyushwa na umeng'enyaji kuendelea, kuna baadhi ya myeyusho wa chakula hupitia sehemu hii ya kidole tumbo au appendix.


Sasa endapo chakula kitapita hapa pamoja na vitu vidogo vidogo vigumu kama vile; mchanga N.K, vitu hivi haviwezi kupita hapa, hivo hujilundika hapa kila siku unapokula chakula kilichochanganyika na vitu hivi vigumu. 


Hali hii huendelea hadi kufikia hatua ya kidole tumbo au appendix kuziba kwa juu pamoja na kuvimba na mtu kuanza kupata maumivu makali. Hapo ndipo chanzo cha tatizo la appendix huanza.


DALILI ZA UGONJWA WA APPENDIX AU KIDOLE TUMBO NI PAMOJA NA;


- Kupatwa na maumivu makali ya tumbo usawa wa kitovu chako kuelekea upande wa kulia


- Joto la mwili kupanda au kuanza kuwa na homa


- Kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika


- Mgonjwa kupatwa na shida ya tumbo kujaa gesi mara kwa mara

N.K


VIPIMO


vipo baadhi ya vipimo ambavyo huweza kufanyika kama vipimo vya damu,ultrasound,Ct Scan N.K


Mgonjwa anaweza kuchunguzwa dalili,historia ya ugonjwa pamoja na uchunguzi kwa njia ya kupapasa mikono ambayo hufanywa na mtaalam wa afya au dactari.



MATIBABU YA UGONJWA WA APPENDIX


- Matibabu ya ugonjwa wa kidole tumbo au appendix huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali katika hatua za mwanzoni za ugonjwa, lakini kama tatizo litaendelea mgonjwa atafanyiwa upasuaji na kuondoa kabsa hicho kidole tumbo.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MATUMIZI YA DAWA AINA YA SILDENAFIL CITRATE (VIAGRA)(kutibu uume kushindwa kusimama)Afyaclass Bongo Social •

 DAWA

• • • • • •

MATUMIZI YA DAWA AINA YA SILDENAFIL CITRATE (VIAGRA)(kutibu uume kushindwa kusimama)


ni dawa inayotumika kutibu tatizo la kusimama kwa uume (erectile dysfunction) na shinikizo la damu kwenye mishipa.


  Erectile dsyfunction ni tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri wakati wa kujamiiana au kushindwa kusimama kwa muda mrefu wakati wa tendo.Tatizo hili husababishwa na vitu mbalimbali vikiwemo ajali,madawa,msongo wa mawazo 


 VIAGRA ZINAFANYAJE KAZI?...


 Viagra huongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume na kuufanya usimame na uwe mgumu wa kujamiiana.Kwa kawaida viagra huanza kufanya kazi dakika 30-60 baada ya kumezwa na hutumika wakati mtu anataka kujamiiana.


  Baada ya tendo kumalizika uume unatakiwa utulie(loose erection) baada ya masaa manne endapo kama itazidi hapo muone daktari.


HUPASWI KUTUMIA VIAGRA KAMA:-


 i.Umetumia dawa zenye nitrates kama nitroglycerine


ii.Umetumia dawa zinazoitwa "poppers" kama amyl nitrate au amyl nitrite na butyl nitrate


iii.Una mzio (allergy) na viambatanisho (ingredients) zilizotumika kutengeneza viagra.


MADHARA YA VIAGRA:


i.Uume kusimama mda mrefu kupitiliza (priapism)


ii.Kupoteza uwezo wa kuona kwenye jicho moja au yote kwa ghafla


iii.Kupoteza uwezo wa kusikia ghafla


iv.Kupatwa na kizunguzungu


v.Maumivu ya kuchwa


vi.Maumivu ya misuli


vii.Mshtuko wa moyo (heart attack)


viii.Kiharusi (stroke)


ix.Kifo


Cc:@_afyazone




0 Comment

FAHAMU FAIDA 5 ZA KUNYWA MAJI KABLA YA KULA CHOCHOTE(unapoamka asubuhi)Afyaclass Bongo Social •

 MAJI YA KUNYWA

• • • • • •

FAHAMU FAIDA 5 ZA KUNYWA MAJI KABLA YA KULA CHOCHOTE(unapoamka asubuhi)


Karibu ufahamu faida 5 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.


1. Huondoa sumu mwilini


Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema.


Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.


2. Huboresha metabolim

Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.


Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia.


3. Husaidia kupunguza uzito


Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili yao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa unapoamka na kuanza kutumia vinywaji kama vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili.


Utafiti unaonyesha kuwa soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.


4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng’enyaji wa chakula


Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo hupelekea tatizo la kiungulia. Sanjari na hayo unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng’enywaji wa chakula.


Hivyo basi, kama unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.


5. Huboresha na kuimarisha ngozi


Utafiti unaonyesha kuwa kunywa maji takriban mililita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.

Cc:@_afyazone 




0 Comment

VITU VYA KUZINGATIA KWENYE MAZIWA YA MTOTOAfyaclass Bongo Social •

  MAZIWA YA MTOTO

• • • • •

VITU VYA KUZINGATIA KWENYE MAZIWA YA MTOTO


Kwanza kabsa nianze kwa kutoa ufafanuzi kuhusu unyonyeshaji wa mtoto(kanuni inasemaje).


Mtoto anapozaliwa anatakiwa kupewa maziwa ya mama pekee bila kuchanganyiwa na kitu kingine chochote kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzoni, Hata maji hapewi, hii kanuni kwa kitaalam tunaita  EXCLUSIVE BREASTFEEDING.


Baada ya kumaliza miezi sita ya mwanzoni,anza kumchanganyia mtoto maziwa ya mama na vyakula vingine, ila usiache kumnyonyesha hadi afikishe umri wa miaka 2 au 3.


VITU VYA KUZINGATIA KWENYE MAZIWA YA MTOTO


- Maziwa ya mtoto hayatakiwi kukamuliwa kutoka kwa mama na kuwekwa kwa muda mrefu mfano; kwa muda wa zaidi ya saa sita ndipo mtoto apewe.

- Maziwa ya mama hayatakiwi kupakwa kitu chochote wakati mtoto ananyonya, bali hakikisha unaosha vizuri matiti yako kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto

- Mtoto hatakiwi kupewa maziwa ambayo yamekaa kwa siku nzima

- Maziwa ya mtoto yasichanganywe na kitu kingine chochote kama vile maji,sukari N.K. yanatakiwa yawe kama yanavyotoka kwa mama vile vile bila mchanganyo wa aina yoyote


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

AFYA KWA MAMA MJAMZITO(nukuu ya leo)Afyaclass Bongo Social •

   MJAMZITO

• • • • •

AFYA KWA MAMA MJAMZITO(nukuu ya leo)


Kuna mambo mbali mbali ambayo yatamfanya mama mjamzito kufurahia maisha yake katika kipindi cha ujauzito. Na mambo hayo ni pamoja na;


1. Kuzingatia lishe bora kipindi cha ujauzito na mara baada ya kujifungua


2. Kujua dalili zote za hatari kipindi cha ujauzito kama vile; kutokwa na damu wakati wa ujauzito, mtoto kutokucheza tumboni kwa wale ambao wamefikia umri wa mtoto kucheza tumboni, kuvimba sana miguu,uso na mikono, Kutokwa na uchafu wenye harufu kali ukeni, Kushikwa na degedege,Joto la mwili kupanda au kuwa na homa N.K


3. Kutokuvaa nguo za kubana tumbo,mikanda N.K


4. Kutokuvaa viatu virefu wakati wa Ujauzito kwani huweza kukuletea madhara mbali mbali kama vile; Maumivu ya kiuno,mgongo,miguu kwenye visigino, kudondoka N.K


5. Pendelea kulala ubavu hasa hasa ubavu wa kushoto na sio kulala kifudifudi


6. Hakikisha unahudhuria kliniki zote 


7. Fanya maandalizi ya kujifungua mapema na jua vitu vyote ambavyo vinahitajika wakati wa kujifungua ambapo kwa kitaalam package hii hujulikana kama Individual birth preparedness(IBP)


8. Hakikisha unatumia vidonge vyekundu maarufu kama FEFOL au vidonge vya Folic acid, ambavyo hufanya kazi mbali mbali kama vile; kuongeza wingi wa damu kwa mama mjamzito kwani damu nyingi hupotea wakati wa kujifungua, kuzuia watoto kuzaliwa na mgongo wazi au tatizo la vichwa vikubwa.


9. Nenda hosptal pale unapohisi una tatizo lolote ambalo hulielewi wala usisubri siku ya kuhudhuria kliniki mfano; Tatizo la Chupa ya uzazi kupasuka N.K


10. Epuka matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya, kwani dawa zingine huweza kukuletea madhara wewe pamoja na mtoto aliyetumboni.



-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAIDA ZA KULA CHAKULA MUDA UNAOFANANA(kila siku)Afyaclass Bongo Social •

  CHAKULA

• • • • •

FAIDA ZA KULA CHAKULA MUDA UNAOFANANA(kila siku)


Kwanza kabsa ifahamike kwamba, hata mwili nao huweza kujenga mazoea wenyewe kutokana na vitu ambavyo umeshazoeshwa kufanya kila siku, Mfano wewe ni shahidi kwamba,kama umezoea kulala usku muda flani, basi ukifika ule mda hata kama hutaki kulala kwa siku hyo utaona jinsi ambavyo utapata usingizi wa ajabu.


Au kama umezoea kukaa mazingira flani kwa muda mrefu basi ukiyabadilisha yale mazingira,tayari unaweza kupata mabadiliko flani kwenye mwili wako


Nidhahiri kwamba mwili hujenga mazoea kwa kitu flani ambacho unakifanya kila siku.


Hata katika Ulaji wa chakula mwili ni hivo hivo hujenga mazoea, na unaweza kupata madhara kama umebadilisha muda wa kula kila siku.


Kwanza unashauriwa kutokukaaa kwa muda mrefu sana bila kula chakula, Pili ukiwa unakula jaribu angalau kula chakula kwa muda unaoendana.


Kitendo cha kubadilisha badilisha muda wa kula chakula pamoja na kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula huweza kusababisha kuwa na vidonda vya tumbo,


Kwani kinachotokea ni kwamba,Enzymes au vimeng'enyaji chakula pamoja na acid tumboni huanza kuzalishwa kwa ule muda ambao umezoea kula, hali ambayo hupelekea endapo tumbo litakuwa halina kitu, basi athari itaanza kutokea taratibu kwenye ukuta wa tumbo.


Kitu ambacho huweza kusababisha ukuta wa tumbo kulika na kuleta tatizo la vidonda vya tumbo.


ANGALIZO; Jitahidi kula kwa muda unaoendana au kufanana kila siku na epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula kwani unaweza kupata madhara mbali mbali kwenye mwili wako ikiwa ni pamoja na vidonda vya tumbo.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI(chanzo,dalili na Tiba)Afyaclass Bongo Social •

  CHANGO LA UZAZI

• • • • •

UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI(chanzo,dalili na Tiba)


Ugonjwa wa chango la uzazi, umekuwa ugonjwa ambao hutesa sana wanawake wengi kwa hivi sasa, japo hata wanaume pia huweza kupatwa na ugonjwa wa chango kama wengine ambavyo hawafahamu kabsa hili.


Madhara ya ugonjwa wa chango kwa mwanamke ni makubwa na huhusisha madhara mbali mbali kama vile; Mwanamke kupoteza uwezo wa kubeba mimba, mimba kuharibika zenyewe,maumivu makali ya tumbo N.K


CHANZO ZA UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI


- Chango la uzazi kwa mwanamke hutokea pale ambapo vifuko vya mayai yaani Ovaries kuwa na shida, Shida hii huhusisha vifuko vya mayai(ovaries) kupoteza uwezo wake wa kawaida wa kuzalisha mayai na kufanya yakue ndani ya wakati wake,kitu ambacho hupelekea baadhi ya wanawake kukosa hedhi,hedhi kutokuwa na mpangilio maalumu au kupoteza uwezo wa kubeba mimba.


- Mabadiliko ya vichocheo vya mwili kama vile; Uzalishaji wa kiwango kikubwa wa kichocheo aina ya Prolactin kwenye damu hali ambayo hudhibiti na kuzuia uzalishwaji wa kichocheo cha Estrogen, Mvurugiko wa vichocheo vya Lutenizing hormones na Folicle stimulating hormones kwenye ubongo N.K


DALILI ZA UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI


- Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo


- Mwanamke kupata maumivu makali ya kiuno


- Mwanamke kupata maumivu makali ya mgongo


- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa pale mwanamke anapokaribia hedhi


- Mwanamke kupatwa na maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi au anapokaribia hedhi yake


- Mwanamke kuwa na uchovu mkubwa wa mwili kipindi cha hedhi


- Kukosa mpangilio maalumu wa hedhi


- Kushindwa kubeba mimba


- Mimba kuharibika zenyewe

N.K


MATIBABU YA UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI


- Zipo dawa mbali mbali za kudhibiti dalili za ugonjwa huu lakini sio za kuondoa kabsa shida hii kwa hospitalin. 


Hivo basi kama mwanamke atapata maumivu makali wakati wa hedhi atapewa dawa za maumivu, kama mwanamke anashindwa kuzalisha mayai atapewa dawa za kuzalisha mayai N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

DAWA YA ALLERGY YA KUJIKUNA KWENYE NGOZI(soma hapa)Afyaclass Bongo Social •

  ALLERGY

• • • • •

DAWA YA ALLERGY YA KUJIKUNA KWENYE NGOZI(soma hapa)


Kuna baadhi ya watu wana shida ya kujikuna sana kwenye ngozi hasa baada ya kufanya mambo kadhaa kwa mfano;


- Baada ya kula nyama flani, kama vile ya ng'ombe,mbuzi,kuku N.K


- Baada ya kuoga na maji ya Mvua


- Baada ya kupaka mafuta flani


- Baada ya kula mafuta flani


- Baada ya kunywa dawa flani


- Baada ya kupaka dawa flani hasa dawa za nywele

N.K


Hivo kwa lugha nyingine tunasema watu hawa wana allegery na vitu hivi, japo zipo allergy nyingine kama zinazotokana na vitu kama vumbi, Perfume, baadhi ya vyakula N.K



Hivo kama unashida hii yakujikuna sana kwenye ngozi,kuna matibabu mbali mbali au dawa mbali mbali ambazo ni nzuri kutumia na hilo tatizo likaisha kabsa, Na moja ya dawa hizo ni Pamoja na CETRIZINE.



Dawa hii ni nzuri sana kukusaidia kama una tatizo la kujikuna kwenye ngozi kutokana na allergy ya matumizi ya vitu mbali mbali



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

KADI YA KLINIKI KWA MTOTO(tangazo)Afyaclass Bongo Social •

 TANGAZO

• • • • •

KADI YA KLINIKI KWA MTOTO(tangazo)


Kuna sehemu kuu mbili katika kadi ya mtoto ya Kliniki ambazo ni kama ifuatavyo;


1. Kuna sehemu ya kadi ya mtoto ya kliniki ambayo hutumika kwa ajili ya chanjo mbali mbali za mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano kama kwenye picha hapa chini


Soma: Chanjo Zote za Mtoto toka anazaliwa mpaka umri wa miaka Mitano


2. Na kuna sehemu ya kadi ya kliniki ya mtoto kwa ajili ya kufwatilia maendeleo ya ukuaji wake, hapa ndipo vipimo kama vya uzito hurekodiwa


KAMA WEWE NI MIONGONI MWA WATU AMBAO KADI HII YA KLINIKI INAKUCHANGANYA HUIELEWI KABSA,NA UNASHINDWA KUFWATILIA CHANJO ZOTE ZA MTOTO TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


1.Soma: Mwanamke Kubeba Mimba Kabla ya Miaka 35


2.Soma: Chanjo Zote za Mtoto toka anazaliwa mpaka umri wa miaka Mitano




0 Comment

TATIZO LA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME (Low sperm count)Afyaclass Bongo Social •

 LOW SPERM COUNT

• • • • • •

TATIZO LA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME (Low sperm count)


Katika hali ya kawaida ya mwili, kuna kiwango cha mbegu ambacho mwanaume hutakiwa kukizalisha kila sekunde. Na mbali na kiwango hicho kuzalishwa, huwa na matokeo ya moja kwa moja hata katika swala nzima la uzazi na kupata watoto.


Kutokana na mazingira ya sehemu za siri za mwanamke yalivyo,mbegu nyingi za mwanaume hufia njiani hata kabla ya kulikuta yai la mwanamke.


Hivo basi kwa mwanaume ambaye anazalisha kiwango kidogo cha mbegu yupo kwenye hatari ya kushindwa kumpa mimba mwanamke kutokana na idadi kubwa ya mbegu kufa hata kabla ya kukutana na yai, Hivo urutubishaji na mtoto kuzaliwa au mimba kutunga huweza kuwa ngumu sana kwa mwanamke.


Tatizo hili la mwanaume kuzalisha kiwango kidogo sana cha mbegu za kiume hujulikana kama low sperm count

.


DALILI ZA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME NI PAMOJA NA;


- Mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke


- Mwanaume kupata maumivu ya korodani,japo sio kila mara


- Mwanaume kupoteza hamu ya kufanya mapenzi

N.K


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI


- Wanywaji wa pombe kupita kiasi


- Wavutaji wa sigara


- Wanaotumia dawa zinazohusu kuongeza au kupunguza vichocheo vya mwili


- Wenye matatizo mengine kama kuziba mirija ya korodani 


- Wanaofanya kazi ambazo huhusisha kuungua sana au kupata joto sana sehemu za korodani

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UGONJWA WA DAMU KUGANDA(chanzo,dalili,tiba)Afyaclass Bongo Social •

 DAMU

• • • • •

UGONJWA WA DAMU KUGANDA(chanzo,dalili,tiba)


Katika hali ya kawaida ya mwili, huwa damu hutakiwa kuganda endapo kumetokea majeraha au hali yoyote ya kuchubuka mwili ambayo hufanya damu kutoka.


Endapo mwili haujapata jeraha lolote,ajali,au mchubuko wowote halafu damu ikaganda,hapo kuna tatizo, na huo ni ugonjwa kabsa wala sio hali ya kawaida.


Ugonjwa huu kwa kitaalam hujulikana kama thrombophilia na zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia kutokea kwa ugonjwa huu.


CHANZO CHA UGONJWA HUU WA DAMU KUGANDA


• Kurithi vinasaba vya tatizo hili katika koo husika. Hivo basi kama kwenye familia yenu kuna tatizo hili,na wewe pia upo kwenye hatari ya kupatwa na tatizo hili la damu kuganda.


• Hitilafu katika protein za mwili wako ikiwa ni pamoja na upungufu wake kwa kiasi kikubwa, Mfano ni; Protein C,protein S,Prothrombin N.K


• Uwepo wa tatizo la kansa


• Hali ya vigandishi damu kufanya kazi kuliko kawaida yake au kwa kupita kiasi


• Kuwa na matatizo mengine ambayo hukufanya ukae sehemu moja kwa muda mrefu pasipo kufanya chochote mfano; watu wenye magonjwa ya kupooza N.K


• Kuwa na shida ya upungufu mkubwa wa vitamins aina ya vitamin B12 Na vitamin B6 mwilini.


• Kuwa na shida ya unene au uzito uliopitiliza.


DALILI ZA UGONJWA WA DAMU KUGANDA NI PAMOJA NA;


1. Mgonjwa kuhisi miguu kuwaka moto mara kwa mara


2. Mgonjwa kushindwa kupumua vizuri


3. Mgonjwa kupata tatizo la kukohoa makohozi ambayo yamechanganyika na damu


4. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kupata homa


5. Miguu ya Mgonjwa kubadilika rangi yake ya ngozi na kuwa myekundu


6.Mgonjwa kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda mbio sanaa


7. Uwezo wa kuona kwa mgonjwa kupungua gafla


8. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu na kutapika


9.Mgonjwa kupatwa na maumivu makali ya kichwa


10. Mgonjwa kutoa jasho sana kwenye mwili wake


MATIBABU YA UGONJWA WA DAMU KUGANDA


- Kuna vipimo vingi ambayo hufanyika kwanza kwa mgonjwa mwenye dalili hizi ikiwa ni pamoja na kipimo cha damu, kipimo cha kuangalia Utendaji kazi wa Protein mwilini,CBC, na vipimo vingine ndipo matibabu yaanze.


Hivo ni vizuri kwenda hospital mapema kama una tatizo hili au una dalili hizi ambazo nimezielezea kwenye makala hii.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD