TANZIA: Mwimbaji maarufu Nchini Afrika Kusini Zahara afariki Dunia

#1

TANZIA: Mwimbaji maarufu Nchini Afrika Kusini Zahara afariki Dunia.
• • • • • •
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Zizi Kodwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mwimbaji maarufu wa Nchi hiyo aitwaye Bulelwa Mkutukana maarufu kama Zahara (35) ambaye alitamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo ‘loliwe’

Zahara amefia Hospitalini Jijini Johannesburg alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya ini yaliyoanza kumsumbua wiki mbili zilizopita.

Kabla ya kifo chake leo, Mwimbaji huyo amekua akizushiwa kifo mtandaoni hivi karibuni hadi kulazimu familia yake kukanusha mara kwa mara na kutaka Watu wamuombee mema.

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code