AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO PAMOJA NA FAIDA ZAKE

MJAMZITO

• • • • • •

AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO


Nidhahiri kwamba mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito,lakini yapi ni mazoezi salama kwa mama mjamzito,Baadhi ya wakina mama wajawazito hushauriwa sana kuhusu kufanya mazoezi lakini hawaambiwi ni aina gani ya mazoezi ambayo ni salama kwao, Na kama ni hivo basi,kwa tafsri nyingine kuna mazoezi ambayo sio salama kabsa kwa mama mjamzito.


AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO NI PAMOJA NA;


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kutembea


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuogelea au Swimming


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli ambayo imesimama(Riding a stationary bike), hapa nitoe angalizo: ni hatari sana kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli inayotembea hasa ya magurudumu mawili tu,kwani ni rahisi sana kukosa balance na kudondoka hivo kuhatarisha ujauzito aliyobeba.


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya YOGA, mazoezi haya ni mazuri japo yanatakiwa kufanyika chini ya usimamizi wa wataalam yaani Instructor, kwani endapo mama atafanya mazoezi ya Yoga ambayo huhusisha zaidi kulalia Tumbo lake au kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First trimester huweza kuwa sio salama kwake.


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo mbali mbali vya mwili, Wakati wa kufanya mazoezi epuka kunyanyua vitu vizito sana


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kukimbia


- Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuruka kamba pamoja na vitu vingine mbali mbali, hapa pia ni muhimu kufanya mazoezi haya kwa msaada wa wataalam au Instructor kuhusu jinsi ya kuruka kamba taratibu,kwa sababu wapo ambao wameruka kamba sana na pia wakapata madhara kwenye ujauzito wao.


Hutakiwi kufanya mazoezi ya kuruka sana au kuruka kupita kiasi, hivo uangalifu mkubwa hutakiwa katika aina hii ya mazoezi Pamoja na mazoezi mengine ambayo sikuyataja hapa,


ANGALIZO: zingatia mambo haya wakati unafanya mazoezi


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kugandamiza tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First tremester


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha mtikisiko mkubwa sana wa tumbo


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kunyanyua vitu vizito sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kubana pumzi yako


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kuruka sana kupita kiasi


• Epuka kufanya mazoezi ya kucheza mpira kama vile mpira wa miguu wakati wa ujauzito

 N.k


FAIDA ZA MAMA MJAMZITO KUFANYA MAZOEZI


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia sana kuleta mzunguko mzuri wa damu kwenye mishipa ya damu,kwenye moyo pamoja na mapafu


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia ongezeko la uzito ambao hutakiwa kwa mama mjamzito


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na matatizo mbali mbali kama vile;


   • Kupatwa na tatizo la Kukosa pumzi


   • Kupatwa na tatizo la choo kigumu


   • Kupatwa na tatizo la kiungulia kikali


   • Kupatwa na tatizo la kuvimba miguu 


    • Kupatwa na tatizo la maumivu ya mgongo,misuli ya mwili 


     • Kupatwa na tatizo la mishipa ya damu kuvimba au Varicose veins N.k


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kupata usingizi wakati wa kulala


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa matatizo kama vile kisukari wakati wa ujauzito yaani Gestational diabetes,kifafa cha mimba n.k


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa mama mjamzito kujifungua kwa upasuaji


- Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia mama kuandaa mwili wake na labor,hata kupelekea urahisi wa mtoto kushuka,njia kufunguka na mama kuwa na pumzi ya kutosha wakati wa kusukuma mtoto.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!