Mwanamke kabeba mimba wakati bado mtoto ananyonya je anaruhusiwa Kumnyonyesha?Afyaclass Bongo Social •

 UZAZI

• • • • • •

Mwanamke kabeba mimba wakati bado mtoto ananyonya je anaruhusiwa Kumnyonyesha?


Hili ni swali ambalo nimeulizwa na watu wengi sana naomba leo nitoe ufafanuzi katika makala hii,


MAJIBU;


Ndyo unaruhusiwa kumnyonyesha mtoto hata kama umebeba mimba nyingine wakati bado mtoto ananyonya, ila fahamu mambo haya;


✓ Mwili wako utaendelea kuzalisha maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto anayenyonya ujauzito ukiwa katika hatua za mwanzoni, ila kadri ujauzito unavyokuwa ndipo na uzalishaji wa maziwa hupungua kwa kiwango kikubwa, hasa ujauzito ukiwa na umri wa miezi 5 na kuendelea


✓ Kadri ujauzito unavyokuwa ndipo na Content za maziwa zinabadilika kama vile COLESTRUM hali ambayo hupelekea ladha ya maziwa kubadilika kabsa,


Hali hii huweza kusababisha mtoto asipate maziwa ya kutosha, kupata maziwa mepesi,kutokushiba N.k,


Hivi vyote huanza kuathiri ukuaji wa mtoto wako na kumfanya mtoto kuwa dhaifu, mwenye kuumwa umwa n.k


Hivo lazima uongee na wataalam wa afya ili wakushauri cha kufanya ikiwa ni pamoja na Lishe sahihi kwa mtoto huyo


✓ Mtoto ataendelea kukuwa tumboni kama kawaida na kupata  virutubisho vyote muhimu kutoka kwa mama, kama mama anazingatia hatua za ulaji bora kwa mama mjamzito


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIPATE VIDONDA KWA MGONJWA WA KISUKARIAfyaclass Bongo Social •

  AFYA TIPS

• • • • • •

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIPATE VIDONDA KWA MGONJWA WA KISUKARI


Una kisukari au mtu wako wa karibu ana tatizo hilo? Watu wanaoishi na tatizo la kisukari huwalazimu kuwa makini sana ili wasipate vidonda vya aina yoyote ile, kwani huweza kuwa vigumu vidonda hivo kupona,


Haya hapa ni baadhi ya mambo yakuzingatia ili usipate vidonda vya aina yoyote hasa kwa wewe ambaye ni mgonjwa wa kisukari



1. Epuka kutembea bila viatu, yaani kutembea peku, kwa maana unaweza kujikata na kitu chenye ncha kali kama sindano, chumba, miiba n.k


2. Epuka kutumia vitu vyenye ncha kali kukatia kucha kwa mfano usitumie wembe au mkasi kukata kucha ili kuepuka kujikata na kupata kidonda, pendelea sana kutumia nail cutter.


3. Epuka kuvaa viatu na soksi za kubana, na pia hakikisha miguu yako ni mikavu kila muda, kwa hiyo basi utokapo kuoga ama kunawa miguu, hakikisha unaikausha vizuri hasa katikati ya vidole, kwa sababu kama ukiacha unyevunyevu ni rahisi kutengeneza lengelenge na pia endapo utapata lengelenge usitumbue na liache likauke lenyewe.


Kwa wanawake, epuka kuvaa viatu virefu kwa sababu vinazuia damu kufanya mvunguko wake wa kawaida (blood circulation)


#afyabongo #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAGONJWA AMBAYO HUTIBIWA KWA ALOE VERA(mmea-Tiba asili)Afyaclass Bongo Social •

 ALOE VERA

• • • • • •

MAGONJWA AMBAYO HUTIBIWA KWA ALOE VERA(mmea-Tiba asili)


Aloe vera hutibu magonjwa mengi sana kwenye mwili wa binadamu, inakadiriwa kwamba Aloe vera huweza kutibu zaidi ya magonjwa 200 kwenye mwili wa binadamu,


Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo huweza kutibiwa na Aloe vera,kitu cha msingi ni kufahamu jinsi ya kuandaa,kutumia na kiwango sahihi kulingana na ugonjwa ulio nao.


1. Ugonjwa wa Bawasiri au kuota kinyama sehemu ya haja kubwa


2. Ugonjwa wa Malaria sugu


3. Ugonjwa wa UTI za mara kwa mara ambazo haziishi


UTI- urinary track infection au maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo ikiwa ni pamoja na Njia ya mkojo,kibofu cha mkojo,Figo,Tezi n.k


4. Tatizo la nguvu za kiume au matatizo ya hormone za kiume kama vile Testosterone n.k


5. Aina mbali mbali za Kansa kama vile; Kansa ya ngozi,shingo ya kizazi n.k


6. Ugonjwa wa Vidonda vya tumbo


7. Ugonjwa wa Shinikizo la Damu au Presha


8. Ugonjwa wa Kisukari


9. Magonjwa mbali mbali yanayoenezwa kwa njia ya kujamiiana au magonjwa ya zinaa


10. Matatizo mbali mbali yanayohusu Uzazi 


11. Tatizo la kuwa na Uzito Mkubwa au uzito kupitiliza

N.K



Matumizi kwa ujumla;


Chukua kipande kimoja kikate kisha uchemshe na kikombe kimoja cha maji kisha unywe nusu asubuh na nusu jion au uloweke kwenye kikombe kisha uiweke juan  kwa muda masaa 6 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

UGONJWA WA GAUCHER,chanzo,dalili na Tiba(GAUCHER DISEASE)Afyaclass Bongo Social •

       GAUCHER DISEASE

• • • • • •

UGONJWA WA GAUCHER,chanzo,dalili na Tiba(GAUCHER DISEASE)


Ugonjwa wa gaucher ni ugonjwa ambao huhusisha mafuta kujikusanya kwenye viungo muhimu sana vya mwili kama vile kwenye INI na Wengu(Spleen).


CHANZO CHA UGONJWA WA GAUCHER


• ugonjwa wa Gaucher hutokana na tatizo la kigenetic ambapo mtu hurithi vinasaba vya tatizo hili katika familia au koo husika (Autosomal recessive),


Mgonjwa mwenye ugonjwa huu baada ya Fatty substances kujikusanya kwa pamoja kwenye viungo hivo huanza kupata dalili mbali mbali,


DALILI ZA UGONJWA WA GAUCHER NI KAMA VILE;


- Mtu kupata maumivu makali ya tumbo


- Kuwa na shida kwenye mifupa ya mwili ikiwa ni pamoja na; kuwa na mzunguko hafifu sana wa damu kwenye mifupa, mifupa kuwa dhaifu, mifupa kuvunjika kwa haraka zaidi n.k


-  Mwili kuchoka kupita kawaida


- Kuathiriwa kwa seli ambazo huhusika na swala la damu kuganda yaani  clotting, hali ambayo hupelekea mgonjwa kuvuja damu kama vile puani n.k


- Kupungua sana kwa seli nyukundu za damu yaani RED BLOOD CELLS hali ambayo hupelekea mtu kuwa na tatizo la damu kuisha mwilini yaani ANEMIA


MADHARA YA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


✓ kuwa na tatizo la mifupa ya mwili kuwa hafifu na kuvunjika kwa haraka zaidi


✓ Kuvuja damu bila kuganda


✓ Kuwa na tatizo la kuishiwa na damu mwilini


✓ Mtu kuchelewa kwenye hatua zake za ukuaji yaani KUBALEHE au puberty


✓ Kuwa na matatizo ya Uzazi


✓ Kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa Parkinsons


✓ Kuwa katika hatari ya kupata kansa au saratani mbali mbali kama vile; Lymphoma, Leukemia, Myeloma n.k


MATIBABU YA UGONJWA WA GAUCHER


- Ugonjwa huu huweza kuhusisha matibabu mbali mbali kama vile;


• Huduma ya Enzyme replacement therapy


• Matumizi ya Dawa mbali mbali kama vile; Cerdelga, Zavesca n.k


• Huduma ya Upasuaji

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYIAAfyaclass Bongo Social •

 DAWA ZA KULEVYIA

• • • • • •

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYIA


Madhara ya kutumia madawa ya kulevyia ni mengi sana ambapo huweza kumpata mtu moja kwa moja au jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla,


Hapa tunazungumzia madawa kama heroin, bangi,kokeini n.k


Kuna madhara ya muda mfupi na kuna madhara ya muda mrefu au yakudumu,


1. MADHARA YA MUDA MFUPI NI PAMOJA NA;


- Hamu ya chakula kupotea kabsa kwa baadhi ya waathiriwa wa madawa ya kulevyia


- Na kwa baadhi yao hamu ya chakula huongezeka na kula kupita kawaida


- Mtu kukosa usingizi kabsa


- Kupatwa na tatizo la mapigo ya moyo kwenda mbio mara kwa mara


- Kuwa na tatizo katika matamshi ya baadhi ya maneno wakati wa kuongea


- Mwili kutetemeka ikiwa ni pamoja na mdomo,mikono n.k


- Kuwa na mahusiano mabaya katika jamii,familia,ndoa kuvunjika n.k



2. MADHARA YA MUDA MREFU NI PAMOJA NA;


- Mwili kuwa dhoofu,kukosa nguvu na mtu kukonda kupita kawaida


- Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa UKIMWI


- kuwa katika hatari ya kupatwa na kansa au saratani mbali mbali kama vile; saratani ya ngozi, Koo,mapafu n.k


- Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na moyo kuwa mkubwa,mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba n.k


- Kupatwa na tatizo la Figo kufeli au kushindwa kufanya kazi


- Kupatwa na tatizo la mapafu ikiwa ni pamoja na mapafu kujaa maji, vifuko vya hewa yaani Alveoli ndani ya mapafu kutoboka n.k


- Kupatwa na magonjwa ya ubongo, matatizo ya akili,mtu kuchanganyikiwa n.k


- Kufanya maamuzi mabaya kama vile kujiua au kuua mtu mwingine


- Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya Ini,ikiwa ni pamoja na Ini kuvimba, Ini kushindwa kufanya kazi n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

Fahamu kuhusu FAIDA za KICHWA CHA SAMAKIAfyaclass Bongo Social •

    SAMAKI

• • • • •

Fahamu kuhusu FAIDA za KICHWA CHA SAMAKI


Watu wengi hawajui kwamba kichwa cha samaki kina faida kubwa sana, na wengi wao hula minofu ya samaki na Kutupa kichwa chake,


Bila shaka wewe ni miongoni mwao ambao hawajui kabsa faida za kichwa cha Samaki na huenda kila siku ukila samaki unakitupa,


FAIDA ZA KICHWA CHA SAMAKI


- Kichwa cha Samaki kina nyongeza kubwa ya ACID YA OMEGA-3, vitamin A, Pamoja na Madini ya Chuma,ZINC na CALCIUM Kuliko kiwili wili chake,


hivo virutubisho hivi vingi vipo kwenye kichwa cha Samaki kuliko sehemu nyingine yoyote,


Usitupe kichwa cha samaki, virutubisho vingi vipo hapo kuliko hata minofu ya kiwili wili chake unachokikimbilia(cc:afyainfo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Tofauti kati ya Dawa za Minyoo za ALBENDAZOLE na MEBENDAZOLEAfyaclass Bongo Social •

  DAWA ZA MINYOO

• • • • •

Tofauti kati ya Dawa za Minyoo za ALBENDAZOLE na MEBENDAZOLE


Katika makala hii tunachambua kuhusu tofauti iliyopo kwenye hizi aina mbili za dawa za minyoo;


1. ALBENDAZOLE


- Hii ni dawa ya minyoo ambayo hutibu vizuri maambukizi ya minyoo jamii ya TAPEWORMS, neurocysticercosis, giardiasis,trichuriasis n.k


- Maudhi madogo madogo yanayoweza kutokea  kwa baadhi ya watu baada ya kutumia dawa hizi ni pamoja na; kuhisi kichefuchefu, maumivu ya tumbo na maumivu ya kichwa


- Dawa ya Minyoo aina ya ALBENDAZOLE hufanya kazi vizuri sana juu ya maambukizi ya Minyoo jamii ya Tapeworms au Flatworms, Nematodes, Giardiasis, Microsporidiosis,granulomatous,amoebic encephalitis,Arthropods n.k


- Dawa hizi sio salama kwa MAMA MJAMZITO hasa katika miezi mitatu ya mwanzoni ya ujauzito yaani FIRST TRIMESTER kwani huweza kusababisha madhara katika uumbaji wa mtoto yaani Teratogenic effects


2. MEBENDAZOLE


- Dawa hizi kufanya kazi vizuri sana dhidi ya minyoo jamii ya PARASITIC WORMS kama vile; HOOKWORMS, Ascariasis, Pinworm N.k


- Dawa hizi ni salama kwa MAMA MJAMZITO, hivo huweza kutumiwa na mama akiwa na mimba


- Maudhi madogo madogo ambayo huweza kuwapata baadhi ya watu baada ya kutumia dawa hizi ni pamoja na; Kupata maumivu ya tumbo


- Dawa hizi ni salama kwa watoto kuanzia miaka 2


- Dawa hizi sio salama sana kwa Watu wenye umri mkubwa au wazee pamoja na watoto kuanzia umri wa miezi 6 mpaka miaka 2


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)Afyaclass Bongo Social •

   FETAL ALCOHOL SYNDROME

• • • • •

MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)


Matatizo ambayo huweza kumpata mtoto baada ya mama kunywa pombe wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalam kama Fetal alcohol syndrome,


Madhara ya mama mjamzito kunywa pombe sio kwa mtoto tu aliyetumboni hata kwa mama mwenyewe, ila katika makala hii tunachambua kwa kina madhara kwa mtoto baada ya mama kunywa pombe wakati wa ujauzito


MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)


- Tatizo la kuharibika kwa ubongo yaani brain damage


- Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo sana


- Mtoto kudumaa au kuchelewa kwenye kila hatua ya ukuaji


- Mtoto kuwa na macho madogo sana kuliko kawaida


- Lips za juu kwenye mdomo kuwa nyembamba


- Kuwa na pua fupi na ambayo imegeukia juu


- Kuwa na matatizo ya joints


- Kuwa na matatizo ya macho ikiwa ni pamoja na shida ya macho kuona


- Kuwa na matatizo ya kutokusikia vizuri


- Mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo sana


- Kuwa na matatizo ya figo


- Kuwa na matatizo ya moyo


- Ngozi ambayo huunganisha pua na lips za juu ya mdomo kuwa nyembamba na laini sana


- Kuwa na tatizo la kusahau vitu haraka au kupoteza kumbukumbu


- Kubadilika mood kwa haraka zaidi


- Kuwa mtu wa kufanya maamuzi ya haraka na ambayo sio sahihi

n.k


CHANZO CHA TATIZO


• Baada ya mama mjamzito kunywa pombe, Pombe huingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu na kupita kwenda kwa mtoto kupitia kwenye kondo la nyuma au placenta, kisha huanza kuleta madhara mbali mbali kwa mtoto kama nilivyokwisha kuelezea hapo juu,


Baada ya pombe kuingia kwenye damu  ambayo huenda moja kwa moja kwa mtoto huathiri usafirishaji wa hewa safi ya OXYGEN kwenda kwa mtoto pamoja na usafirishaji wa virutubisho muhimu kwa mtoto yaani nutrients,


Pombe huanza kuharibu tissu pamoja na viungo mbali mbali vya mtoto ikiwa ni pamoja na kuharibu kabsa Ubongo wake



KUMBUKA; Tatizo la Fetal Alcohol syndrome halina tiba, hivo ni muhimu sana mama mjamzito kuepuka matumizi ya pombe


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

MADHARA YA MTOTO KUNYWA MAJI YA UCHUNGU AU UZAZIAfyaclass Bongo Social •


MAJI YA UZAZI

• • • • •

MADHARA YA MTOTO KUNYWA MAJI YA UCHUNGU AU UZAZI

Moja ya ishara ya tatizo hili ni mtoto kutokulia baada ya kuzaliwa

Baada ya mtoto kunywa maji ya uchungu au uzazi wakati wa kuzaliwa huweza kupata madhara mbali mbali kama vile;

1. Kuziba kwa njia ya hewa ambayo huweza kusababisha tatizo la upungufu wa oxygen kwenye ubongo

2. Kuwa na matatizo ya ubongo

3. Kuwa na tatizo la upumuaji

4. Kuwa na tatizo la mapafu 

5. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa baada ya mtoto kunywa maji ya uzazi ambayo yamechanganyika na kinyesi kwa kitaalam hujulikana kama meconium

6. Kupatwa na tatizo la kukakamaa mwili

7. Kulegea viungo mbali mbali vya mwili

8. Kuwa na tatizo la kuharisha 

9. Kuwa na tatizo la kutapika

10. Mtoto kupatwa na tatizo la Pneumonia

N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Maji haya ya Uzazi hufanya kazi muhimu wakati Mtoto anakua kwenye uterasi ya mama yake.  Majimaji haya humkinga mtoto anayekua dhidi ya matuta na mapigo kwa mwili wa mama. Maji haya yanakuza ukuaji wa misuli na mifupa.  Na, wakati mwingine mtoto akimeza ndani ya tumbo, maji ya amniotic husaidia njia ya utumbo wa mtoto kuendelea vizuri.

 Kwa bahati mbaya, ikiwa mtoto huvuta maji ya amniotic wakati wa mchakato wa kuzaliwa, matatizo makubwa yanaweza kutokea.  Kupitisha maji haya kwenye bomba la upepo au mapafu kwa bahati mbaya huweza kusababisha tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama aspiration, and amniotic fluid aspiration, Na hali hii huweza kusababisha matatizo makubwa ikiwa haitatambuliwa na kutibiwa mara moja.

Jinsi ya Kugundua Kwamba Mtoto amekunywa Maji ya Uzazi

Kupitia Dalili Mbali mbali ikiwemo hizi;
  • Mtoto kupata Shida ya Kupumua
  • Mtoto kukoroma sana
  • Mtoto kuwa na kikohozi ambacho hakiishi
  • Kupatwa na tatizo la kukakamaa mwili 
  • Kuwa na tatizo la kutapika
  • Kuwa na tatizo la kuharisha 
  • Kulegea viungo mbali mbali vya mwili n.k

Wafanyikazi wa Afya wanaweza kugundua tatizo la meconium aspiration kwa kuangalia kiowevu cha amniotiki wakati wa kuzaliwa ikiwa kuna uwepo wa meconium. 

 X-ray ya kifua pia inaweza kufanywa.  Mtoto ambaye amekunywa meconium anaweza kuwa na shida ya kupumua, au kupumua haraka;  kutoa sauti au kelele za gurgling wakati wa kupumua;  shida inayoonekana wakati wa kupumua au kuonekana kuwa na kifua kilichojaa;  au kuwa na rangi ya tofauti kwenye ngozi na kucha.

Kunywa meconium ni hali ambayo hutokea kwa idadi ndogo ya watoto wanaozaliwa,Ila  Inapotokea, inaweza kutishia maisha yao.

Meconium, kama ilivyo kwa kinyesi chochote, ina bakteria ambayo, ikiwa haitatibiwa mara moja, inaweza kusababisha nimonia kukua.  Katika baadhi ya matukio, nimonia inaweza kusababishwa na maambukizi ya virusi, lakini visa vingi vya nimonia kwa watoto wachanga ni maambukizi ya bakteria.

 Nini cha Kufanya Ikiwa Mtoto kanywa Maji ya Uchungu au Uzazi?

 Ikiwa mtoto anashukiwa kunywa maji ya Uzazi anaweza kupewa dawa mbali mbali ikiwemo jamii ya antibiotics.  Kwa sababu mtoto mchanga anaweza kuwa na mfumo mdogo au Dhaifu wa kinga, antibiotics inaweza kuwa msaada muhimu.  

Ikihitajika, wataalam wa Afya wanaweza kumweka mtoto kwenye kipumuaji ili kupunguza mzigo kwenye mapafu ya mtoto mchanga na kuleta utulivu wa kupumua.

 Oksijeni pia inaweza kuhitaji kusimamiwa.  Katika hali mbaya zaidi, mtoto anaweza kuhitaji oksijeni ya membrane ya nje (ECMO) kusaidia au kuchukua nafasi ya utendakazi wa mapafu.

 Wakati mwingine inawezekana kuzuia mtoto kunywa maji ya Uzazi yenye meconium.  Kwa mfano, ikiwa wafanyakazi wa Afya wanashuku kuwa kiowevu cha amniotiki kina meconium, wanaweza kuagiza utiaji amnioin wakati wa leba, ambayo inaruhusu kiowevu kilicho na meconium kutolewa.

Lakini kwa Hali Flani,matibabu ya Upasuaji kwa Ajili ya mama kujifungua(C-section) inaweza pia kufaa Zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

3 Comment

Madhara ya kutumia dawa za Kujikondesha au kupunguza unene na uzito mkubwa(Diet pills)Afyaclass Bongo Social •

   DIET PILLS

• • • • • •

Madhara ya kutumia dawa za Kujikondesha au kupunguza unene na uzito mkubwa(Diet pills)


Kulingana na dawa ulizotumia, Baadhi ya dawa ambazo hutumika kwa lengo la kupunguza unene na uzito mkubwa kwa mtu, ambazo ni maarufu kama Diet pills huweza kusababisha madhara mbali mbali mwilini kama vile;


1. mtu Kupatwa na tatizo la tumbo kujaa gesi au tatizo la bloating


2. Mtu Kupatwa na tatizo la kuanza kuharisha


3. Mtu Kupatwa na tatizo la kukosa usingizi kabsa


4. Mtu Kujisaidia kinyesi kama chenye mafuta yaani Oily stool


5. Mtu Kupatwa na kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara


6. Mtu kupatwa na tatizo la Kushuka kwa presha ya mwili


7. Mtu kupatwa na tatizo la choo kigumu


8. Mtu kupatwa na maumivu makali ya kichwa mara kwa mara


9. Mtu kupatwa na tatizo la kizunguzungu


10. Mtu kupatwa na shida ya kukauka sana mdomo


11. Mtu kupatwa na maumivu makali ya tumbo


12. Kuathiriwa kwa mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula mwilini hasa vyakula jamii ya mafuta au Fat


13. Kupatwa na tatizo la presha kuwa juu sana


14. Kupatwa na matatizo ya kutokuona vizuri


15. Kusababisha matatizo ya figo


16. Kusababisha matatizo mbali mbali ya moyo

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UGONJWA WA SELI MUNDU AU SICKLE CELL pamoja na Madhara yakeAfyaclass Bongo Social •

 SICKLE CELL

• • • • • •

UGONJWA WA SELI MUNDU AU SICKLE CELL pamoja na Madhara yake


Ugonjwa wa seli Mundu au sickle cell kama inavyofahamika kwa wengi, ni ugonjwa ambao huathiri Haemoglobin, sehemu muhimu sana kwenye muundo na ufanisi wa seli nyekundu za damu(Red blood cells)


Sickle cell ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri sana watoto wadogo na kuleta madhara mbali mbali mwilini,


Wakati mwingine mgonjwa wa sickle cell hupatwa na hali ya maumivu makali katika sehemu mbali mbali za mwili wake pamoja na tatizo la kuishiwa na Damu,ikiwa ni pamoja na matatizo mengine kama vile;


1. Matatizo ya kuziba kwa mishipa midogo ya damu (Vaso-occlusive crisis): Kutokana na umbile lake, kiini mundu au sickle cell huwa rahisi sana kuvunjika vunjika pindi zinapopita katika mishipa midogo midogo ya damu.


 Hali hii hupelekea kuziba kwa mishipa ya damu na hivyo kusababisha maumivu makali na kuzuia usambazaji wa oxijeni katika sehemu zilizozibwa, na hivyo kuathiri viungo vingine mwilini.


2. Matatizo ya damu kujilundika kwenye wengu (Splenic sequestration crisis): Katika hatua hii, wengu huathirika na huwa kubwa kuliko kawaida na pia huwa na maumivu makali.


 Hukusanya damu nyingi na kuvunja chembe nyekundu zote zilizoathirika na kusababisha upungufu wa ghafla wa damu mwilini.


3. Matatizo ya kupungua kwa damu (Aplastic crisis): Katika hatua hii, upungufu wa damu huzidi kuongezeka na kusababisha, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi zaidi na hivyo kuvuruga kitendo cha kutengeneza chembe chembe nyekundu za damu au erythropoeisis kwa kuvamia na kuharibu vyanzo vyake.


4. Matatizo ya kuvunjwa vunjwa kwa chembe nyekundu za damu (Hemolytic crisis): Katika hatua hii, chembe chembe nyekundu za damu huvunjwa kwa wingi zaidi na kusababisha upungufu mkubwa wa damu.


5. Matatizo ya maumivu katika viganja (Dactylitis): Maumivu katika viganja vya mikono na miguuni hutokea mara nyingi kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita na zaidi.


6. Matatizo ya ghafla ya kifua (Acute chest syndrome): Katika ali hii, mgonjwa hupata homa, maumivu makali ya kifua, ushindwa kupumua vizuri, na iwapo mgonjwa atafanyiwa kipimo cha x-ray ya mapafu, kipimo kitaonesha mabadiliko yasiyo ya kawaida (pulmonary infiltrates). Cr: Drtareeq




0 Comment

Tatizo la mtoto kuchemka au Kuwa na homaAfyaclass Bongo Social •

 HOMA

• • • • • •

Tatizo la mtoto kuchemka au kuwa na homa


Joto la mtoto huweza kuwa juu sana au mtoto kuwa na homa na wengine hutumia kiswahili cha mtoto kuchemka. Hali hii ni pale ambapo joto la mtoto ni kuanzia nyuzi joto 38 na kuendelea.


wataalam wa afya hushauri mtoto kupimwa joto lake la mwili mara kwa mara ili kujua joto lake halisi akiwa katika hali yake ya kawaida,


SABABU ZA JOTO LA MTOTO KUWA JUU


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia joto la mtoto kuwa juu kama vile;


1. Mtoto kuwa na tatizo la upungufu wa maji ya mwili


2. Mtoto kuvalishwa nguo nyingi na nzito wakati wa joto,


Inashauriwa kwamba mtoto hutakiwa kuvaa nguo mara mbili zaidi yako ulivyovyaa kulingana na hali ya mazingira ilivyo,


mfano; Kama wewe ukivaa nguo tatu kutokana na hali ya hewa ilivyo unajisikia vizuri,basi mtoto mvalishe nguo nne, kama wewe umevaa mbili yeye avae tatu, kama wewe umevaa mbili basi yeye avae tatu.


3. Joto la mtoto huweza kuwa juu tokana na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Virusi n.k


4. N.k


Hata hivo tatizo la mtoto kuwa na homa katika umri mdogo sana sio dalili nzuri, hivo mtoto huyu huhitaji uchunguzi wa kina kutoka kwa wataalam wa afya


✓ FAHAMU; Mwili kupandisha joto kukiwa na mashambulizi ya magonjwa husaidia mwili kupambana na maambukizi hayo pamoja na kuwa rahisi sana kwa Bacteria au Virusi ambao hawapendi mazingira ya joto kuharibiwa na Mfumo wa kinga ya mwili wako.


KWA USHAURI  ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA  +255758286584.




0 Comment

Mabadiliko ambayo mwanaume huyapata Baada ya mke wake kuwa Mjamzito(HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI)Afyaclass Bongo Social •

happy father's day

• • • • • •

Mabadiliko ambayo mwanaume huyapata Baada ya mke wake kuwa Mjamzito(HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI)


Japo akina baba wengi huonekana kutojihusisha sana na ujauzito, ukweli ni kuwa wanajali japo wengi wao hawaoneshi dhahiri. Mama humbeba mtoto tumboni ila BABA HUMBEBA MTOTO KICHWANI NDANI YA MAWAZO YAKE. 


Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Michigan ulioongozwa na Prof. Robin Edelstein unaeleza kuwa baadhi ya wanaume hupitia mabadiliko ya homoni (hormonal changes) kipindi wenza wao wanapokuwa wajawazito, kwa homoni ya kiume ya Testosterone kushuka kama vile inavyokuwa kwa wenza wao. 


Prof huyo anaeleza kuwa hakuna ushahidi kwa nini wanaume pia hupungua homoni hiyo kama wenza wao lakini anahusisha na wazo kuwa: 


Wanaume hao ni wale wenye kuwajali zaidi wenza wao (better caregivers) kwa kuwa hupunguza ukali (aggressiveness) unaohusishwa na kiwango cha juu cha homo hiyo. 


HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI!!!

Cr:afyabongo




0 Comment

TATIZO LA KUVIMBA MAGOTI(chanzo,dalili na Tiba)Afyaclass Bongo Social •

 MAGOTI KUVIMBA

• • • • • •

TATIZO LA KUVIMBA MAGOTI(chanzo,dalili na Tiba)


Tatizo la kuvimba magoti huwapata watu wengi kutokana na sababu mbali mbali na hapa nitofautishe na tatizo la kuvimba miguu yote, hapa nazungumzia kuvimba sehemu ya magoti tu, lakini kwa asilimia kubwa husababishwa na maji mengi kujikusanya ndani ya magoti kutokana na vyanzo mbali mbali kama vile;


✓ Mtu kuumia


✓ Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile;


• OSTEOARTHRITIS


• RHEUMATOID ARTHRITIS


• TATIZO LA GOUT


• TATIZO LA PSEUDOGOUT


• Tatizo la BURSITIS


• Tatizo la Cysts


• TATIZO LA TUMORS


N.K


DALILI ZA TATIZO HILI LA KUVIMBA MAGOTI NI PAMOJA NA;


- Kupata maumivu makali eneo la goti


- Goti kukakamaa


- Hatimaye Goti kuvimba


MATIBABU YA KUVIMBA KWA GOTI


• Tatizo hili hutibika kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na Dawa pamoja na huduma ya Upasuaji kulingana na chanzo cha tatizo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAJI NI MUHIMU SANA KWA MAMA MJAMZITOAfyaclass Bongo Social •

 MJAMZITO

• • • • • •

MAJI NI MUHIMU SANA KWA MAMA MJAMZITO


Maji ni muhimu kwa mjamzito , na mahitaji ya maji huongezeka pia unapokua mjamzito . Kwahiyo kunywa maji ya kutosha kadiri unavyojisikia kiu au uhitaji

.

.

Pia vinywaji vingine salama na vizuri kwa mjamzito ni kama vile juice ya limao , maziwa, juice ya matunda , juice ya mbogamboga (mfano juice ya karoti 🥕)

.

Juice ya limao itakusaidia kupunguza pia hali ya kujisikia kichefuchefu na kutapika,  ijaribu uone 🤝

.

.

 Epuka kunywa pombe , energy drinks , juice mimea tiba asili ( Labda kama upo katika uangalizi au daktari wako anafahamu - Ni rahisi sana ujauzito wako kupata madhara , endapo hamna uthibitisho wowote wa viwango unavyotumia )


#afyasolution




0 Comment

Dawa za Kukausha kidonda,kuzuia maambukizi Na SABABU za Kidonda Kutokupona HarakaAfyaclass Bongo Social •

KIDONDA

• • • • • •

Dawa za Kukausha kidonda,kuzuia maambukizi Na SABABU za Kidonda Kutokupona Haraka

SABABU ZA KIDONDA KUCHELEWA KUPONA

Tukianzia hapa, kuna baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huzuia kidonda kupona kwa haraka au kuchelewesha vidonda kupona au kusababisha vidonda kutokupona kabsa,na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;

1. Mtu kuwa na tatizo la sukari

2. Mtu kuwa na kinga ya mwili ndogo huweza kusababisha kidonda kuendelea kushambuliwa zaidi

3. Kuwa na mzunguko wa damu mbaya hasa kuzunguka eneo la kidonda yaani poor blood circulation

4. Kuwa na tatizo la unene au uzito kupita kawaida au Obesity

5. Eneo la Kidonda kutokufanyiwa usafi

6. Mtu kupata kidonda katika umri mkubwa

7. Lishe duni

8. Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu na kutokufanya mazoezi yoyote

N.k

DALILI ZA KIDONDA AMBACHO KIMESHAMBULIWA NA VIMELEA VYA MAGONJWA KAMA BACTERIA N.K

- kidonda kutoa usaha muda wote

- kidonda kutoa harufu mbaya

- Rangi ya kidonda pamoja na ngozi kuzunguka kidonda kuwa na rangi ya njano

- Kidonda kukusababishia homa mara kwa mara

N.K

DAWA ZA KUKAUSHA KIDONDA,KUZUIA PAMOJA NA KUTIBU MAAMBUKIZI KWENYE KIDONDA

Zipo dawa mbali mbali kwa ajili ya Kukausha, kuzuia na kutibu maambukizi kwenye kidonda na tatizo lako likaisha kabsa.

Kama Una Tatizo hili na bado hujapata Msaada kabsa;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUCHELEWA KUONGEA HADI KUFIKIA MIAKA 3 NA KUENDELEAAfyaclass Bongo Social •

  MTOTO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUCHELEWA KUONGEA HADI KUFIKIA MIAKA 3 NA KUENDELEA


Kuna baadhi ya watoto hupatwa na tatizo hili la kuchelewa kuongea kupita kawaida hadi kufikia umri wa Miaka 3 na zaidi bado mtoto hajaanza kuongea.


Je tatizo hili husababishwa na kitu gani? au chanzo ni nini?


CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUCHELEWA KUONGEA HADI KUFIKIA MIAKA 3 NA KUENDELEA


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia tatizo hili kama vile;


1. Mtoto kupatwa na matatizo mdomoni au kwenye Ulimi kama vile; Tatizo la Tongue-Tie ambapo ulimi wa mtoto umeunganika na kujishikiza kwa chini ya mdomo n.k


2. Kuwa na tatizo la Ubongo kushindwa kujifunza lugha kwa haraka


3. Kuwa na matatizo ya kutokusikia, Asilimia kubwa ya watoto wenye matatizo ya kutokusikia vizuri, hata kuongea pia huchelewa zaidi


4. Kuwa na matatizo kama vile; Autism Spectrum disorder


5. Kuwa na matatizo kwenye mfumo wa fahamu kama vile; Cerebral palsy n.k


6. Kuumia ubongo kwa sababu mbali mbali kama vile kuanguka n.k hali ambayo kitaalam hujulikana kama Traumatic brain Injury


N.K


Hizo ni baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia tatizo la mtoto kuchelewa sana kuongea


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

MBILIKIMO NI UGONJWA AU NI NINI?(soma hapa kujua)Afyaclass Bongo Social •

   MBILIKIMO

• • • • • •

MBILIKIMO NI UGONJWA AU NI NINI?(soma hapa kujua)


Mbilikimo kwa hali ya kawaida ni watu wafupi sana kupita kawaida, Watu hawa wamekuwa maarufu sana katika maeneo mbali mbali kama vile KONGO(DRC) n.k kutokana na ufupi wao. 


Mbilikimo wamegawanyika kwa aina mbili;


- Kuna mbilikimo kutokana na asili ya watu wa jamii flani katika maeneo mbali mbali duniani


- Na kuna mbilikimo kama ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Dwarfism.


JE UGONJWA WA DWARFISM AU MBILIKIMO NI NINI?


Hili ni tatizo ambalo husababisha mtu kuwa mfupi sana kupita kawaida kutokana na sababu mbali mbali kama vile za vinasaba au Genetics na matatizo mengine ya kiafya.


Watu wenye tatizo la dwarfism huwa wafupi sana kwa kiwango cha chini au sawa na Cm 147,122 n.k ukipima urefu wao.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA DWARFISM


- Asilimia kubwa ya watu wenye tatizo la Dwarfism hutokana na shida ya achondroplasia


- Tatizo lingine ni Turner syndrome,ambapo mwanamke huzaliwa huku akiwa hana chromosome moja(X), hivo badala ya kuwa na chromosome mbili (XX) kama wanawake wengine, humiss chromosome moja ya X.


- Matatizo ya vichocheo mwilini hasa vichocheo vinavyohusika na ukuaji wa mtu kuwa pungufu yaani Growth hormone deficiency

N.k



MATIBABU YA TATIZO HILI


- Hakuna tiba ya kuongeza Urefu wa mtu bali kuna Matibabu juu ya dalili mbaya ambazo huweza kumpata mtu mwenye shida hii kama vile; Kushindwa kutembea,kuongea vizuri, maumivu ya viungo N.k


Tiba hiyo huweza kuhusisha kuongeza kiwango cha vichocheo mwilini yaani Hormonal therapy, matibabu ya Upasuaji N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Ugonjwa wa Kuvimba kwa Ini,Chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

 INI

• • • • •

Ugonjwa wa Kuvimba kwa Ini,Chanzo,dalili na Tiba yake


Ini ni miongoni mwa viungo ambavyo hufanya kazi nyingi kuliko viungo vingine mwilini, Katika makala hii tunazungumzia matatizo ambayo huweza kukumba Ini lako ikiwa ni pamoja na tatizo la kuvimba kwa Ini.


CHANZO CHA KUVIMBA KWA INI PAMOJA NA MATATIZO MENGINE YA INI


- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwa ni Pamoja na mashambulizi ya VIRUSI kama vile; Hepatitis Virus A,B,C n.k


- Matatizo katika mfumo wa kinga ya mwili kama vile;Primary Biliary Cholangitis, Autoimmune hepatitis n.k


- Matatizo ya kigenetics kama vile; Wilson's disease, Hemochromatosis n.k


- Aina mbali mbali za kansa au Saratani kama vile; Saratani ya Ini, Saratani ya mrija wa nyongo yaani Bile duct cancer n.k


- Matumizi ya pombe kupita kiasi


- Mafuta kujikusanya kwa kiwango kikubwa kwenye Ini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ya Unene kupita kawaida

N.k


DALILI ZA  KUVIMBA KWA INI PAMOJA NA MATATIZO MENGINE YA INI NI PAMOJA NA;


1. Macho pamoja na ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa manjano ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Jaundice


2. Kuwa na tatizo la kuvimba miguu


3. Kuwa na tatizo la kuwashwa mwilini


4. Kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi


5. Kujisaidia kinyesi ambacho hakina rangi yake ya kawaida au tunasema pale stool color


6. Kupata uchovu wa mwili ambao hauishi


7. Kukosa kabsa hamu ya chakula


8. Kuwa na tatizo la kichefuchefu pamoja na Kutapika

N.K


MATIBABU YA MATATIZO YA INI


Tiba ya matatizo ya Ini hutegemea na chanzo chake,hivo kama una dalili hizi ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya vipimo pamoja na Matibabu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

KUPEVUSHWA KWA YAI/MAYAI au Ovulation(Kwa Wanawake)Afyaclass Bongo Social •

 OVULATION

• • • • •

KUPEVUSHWA KWA YAI au Ovulation(Kwa Wanawake)


Kupevushwa kwa yai, ni pale ambapo yai hutoka kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries na kuingia kwenye mirija ya uzazi ambayo hujulikana kwa kitaalam kama fallopian tubes, kitendo hiki ndyo kinaitwa OVULATION.


FAHAMU BAADHI YA MAMBO KUHUSU UPEVUSHAJI WA MAYAI AU OVULATION


1. Upevushaji wa mayai huhusiana na yai kutoka kwenye vifuko(ovaries) vyake kwenda kwenye mirija ya uzazi


2. Upevushaji wa mayai au Ovulation hutokea siku ya 14 kwa Wanawake wenye mzunguko wa siku 28


3. Ili mwanamke apate mimba lazima upevushaji wa mayai utokee


4. Kuna baadhi ya wanawake wenye matatizo ya mayai kutokupevushwa kabsa au kutokupevushwa kwa wakati


5. Mwanamke huweza kupevusha mayai mawili kwa wakati mmoja yaani kutoka ovary ya kulia na kushoto japo ni mara chache kutokea, hapa ndipo mapacha wasio Fanana huweza kupatikana yaani Fraternal twins baada ya urutubishaji wa mayai yote mawili


6. Baada ya mayai kutoka kwenye vifuko vyake(ovaries) huingia kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes, Na endapo mwanamke akafanya mapenzi na mwanaume kipindi hiki huweza kupata ujauzito


7. Kama urutubishaji wa yai umeshatokea,moja kwa moja kiumbe huenda kujishikiza kwenye kuta za mji wa mimba kitendo ambacho hujulikana kama Implantation na kuendelea kukua mpaka mtoto azaliwe,


Na kama urutubishaji haukutokea basi yai lile huharibika na kutoka kwa Njia ya HEDHI au period.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

KITU AMBACHO HUKIJUI KUHUSU UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI(Golden test)Afyaclass Bongo Social •

  UKIMWI

• • • • •

KITU AMBACHO HUKIJUI KUHUSU UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI(Golden test)


Fahamu kwamba upimaji wa virusi vya Ukimwi huhusisha hatua Kuu Mbili, na hatua hizi mbili huhusisha vipimo viwili Tofauti, 


UPIMAJI HATUA YA KWANZA


- Upimaji hatua ya kwanza huhusisha kipimo ambacho hujulikana kama RAPID TEST,


ambapo mtu hupimwa kwa mara ya kwanza afikapo Hospitalini au kituo chochote cha afya,


ENDAPO; majibu ni NEGATIVE, basi mtu huyu hushauriwa kurudi baada ya Kipindi cha MIEZI 3 ili kurudia vipimo, kwani maambukizi mapya huonekana baada ya miezi 3 kwa asilimia 98% ya Wagonjwa


ENDAPO; majibu ni POSTIVE kwa kipimo cha Kwanza yaani Rapid Test, Basi mtu huyu huingia hatua ya Pili ya vipimo


UPIMAJI HATUA YA PILI


- Baada ya kipimo cha kwanza(Rapid test) kuonyesha kwamba mtu ni POSITIVE, basi huingia vipimo hatua ya pili


- Vipimo hatua ya pili huhusisha kipimo kinachojulikana kama GOLDEN TEST,


Endapo kipimo hiki kikionyesha POSITIVE tena, basi moja kwa moja mtu huyu ni Muathirika wa Virusi vya Ukimwi


KUMBUKA; Huwezi kusema mtu ni muathirika wa virusi vya ukimwi kwa kipimo kimoja cha Awali, lazima uingie kwenye Confirmatory TEST yaani Golden Test.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

FAHAMU KWA KINA KUHUSU CD4 NA FAIDA ZAKE MWILINIAfyaclass Bongo Social •

 CD4

• • • • •

FAHAMU KWA KINA KUHUSU CD4 NA FAIDA ZAKE MWILINI


Bila shaka sio Mgeni kuhusu kusikia kitu kinaitwa CD4, Lakini hufahamu kwa kina CD4 ni kitu gani na faida zake ni zipi. Soma hapa kujua zaidi..!!!


CD4 NI NINI?


CD4 ni kifupi cha maneno haya "Cluster of differentiation 4" ambapo maana yake halisi, tunazungumzia kuhusu Aina ya Glycoprotein ambayo hupatikana kwenye seli za kinga ya mwili au kwa lugha nyingine seli nyeupe za damu(WHITE BLOOD CELLS),


Kama vile; T-helper cells, monocytes, macrophages, Dendritic cells n.k


CD4 zimegundulika miaka ya 1970 ambapo zilikuwa zinajulikana kama Leu-3 na T4 ndani ya mwili wa binadamu kama ilivyokuwa inajulikana sana ndani ya miaka ya 1984


FAIDA YA CD4 MWILINI


CD4 cells ni sehemu ya white Blood cells ambazo kazi yake kubwa ni kuhakikisha Kinga ya mwili Inaimarika yaani Health body immune system na kusaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali


JE UNATAKIWA UWE NA SELI ZA CD4 KIASI GANI MWILINI?(CD4 COUNT)


- Kwa mtu ambaye ana afya njema anatakiwa awe na CD4 seli kuanzia 500 mpaka 1,400 per Cubic millimeter za damu


- Kuwa na kiwango cha chini ya seli 200  per cubic millimeter za damu upo kwenye hatari ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali mwilini,kwani mwili wako utakuwa hauna kinga ya kutosha ya kupambana na magonjwa mbali mbali.


KUMBUKA;


✓ Kwa mtu ambaye ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI kama hatumii dawa yaani ART, seli hizi huendelea kupungua kwa kiwango kikubwa sana, na kumuweka kwenye hatari ya kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa


✓ CD4 count huweza kushuka chinu kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


• Maambukizi ya magonjwa kama HIV


• Matumizi ya baadhi ya dawa

N.k


NA tatizo la LEUKOPENIA hupunguza CD4 count lakini kwa tatizo kama LEUKOCYTOSIS huongeza sana CD4 count.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAZIKO YA KISAYANSI-CAPSULA MUNDI-MWILI WAKO KUGEUKA MTI BAADA YA KUFAAfyaclass Bongo Social •

FAHAMU

• • • • •

MAZIKO YA KISAYANSI-CAPSULA MUNDI-MWILI WAKO KUGEUKA MTI BAADA YA KUFA



U hali gani mdau wangu,leo nataka nishee na  wewe jambo moja na la muhimu sana kwa ulimwengu wetu na jambo lenyewe ni kuhusu kuzikwa bila jeneza na kugeuka mti baada ya kufa


Kama sote tujuavyo binadamu hufariki kila siku,huzikwa na wengine huzaliwa. Kumekua na taratibu za kuzika mwili ardhini kwa kutumia majeneza nk,kwa ndugu zetu wahindi wamekua wakichoma mwiliKuzika mwili kwenye majeneza kumekua hakuleti faida kwa jamii iliyobaki na san asana imekua ikichukua nafasi za ardhi ambayo hutumika kama makaburi;


ambayo ingekua na faida nyingine kwa viumbe walio hai.Ikumbukwe kwamba binadamu anapokufa mwili wake unakua una virutubisho vingi sana na ambavyo tunapoufukia mwili chini tunakua tumepoteza au kupata hasara kubwa kwani tutakua hatujapata faida za kimazingira kutokana na huo mwili


Kwa sasa kuna teknolojia ya capsula mundi ambayo binadamu aliefariji huwekwa kwenye mfuko maalumu wenye umbo la yai na ndipo huchimbiwa ardhini k pamoja na kuweka mbegu ya mti.


 Mwili huo unapokua unaoza kwa msaada wa bacteria basi mti utakaokua unaota hapo basi hunawiri na kukua vizuri kwani ule mwili utakua ni mbolea tosha yenye virutubisho vyote.


kadhalika heshima ya aliezikwa na kua mti itaendelea kuwepo na ndugu wataendelea kutoa heshima zao sema kwa sasa watakua wanatembea mashambani na kuona mti uliotokana na mwili wa Fulani.


Hii teknolojia ni nzuri sana kwani kwanza husaidia kulinda mazingira yetu kwa kuongeza idadi ya miti yenye afya,kupunguza hewa ya ukaa duniani,kuongeza kiasi cha hewa safi ya oksijeni,kupunguza madhara ya athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi na hizi faida ni kwa sababu ya miti mingi itakayoota kutokana na miili ya waliokufa. Huu ndo utakua mwisho wa matumizi ya majeneza na mwanzo wa kuongezeka kwa miti ulimwenguni.


Ama kweli hili ni jambo jema sasa,hebu fikiria watu wote walozikwa kwa majeneza wangezikwa kwa teknolojia hii tungekua na miti mingapi yenye afya?,tungepunguza adhari za mabadiliko ya hali ya hewa,tungepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa mvua na ongezeko la joto dunia. Cr:Dr.mathew 




0 Comment

Ugonjwa wa SAFURA,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

   SAFURA

• • • • •

Ugonjwa wa SAFURA,chanzo,dalili na Tiba yake


Ugonjwa wa Safura ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi hasa watoto wadogo.


CHANZO CHA UGONJWA WA SAFURA


- Ugonjwa wa Safura ni ugonjwa ambao husababishwa na Mashambulizi ya Minyoo aina ya HOOKWORMS


DALILI ZA UGONJWA WA SAFURA Ni pamoja na;


✓ Mtu kukosa hamu ya chakula


✓ Baadhi ya watu kula kupita kawaida


✓ Mwili kudhoofika ikiwa ni pamoja na kukonda sana


✓ Mwili kukosa nguvu kabsa


✓ Misuli ya mwili kuwa dhaifu


✓ Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara


✓ Mgonjwa kuharisha mara kwa mara


✓ Kuhisi dalili ya Minyoo njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia


✓ Nywele kunyonyoka zenyewe


✓ Kupata dalili zote za kuishiwa na damu yaani Anemia

N.k



MATIBABU YA UGONJWA WA SAFURA


Ugonjwa huu wa safura hutibiwa kwa dawa mbali mbali,ikiwa ni pamoja na dawa za Minyoo jamii ya Albendazole,mebendazole(kwa wajawazito) N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA KUPIMA MIMBA UPT yaani Urinary pregnancy testAfyaclass Bongo Social •

  UPT

• • • • •

FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA KUPIMA MIMBA UPT yaani Urinary pregnancy test


UPT ni kipimo cha kupima mimba kwa Njia ya mkojo ambapo kirefu chake ni urinary pregnancy test,


Wanawake wengi hutumia kipimo hiki ili kuangalia kwamba wana Mimba au la!


JE KIPIMO HIKI CHA UPT KINAFANYAJE KAZI?


Ufanyaji kazi wa kipimo cha UPT kwenye mkojo hutegemea na Kichocheo au hormone inayojulikana kwa jina la human chorionic gonadotropin(HCG),


Hapa ndipo tunaweza kupata majibu ya aina mbili yaani;


1. Postive/reactive- mwanamke ni mjamzito


2. Negative/non-reactive- au mwanamke sio mjamzito


HUMAN CHORIONIC GONADOTROPIN HORMONE(HCG)


- Hii ni hormone ambayo huzalishwa na Placenta au kondo la nyumba,ndipo baadae huwepo ndani ya Mkojo, 


Na wataalam wanasema hormone hii huzalishwa kutoka kwa Placenta kuanzia siku ya 10,12 N.k Baada ya urutubishaji wa yai.


KUPIMA MIMBA KWA KUTUMIA UPT


- Mwanamke atatumia kipimo cha UPT ambapo ataweka kipimo chake kwenye Mkojo ili kisome,


Na majibu yatakuwa hivi;


1. Endapo mwanamke ni mjamzito na kichocheo cha HCG kimezalishwa na Placenta na kuwepo ndani ya Mkojo, basi majibu yataonyesha MISTARI MIWILI KWENYE KIPIMO au Mistari zaidi ya Mmoja.


2. Na endapo mwanamke sio mjamzito, basi hakuna kichocheo chochote cha HCG ambacho kinaweza kuwepo kwenye mkojo,hivo kipimo kitasoma MSTARI MMOJA TU wa Control.


Ni matumaini yangu kwamba umepata mwanga kuhusu kipimo hiki cha UPT.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD