TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI (Acanthosis nigricans)Afyaclass Bongo Social •

 NGOZI

• • • • •

TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI  (Acanthosis nigricans)


Tatizo la ngozi ya baadhi ya sehemu za mwili kuwa nyeusi zaidi ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama "Acanthosis nigricans" na tatizo hili hutokea sana kwenye maeneo ya SHINGONI,KWENYE KWAPA,NA SEHEMU ZA SIRI.


Mabadiliko haya ya rangi ya ngozi kwa asilimia kubwa huwapata watu wanene,wenye tatizo la kisukari, watoto wadogo ambao wapo kwenye hatari ya kuwa na kisukari yaani type 2 diabetes, na mara chache sana huweza kuwa kama dalili ya saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya ndani ya mwili kama vile ini,tumbo n.k


CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?


- Tatizo la acanthosis nigricans huweza kutokea baada ya Hormone au kichocheo cha INSULIN kushindwa kufanya kazi hali ambayo hupelekea pia kutokea tatizo la kisukari yaani type 2 diabetes.


- Matatizo kwenye vichocheo vya mwili(Hormone disorders) kama vile kichocheo kinachoipa ngozi rangi yake ya asili kuzidi sana yaani Melanini hyperpigmentation kwenye sehemu zilizoathirika na pia kwa watu wenye matatizo kama vile; tatizo la ovarian cysts, matatizo kwenye tezi la thyroid kama vile underactive thyroids au matatizo ya tezi la Adrenaline(adrenal glands).


- Matumizi ya baadhi ya dawa pamoja na virutubisho mfano; Mtu kutumia dose kubwa ya niacin, vidonge vya majira yaani birth control pills, dawa za prednisone pamoja na dawa zingine kama vile dawa jamii ya corticosteroids huweza kusababisha tatizo hili la acanthosis nigricans.


- Na pia kama nilovyosema hapo awali,mara chache sana tatizo hili huweza kuhusishwa na saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya mwili kama vile Ini, Tumbo,utumbo n.k


KUMBUKA; Tatizo hili huwapata sana watu ambao;


• Ni wanene au wenye tatizo la uzito uliopita kiasi


• Wenye magonjwa kama kisukari


• Na wale ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wenye tatizo hili


MATIBABU YA TATIZO HILI LA ACANTHOSIS NIGRICANS


Tatizo hili huhisisha tiba za aina mbali mbali kulingana na chanzo chake,japo kwa ujumla kuna tiba kama vile;


✓ Kupunguza uzito wa mwili kama tatizo hili limetokana na mtu kuwa mnene au na uzito mkubwa


✓ Kuacha matumizi ya dawa ambazo huweza kusababisha tatizo hili


✓ Wengine hufanyiwa mpaka upasuaji ili kuondoa vivimbe au tumors kisha kusaidia ngozi ya mwili irudi kwenye rangi yake ya asili


✓ Lakini pia mtu huweza kutumia dawa mbali mbali kama vile;


   • Cream za kupaka kwenye ngozi


   • Baadhi ya sabuni za kuogea ambazo ni Antibacterial soaps


    • Dawa za kunywa yaani Oral acne medications N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO PAMOJA NA FAIDA ZAKEAfyaclass Bongo Social •

MJAMZITO

• • • • • •

AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO


Nidhahiri kwamba mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito,lakini yapi ni mazoezi salama kwa mama mjamzito,Baadhi ya wakina mama wajawazito hushauriwa sana kuhusu kufanya mazoezi lakini hawaambiwi ni aina gani ya mazoezi ambayo ni salama kwao, Na kama ni hivo basi,kwa tafsri nyingine kuna mazoezi ambayo sio salama kabsa kwa mama mjamzito.


AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO NI PAMOJA NA;


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kutembea


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuogelea au Swimming


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli ambayo imesimama(Riding a stationary bike), hapa nitoe angalizo: ni hatari sana kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli inayotembea hasa ya magurudumu mawili tu,kwani ni rahisi sana kukosa balance na kudondoka hivo kuhatarisha ujauzito aliyobeba.


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya YOGA, mazoezi haya ni mazuri japo yanatakiwa kufanyika chini ya usimamizi wa wataalam yaani Instructor, kwani endapo mama atafanya mazoezi ya Yoga ambayo huhusisha zaidi kulalia Tumbo lake au kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First trimester huweza kuwa sio salama kwake.


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo mbali mbali vya mwili, Wakati wa kufanya mazoezi epuka kunyanyua vitu vizito sana


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kukimbia


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuruka kamba pamoja na vitu vingine mbali mbali, hapa pia ni muhimu kufanya mazoezi haya kwa msaada wa wataalam au Instructor kuhusu jinsi ya kuruka kamba taratibu,kwa sababu wapo ambao wameruka kamba sana na pia wakapata madhara kwenye ujauzito wao.


Hutakiwi kufanya mazoezi ya kuruka sana au kuruka kupita kiasi, hivo uangalifu mkubwa hutakiwa katika aina hii ya mazoezi Pamoja na mazoezi mengine ambayo sikuyataja hapa,


ANGALIZO: zingatia mambo haya wakati unafanya mazoezi


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kugandamiza tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First tremester


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha mtikisiko mkubwa sana wa tumbo


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kunyanyua vitu vizito sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kubana pumzi yako


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kuruka sana kupita kiasi


• Epuka kufanya mazoezi ya kucheza mpira kama vile mpira wa miguu wakati wa ujauzito

 N.k


FAIDA ZA MAMA MJAMZITO KUFANYA MAZOEZI


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia sana kuleta mzunguko mzuri wa damu kwenye mishipa ya damu,kwenye moyo pamoja na mapafu


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia ongezeko la uzito ambao hutakiwa kwa mama mjamzito


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na matatizo mbali mbali kama vile;


   • Kupatwa na tatizo la Kukosa pumzi


   • Kupatwa na tatizo la choo kigumu


   • Kupatwa na tatizo la kiungulia kikali


   • Kupatwa na tatizo la kuvimba miguu 


    • Kupatwa na tatizo la maumivu ya mgongo,misuli ya mwili 


     • Kupatwa na tatizo la mishipa ya damu kuvimba au Varicose veins N.k


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kupata usingizi wakati wa kulala


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa matatizo kama vile kisukari wakati wa ujauzito yaani Gestational diabetes,kifafa cha mimba n.k


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa mama mjamzito kujifungua kwa upasuaji


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia mama kuandaa mwili wake na labor,hata kupelekea urahisi wa mtoto kushuka,njia kufunguka na mama kuwa na pumzi ya kutosha wakati wa kusukuma mtoto.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO(afyatips)Afyaclass Bongo Social •

 TUMBO

• • • • •

JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO(afyatips)


Kwa hivi sasa watu wengi hupambana na njia mbali mbali za kupunguza matumbo yao hasa wadada ili kuonekana warembo zaidi, na kuvaa nguo ipendeze, Hivo basi huwapelekea kutumia njia mbali mbali ili kupunguza tumbo, huku zingine zikiwa sahihi na zingine zikiwa hatari zaidi kwa afya zao. Hapa kuna baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati unahitaji kupunguza tumbo lako,


1. Hakikisha unapendelea zaidi kula vyakula pamoja na matunda yenye nyuzi nyuzi au Fibers kama vile machungwa,maembe,maparachichi n.k


2. Epuka kula vyakula vyenye mafuta zaidi ikiwemo chips


3. Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi


4. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha PROTEIN na sio kiwango kikubwa cha MAFUTA mfano; Maharage n.k


5. Punguza au epuka kabsa kuwa na msongo wa mawazo,watu wengi hawajui kwamba msongo wa mawazo huweza kusababisha tatizo la kuongezeka kwa tumbo au hata uzito kwa baadhi ya watu


6. Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari


7. Fanya mazoezi ya mwili kila siku,angalau kwa dakika 30 au Nusu saa kila siku


8. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kupumzika pamoja na kulala


9. Unaweza kupendelea kula vyakula jamii ya samaki zaidi huku ukiepuka mafuta mengi


10. Japo juice za matunda ni nzuri sana, ila baadhi zina kiwango kikubwa sana cha sukari,hivo epuka juice kama hizi


11. Kunywa chai ya kijani maarufu kama GREEN TEA, najua wengi wenu hamjawahi kusikia hii,ila ipo na watu wanaitumia hivo ulizia itakusaidia pia.


12. Pamoja na Tips zingine za Afya


KUMBUKA; kufunga mkanda tumboni ili tumbo lipungue au kushinda na njaa kila siku huweza kuwa hatari kwako na sio njia salama ya kupunguza tumbo


• Soma pia: Jinsi ya Kupunguza Uzito wa Mwili


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

JINSI YA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI(afyatips)Afyaclass Bongo Social •

UZITO

• • • • •

JINSI YA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI(afyatips)


 Uzito mkubwa ni tatizo kwa watu wengi siku hizi huku baadhi yao wakiwa tayari wameshapata matatizo kwa sababu ya uzito kuzidi mwilini na wengine wakiwa katika harakati mbali mbali za kupunguza uzito, Je kama una tatizo la uzito mkubwa na unataka upungue ufanyeje? soma hapa katika makala hii..!!!


Kupungua uzito kunategemea na kiwango cha mafuta cha mtu mwilini (body fat), uzito wa mtu, calories anazohitaji kwa siku, BMI yake pamoja na lengo la mtu la kupungua uzito. Je vyakula ninavyokula hunipa nguvu (calories) na uwezo wa kumudu majukumu yangu ya kila siku? Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha mafuta mwilini.


Kwa maana hiyo, si kila diet plan humfaa kila mtu, inaweza ikakufaa wewe lakini isimfae mtu mwingine.


Cha kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa lishe (nutritionists), daktari, wataalamu wa mazoezi na nk. Kama utafuatilia diet plan hii, utaona kila siku unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa, ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na  kadhalika. Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu (hypertension), anxiety disorders na nk, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.


• Siku ya Kwanza (Day 1)


Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula chochote. Kwa wale wenye mashine ya tredmill basi pia tembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na spidi ndogo (kama namba 5 na kuongeza hadi spidi namba 8). Unaweza pia kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa. Anza kukimbia kwa spidi ndogo (kwenye tredmill) halafu ongeza spidi yako, au unaweza kukimbia kwa spidi ya juu kama spidi 8 kwa muda wa dakika 5 na kisha kupunguza hadi spidi 5, hii inaitwa interval training, lengo ni kukupa uwezo wa kufikisha dakika 30, kuchoma mafuta mwilini, kupunguza mapigo ya moyo yarudi kwenye kiwango cha kawaida kwani wakati unafanya mazoezi mapigo ya moyo huongezeka sana, kuupa uwezo moyo wako wa kufanya kazi vizuri.


Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo haya kama atrial fibrillation, ventricular tarchycardia na nk, wagonjwa wa pumu, ni vizuri kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi (sports therapist) pamoja na kushauriana na daktari. 


Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) kati ya 15-20. Ukiona ni ngumu sana unaweza kuanza hata na sit-ups 10 na utakuwa unaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na tumbo. 


Unaweza kutumia bench au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati mmoja. Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glasi 4 ziishe. Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini. 


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka kijiko kimoja kidogo cha sukari (2.5ml spoon). Yai moja la kuchemsha. Slice moja ya mkate wa brown bread (mikate inayotengenezwa kwa ngano nzima nzima). Usithubutu kuweka siagi wala vinavyofanana  na hivyo.Kula matunda kadri uwezavyo lakini epuka ndizi tamu.


Chakula cha mchana (Lunch): ¼  Kuku wa kuchoma au wa kuchemsha na si vinginevyo. Salad au kachumbari ya mboga mboga tofauti lakini isiwe na mayonnaise. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks kama ice cream, chocolate, biskuti nk. Jizoeshe kula matunda kwa wingi kila unapohisi njaa.


Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) pamoja na kufanya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku.


Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha. Unaweza kutumia karoti, nyanya au tungule, broccoli, cauliflower, pilipili boga na za kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na thomu na nk, epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.


• Siku ya pili (Day 2)


Tembea kwa nusu saa asubuhi (dakika 30) na fanya sit-ups 15-30. Baada ya mazoezi kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa kuweka kijiko kimoja cha sukari kidogo kama nilivyoeleza hapo awali. Sausage moja ya kuchemsha ya kuku au ya nyama ya ngombe. Slice moja ya brown bread pamoja na matunda mengi.


Chakula cha  mchana (Lunch): Ndizi moja ya kuchoma pamoja na kachumbari au salad ya mboga mboga aina yoyote lakini isiwe na mayonnaise. Mishikaki 2-3 ya nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku, samaki.


Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) na baada ya hapo fanya sit-ups 15-20 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Epuka juisi aina yoyote ile iwe fresh au za kwenye boksi kwani mara nyingi watu wanahadaiwa na juisi za kwenye boksi zinazosema ni fresh na hazina kemikali yoyote, ukweli ni kwamba kampuni zinazotengeneza juisi hizi huwapa tenda kampuni za kutengeneza manukato ambazo ndizo hutengeneza maboksi haya na kuweka syrup na harufu kulingana na harufu ya tunda linalohitajika, mfano kama kampuni ya kutengeneza juisi inahitaji boksi la harufu ya embe basi watawatengenezea boksi hilo kwa kutumia syrup ya embe na harufu ya embe.


Pia juisi za kwenye boksi, wakati wa kutengenezwa huhifadhiwa kwa muda mrefu na kupitia mlolongo mrefu wa utengenezaji hivyo kuondoa virutubisho asilia muhimu pamoja na fibre ambazo ni muhimu sana kiafya.


Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda. Epuka ndizi mbivu. Epuka vilevi vya aina yoyote vile km pombe, wine, sigara, tumbaku, khuberi na nk.


• Siku ya Tatu (Day 3)


Mazoezi kama kawaida. Kimbia au tembea kwa dakika 30, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kikiwa na kijiko kimoja cha sukari.


Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla au baada ya kula. Ndizi 2 za kuchemsha Bukoba siyo ndizi tamu (sweet banana). Bakuli la kutosha la supu ya mboga mboga (vegetable soup) ukishushia kwa matunda kwa wingi. Epuka ndizi mbivu. Hakikisha wakati wa kupika supu yako huweki mafuta ya kupikia au siagi n.k.


Jioni: Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 baada ya kufanya mazoezi. Unaweza kula matunda wakati unasubiria chakula cha usiku.


Chakula cha Usiku (Dinner): BBQ sausage 3 pamoja na salad au kachumbari.


• Siku ya nne (Day 4)


Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai, weka kijiko kimoja cha sukari. Sindikiza kwa matunda ya aina yoyote. Epuka ndizi mbivu.


Chakula cha mchana (Lunch): Kiazi kimoja cha kuchemsha pamoja na mboga mboga za majani kama njegere, karoti, pilipili boga, broccoli, cauliflower, na nk. Sukumizia na supu ya uyoga (mushroom soup). Jitahidi supu zako usiweke mafuta wakati unapika. Glasi moja ya maziwa fresh (250ml-300ml).


Jioni: Mazoezi kama kawaida.


Chakula cha Usiku (Dinner): Vegetable platter, mboga za aina zozote unazopenda bila kuweka mafuta hata tone ikishindikana weka kijiko kimoja cha olive oil au mafuta ya alizeti. Samaki wa kuchoma au kuchemsha, kula mzima lakini asizidi robo kilo. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.


• Siku ya Tano (Day 5)


Kimbia kwa dakika 30, kama utatembea, tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu galsi 4.


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai chenye sukari kijiko kimoja. Slice 1 ya mkate mweupe uliyopakwa siagi kidogo sana pamoja na mayai mawili ya kukaanga (Spanish omelet). Malizia kwa matunda.


Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula chakula cha mchana. Supu ya kuku bakuli moja tu. Hakikisha kuku wako umemtoa ngozi ya juu kabla ya kumpika. Unaweza kuweka tambi (spaghetti) kidogo kwenye bakuli la supu lakini siyo lazima. Tambi zisipikwe kwa mafuta bali zichemshwe tu.


Jioni: Kimbia kwa dakika 30 au tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.


Chakula cha usiku (Dinner): Kula mboga mboga aina yoyote ile pamoja na matunda kwa wingi.


• Siku ya Sita (Day 6) 


Tembea kwa dakika 45 au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. 


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Cornflakes na maziwa ambayo ni skimmed milk ama low fat (yenye mafuta kidogo). Kula matunda yoyote unayopenda. 


Chakula cha Mchana (Lunch): Kula beefcubes zilizochemshwa kiwango kidogo kama robo kilo. Unaweza kupendezesha kwa karoti, cauliflower, broccoli, pilipili hoho au njegere nk, weka kijiko kimoja cha mafuta ya alizeti au olive oil. 


Jioni: Mazoezi kama kawaida. 


Chakula cha usiku (Dinner): Kula tambi (noodles au spaghetti) zilizochemshwa na sauce yoyote utakayopenda ila isiwe na mafuta zaidi ya kijiko kimoja. Usisahau matunda kwa wingi.


• Siku ya Saba (Day 7) 


Tembea kwa dakika 30-45, kama unakimbia basi kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. 


Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa, yai moja la kuchemsha pamoja na maziwa fresh glasi moja. 


Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula. Supu ya mboga mboga bakuli moja la kutosha, ndizi ya kuchemsha moja (ndizi bukoba), malizia kwa matunda mengi, leo unaruhusiwa hata kula ndizi  mbivu au ndizi tunda. 


Jioni: Mazoezi kama kawaida 


Chakula cha usiku (Dinner): Nusu kuku au beef sausage, pamoja na wali maharage na salad au kachumbari ya aina yoyote ile ya kutosha lakini isiwe na mayonnaise, cheese au butter. 


Unaruhusiwa kunywa glasi 2 za white wine baada au wakati unakula kama ni kuku. Au glasi 2 za red wine baada au wakati unakula kama ni beef sausage. Ila kama ni kuku iwe kuku, kama ni beef sausage iwe hiyo na siyo vyote viwili.

Credit: @TanzMed


 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

SABABU ZA VIFO VYA WAJAWAZITOAfyaclass Bongo Social •

UZAZI/WAJAWAZITO

• • • • • •

SABABU ZA VIFO VYA WAJAWAZITO


Kuna Vifo mbali mbali amabavyo hutokea kwa wakina mama wajawazito,wakati wanajifungua au hata kabla ya muda wa kujifungua kufika,je vifo hivi hutokana na nini? Hizi hapa chini ni baadhi ya sababu za vifo kwa wakina mama wajawazito


- Tatizo la mama kuvuja damu nyingi kupita kiasi wakati na baada ya kujifungua ambapo kwa kitaalam hujulikana kama postpartum hemorrhage(PPH),


Asilimia kubwa ya tatizo hili hutokea ndani ya masaa 24 baada ya mama kujifungua,na vifo vingi ambavyo hutokana na tatizo hili la kuvuja damu nyingi kwa wakina mama hutokea wakati wa kujifungua au muda mfupi tu baada ya kujifungua


- Maambukizi ya magonjwa ambapo hujulikana kama Sepsis au Infection, Pia maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Virusi,Bacteria n.k huweza kuchangia vifo kwa wakina mama wajawazito


- Tatizo la Kifafa Cha Mimba, Pia wakina mama wengi hupoteza maisha wakati wa ujauzito kutokana na kupatwa na tatizo la kifafa cha mimba,


Ndyo mana kuna umuhimu mkubwa sana kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki, lakini pia kupata vipimo mbali mbali kama vile; kipimo cha Presha, kupima Uwepo wa Protein kwenye Mkojo n.k ili kama kuna viashiria vyovyote vya tatizo la kifafa cha mimba mama mjamzito aanze kupata msaada mapema.


- Mama kuvuja damu nyingi wakati wa ujauzito kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


  • Kupatwa na tatizo la damu kushindwa kuganda yaani Coagulopahty


  • Kondo la nyuma yaani Placenta kuachia sehemu lilipojishikiza ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Placenta abruption


  • Kuvuja damu baada ya kupata ajali, kupigwa,kuanguka n.k


- Mama mjamzito kuwa na matatizo mbali mbali ya Moyo kama vile; Cardiomyopathy,tatizo la mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba n.k


- Mama mjamzito kupatwa na tatizo la clots za damu iliyoganda kwenda moja kwa moja kwenye mapafu hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Pulmonary embolism,


Tatizo hili ni hatari sana na huweza kusababisha mama mjamzito kupoteza maisha yake ndani ya muda mfupi


- Mama mjamzito kupatwa na tatizo la maji ya uzazi yaani Amniotic fluid kuingia kwenye mzunguko wa damu hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Amniotic fluid embolism,


Na hiki ndyo chanjo kikubwa cha vifo kwa wakina mama wajawazito ambao wanajaribu Kutoa MIMBA kwa sababu moja au nyingine.


- SABABU ZINGINE NI PAMOJA NA;


  •Tatizo la Presha au shinikizo la damu wakati wa ujauzito


  • Ugonjwa wa kisukari


  • Mimba kutunga nje ya Kizazi yaani Ectopic pregnancy


  • Tumbo la uzazi kupasuka yaani Uterine rupture


  • Mtoto kukaa vibaya tumboni na sababu zingine, japo huchangia kwa asilimia ndogo


  • Kondo la nyuma kushuka chini zaidi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Placenta praevia, Pamoja na Sababu zingine..!!!



• Soma pia: Sababu za Wanawake Wengi kujifungua kwa upasuaji


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA KIKOHOZI KIKAVU KISICHOISHA KWA MTOTO BAADA YA KUZALIWAAfyaclass Bongo Social •

 WATOTO

• • • • • • 

CHANZO CHA KIKOHOZI KIKAVU KISICHOISHA KWA MTOTO BAADA YA KUZALIWA


Tatizo hili la mtoto kukohoa kikohozi kikavu ambacho hakiponi au kisichoisha ni tatizo ambalo huwapata watoto wengi kwa hivi sasa,na wengine tatizo hili huendelea mpaka wakiwa watu wazima bado husumbuliwa na kikohozi kikavu kisichoisha,matatizo ya kifua n.k


Baada ya kukutana na Cases nyingi za watoto wenye tatizo hili,nmeamua kutoa ufafanuzi kwa kina katika makala hii, soma kwa makini ili uelewe vizuri kuhusu tatizo hili kwa watoto.


Baada ya mtoto kupatwa na tatizo hili endapo hakupata tiba na kuendelea nalo hadi utu uzima, kwa asilimia kubwa huwa na matatizo ya kifua hasa pale ambapo hali ya hewa ikibadilika,kama vile kukiwa na mvua,baridi sana,akishika maji ya baradi au kuoga na maji ya baridi n.k, Je chanzo cha tatizo hili ni nini? soma hapa kujua..!!!


CHANZO CHA KIKOHOZI KIKAVU KISICHOISHA KWA MTOTO BAADA YA KUZALIWA


Tatizo hili huweza kuchangiwa na sababu zaidi ya moja tofauti na watu wengi kufikiria tatizo moja tu la ASTHMA kwa mtoto, Hivo zifuatazo ni baadhi ya sababu za kutokea kwa tatizo hili kwa mtoto;


1. Tatizo la ASTHMA kwa mtoto, Ugonjwa wa asthma huweza kuwa ni miongoni mwa sababu kubwa ya mtoto kuwa ma kikohozi kikavu ambacho hakiishi kila siku


2. Tatizo la Pneumonia, Pia shida hii ya pneomonia huweza kuleta kikohozi kwa mtoto mara kwa mara baada ya kupatwa na maambukizi ya bacteria,fangasi au Virusi kwenye mfumo wa hewa ikiwa ni pamoja na kwenye vifuko vya hewa yaani Alveoli ndani ya mapafu


3. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kwenye mfumo mzima wa hewa, hapa tunazungumzia vimelea vya magonjwa mbali mbali kama vile Bacteria,fangasi na Virusi,


Mtoto huweza kupata maambukizi haya kwenye mapafu,vifuko vya hewa yaani Alveoli ndani ya mapafu,kwenye koo la Hewa n.k


4. Mtoto kunywa maji ya Uzazi, Sababu hii ni miongoni mwa sababu kubwa za tatizo hili,japo kwa watu wengi hawagundui hili, ila kuna watoto hunywa maji ya uzazi hasa wakati wa kujifungua hali ambayo hupelekea mtoto kuanza kuwa na tatizo la kikohozi kikavu ambacho hakiishi,


Baada ya mtoto kunywa maji ya uzazi wakati anazaliwa huweza kupatwa na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na hili la kikohozi, kukosa hewa ya oxygen kwenye ubongo,mwili kuanza kudhoofika, mtoto kuchelewa hatua za ukuaji n.k . 


• KUHUSU MTOTO KUNYWA MAJI YA UZAZI NA MADHARA YAKE SOMA ZAIDI HAPA...!!!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA+255758286584.




0 Comment

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)Afyaclass Bongo Social •

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

Tinnitus, Tatizo hili huhusisha mtu kusikia sauti za makelele au kitu kinaita(ringing) ndani ya sikio moja au yote mawili na sauti hizo hazitoki nje na wala hakuna mtu mwingine anazisikia zaidi ya mhusika mwenyewe.

Tatizo hili hutokea kwa watu wengi takribani asilimia 15% mpaka 20%, na hasa kwa watu wenye umri mkubwa au wazee, 

Mtu mwenye tatizo hili huweza kusikia sauti mbali mbali kati ya hizi hapa chini;

- Muito au ringing ndani ya sikio

Kubweka

- Kunguruma

- Kitu kinagonda ndani ya sikio

- sauti za Kusisimua au kutekenya N.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA TINNITUS

Hakuna sababu moja ambayo inasababisha tatizo hili,ila kuna mjumuisho wa sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili,na sababu hizo ni kama vile;

1. Tatizo la kupoteza usikivu,ambapo seli za vinyeleo ndani ya sikio kwenye sehemu ya ndani(Cochlea) ambazo zinasaidia sikio kupokea mawimbi ya Sauti kwa kupitia Auditory nerves kwenda kwenye ubongo,

Lakini baada ya ubongo kupokea hizo Electrical signals hutafsiri kama kelele badala ya sauti ya kawaida,na ndipo tatizo hutokea.

2. Nywele ndani ya sikio kupinda au kutoka zenyewe kutokana na sababu mbali mbali kama vile umri mkubwa au kuwa katika mazingira ambayo kunakuwa na sauti kubwa sana mara kwa mara kama vile ya muziki n.k, 

hali hii ya kuwa katika mazingira haya ya SAUTI KUBWA SANA inayopenya masikioni huweza kusababisha mtu kuwa na tatizo hili

3. Maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kwenye sikio kama vile bacteria,Fangasi,Virusi n.k

4. Tatizo la sikio kuziba kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuwa na maji mengi sikioni, nta kuzidi(EarWax), uchafu au kitu chochote ambacho kinaweza kuziba sikio lako

5. Kuumia kichwani au shingoni, hali hii huweza kuathiri sikio la ndani, nerves zinazosaidia sikio kusikia pamoja na utendaji kazi wa ubongo

6. Matumizi ya baadhi ya dawa, Mtu kuoverdose dawa au kutumia dawa kwa muda mrefu huweza kusababisha tatizo hili, na hapa tunazungumzia matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;

 dawa jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs(NSAIDs), Baadhi ya antibiotics, Dawa za kutibu kansa au saratani, Dawa jamii ya Diuretics, Antidepressants, Dawa za Malaria N.k

7. Matatizo ya muda mrefu yanayohusisha Nerves au mfumo wa Fahamu

8. Magonjwa kama vile Menieres ambayo huweza kusababisha abnormal Inner Ear fluid pressure n.k

9. Kutokufanya kazi vizuri kwa Eustachian tube ndani ya sikio

10. Tatizo kwenye mifupa ya sikio kama vile kukakamaa ndani ya sikio ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Otosclerosis

11. Tatizo la misuli yaani Muscle spasms ndani ya sikio

12. Matatizo kwenye mishipa ya damu ndani ya sikio ambayo huweza kuathiri mzuguko wa damu kwenye sikio, na matatizo hayo ni pamoja na; Atherosclerosis, Shinikizo la Damu(High blood pressure), Kinked, n.k

13. SABABU ZINGINE NI KAMA VILE;

- Ugonjwa wa kisukari

- Matatizo kwenye tezi la Thyroid

- Tatizo la maumivu makali sana ya kichwa cha mara kwa mara au Migraines

- Tatizo la Anemia au upungufu wa damu mwilini

- Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune disorders kama vile; Rheumatoid arthritis, Lupus n.k

MADHARA YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA

1. Mwili kuchoka kupita kiasi

2. Kupatwa na tatizo la mfadhaiko,msongo wa mawazo n.k

3. Kupata tatizo la kukosa usingizi

4. Kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu

5. Kushindwa kufanya kitu kimoja vizuri na kwa utulivu au kuloose concetration

6. Kuanza kupatwa na tatizo la wasiwasi kila mara

7. Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Matibabu ya tatizo hilo hutegemea na chanzo chake,hivo kwa ujumla zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile;

✓ Kuondoa nta au uchafu wowote ambao umeziba sikio

✓ Kutibu tatizo la mishipa ya damu,tatizo la presha,kisukari n.k

✓ Kuacha baadhi ya dawa au kubadilisha baadhi ya dawa

✓ Kupewa vifaa vya kukusaidia kusikia yaani Hearing aids n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Tatizo la Kelele Masikioni

1.Kukaa Sehemu Zenye Makelele mengi,

Kelele kubwa, kama vile zile za vifaa vizito,Vyuma kugongwa, misumeno ya minyororo na silaha za moto, ni vyanzo vikubwa vya upotezaji wa kusikia unaohusiana na kelele. 

Vifaa vya muziki vinavyotumia Sauti Kubwa Sana, vinaweza pia kusababisha upotevu wa kusikia unaohusiana na kelele kikichezwa kwa sauti kubwa kwa muda mrefu.  Watu wanaofanya kazi katika mazingira yenye kelele - kama vile wafanyikazi wa kiwanda na ujenzi, wanamuziki na wanajeshi - wako hatarini pia kupata tatizo hili la Kelele masikioni.

2. Umri

Unapozeeka, idadi ya nyuzi za neva zinazofanya kazi katika masikio yako hupungua, na hivyo kusababisha matatizo ya kusikia ambayo mara nyingi huhusishwa na tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.

3. Jinsia

Wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus kuliko wanawake.

4. Matumizi ya Pombe,na Tumbaku. 

Wavutaji sigara wana hatari kubwa ya kupata tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.  Kunywa pombe pia huongeza hatari ya kupata tatizo hili la masikio kupiga kelele tinnitus.

5. Baadhi ya Matatizo ya Kiafya.

 Hapa Nazungumzia matatizo mbali mbali ikiwemo;

  • Tatizo la Uzito mkubwa au Unene(Overweight/Obesity)
  • Matatizo ya Moyo(cardiovascular problems), 
  • Tatizo la Shinikizo la juu la Damu(high blood pressure)
  • Kuwa na historia ya kuumwa tatizo la arthritis 
  • Kuumia eneo la kichwani n.k

Jinsi ya Kuzuia Tatizo hili la Masikio kupiga Kelele au Masikio kunguruma

Katika hali nyingi, tatizo la Masikio kunguruma au masikio kupiga kelele(tinnitus) ni matokeo ya kitu ambacho hakiwezi kuzuiwa.  Hata hivyo, baadhi ya tahadhari zinaweza kusaidia kuzuia aina fulani za tinnitus;

Tumia vizuia kelele masikioni

 Baada ya muda, Makelele yatokanayo na sauti kubwa yanaweza kuharibu mishipa katika masikio, na kusababisha hasara ya kusikia na kupata tatizo la masikio kupiga kelele(tinnitus),

Hivo iwapo upo kwenye mazingira yenye kelele kubwa ambazo huwezi kuziepuka Jaribu kupunguza mawimbi makubwa ya sauti kwa kutumia vifaa vya kuzuia kelele masikioni.

 Na ikiwa huwezi kuepuka sauti kubwa, tumia kinga ya Masikio ili kulinda usikivu wako.  Ikiwa unatumia misumeno ya minyororo, ni mwanamuziki, unafanya kazi katika tasnia inayotumia mashine zenye sauti kubwa au kutumia bunduki (hasa bastola au bunduki), kila wakati vaa kinga ya kuzuia Sauti kubwa masikioni.

✓ Epuka mazingira yenye Sauti kubwa

Kama inawezekana kaa mbali na mazingira yenye Sauti kubwa,ikiwemo;

  • Mazingira yenye kelele kubwa za vifaa vya chuma,vyuma kugongwa
  • Misemo inayopiga kelele
  • Mashine za viwandani
  • Muziki mkubwa sana
  • Na aina zingine zote za Kelele kubwa

✓ Punguza sauti

Kukaa kwa muda mrefu kwenye mazingira ya kelele kubwa kama vile muziki mkubwa huweza kuathiri masikio yako na kusababisha tatizo la kelele masikioni,

Hivo kusikia sauti hizi bila ulinzi wa sikio au kusikiliza muziki kwa sauti ya juu sana kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani kunaweza kusababisha upotevu wa kusikia na tatizo la tinnitus.

Punguza Sauti kubwa ya Vifaa vya muziki Kama vile Earphone,Sabufa,Spika n.k

 ✓ Linda afya yako kwa Ujumla

Jikinge na matatizo mbali mbali ikiwemo;

  • Tatizo la Uzito mkubwa au Unene(Overweight/Obesity)
  • Matatizo ya Moyo(cardiovascular problems), 
  • Tatizo la Shinikizo la juu la Damu(high blood pressure)
  • Kuwa na historia ya kuumwa tatizo la arthritis 
  • Kuumia eneo la kichwani n.k

Fanya Mazoezi ya mara kwa mara, kula Mlo bora kiafya na kuchukua hatua nyingine ili kuweka mishipa yako ya damu kuwa na afya, Hii inaweza kusaidia kuzuia tatizo la tinnitus Linayohusishwa na fetma na matatizo ya mishipa ya damu.

✓ Acha kabsa au Punguza matumizi ya pombe, Sigara,Tumbaku au vitu vyenye kafeini nyingi na nikotini.

Vitu hivi zinapotumiwa kwa kiwango kikubwa, vinaweza kuathiri mtiririko wa damu na kuchangia kwenye tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO BAADA YA KUZALIWAAfyaclass Bongo Social •

 MTOTO

• • • • • •

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO BAADA YA KUZALIWA


Zifahamu hatua mbali mbali za ukuaji kwa mtoto(Stages of development) au kwa kitaalam zaidi hujulikana kama Developmental milestones, Hatua hizi za ukuaji zinahusisha mtoto mwenye afya bora ambaye hana tatizo lolote ambalo linaweza kuchelewesha ukuaji wake.


Fahamu kwamba matatizo kama vile; Utapiamlo, upungufu wa baadhi ya vichocheo au hormones mwilini, matatizo ya Ubongo,mtoto kukosa hewa ya kutosha ya oxygen kwenye ubongo n.k vyote hivi huweza kuchelewesha ukuaji na maendeleo ya mtoto wako


Tangia mtoto anazaliwa mpaka anakuwa mtu mzima kuna hatua mbali mbali za ukuaji ambazo anazipitia huku zikihusisha mambo mbali mbali kama vile mabadiliko ya mwili,tabia n.k


HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO BAADA YA KUZALIWA


1. MARA TU BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Mara tu baada ya mtoto kuzaliwa huanza kupata mabadiliko mbali mbali kwenye mwili wake, ndani ya siku 7-10 baada ya mtoto kuzaliwa huanza kupungua uzito wake wa mwili kwa asilimia 5% mpaka 10%,


Baadae mtoto huanza kuongezeka uzito wake wa mwili tena, Watoto wengi huzaliwa na urefu wa sentimita 50, baada ya mwaka mmoja hufikisha sentimita 75 na baada ya miaka minne hufikisha urefu wa sentimita 100.

Kwa kawaida mtoto huzaliwa na kichwa chenye mzunguko  wa sentimita 35 na kuongezeka sentimita moja kila mwezi na baada ya miezi 12 kichwa hufikisha sentimita 46


2. WIKI YA SITA BAADA YA MTOTO KUZALIWA


Katika kipindi hiki au umri huu mtoto huendelea kupata mabadiliko mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kutabasamu pasipo kuongea kitu chochote.


3. MWEZI WA PILI BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Kwenye mwezi wa pili, mtoto huanza kukunja na kunyoosha mikono huku akivuta nguo zake na za mtu mwingine aliyembeba.


4. MWEZI WA NNE BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Mtoto anapofikisha umri wa miezi minne huanza kushika vitu na kuviweka mdomoni na kuanza kugeuka pale anaposikia sauti ya mtu inaita na kuweza kutumia shingo yake vizuri zaidi.


5. MWEZI WA SITA BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Katika kipindi hiki mtoto huendelea kupata mabadiliko mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kuanza kuota meno, kuanza kutambaa, kuanza kukaa mwenyewe na kupata wasiwasi akimuona mtu ambaye hamfahamu.


6. MWEZI WA TISA BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Kwenye mwezi wa tisa; mtoto huanza kusimama mwenyewe na kuanza kuita majina mbali mbali kama vile mama,baba,dada, kaka na kuanza kucheza michezo ya kitoto.


7. MWEZI WA 12 BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Baada ya mtoto kufikisha umri wa mwaka mmoja toka azaliwe yaani miezi 12, ndipo huanza kutembea mwenyewe kwa kukusaidiwa na vitu mbali mbali baada ya kuvishika au kwa  kushikwa na mtu japo baadhi ya watoto wengine huwahi zaidi kuanza kutembea hata kabla ya mwaka kuisha. 


8. MWEZI WA 15 BAADA YA MTOTO KUZALIWA


Mwezi wa 15 mabadiliko mbali mbali huendelea kutokea ikiwa ni pamoja na uwezo wa mtoto kutembea mwenyewe, Mtoto kuweza kuchora mstari na kuonyesha kitu anachokihitaji kwa kidole pamoja na vitu vingine.


9. MWEZI WA 18 BAADA YA MTOTO KUZALIWA


 Hapa mtoto huweza kupanda ngazi, huongeza idadi ya maneno na hufuata akiagizwa kufanya au kutofanya kitu fulani, hapa huanza kutumia kijiko na kujishika sehemu za mwili wake.


10. MIAKA MIWILI(2) BAADA YA MTOTO KUZALIWA


Mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili, huweza kufanya vitu vingi zaidi kama vile; kukimbia na kupiga mpira, huweza kuvua nguo na kuanza kutamka maneno kama mimi, wewe yule na kadhalika.



11. MIAKA MITATU(3) BAADA YA MTOTO KUZALIWA


Umri wa miaka mitatu tayari mabadiliko makubwa yameshatokea mwilini na bado yanazidi kutokea hapa mtoto anazidi kua mkubwa na kuanza kusimama kwa mguu mmoja, kukimbia zaidi, kujua jinsia na umri wake, huweza kuvaa na kuvua nguo lakini hawezi kufunga vifungo, anaweza kuhesabu moja mpaka kumi kama akifundishwa, anaweza kuruka na kuchora duara.


12. MIAKA MINNE(4) BAADA YA MTOTO KUZALIWA


Mtoto mwenye umri wa miaka minne huweza kufanya mambo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuweza kusimulia kitu kilichomtokea,kufunga vifungo vya shati mwenyewe,kuweza kutumia choo mwenyewe na kwenda kujisaidia bila shida yoyote, Kuweza kucheza michezo mingi zaidi, kuweza kuruka kwa mguu moja bila kuanguka n.k.


13. MIAKA MITANO(5) BAADA YA MTOTO KUZALIWA

Katika umri huu wa miaka mitano; mtoto anaweza kuzitambua rangi nne za msingi, anaweza kuendesha baiskeli, anaongea kama watu wengine bila kuchanganya wakati uliopo na ujao,uelewa na akili yake kuzidi kukua zaidi pamoja na kufanya mambo mengine mengi sana.


Hizo ndyo baadhi ya Hatua za Ukuaji wa mtoto toka anazaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

KANSA YA KWENYE UUME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKEAfyaclass Bongo Social •

UUME
• • • • •
KANSA YA KWENYE UUME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Kansa ya Uume, ni ukuaji wa seli usio wa kawaida na usiodhibitika ndani ya uume ambapo kwa asilimia kubwa huanza kwenye seli za ngozi ya uume kisha kuingia ndani,
 Bila shaka aina hii ya kansa ya Uume itakuwa haitajwi sana kama aina zingine za kansa kwa wanaume kama vile kansa ya Tezi dume n.k, lakini kansa hii ipo na inapata baadhi ya Wanaume pia.


CHANZO CHA KANSA YA UUME

- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa aina hii ya Kansa,japo kutokana na tafiti mbali mbali imeonekana Kansa ya Uume hupata sana makundi haya yafuatayo;


1. Wanaume wenye kirusi cha HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)


2. Wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60


3. Wanaume wanaovuta sana Sigara


4. Wanaume wenye kinga ndogo ya mwili kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya UKIMWI au matumizi ya baadhi ya dawa n.k


5. Wanaume ambao hawajatahiriwa,ambapo maji maji pamoja na uchafu unaojulikana kama "smegma" hujikusanya chini ya ngozi ya uume na kukuweka katika hatari zaidi


6. Mwanaume kuwa na tatizo la phimosis ambapo ngozi ya uume hushikamana zaidi na kukakamaa hali ambayo hupelekea kuwa vigumu kusafishwa vizuri


7. Mwanaume kuwa kwenye matibabu ya psoriasis pamoja na matumizi ya dawa za psoralen au huduma ya mionzi(ultraviolet (UV) light



DALILI ZA KANSA YA KWENYE UUME NI PAMOJA NA;


• Ngozi ya kwenye uume kuanza kubadilika rangi hasa ngozi ya mbele kwa wale ambao hawajatahiriwa

• Ngozi ya uume kuwa laini zaidi kuliko kawaida

• Ngozi ya uume kuanza kuwa na vipele pele au rashes, makovu au vidonda kwenye uume n.k

• Kuwa na uvimbe ambao unakuwa au kuongezeka ambao una rangi ya blue kwenda brown

• Ngozi ya uume kuanza kutoa harufu mbaya

• Kuwa na vidonda kwenye uume ambavyo wakati mwingine huvuja damu

• Uume kuvimba kwa mbele au kuwa na uvimbe chini ya ngozi ya uume


KUMBUKA; Uwepo wa dalili hizi haimaanishi moja kwa moja una kansa ya Uume,inawezekana pia ukawa na magojwa mengine kama magonjwa ya zinaa,maambukizi mbali mbali au tatizo la Allergy,hivo ukiona dalili kama hizi ongea na wataalam wa afya kwanza kwa ajili ya vipimo zaidi.


MATIBABU YA KANSA KWENYE UUME

Kama ilivyo aina zingine za kansa, Mgonjwa ambaye kagundulika mapema kuwa na tatizo hilo la kansa ya uume hupata tiba na kupona kwa haraka zaidi kuliko ukichelewa kugundulika na kuanza tiba mapema, matibabu huhusisha njia mbali mbali kama vile;

- Matumizi ya baadhi ya dawa mbali mbali ikiwemo cream za kupaka pamoja na vidonge vya kunywa

- Mwanaume kutahiriwa kwanza kama hakutahiriwa

- Huduma ya Cryotherapy n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment

AINA ZA BIMA YA AFYA ZINAZOPATIKANA NCHINI TANZANIAAfyaclass Bongo Social •

BIMA YA AFYA

• • • • • •

AINA ZA BIMA YA AFYA ZINAZOPATIKANA NCHINI TANZANIA

1. National Health Insurance Fund (NHIF)

2. Social Health Insurance Benefit (SHIB)

3. Community Health Fund (CHF) 

4. Tiba Kwa Kadi (TIKA)

5. Pamoja na Bima zingine zote za afya za makampuni binafsi ambazo ni Private health insurance Companies

NB: Kutokana na Takwimu za Mwaka 2019 kuhusu Health insurance coverage nchini Tanzania zinaonyesha kwamba; asilimia 32% ya Watanzania ndyo Wanaotumia Bima ya afya ambapo;

• Asilimia 8%- Ni wanachama wa Bima ya Taifa yaani  National Health Insurance Fund (NHIF)

• Asilimia 23%- Ni wanachama wa Community Health Fund(CHF)

• Asilimia 1%- Ni wanachama wa Bima za afya za makampuni binafsi yaani Private health insurances Companies

1. National Health Insurance Fund (NHIF)

Bima hii ya Afya ya Taifa imeanzishwa chini ya sheria ya Bunge "the Act of Parliament No. 8 ya mwaka 1999 " na kisha kuanza kufanya kazi kuanzia June 2001,

Mwanzoni bima hii ililenga zaidi watumishi wa uma yaani Public Servants lakini kwa hivi sasa hata ambao sio watumishi wa Uma wanaweza kutumia Bima hii ya Afya.

2. Social Health Insurance Benefit (SHIB)

Bima hii ya afya ni sehemu ya National Social Security Benefits iliyoanzishwa mwaka 2007,ambapo wanachama wote wa mfuko wa NSSF walikuwa wanapata huduma za afya kupitia Bima hii.

3. Community Health Fund (CHF) na Tiba Kwa Kadi (TIKA)

Community Health Fund (CHF)-Hii ni Bima ya afya ambayo ililenga sana jamii nzima kwa ujumla ambayo ipo maeneo ya kijijini pamoja na watu wachini kabsa na kujiunga kwenye bima hii ni Hiari yako mwenyewe,tofauti na bima zingine za afya kama ya taifa NHIF ambapo ilikuwa nilazima mtumishi wa uma kukatiwa Bima hii ya Afya.

Tiba Kwa Kadi (TIKA),hii ilikuwa tofauti kidogo na Community Health Fund (CHF), kwani ililenga zaidi jamii ambazo zipo maeneo ya Mjini

- Kwa pamoja CHF na TIKA ziliundwa chini ya CHF act 2001 na kufanya kazi kwenye maeneo ngazi ya Wilaya. Ambapo kwenye ngazi hiyo ya Wilaya, council health service boards (CHSB) na health facilities governing committees (HFGC) ndyo wahusika wakuu wa kusimamia utendaji kazi wa CHF, Lakini mnamo mwaka 2009 Kazi zote za CHF kitaifa zilikabidhiwa kwa NHIF.

4. Bima zingine zote za afya za makampuni binafsi ambazo ni Private health insurance Companies

Hapa ni bima za makampuni yote binafsi yawe ni ndani ya Tanzania au Nje ya nchi wana Bima zao za afya, hapa huweza kuhusisha kampuni au hata mtu Binafsi pia

Mpango huu ulianzishwa miaka ya (2002) ambapo kulikuwa na Bima za afya binafsi yaani private health insurance firms in Tanzania, na ndipo mpango ukawa mkubwa zaidi hadi kuhusisha makampuni mbali mbali pia kama vile AAR, Jubilee Insurance, Resolution Health and Metropolitan Insurance.

Source:Wikipedia

Bima za Afya na Gharama Zake Tanzania

Katika jamii ya kisasa, bima za afya zimekuwa chombo muhimu katika kuhakikisha watu wanapata huduma bora za afya bila kutegemea uwezo wao wa kifedha. Nchini Tanzania, bima za afya zinajulikana kama mfumo wa kuhakikisha kwamba watu wanapata matibabu wanapohitaji, bila kuathiri sana bajeti zao. Katika makala hii, tutaangazia aina za bima za afya, gharama zake, na changamoto zinazokabili mfumo huu nchini.

Aina za Bima za Afya

Tanzania ina aina kadhaa za bima za afya ambazo zinapatikana kwa wananchi. Kwanza, kuna bima za afya za jamii ambazo zinatoa huduma za matibabu kwa wanachama kupitia makundi ya kijamii. Mfumo huu umeanzishwa ili kuhakikisha watu wa kipato cha chini wanapata huduma bora za afya. 

Mfano mzuri ni Mfumo wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF), ambao unalenga jamii zisizo na uwezo wa kulipia gharama za matibabu. Bima nyingine ni bima ya Taifa,NHIF n.k

Pili, kuna bima za afya za binafsi zinazotolewa na makampuni ya bima. Hizi ni bima ambazo mtu binafsi anaweza kujisajili kwa hiari yake, na mara nyingi zinatoa huduma zaidi na kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na bima za jamii. Watu wanaweza kuchagua mipango inayowafaa kulingana na mahitaji yao na uwezo wao wa kifedha.

Gharama za Bima za Afya

Gharama za bima za afya nchini Tanzania hutofautiana kulingana na aina ya bima, kiwango cha huduma zinazotolewa, na uwezo wa kifedha wa mteja. Kwa bima ya afya ya jamii kama CHF, gharama za mwaka zinaweza kuwa kati ya shilingi 30,000 hadi 50,000 kwa mtu mmoja. Hii ni gharama nafuu ikilinganishwa na gharama za matibabu bila bima.

Kwa upande mwingine, bima za afya za binafsi zinaweza kuwa na gharama kubwa, kuanzia shilingi 100,000 hadi milioni kadhaa kwa mwaka, kulingana na kiwango cha huduma na umri wa mteja. Wakati bima hizi zinaweza kuonekana kuwa ghali, zinatoa faida za haraka na huduma bora zaidi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa madaktari wa kitaaluma, vipimo vya kisasa, na huduma katika hospitali za kibinafsi.

Changamoto za Mfumo wa Bima za Afya

Ingawa bima za afya zina umuhimu mkubwa, mfumo huu unakabiliwa na changamoto kadhaa. Kwanza, ufahamu wa bima za afya bado ni mdogo miongoni mwa wananchi wengi. Watu wengi hawaelewi faida za bima za afya, na hivyo wanakosa fursa ya kujihusisha nayo. Pia, kuna tatizo la ufisadi katika baadhi ya maeneo ya huduma za afya, ambapo fedha za bima hazitumiki ipasavyo, na kupelekea wananchi kutopata huduma wanazotarajia.

Pili, kuna tatizo la upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini. Ingawa bima za afya zipo, watu katika maeneo ya mbali wanaweza kukosa vituo vya afya vinavyokubalika, na hivyo kuhatarisha afya zao. Mambo haya yanahitaji hatua za haraka ili kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa kila mtu bila kujali mahali alipo.

Hitimisho

Bima za afya ni muhimu sana katika kuboresha huduma za afya nchini Tanzania. Zinasaidia kupunguza mzigo wa gharama za matibabu na kuhakikisha kwamba watu wanapata huduma zinazohitajika. Hata hivyo, ili mfumo huu uweze kufanya kazi vizuri, ni lazima kuimarisha ufahamu wa bima za afya, kupunguza ufisadi, na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yote, hususan vijijini. Serikali na wadau wa afya wanapaswa kushirikiana ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya bora na salama, bila kujali hali yake ya kifedha.

0 Comment

MADHARA YA SINDANO ZA KUZUIA MIMBA PAMOJA NA NJIA NYINGINEAfyaclass Bongo Social •

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

. . . . . .

MADHARA YA SINDANO ZA KUZUIA MIMBA PAMOJA NA NJIA NYINGINE


MADHARA YA SINDANO


(1) Kuwa na tatizo la hedhi isiyosawa, kubadilika badilika,kublid damu nyingi na kwa muda mrefu,kukosa kabsa hedhi kwa muda mrefu zaidi n.k


(2) Kuumwa na kichwa mara kwa mara 


(3) Kupatwa na Kizungu zungu


(4) Tatizo la kuhisi Kichefu chefu mara kwa mara


(5) Kuongezeka uzito wa mwili kwa baadhi ya watumiaji


(6) Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa kwa baadhi ya wanawake


(7) Mwanamke kukaa muda mrefu sana bila kubeba mimba baada ya kuacha kutumia njia hii


(8) Sindano za uzazi wa mpango huweza kulainisha mifupa ya mwili pia n.k


MADHARA YA VIDONGE VYA KUZUIA MIMBA


(1) Huweza kuathiri mzunguko wa hedhi kwa mwanamke pia


(2) Kuongeza uzito wa ute utokao katika njia ya uke ili kuzuia mimba kutunga 


(3) Tatizo la Kuumwa na kichwa mara mara


(4) Baadhi ya wanawake hupata kichefu chefu mara kwa mara


(5) Kutopata hedhi kwa baadhi ya wanawake

N.k


MADHARA YA KIJITI


(1) Huweza kusababisha mabadiliko makubwa kwenye mzunguko wa hedhi ikiwa ni pamoja na mwanamke kupata blid ya vitone vitone


(2) Kusababisha maumivu makali ya kichwa mara kwa mara


(3) Kusababisha tatizo la kichefuchefu mara kwa mara


(4) Kusababisha tatizo la kizungu zungu cha mara kwa mara

 

(5) Kupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa baadhi ya wanawake n.k


KUMBUKA:


Sio madhara yote humpata kila mtu, kuna wengine wanaweza wasipate pia!


Soma zaidi kuhusu njia za uzazi wa mpango hapa..!!!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

TATIZO LA KUPOTEZA UWEZO WA KUNUSAAfyaclass Bongo Social •

 PUA/HARUFU

• • • • • •

TATIZO LA KUPOTEZA UWEZO WA KUNUSA


Tatizo hili la kupoteza uwezo wa kunusa au mtu kusikia harufu ya kitu chochote ambapo kwa kitaalam hujulikana kama ANOSMIA hutokea sana kwa watu wengi hivi sasa, na kwa asilimia kubwa huendana na tatizo la kupoteza uwezo wa kutambua ladha ya kitu chochote kama chakula n.k, je chanzo chake ni nini?


CHANZO CHA TATIZO LA KUPOTEZA  UWEZO WA KUNUSA NI PAMOJA NA;


1. Kuvimba au kuziba kwenye pua kutokana na sababu mbali mbali kama vile; Uwepo wa uvimbe, tatizo la Nasal Polyps, Matatizo kwenye mifupa ya puani yaani Bone deformities n.k


hali ambayo hupelekea pua kushindwa kuhisi harufu pamoja na kuathiri mfumo mzima wa kutuma taarifa zinazohusiana na harufu kutoka puani kwenda kwenye ubongo.


2. Tatizo la kuharibika kwa ubongo pamoja na nerves kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


- Kupata ajali na kugongwa kichwani


- tatizo la uvimbe kwenye ubongo au Brain tumors


- Umri kuwa mkubwa zaidi


- Ugonjwa kama vile Alzheimers disease


- Matatizo ya mvurugiko wa vichocheo mwilini


- Matatizo ya tezi la thyroid kama vile underactive thyroid n.k


- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile viuwajisumu yaani antibiotics,dawa za presha n.k


- Ugonjwa wa kisukari


- Tatizo la kifafa au Epilepsy


- Matatizo kama vile multiple sclerosis


- Kuumia kichwani au kwenye ubongo


- Kufanyiwa upasuaji unaohusisha ubongo


- Kupata huduma ya mionzi yaani Radiotherapy


- Matumizi ya pombe kwa muda mrefu


- Tatizo la kiharusi au Stroke n.k


3. Sababu zingine ni kama vile;


- Tatizo la maambukizi ya magonjwa kama vile Sinus infections


- Tatizo la mafua makali au ya mara kwa mara, hii huchangia kwa asilimia kubwa mtu kushindwa kuhisi harufu ya kitu chochote


- Uvutaji wa sigara


- Tatiizo la Mzio au Allergy kama vile; Allergic rhinitis n.k


- Tatizo la kuziba pua kwa muda mrefu n.k


MATIBABU YA TATIZO LA KUPOTEZA  UWEZO WA KUNUSA


- Watu wenye tatizo hili huweza kupata tiba mbali mbali kulingana na chanzo cha tatizo hili, ikiwa ni pamoja na; matumizi ya dawa jamii ya

• DECONGESTANTS kama vile Phenylephrine


• au Jamii ya ANTIHISTAMINES


• Dawa jamii ya Steroids-nasal sprays


• Antibiotics mbali mbali


• Dawa za Allergies kama vile CETRIZINES n.k


KUMBUKA DAWA HIZI HUWEZA KULETA MAUDHI MADOGO MADOGO MWILINI BAADA YA MATUMIZI YAKE KAMA VILE;


✓ Mtu kuhisi kizunguzungu


✓ Hamu ya chakula kuisha kabsa


✓ Mtu kuhisi usingizi mzito au kukosa kabsa usingizi


✓ Presha kupanda juu


✓Hali ya kuwa na wasiwasi,kutokutulia n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD