Mvua kubwa,mvua za el nino mpaka Aprili: TMA TanzaniaAfyaclass Bongo Social •

Mvua kubwa,mvua za el nino mpaka Aprili: TMA Tanzania

TMA imesema kuna viashiria vya El-Nino kuendelea hadi Aprili, 2024.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema bado kuna viashiria vya uwepo wa El-Nino hadi Aprili mwaka huu.

El-nino ni mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki kwenye Bahari ya Pasifiki.

Mwaka jana, TMA ilieleza kuwepo kwa El-Nino katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zilizotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba.

Mvua zimeendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali nchini hadi sasa, TMA ikizitaja kuwa ni za nje ya msimu ambazo zimechangiwa na unyevunyevu kutoka magharibi ya misitu ya Congo, pia kuendelea kwa viashiria vya El-Nino.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Januari 30, 2024  Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema viashiria vya El-Nino bado vipo hadi Aprili.

“Viashiria vyake bado vipo, ingawa nguvu yake si kubwa kama ilivyokuwa awali, mwanzo ilionyesha kilele chake ni Desemba au Januari, lakini viashiria bado vipo hadi Aprili,” amesema.

Akizungumzia wingi wa mvua katika maeneo mbalimbali nchini, amesema unasababishwa na migandamizo midogo ya hewa iliyoko mashariki mwa Kisiwa cha Madagascar.

“Hii migandamizo imekuwa na mchango mkubwa kwenye kuvuta upepo wenye unyevunyevu kutoka magharibi ya misitu ya Congo kuja maeneo mengi ya nchi.

“Kuwepo kwa migandamizo hii kwa takribani wiki tatu na kuimarika kwa ukanda wa mvua kumesababisha uwepo wa mvua hizi, ingawa inaonyesha Februari mosi na pili, 2024 migandamizo hii itakwenda kusini mwa ncha ya Bara la Afrika, hivyo hata mvua zitaanza kupungua,” amesema.

Akizungumzia athari kwa wakulima, amesema maeneo ambayo mvua inanyesha kwa wingi, kiwango cha unyevunyevu kwenye udongo huongezeka.

“Unyevunyevu ukipitiliza unaweza kuathiri mazao ambayo hayaendani na maji mengi, ni vema wakulima wachukue ushauri kutoka kwa maofisa ugani,” amesema.

Amesema katikati ya Februari, 2024 watatoa utabiri wa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza Machi hadi Mei na kutoa mwelekeo wake.

Jana Januari 29, 2024, TMA ilitoa angalizo la uwepo wa hali mbaya ya hewa kwenye mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma kwa siku tano kuanzia leo Januari 30, 2024, ikiwataka watu wachukue tahadhari.

Angalizo hilo limetolewa tayari, baadhi ya mikoa kama vile Dar es Salaam na Morogoro ikishuhudia madhara makubwa ya miundombinu ya barabara, madaraja na nyumba yaliyotokana na mvua.

Mvua kubwa,mvua za el nino mpaka Aprili: TMA Tanzania
0 Comment

Daktari mkuu wa ganzi apitiwa na Usingizi mzito baada ya kumlaza mgonjwa kwa ganziAfyaclass Bongo Social •

Daktari mkuu wa ganzi apitiwa na Usingizi mzito baada ya kumlaza mgonjwa kwa ganzi.

Daktari mkuu wa ganzi ambaye alipitiwa na ‘usingizi mzito’ katika Chumba cha upasuaji dakika chache baada ya kumlaza mgonjwa kwa ganzi amesimamishwa kazi.

Daktari mkuu wa NHS nchini Uingereza amesimamishwa kazi baada ya kulala ‘usingizi mzito’ katika chumba cha upasuaji, mgonjwa alipokuwa akifanyiwa upasuaji.

Daktari mshauri, Thomas Herbst, mwenye umri wa miaka 61, alisinzia muda mfupi baada ya kumweka mgonjwa chini ya ganzi na ikasemekana kuwa alikuwa kwenye usingizi mzito hivi kwamba ilibidi agongwe begani na mwenzake ili kumwamsha.

Alipoulizwa kama alikuwa fiti kwa ajili ya kazi, Herbst alikunywa kikombe cha kahawa nyeusi na kusisitiza kuwa yuko sawa lakini alizungumza ‘bila mpangilio’ na kujirudia, kulingana na Mail Online.

Baadaye nje ya chumba cha kubadilishia nguo, inasemekana alihangaika kukamilisha karatasi huku suruali yake ya ‘scrub’ ikiendelea kuanguka bila yeye kujitambua.

Herbst ambaye alifanya kazi kama locum katika South West London Elective Orthopaedic Center iliyopo katika Hospitali Kuu ya Epsom huko Surrey awali alikanusha kusinzia lakini baadaye alisema alikuwa akifanya kazi kwa muda mrefu na kudai ugonjwa ambao haukutambuliwa ambao alisema kuwa ulimwacha kitandani kwa wiki tatu ulikuwa chanzo cha uchovu wake.

Iliibuka kuwa daktari huyo hapo awali alipewa onyo na Baraza Kuu la Madaktari kwa kulala kwenye chumba cha Upasuaji mnamo 2020 wakati mwenzake mwingine alikuwa akikamilisha upasuaji.

Katika Huduma ya Mahakama ya Madaktari, Herbst, wa East Sheen huko Richmond-on-Thames alikabiliwa na kufutwa kazi baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu lakini alisimamishwa kazi kwa miezi sita baada ya kujitolea kupunguza idadi ya zamu. alifanya kazi kila wiki.

Daktari mkuu wa ganzi apitiwa na Usingizi mzito baada ya kumlaza
mgonjwa kwa ganzi
0 Comment

Huduma za Kitabibu kutolewa kwa kutumia RobotiAfyaclass Bongo Social •

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Profesa Abel Makubi amesema Taasisi hiyo inatarajia kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa kutumia roboti ndani ya miaka mitatu ijayo.

Akiongea kwenye mahojiano maalum na @AyoTV_ , Prof. Makubi amesema “Sasa hivi tunafanya evaluation tuweze kujua kwani tayari tuna vitu vingi tunafikiria kuvifanya lakini tunawaangalia wenzetu walifanya vitu gani ili kufikia hapa kwa haraka, kwahiyo tunafanya hiyo evaluation itatusaidia kutochukua muda mrefu kufikia hapo kama wenzetu”

“Kuna timu inafanya assignment kwenye suala la kutumia roboti na mitambo mingine zaidi ya kiteknolojia ya kisasa ambayo inatumia akili za kibinadamu (Artificial Intelligence) kufanya yenyewe badala ya kumtumia Binadamu ili kurahisisha kazi na kupunguza muingiliano na kumfanya Binadamu mwenyewe akifanyiwa oparesheni awe na matokeo mazuri zaidi, kwahiyo maandalizi yanafanyika tunategemea ndani ya miaka miwili ama mitatu ijayo tuweze kufanya oparesheni hiyo hapa MOI na hiyo itasaidia kwa asilimia 99 kupunguza oparesheni za Wananchi kwenda nje”

Huduma za Kitabibu kutolewa kwa kutumia Roboti
0 Comment

Binadamu wa kwanza kuwekewa kipandikizi kutoka Neuralink anaendelea vizuri - Elon MuskAfyaclass Bongo Social •

“Binadamu wa kwanza kuwekewa kipandikizi kutoka Neuralink anaendelea vizuri”. – Elon Musk

Bilionea wa teknolojia Elon Musk amesema kwa mara ya kwanza kampuni yake ya Neuralink imefanikiwa kupandikiza kifaa maalum cha eletroniki kwenye Ubongo wa binadamu kisichotumia nyaya.

Lengo la kampuni ni kuunganisha akili za binadamu na kompyuta ili kusaidia kukabiliana na changamano za neva.

Inatarajiwa kuwa kifaa hicho kuwa kiunganishi cha ubongo na kitawasaidia watu waliopooza viungo kuweza kudhibiti vifaa kama simu na kompyuta wakitumia fikra zao.

Katika chapisho lake kwenye X, zamani Twitter, Musk alisema kwamba mgonjwa “anaendelea vizuri,” na kwamba matokeo ya awali yanaonesha matumaini.

Binadamu wa kwanza kuwekewa kipandikizi kutoka Neuralink anaendelea
vizuri - Elon Musk
0 Comment

Upasuaji Mkubwa wa kuwatenganisha mapacha walioungana tumbo na kifua KukamilikaAfyaclass Bongo Social •

Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo mkoani Dar es Salaam kwa mara nyingine imeandika historia kwa kufanya upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumbo na kifua na kuwa upasuaji wa kwanza kufanywa na madaktari wazawa hapa nchini.

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville amesema upasuaji huo umefanikiwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa kununua vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuwasomesha wataalamu.

“Tunachojivunia katika upasuaji huu ni kuwa umefanywa na timu ya madaktari wazawa, umefanyika kwa mafaniko makubwa na watoto wanaendelea vizuri kabisa. Lakini pamoja na kufanikiwa kufanya upasuaji huu bado tutaendelea kushirikiana na wataalamu wengine kwa ajili ya kuendelea kupata ujuzi zaidi na kuendeleza uhusiano”. Amesisitiza Dkt. Mhavile.

Kwa upande wake daktari bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Victor Ngota ameeleza kuwa upasuaji wa kuwatenganisha watoto unahitaji utaalamu wa hali ya juu, hivyo ulihusisha jopo la wataalamu mbalimbalI.

“ Tuliwapokea watoto hawa tarehe 11 Machi 2023 hivyo tulianza mchakato wa kuwahusisha wataalamu ambao wanahusika na huduma hizi, ilituchukua takribani muda wa miezi kumi kuangalia mwenendo wao wa afya kwa ujumla kabla ya kuwatenganisha ili kuweza kupata dira ya namna watakavyoishi mara baada ya kutenganishwa”. Amefafanua Dkt. Ngota.

Upasuaji huo umefanyika kwa muda wa takribani saa sita hadi kukamilika.

Upasuaji Mkubwa wa kuwatenganisha mapacha walioungana tumbo na kifua
Kukamilika
0 Comment

Mjamzito kuumwa tumbo,chanzo chake hiki hapaAfyaclass Bongo Social •

Mjamzito kuumwa tumbo,chanzo chake hiki hapa

Chanzo cha Mjamzito kuumwa tumbo

Mjamzito kuumwa tumbo ni tatizo ambalo huwapata wanawake wengi pindi wakiwa wajawazito, tatizo hili hujulikana kama Stomach (abdominal) pains or cramps na ni kawaida kutokea hivi.

Sio tatizo ambalo ni la kukupa wasiwasi sana,Ingawa wakati mwingine hii ni Ishara mbaya, hivo huhitaji uchunguzi Zaidi.(Soma hapa Dalili za hatari kwa mama mjamzito)

Sio kitu cha kuwa na wasiwasi ikiwa maumivu ni kidogo na yanaondoka unapobadilisha mkao, kupumzika, kujisaidia au kupitisha upepo. Lakini ikiwa una maumivu ya tumbo na una wasiwasi, hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwanza, au tuwasiliane hapa ndani ya @afyaclass

Mjamzito kuumwa tumbo ambako sio kwa kutilia Mashaka hutokana na;

  • Maumivu yanayojulikana kama ligament pain au “growing pains” haya ni maumivu unayoyapata wakati ligaments zinapojivuta ili kusupport ujauzito unaokua, Hii huweza kusababisha ujisikie maumivu(sharp cramp) hasa upande mmoja wa chini ya tumbo
  • Maumivu ya tumbo kwa Sababu ya shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation)– ambako hii ni kawaida kutokea kwa mjamzito. Soma hapa jinsi ya kudhibiti hali hii
  • Pamoja na Sababu zingine…!!!!

Dalili za hatari kwa mjamzito

Hakikisha Unapata Msaada wa Haraka ikiwa ni Mjamzito halafu unapata Maumivu ya Tumbo yanayoambatana na vitu hivi;

– Kuvuja Damu Ukeni

– Kupata maumivu ya tumbo yanayoambatana na tumbo kukaza sana mara kwa mara(regular cramping or tightenings)

– Kutokwa na Uchafu Ukeni ambao siokawaida(wenye harufu mbaya, rangi ya njano n.k)

– Kupata maumivu makali chini ya mgongo(lower back pain)

– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa

– Kupata maumivu makali ya tumbo na ambayo hayaishi hata baada ya kupumzika kwa zaidi ya dakika  30 mpaka 60 n.k

Yoyote kati ya hizi inaweza kuwa dalili za kitu ambacho kinahitaji kuchunguzwa au kutibiwa haraka(dalili ya hatari).

Chanzo cha Maumivu ya Tumbo ambayo ni Hatari

Baadhi ya  hali hizi huweza kuwa chanzo cha Maumivu makali ya tumbo ambayo yanahitaji msaada wa haraka;

1. Tatizo la Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Huu ndio wakati yai lililorutubishwa hupandikizwa nje ya tumbo la uzazi, kwa mfano kwenye mrija wa fallopian. Mimba haiwezi kuishi na inahitaji kuondolewa kwa dawa au upasuaji.

Dalili kawaida huonekana kati ya wiki 4 na 12 za ujauzito na zinaweza kujumuisha:

  • maumivu ya tumbo na kutokwa na damu
  • maumivu katika ncha ya bega lako
  • usumbufu wakati wa kukojoa au kujisaidia haja kubwa n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu mimba kutunga nje ya kizazi ectopic pregnancy hapa.

2. Tatizo la Mimba kutoka(Miscarriage)

Kupata maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na hali ya tumbo kuvuta(Cramping pains) pamoja na kuvuja damu ukeni kabla ujauzito haujafika wiki 24 au 28,

Hii ni dalili kubwa ya mimba kutoka au kutishia kutoka(Sign of miscarriage or threatened miscarriage).

3. Tatizo la Kifafa cha Mimba(Pre-eclampsia)

Maumivu chini ya mbavu ni ya kawaida katika ujauzito wa baadaye kutokana na mtoto anayekua na uterasi kusukuma chini ya mbavu.

Lakini ikiwa maumivu haya ni mabaya/makali au ya kudumu, hasa upande wa kulia, inaweza kuwa ishara ya pre-eclampsia (shinikizo la damu wakati wa ujauzito au kifafa cha mimba) ambayo huwapata baadhi ya wajawazito. Kawaida huanza baada ya wiki 20 au tu baada ya mtoto kuzaliwa.

Dalili zingine za preeclampsia ni pamoja na:

  • maumivu ya kichwa kali
  • matatizo ya kuona marue rue au kutokuona vizuri
  • kuvimba sana miguu, mikono na uso n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu pre-eclampsia

4. Uchungu wa mapema(Premature labour)

Iwapo una mimba ya chini ya wiki 37 na unakuwa na mikazo ya mara kwa mara ya tumbo au kubanwa pamoja na tumbo kuuma sana, wasaliana na wataalam wa afya mapema.

Hii inaweza kuwa ishara ya leba ya mapema, na utahitaji kufuatiliwa hospitalini.

5. Kupata tatizo la Placental abruption

Huu ndio wakati placenta inapoanza kutoka kwenye ukuta wa tumbo la uzazi, kwa kawaida husababisha kutokwa na damu na maumivu makali ya mara kwa mara ambayo hayaji na kuondoka kama maumivu ya kubana kwa tumbo.

Wakati mwingine ni dharura kwa sababu ina maana kwamba kondo la nyuma linaweza kukosa kumudu mtoto wako ipasavyo.

Unapaswa kwenda hospitali ili wewe na mtoto wako mchunguzwe.

Pata maelezo zaidi kuhusu tatizo la Placental abruption

6. UTI (maambukizi ya njia ya mkojo)

UTI ni ya kawaida wakati wa ujauzito na inaweza kutibiwa kwa urahisi.

Maambukizi haya ya njia ya Mkojo yanaweza kusababisha maumivu ya tumbo wakati mwingine, lakini si mara zote, unaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu tatizo la UTI.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mjamzito kuumwa tumbo,chanzo chake hiki hapa
0 Comment

Wapona sikoseli baada ya kupandikizwa ulotoAfyaclass Bongo Social •

Wapona sikoseli baada ya kupandikizwa uloto

Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma imeandika historia ya watoto watatu kupona ugonjwa wa Sikoseli baada ya kuwafanyia matibabu ya upandikizaji wa Uloto.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakati akitoa taarfa rasmi kwa vyombo vya habari leo jijini Dodoma baada ya mwaka mmoja tangu Hospitali hiyo ifanye Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto kumtibu mtoto mwenye Ugonjwa wa Sikoseli

Dkt. Chandika amesema watoto hao hawana maradhi ya Selimundu tena, na kwamba serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi ya Billioni 3.6 kuwezesha huduma hizo ili kuokoa maisha watanzania.

“Leo ni siku muhimu sana, ninawataarifu watanzania, Afrika na Dunia nzima kwa Ujumla kwamba Watoto tuliyowapandikiza Uloto hawana Ugonjwa wa Selimundu, wana afya njema, na vipimo vimethibitisha hawana ugonjwa huo tena” ameeleza Dkt. Chandika.

Aidha, Dkt. Chandika, amewashukuru wazazi wa Watoto hao, ambao ni Grace Hosea (8), Elisha John (11), na Isack Kedmond (10), kwa kuiamini hospitali hiyo na kuruhusu Watoto wao kuwa wa kwanza kupokea Huduma za Upandikizaji wa Uloto.

Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto yanagharimu kati ya Shilingi milioni 55-65, hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa, kumhudumia mtoto mwenye Seilimundu dawa za kupunguza makali ya ugonjwa, fedha hizo zinaweza kukidhi huduma kwa miaka mitano pekee.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1 katika bajeti ya Mwaka huu wa Fedha kwa ajili ya Matibabu ya Selimundu, hakuna hata mzazi mmoja ametoa fedha, gharama zote zimebebwa na serikali” ameshuku Dkt. Chandika.

Akitoa ushuda Mtoto Elisha John (11), kwa niaba ya Watoto wenzake waliyopokea huduma ya kupandikizwa Uloto, amesema changamoto zote alizokuwa nazo zimetoweka.

“Nilikuwa napata shida ya kuumwa kichwa, damu yangu ilikuwa haizidi sita, shuleni nilikuwa simalizi mwezi, lazima nitalazwa wiki nzima, sihudhurii vipindi shule, tangu nimetibiwa sijasikia maumivu yoyote”ameeleza Mtoto Elisha.

Kwa mujibu wa Mzazi wa Elisha, kumhudumia mtoto mwenye Sikoseli ni kujitoa sadaka, ambapo mzazi mmoja alilazimika kuacha kazi ili kuwa karibu na mtoto wao.

“Kupata wiki moja ya kutokuugua kwake lilikuwa jambo la muujiza, kwa miaka hiyo 11 ya kuugua kwake, ilibidi mama yake aache kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, kwa sababu Ugonjwa huo hauna muda maalumu, hali ingeweza kubadilika muda wowote” alisema Joseph John.

Mbali na Shukrani kwa BMH na Serikali kwa nafuu aliyoipata mtoto wake, ametoa wito kwa serikali kuangalia uwezekano wa kujenga Hosteli Jirani na Hospitali hiyo, ili kusadia familia zinazotoka nje ya Dodoma kufuata huduma hiyo BMH.

Wito huo uliungwa mkono na Profesa, Cornell Uderzo, Bingwa wa Magonjwa ya Damu na Upandikizaji Uloto kutoka Shirika la Help 3 la nchini Italia, Washirika wa BMH katika huduma za Upandikizaji wa Uloto, kwa kusema kuwa hitaji la Hosteli ni Muhimu si tu kwa BMH, bali ni protokali ya matibabu hayo.

“Kote duniani, si hapa pekee, kunakuwa na makazi ya familia Jirani na Hospitali, kuziwezesha familia kukaa angalau kwa miezi 3 baada ya kuruhusiwa kutoka wodini, kuruhusu madaktari kumfuatili mgonjwa kwa karibu, ikiwa kuna changamoto yoyote, hasa maambukizi” alisema Profesa Uderzo.

Tanzania inashika nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Selimundu, ni ya 3 kwa nchi za Afrika, huku idadi ya Watoto 11,000 wakikadiliwa kuzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka, ambapo asilimia 50 hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka 5.

Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianza kutoa huduma za Upandikizaji wa Uloto mwaka jana, ikiwa ya kwanza kutoa huduma hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki na kati, hadi sasa Watoto 7 wamenufaika na huduma hiyo, huku wengine tisa wakiwa katika mlolongo wa matibabu.

Wapona sikoseli baada ya kupandikizwa uloto
0 Comment

Kuelewa Ugonjwa wa bawasiri: Chanzo, Dalili, na Matibabu BoraAfyaclass Bongo Social •

Kuelewa Ugonjwa wa bawasiri: Chanzo, Dalili, na Matibabu Bora

Utangulizi:

Bawasiri, inayojulikana pia kama “piles au hemorrhoids,” inahusisha uvimbe na kutuna kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa, ikisababisha changamoto wakati wa kutoa kinyesi au kujisaidia haja kubwa.

Ugonjwa wa bawasiri huweza kumpata mtu wa jinsia yoyote(mwanaume&mwanamke)

Aina za Ugonjwa wa Bawasiri:

Kuna aina mbili kuu za bawasiri:

  1. Bawasiri za Ndani
  2. Bawasiri za Nje

Sababu za Ugonjwa wa Bawasiri:

Ingawa chanzo kamili cha ugonjwa wa bawasiri hakijulikani, wataalamu wa afya mara nyingi huzungumzia mambo kadhaa yanayochangia kutokea kwa bawasiri ikiwemo:

1. Kuwa na shida ya kupata Choo kigumu hasa ikiwa kwa muda mrefu(chronic constipation)

2. Kujitahidi,kujikaza au kutumia nguvu sana wakati wa kutoa kinyesi

3. Kuketi chooni kwa muda mrefu

4. Bawasiri pia inaweza kutokea kutokana na shughuli za kimwili kama vile;kunyanyua vitu vizito, vikisababisha shinikizo zaidi kwenye eneo husika.

Viashiria vya Hatari vya kupata Ugonjwa wa bawasiri;

Baadhi ya mambo yanayoongeza hatari ya kuwa na bawasiri ni pamoja na:

  • Ujauzito, kutokana na shinikizo kubwa la tumbo
  • Shida hii kuwa Zaidi kwenye familia
  • Uzito Mkubwa
  • Kupata Choo kigumu mara kwa mara n.k

Kutambua Ugonjwa wa Bawasiri:

Kufahamu dalili za Ugonjwa wa bawasiri ni muhimu. Ishara na dalili ambazo huonekana sana ni pamoja na:

– Kuwashwa sehemu ya haja kubwa

– Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa

– Kuwa na Uvimbe au kutokeza kwa Kinyama sehemu ya haja kubwa

– Kuhisi kuchomwa au mchanga sehemu ya haja kubwa n.k

Ni muhimu kutofautisha maumivu ya bawasiri na matatizo mengine kama vile michubuko au proctitis.

Uchunguzi na Vipimo:

Wataalamu wa afya hufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia anoscope, kifaa maalum kinachoingizwa sehemu ya haja kubwa, ili kuona hali ya njia ya haja kubwa na kutambua kama una Ugonjwa wa bawasiri au la!

Pia kupitia dalili na Ishara alizonazo mgonjwa huweza kusaidia kuitambua bawasiri kwa haraka.

Tiba na Mabadiliko ya Maisha:

Matibabu ya Ugonjwa wa bawasiri yanaweza kufanyika nyumbani au hospitalini. Mabadiliko ya maisha, kama vile kuongeza unywaji wa maji na lishe yenye wingi wa nyuzi nyuzi, ni muhimu kwako.

Ongeza matunda, mboga, na nafaka nzima kwenye lishe.

Fikiria virutubisho vya nyuzi nyuzi kama vile psyllium au methylcellulose kama lishe haijatosheleza.

Hakikisha unakunywa maji ya kutosha, angalau glasi sita hadi nane kwa siku.

Ushauri wa Kitaalam:

Kwa ushauri Zaidi, elimu, au matibabu, wasiliana nasi kupitia +255758286584. Tupo hapa kukusaidia.

Hitimisho:

Kuelewa chanzo, dalili, na chaguzi sahihi za matibabu ya ugonjwa wa bawasiri kunawawezesha watu kushughulikia na kuzuia tatizo hili kwa ufanisi. Jisikie huru kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi na taarifa.

Kuelewa Ugonjwa wa bawasiri: Chanzo, Dalili, na Matibabu Bora
0 Comment

Dawa ya gono kwa mwanaumeAfyaclass Bongo Social •

Dawa ya gono kwa mwanaume

Je, ni ipi dawa sahihi ya kutibu ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?

Dawa ya gono kwa Mwanaume; Baada ya kupata Maswali mengi kuhusu dawa sahihi ya Gono kwa Mwanaume,tumeambua kukuandalia Makala hii hapa;

Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,

Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;

Dawa ya gono kwa mwanaume huweza kutibu kabsa tatizo hili ikiwa umepata tiba Sahihi,

Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati unapata au Kutumia Dawa ya Gono kwani badala ya kutibu gono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”

Kwa hivi Sasa,Ukinzani wa viua vijidudu kwenye ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Mgumu.

Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kudundulika una ugonjwa wa gono, hakikisha unapata dawa ya Gono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.

Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Gono – ufuatiliaji wa dawa ya gono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.

Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,

Kipimo cha tiba kinahitajika siku 7-14 baada ya matibabu kwa watu wanaotibiwa maambukizi ya koo. Kwa sababu kuambukizwa tena ni kawaida,

wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.

Dawa ya gono kwa mwanaume

Dawa ya gono;

Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”

Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ambapo huweza kutumika ni pamoja na;

  • Sindano
  • Na Vidonge

Ingawa dawa hizi Zitazuia maambukizi ya Gono hazitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.

NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dawa ya gono kwa mwanaume
0 Comment

Fahamu haya kuhusu ulaji wa ‘kuku wa kizunguAfyaclass Bongo Social •

Fahamu haya kuhusu ulaji wa ‘kuku wa kizungu’

Wafugaji wengi wanapendelea kuku wa kizungu

Barani Afrika, wafugaji wengi hutegemea zaidi kuku kizungu. Kuku hawa pia nyama pia huitwa “kuku wa kisas, kuku wa nyama ” ambapo huitwa majina hayo kwamepewa kutokana na nyama yake na ukuaji wake wa haraka.

“Kuku hawa karibu wamekuwa maarufu kwasababu huwaingizia pesa nyingi wafugaji na ni tofauti na kuku wa kienyeji ambao kwa kawaida tunawaita kuku wa baiskeli nyumbani nchini Togo, ambao huchukua muda mrefu zaidi kukua.

Kwa vyovyote vile, kula kile unachozalisha nyumbani ni bora kuliko kuku waliogandishwa kutoka nje,” anaamini Eugène Menou, Mjasiriamali, mmiliki wa shamba la kuku katika mkoa wa Vo nchini Togo.

Katika soko la Afrika, walaji, hasa wale wenye bajeti ndogo, wanapendelea kuku wa kizungu au wa kisasa kwa sababu ni wanauzwa kwa bei nafuu kuliko kuku wa kienyeji ambao ni ghali zaidi.

Na kutaokana na hili leo tumeamua kuangazia zaidi kuku wa kizungu katika makala hii.

‘’Kwa sababu unapoweka kuku wa kienyeji au wa asili sokoni, watu wanawaona kuwa ni wa gharama sana ingawa ni kuku wenye afya zaidi na wana virutubisho muhimu zaidi kwa mwili,” anasema Eugène.

Kwa ujumla, wataalamu wa lishe wanapendekeza ulaji wa nyama nyeupe kwa faida nyingi zilizomo. Na kuku ni mmoja wao. Kuku wa kienyeji ambao wanapendekezwa zaidi wanakuwa vyakula adimu, kwani wafugaji hupata faida zaidi katika ufugaji wa kuku wa nyama.

“Uzalishaji wao ni wa haraka na wana faida zaidi kuliko kuku wa kienyeji ambao huchukua muda zaidi na rasilimali,” anaongeza.

Aidha anadokeza kuwa inachukua siku 21 kwa yai la kuku wa nyama kukomaa na kuwa kifaranga ambacho kitakuwa tayari kuliwa ndani ya miezi mitatu pekee.

“Hapa, katika soko la Gbossimé, kuku wa kienyeji wanauzwa 4,500 FCFA huku wale wa nyama wakigharimu 3,500 FCFA. Unaweza kuona tofauti kidogo. Ni wazi kwamba tunaweza kumudu kununua tu kile ambacho ni cha bei nafuu, kutokana na matatizo ya sasa ya kifedha,” Bi. Kayi, mama wa nyumbani, anaiambia BBC Africa kutoka Lomé.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe na mtaalamu wa usafi na ubora wa chakula, Dk Matthieu Tobossi, kuku wa kisasa wanafaa kuliwa kwa kiasi, ikizingatiwa kuwa ni sehemu ya GMOs (viumbe vilivyobadilishwa vinasaba).

Kulisha umma kwa ujumla

Kuku hawa lazima wazalishwe haraka na kwa wingi ili kukidhi mahitaji duniani

Hii ndiyo sababu kuu ya ufugaji wa kuku duniani hivi sasa. Kuku hawa lazima wazalishwe haraka na kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya nyama yanayoongezeka kila mara.

“Migahawa na hoteli ndio inayowahitaji zaidi. Ni lazima tuweze kukidhi mmahitaji yao. Kwa hivyo hatuwezi kutarajia kuku wa kienyeji au wa asili katika kiwango hiki.

Kuku wa nyama hukidhi vyema mahitaji haya. Tunajaribu kupunguza usambazaji wa kemikali kwa kuku hawa kwa njia bora iwezekanavyo,” anasema Koffi G,mfugaji mwingine nchini Togo.

Kuku hawa wanaofugwa kwa ajili ya uzalishaji wa nyama yao, pia huitwa grill, pia huwapa walaji virutubisho, kulingana na wataalamu wa lishe. Ni chanzo muhimu cha lishe kwa umma kwa ujumla.

Thamani ya lishe

Mbali na maonyo hayo kutoka kwa wataalamu wa lishe, mara nyingi yanaonyesha kuwa kuku kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na nyama, ina vitamini nyingi na vitu vingine vingi vinavyotoa thamani kubwa ya lishe kwa mwili wa binadamu.

Zaidi ya kemikali zinazodungwa kwenye kuku wa nyama ili kuwafanya waweze kuliwa haraka, pia wana vitu vya kuvutia kama kuku wengine.

Kuku haw awa kisasa mara nyingi hulishwa ngano, mahindi, lakini pia protini, vitamini na kufuatiliwa kiafya. Asidi muhimu za mafuta pia ni sehemu ya lishe yao mbayo huchangia thamani ya lishe ya nyama yao kwa mwili wa binadamu, kulingana na Dk Tobossi.

Tunaweza kuelewa kuwa kuku huyu ana thamani ya lishe kama nyama nyingine nyeupe.

Kuku wa nyama huwa na protini zinazochangia ukuaji wa misuli.

Seli zote za tishu zilizo hai, na protini ni muhimu kwa utendaji mzuri wa mwili. Kuku wa nyama huwa na protini zinazochangia ukuaji wa misuli. Kwa hiyo, kula kuku ni muhimu kwa misuli, mifupa na homoni, kulingana na wataalamu wa lishe.

Wanasema, nyama ya kuku hutoa asidi ya amino ambayo mwili hauwezi kuizalisha. Ni kupitia chakula, hasa kuku, kwamba asidi hizi muhimu za amino hutolewa kwa mwili.

Kutokana na lishe yake, kuku hawa wana vitamini nyingi. Nyama yake hutoa vitamini B3 inayoitwa niasini. Ni vitamini ambayo husaidia kuweka ngozi kuwa na afya. Pia kuna vitamini B6 ambayo inashiriki katika mchakato wa udhibiti na ujenzi wa tishu kutoka kwa protini.

Kuku pia wana vitamini B5 au asidi ya pantothenic, muhimu kwa upyaji wa ngozi na nywele. Pia husaidia utendaji mzuri wa mfumo wa kinga.

Wataalamu wa lishe wanapendekeza ulaji wa nyama ya kuku badala ya ngozi. 100g ya nyama ya kuku hutoa zaidi ya 50% ya lishe ya kila siku. Hizi ni kalori, vitamini na madini ambayo hutolewa kwa mwili. Kuku huitwa chakula cha wajenzi, kulingana na Dk Tobossi. “Inapendekezwa kwa watoto, wazee, wajawazito, wanamichezo, wagonjwa n.k. “, anasisitiza.

Lakini jihadhari na kuku wa nyama (kuku wa kisasa, au wa kizungu)

Wafugaji wengi hutumia kemikali na homoni za ukuaji ili kuwa na kiasi kikubwa cha kuku wa nyama kwa muda mfupi sana. Na kwa hiyo matumizi yake ya mara kwa mara yanaweza kusababisha matatizo ya kiafya, kwa mujibu wa wataalamu wa lishe wanaodai kuwa ni kwa sababu ya kemikali zinazotumika kwa ukuaji wa haraka wa kuku hawa.

“Tuligundua kuwa baadhi ya wafugaji hutumia kupita kiasi dawa za antibiotiki kwa kuku kupita kiasi. Hii husababisha bakteria wa matumbo na straphylococci kuongezeka,” anasema Dk Tobossi, ambaye anasisitiza kuwa ndio chanzo cha magonjwa ya moyo na mishipa na kudhoofika kwa mfumo wa kinga.

“Hii ndiyo sababu kila mara tumeshauri ulaji wa kuku wa nyama kwa kiasi, wakati hakuna kuku wa kienyeji au wa asili,” anasisitiza.

Nyama hii ina mabaki na chembe chembe nyingine za kemikali ambazo ni hatari, hasa kwa moyo. Zaidi ya hayo, kuku wa nyama hulelewa katika mazingira ambayo sio ya asili kwa ndege hawa, ambayo hupunguza ubora wa nyama yao.

Kwasababu ya matunzo yao wana uwezekano wa kuwa sababu ya magonjwa fulani, kwamba watu wanaombwa kupika nyama vizuri kabla ya kuwala.

Mjasiriamali Eugène Menou anaongeza: “Kuna washiriki wa chama chetu ambao hujiingiza katika mazoea ya kuchinja kuku wanapotambua kwamba ni wagonjwa. Bila kujaribu kuelewa, wanazichinja na kuzipeleka sokoni. Hii ni tabia ambayo tunajaribu kuipiga marufuku.”

Kwa mtaalamu wa lishe, aina hizi za kuku lazima zichomwe ili kuepusha tatizo la afya ya umma.

Kwa vyovyote wasemavyo watu Chochote kuku ni chakula kizuri ambacho hutoa virutubisho vingi kwa mwili. Lakini lazima tuwe waangalifu tunapotumia kuku wa nyama ambao, ingawa pia wana viwango vya lishe, lazima waliwe kwa kiasi kwa sababu ya hali ambayo wanafugwa .

Via:Bbc

Fahamu haya kuhusu ulaji wa ‘kuku wa kizungu
0 Comment

Wateka nyara watishia kumuua daktari aliyetekwa nyara KadunaAfyaclass Bongo Social •

Wateka nyara watishia kumuua daktari aliyetekwa nyara Kaduna, mume na mvulana wa miaka 16 ikiwa familia itashindwa kulipa fidia ya N100m.

Watekaji nyara wa daktari wa macho wa Jimbo la Kaduna nchini Nigeria, Ganiya Olawale-Popoola, mumewe, afisa wa Jeshi la Wanaanga, Nurudeen Popoola, na mgeni wao, AbdulMugniy Folaranmi, wametishia kuwaua waathiriwa hao ikiwa familia zao zitashindwa kulipa fidia ya N100m.

LIB iliripoti kuwa waathiriwa walitekwa nyara katika Kituo cha Kitaifa cha Macho kilicho katika Eneo la Serikali ya Mitaa ya Igabi katika Jimbo la Kaduna mnamo Desemba 27, 2023.

Chanzo cha familia kilichozungumza na Punch kwa masharti ya kutotajwa jina, kilisema kuwa licha ya jitihada zilizofanywa na familia hiyo kujadili kupunguzwa kwa fidia, watekaji nyara walisisitiza juu ya fidia ya N100m.

Ilikusanywa kuwa hakuna chochote kilichosikika kutoka kwa watekaji nyara hadi siku ya nne baada ya kutekwa nyara walipopiga simu na kutaka malipo ya N100m kama fidia kabla ya kuachiliwa kutoka utumwani.

Chanzo cha familia kilisema kuwa watekaji nyara hao wanadaiwa kutishia kuwaua wenzi hao ikiwa N100m haitalipwa kabla ya Januari 18.

Watekaji nyara waliwasiliana na familia mnamo Ijumaa, Januari 26,  wakisisitiza kwamba wangewaua waathiriwa ikiwa fidia haitalipwa.

“Watekaji nyara walitufikia siku ya Ijumaa. Wakati wowote walipofikia, walimwomba mmoja wa waathiiriwa ambaye alielewa Kihausa na Kiingereza azungumze nasi. Walisisitiza kwamba hawakurudi nyuma kwenye fidia ya N100m,” chanzo kilisema.

“Tumewasihi hata kufikiria kukusanya N20m ambazo familia iliweza kuzileta lakini walikataa. Kila mtu katika familia yuko katika hali ya kuchanganyikiwa ni nini kifanyike.”

Chanzo hicho kilieleza zaidi kuwa familia hiyo ilipofika Jeshi la Anga na mamlaka ya polisi ilielezwa kuwa wanafanya kazi ya kuachiwa bila kupata majeruhi huku wakiomba mamlaka zinazohitajika kusaidia kufanikisha kuachiwa kwa familia yao.

“Tumefika polisi na Jeshi la Anga lakini walichokuwa wanatueleza ni kwamba walikuwa wanafanya kazi ya kuwafanya waachiwe kutoka kwa watekaji wao, wao (Jeshi la Polisi na Jeshi la Anga) walituambia kuwa wamekuwa makini ili wasipate waathiriwa wakiwa wamejeruhiwa wakati wa kuwaokoa.

“Tunaiomba kama familia kwa serikali ya Nigeria itusaidie kuachiliwa kwa wanafamilia wetu. Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu watekwe nyara na tumechoka kama familia. Hakuna jinsi tunaweza kuongeza fidia ya N100m. watekaji wanadai,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Jumatatu, Ofisa Uhusiano wa Polisi wa Jimbo la Kaduna, Mansir Hassan, alisema kamandi hiyo ilikuwa ikifanya juhudi za kuwaachilia watu waliotekwa nyara bila majeruhi.

“Kuna matukio mengi ya utekaji nyara ambayo tuliyarekodi siku za hivi karibuni, tumeweza kuwaokoa baadhi ya wahanga na kuwatia mbaroni baadhi ya watekaji nyara, polisi hawalegei katika kuhakikisha wahanga wote waliotekwa wanaokolewa kutoka kwa watekaji. tunataka kuhakikisha hakuna majeruhi tunapowaokoa,” Hassan alifichua.

Wateka nyara watishia kumuua daktari aliyetekwa nyara Kaduna
0 Comment

Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea madaktari bingwa wa mifupa na ubongo kutoka ChinaAfyaclass Bongo Social •

Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea madaktari bingwa wa mifupa na ubongo kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakaohudumu kwa kipindi cha miaka miwili ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano baina ya Tanzania na China.

Akizungumza leo Januari 29, 024 wakati wa hafla fupi yakuwapokea madaktari hao kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo wa MOI Dkt. Lemeri Mchome ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kuongeza kuwa ujio huo utaongeza ujuzi na umahiri kwa madaktari wazawa.

“Wenzetu China wamepiga hatua katika tiba za mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, hivyo uwepo wao hapa utasaidia kuwajengea uwezo kwa madaktari wetu, ninaaamini walivyotukuta sivyo ndivyo watakavyotuacha, umahiri wetu utakuwa umepanda” amesema Mchome

Kwa upande wake mwenyeji wa madaktari hao Dkt. Liggy Vumilia kutoka wizara ya afya amesema madaktari hao 11 watakuwapo nchini kwa miaka miwili wakitoa huduma katika Taasisi ya MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

“Tanzania na China zimekuwa katika uhusiano kwa zaidi ya miaka 60 sasa…ujio wa madaktari hawa ni muendelezo wa ushirikiano huo, wito wangu kwenu kuhakikisha mnawatumia vyema madaktari hawa ili tupate ujuzi walio nao, ni imani ya wizara kuwa huduma zetu zitaboreshwa kwa kuwatumia vizuri madaktari hawa”

Mratibu wa Mafunzo na Utafiti wa MOI Dkt. Joel Bwemelo amesema ujio wa madaktari bingwa hao unalenga kubadilishana uzoefu wa kutoa tiba kwa ufaninsi na hivyo kuboresha huduma kwa wagonjwa.

“Tumepokea madaktari bingwa watatu, mmoja wa usingizi, mwingine wa mifupa na wa tatu ni wa ubongo, wawili watakuwapo hapa kwa mwezi mmoja na nusu kabla ya kwenda hospitali ya rufaa Mbeya, na huyu mmoja atakuwa MOI kwa miaka yote miwili.

Kiongozi wa madaktari hao Dkt. Cheny Jiyong ameishukuru MOI kwa mapokezi na kuahidi kutoa ushirkiano wa dhati katika kutekeleza majukumu yao.

Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea madaktari
bingwa wa mifupa na ubongo kutoka China
0 Comment

kusagana ni nini? Maana yake na Madhara yakeAfyaclass Bongo Social •

kusagana ni nini? Maana yake na Madhara yake.



kusagana ni nini?

Kusagana maana yake; ni pale ambapo Mwanamke na mwanamke hufanya mapenzi,

Tafiti zinaonyesha Wanawake wanaojihusisha na Kusagana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo la Msongo wa mawazo pamoja na wasiwasi kuliko wanawake wengine.

Hii inaweza kutokana na ubaguzi, kukataliwa na wapendwa wao, Jamii, dhuluma au vurugu. Tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kwa wale ambao hawajawaambia wengine kuhusu mwelekeo wao wa ngono au kwa wale ambao hawana usaidizi kutoka kwa marafiki au familia.

MADHARA YA WANAWAKE KUSAGANA

Kuna madhara mengi ya kiafya kwa wanawake wanaosagana, na katika makala hii tumejadili Baadhi ya madhara hayo.

MADHARA YA WANAWAKE KUSAGANA AU KUJICHUA NI PAMOJA NA;

– Kuharibika Nerves kwa kiasi kikubwa katika eneo la kinembe au Clitoris hali ambayo husababisha mwanamke kuwa vigumu sana kuridhika na kufurahia wakati akifanya mapenzi na mwanaume.

– Mwanamke kuanza kukonda  na mwili kuwa dhaifu sana kama hatazingatia ulaji mzuri wa chakula

– Kuathiriwa kwa utendaji kazi wa tezi la Bartholin hali ambayo huweza kupelekea kupungua hali ya ute ute na unyevu unyevu ukeni

– Sehemu za siri au uke kulegea sana

– Kuanza  kupata maumivu ya mara kwa mara ukeni

– Huweza kusababisha mwanamke kukosa kabsa hamu ya kufanya mapenzi na mwanaume

– Athari huweza kuonekana hadi kwenye kizazi(mara chache sana) n.k

Bonus Tips; Zingatia Mambo haya Muhimu kwa Watu wote Wanaofanya Mapenzi

1. Hakikisha unajikinga na magonjwa yote ya Zinaa kwa kutumia kinga/Condomu

2. Hakikisha Mwenza wako kapimwa magonjwa yote ikiwemo ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

3. Fanya Ngono Salama

4. Kuwa na Mpenzi mmoja(Have only one sexual partner)

5. Dhibiti matumizi ya Pombe,Sigara pamoja na dawa zingine za kulevyia.

6. Pata Chanjo kwa magonjwa yanayohitaji chanjo,

Mfano; Magonjwa kama vile

  • Homa ya Ini(hepatitis A, hepatitis B).
  • Virusi vya HPV(human papilloma Virus)

6. Ikiwa umefanya mapenzi kwenye mzingira hatarishi ya kupata VVU, hakikisha unapata (PEP) Ndani ya Saa 72.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMAAfyaclass Bongo Social •

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMA 

Kama unaishi mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma, basi kaa mguu sawa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano.

Utabiri huo unakuja siku chache tangu baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam na Morogoro kushuhudia mvua kubwa iliyoathiri miundombinu na kusababisha vifo.

Utabiri huo wa TMA uliotolewa leo Januari 29,2024 utaanza kesho Januari 30 na utadumu hadi Februari 2 mwaka huu.

“Angalizo la mvua kubwa limetolewa katika maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma,”imeandikwa kwenye taarifa hiyo.

Wakazi katika mikoa hiyo watashuhudia athari ya makazi yao kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Mkoani Morogoro hivi karibuni waliripotiwa watu watano kufariki dunia na wengine 246 kuokolewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Morogoro na kusababisha mafuriko yaliyoharibu makazi na barabara.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam mvua hizo zilisababisha barabara kutopitika, nyumba kuzingirwa maji na wananchi kupita  adha ya usafiri.

Mara kadhaa Serikali imekuwa ikisisitiza wananchi wote waliojenga bondeni kuhama mara moja kuepuka athari za mvua.

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMA
0 Comment

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMA Afyaclass Bongo Social •

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMA 

Kama unaishi mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma, basi kaa mguu sawa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano.

Utabiri huo unakuja siku chache tangu baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam na Morogoro kushuhudia mvua kubwa iliyoathiri miundombinu na kusababisha vifo.

Utabiri huo wa TMA uliotolewa leo Januari 29,2024 utaanza kesho Januari 30 na utadumu hadi Februari 2 mwaka huu.

“Angalizo la mvua kubwa limetolewa katika maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma,”imeandikwa kwenye taarifa hiyo.

Wakazi katika mikoa hiyo watashuhudia athari ya makazi yao kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Mkoani Morogoro hivi karibuni waliripotiwa watu watano kufariki dunia na wengine 246 kuokolewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Morogoro na kusababisha mafuriko yaliyoharibu makazi na barabara.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam mvua hizo zilisababisha barabara kutopitika, nyumba kuzingirwa maji na wananchi kupita  adha ya usafiri.

Mara kadhaa Serikali imekuwa ikisisitiza wananchi wote waliojenga bondeni kuhama mara moja kuepuka athari za mvua.

Tahadhari ya Mvua kubwa kwa Siku Tano Mfululizo-TMA
0 Comment

Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapa

Nimonia(Pneumonia) ni maambukizi ya mapafu ambayo husababishwa na virusi au bakteria, Vijidudu hivi hufanya vifuko vya hewa kwenye mapafu kujazwa na majimaji (kohozi au ute). Hii inafanya kuwa vigumu kupumua na kusababisha mtoto wako kukohoa.

Fahamu: Nimonia huua watoto zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa kuambukiza.

Ingawa hata watu wazima huweza kupata ugonjwa wa nimonia, ugonjwa huu hushambulia na kuua Watoto Zaidi ulimwenguni kote.

Kila mwaka, Nimonia inaondoa maisha ya zaidi ya watoto 725,000 walio chini ya umri wa miaka 5, ikiwa ni pamoja na karibu watoto wachanga 190,000, ambao wako katika hatari ya kuambukizwa.

Kila siku, angalau Mtoto mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa Nimonia kwa kila sekunde 43, na Karibu Vifo vyote vinaweza kuzuilika.

Ni jambo lisilo na udhuru kwamba maelfu ya watoto hawawezi kupata huduma muhimu za afya na matibabu, ambayo yanaweza kuzuia nimonia na kuokoa maisha yao.

Chanzo cha ugonjwa wa Nimonia(pneumona)?

Nimonia ni maambukizi ya mfumo wa kupumua ambayo huathiri mapafu. Maambukizi haya hayana sababu moja – yanaweza kutokana na maambukizi ya vimelea kama vile;

  • bakteria,
  • virusi
  • au fungi

Wakati mtoto ameambukizwa, mapafu yake yanajaa maji na inakuwa vigumu kupumua. Watoto ambao kinga zao hazijakomaa (yaani watoto wachanga) au dhaifu – kama vile wenye utapiamlo, au magonjwa kama VVU – wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa wa nimonia.

Dalili za nimonia kwa mtoto

Fahamu hapa kuhusu dalili za ugonjwa wa pneumonia;

Kwa vile nimonia ni maambukizi ya mapafu, dalili za kawaida ni;

  • kukohoa,
  • kupumua kwa shida
  • na homa.
  • Watoto walio na nimonia kwa kawaida hupumua haraka, au kifua chao kinaweza kuvuta au kujirudisha nyuma wakati wa kuvuta pumzi (kwa mtu mwenye afya njema, kifua hupanuka wakati wa kuvuta pumzi).

– Kupumua haraka na kwa shida

– Kupata homa

– mwili kutetemeka sana

– Kupata maumivu ya misuli ya mwili

– Kukosa hamu ya kula chakula au kunyonya

– Kukohoa

– Kupata maumivu ya kifua

– Kupata Uchovu sana wa mwili

– Mwili kuwa Dhaifu sana

– Kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Nimonia inayosababishwa na virusi mara nyingi sio kali kuliko inayosababishwa na bakteria. Dalili kwa kawaida huanza kama mafua. Na zinazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku chache.

Nimonia inayosababishwa na bakteria inaweza kuja ghafla na homa kali, kupumua haraka na kukohoa.

Aina zote mbili za pneumonia zinaweza kusababisha kikohozi kwa mtoto kwa wiki kadhaa baada ya homa kukoma.

Nimonia inasambaa Je?

Nimonia inaambukiza na inaweza kuenea kupitia chembechembe zinazopeperuka hewani  kupitia (kikohozi au kupiga chafya). Inaweza pia kusambazwa kupitia vimiminika vingine, kama vile damu wakati wa kujifungua, au kutoka kwenye sehemu zilizochafuliwa.

Jinsi gani Nimonia hugundulika kwa mtoto?

Njia ambazo ugonjwa wa Nimonia huweza kugundulika kwa mtoto ni pamoja na;

  •  physical exam, ikiwa ni pamoja na kuangalia mifumo isiyo ya kawaida ya kupumua na kusikiliza mapafu ya mtoto.
  • chest x-rays
  • Au vipimo vya damu(blood tests)

Matibabu ya Ugonjwa wa Nimonia)pneumonia)

Matibabu ya nimonia inategemea na aina ya nimonia. Katika nchi zinazoendelea, idadi kubwa ya matukio ya nimonia husababishwa na bakteria na inaweza kutibiwa na antibiotics za gharama nafuu.

Hata hivyo watoto wengi wenye nimonia hawapati dawa za kuua vijasumu wanazohitaji kwa sababu wanakosa huduma bora za afya. Sababu nyingine za nimonia ni virusi au mycobacteria (k.m. zile zinazosababisha kifua kikuu) zinazohitaji matibabu mengine. Kifua kikuu haswa mara nyingi hubaki bila kutambuliwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapa
0 Comment

Mfalme Charles atoka hospitalini siku tatu baada ya upasuaji wa tezi dume(Picha)Afyaclass Bongo Social •

Mfalme Charles atoka hospitalini siku tatu baada ya upasuaji wa tezi dume kuongezeka (Picha)

Mfalme Charles III ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutibu Tezi dume iliyoongezeka, kulingana na Taarifa ya Buckingham Palace.

Charles, mwenye umri wa miaka 75, alipigwa picha akiondoka The London Clinic Jumatatu alasiri, Januari 29,  na mkewe, Queen Camilla, kando yake.

“Mfalme aliruhusiwa kutoka hospitalini alasiri ya leo kufuatia matibabu yaliyopangwa na amepanga tena mazungumzo na umma yawe hapo baadae ili kuruhusu muda wa kupata nafuu binafsi,”

ikulu ilisema katika taarifa. “Mkuu wake anapenda kuwashukuru timu ya madaktari na wote waliohusika katika kuunga mkono ziara yake hospitalini, na anashukuru kwa ujumbe mzuri ambao amepokea katika siku za hivi karibuni.”

Charles aliaruhusiwa kutoka Kliniki ya London siku hiyo hiyo ambayo binti-mkwe wake Kate, Princess wa Wales, aliruhusiwa kutoka hospitali hiyo hiyo.

Kate, umri miaka 42, alienda nyumbani kutoka hospitali kwa faragha Jumatatu baada ya kukaa kwa takriban wiki mbili kufuatia “upasuaji uliopangwa wa tumbo” ambao ulifanyika Januari 16, kulingana na Kensington Palace.

Upasuaji huo “ulifanikiwa,” kulingana na ikulu. Kate, ambaye ameolewa na Prince William, mtoto wa Charles na mrithi wa kiti cha enzi ni mama wa watoto wao watatu.

Ikulu haikutoa maelezo zaidi juu ya aina ya upasuaji aliofanyiwa Kate, lakini ilisema kuwa hana uwezekano wa kurejea majukumu yake ya umma hadi baadaye msimu huu wa kuchipua.

Charles anatarajiwa kuanza tena mazungumzo ya umma baada ya “muda mfupi wa kupona.”

Mfalme Charles atoka hospitalini siku tatu baada ya upasuaji wa tezi
dume(Picha)
0 Comment

Usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa nimoniaAfyaclass Bongo Social •

Usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa nimonia

Pneumonia ni maambukizi kwenye mapafu. Mara nyingi husababishwa na bakteria au virusi. Ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumua.

Watoto lakini pia watu wazima wanaweza kuugua ugonjwa huu. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Watoto 740,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wamefariki kutokana na homa hiyo ya mapafu mnamo 2019. Kila Novemba 12 ulimwengu huadhimisha “Siku ya kimataifa ya kupambana na Pneumonia”.

Pneumonia au homa ya mapafu ni nini?

Kwa lugha nyepesi, ni maambukizi yanayotokea katika mfumo wa kupumua. Na mara nyingi maambukizi haya hutokana na virusi, bakteria au hata kuvu.

Maambukizi yakitokana na bakteria, maji na usaha hukusanyika katika eneo linalofanya kazi kuchuja hewa ya oxygen na carbon dioxide wakati tunapopumua.

Hivyobasi kufanya upumuaji hewa kuwa vigumu, hatua inayosababisha pia kiwango cha oxgen kupungua katika damu mwilini.

Maambukizi yanaweza kuwa mepesi au mara nyingine husababisha hata kifo cha muathiriwa.

Dalili za homa ya mapafu ni zipi?

Mtu yoyote anaweza kuugua homa ya mapafu. Dalili zake ni pamoja na

• Kupata matatizo ya kupumua

• Kuongozeka kwa mapigo ya moyo

• Joto mwilini

• Kutetemeka, kutokwa na jasho mwilini

• Kukohoa

• Maumivu kifuani

• Kuumwa na kichwa, kuhisi kutapika, kutapika, kuharisha

Wataalamu wanasema ni muhimu kutambua aina ya homa ya mapafu kwa kufanyiwa utafiti wa maabara na kupata matibabu.

Shirika la afya duniani linasema kwamba iwapo maambukizi yametokana na bakteria au virusi madhara yake yako sawa. Hatahivyo dalili hutofautiana kidogo.

Iwapo homa hiyo imetokana na maambukizi ya virusi basi baadhi ya dalili anazokuwa nazo mgonjwa ni pamoja na kikohozi, joto mwilini, mafua na kupata matatizo ya kupumua.

Vipi unaweza kutambua mtoto anaugua homa ya mapafu ?

Joto mwilini

Watoto wanaweza kupata joto mwilini kwa sababu tofuati. Mara nyingi joto mwilini hutokea wakati mwili unapambana na ugonjwa. Lakini iwapo joto ni jingi sana au halishuki hata unapompatia mtoto dawa, ni lazima umfikishe mtoto kwa daktari. Matatizo ya kupumua

Upumuaji wa watoto huwa tofuati kila saa mchana. Wao hupata matatizo ya kupumua wanapopata maambukizi ya homa ya mapafu. Baadhi hutoa sauti kama firimbi kuashiria ugumu wanaopata kupumua. Hapa mzazi unahitaji kuwa na uangalifu mkubwa.

Uchovu.

Mapafu hujaa maji kutokana na homa hii. Na ndicho kinachosababisha shida ya kupumua. Mtoto anahisi kuchoka. Iwapo mtoto wako anaonekana kuchoka saa zote, basi ni muhimu apate ushauri wa daktari haraka iwezekanavyo.

Je homa ya mapafu inatibiwa vipi?

Ni muhimu kuzitambua dalili na mapema. Ni rahisi kutambua homa ya mapafu kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Anapopata matatizo ya kupumua ni muhimu kumfikisha hospitalini haraka iwezekanavyo.

Virusi ndani ya mapafu vinaweza kuchukua siku kadhaa hadi wiki kusambaa mwilini.

Maambukizi ya bakteria yanaweza kutibiwa kwa dawa za antibiotics.

Hatahivyo iwapo maambukizi ni makali huenda mgonjwa akahitaji kulazwa hospitalini.

Wataalamu wanashauri kwamba wagonjwa wanaweza kupoa haraka kwa kuchukua hatua kama vile kupumzika na kunywa maji mengi.

Usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa nimonia
0 Comment

Dalili za siku ya kushika mimba,Zifahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za siku ya kushika mimba

Siku ya kushika mimba; Siku za kushika mimba ndyo zile kwa jina lingine hujulikana kama “Siku za Hatari”, hapa tunazungumzia kipindi cha yai kutoka kwenye Ovari(Ovulation) ili likutane na mbegu ya kiume kwa ajili ya Urutubishaji.

Wanawake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushika mimba ndani ya siku moja au mbili baada ya ovulation, ambapo ni wakati ovari hutoa yai.

Hata hivyo, inawezekana kupata mimba katika siku zinazoongozana kwenye ovulation, kwani manii inaweza kuishi kwa siku kadhaa ndani ya mwili wa kike.

Hivo basi, hata wale wanaohitaji kubeba mimba ni lazima Ujue siku za hatari ni Zipi ili ufanye mapenzi kwenye siku ambazo unaweza kushika mimba,

Changamoto inakuja, nitajuaje niko kwenye siku za kushika mimba? hasa kwa wale ambao mzunguko wao wa hedhi haueleweki(Irregular menstrual cycle).

Kupitia Dalili, itakusaidia kujua kama Upo kwenye Siku ya Kushika Mimba, na katika Makala hii tumechambua baadhi ya dalili hizo.

Dalili za siku ya kushika mimba

Hapa tunazungumzia dalili za ovulation kwa lugha nyingine,

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Siku ya kushika mimba;

– Tumbo kuanza kukaza kidogo sehemu ya chini(mild cramping in the lower abdomen)

– Kutoa ute mweupe Ukeni wenye kuvutika Zaidi kama ule wa Yai,

Ukiona hii ujue upo kwenye siku za hatari.

– Kuongezeka kwa Joto Mwilini(mwili kuwa wa moto)

– Kuwa na hamu Zaidi ya kufanya Mapenzi(higher sex drive) kuliko kawaida

Baadhi ya ishara hizi, kama vile joto la Mwili, zitaendelea kubadilika baada ya ovulation. Kwa sababu hii, mtu haupaswi kutumia halijoto pekee kutabiri kama upo kwenye siku kamili ya yai kutoka.

Inaweza kusaidia kwa mtu kufuatilia ishara kwa miezi michache ili kupata wazo la nini ni kawaida kwa mwili wako.

Lakini Unapaswa kukumbuka kuwa kuna vigezo kadhaa, na wakati wa ovulation unaweza kubadilika, mwezi hadi mwezi.

Chaguo jingine ni kutumia Vifaa vya kutabiri Siku wa mayai kutoka au kichunguzi cha uwezo wa kuzaa.

Ovulation kawaida hutokea kwenye nusu ya mzunguko wako wa hedhi. Hii ni takriban siku 14 kabla ya siku ya kwanza ya kipindi chako kinachofuata katika mzunguko wa Hedhi wa siku 28,

lakini muda kamili unaweza kutofautiana. Ishara kwamba unakaribia kutoa Yai inaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuzingatia na kufuatilia baada ya muda ili kukusaidia kutabiri Siku ya kushika Mimba.

– Dalili Zingine za Siku ya kushika Mimba ni pamoja na;

  • Kupata vimaumivu vya matiti
  • Kuwa na hamu ya kufanya Mapenzi isiyoyakawaida
  • Joto la mwili kuwa juu n.k

NB: Ingawa, kutumia ishara hizi Pekee kutabiri siku ya Kushika Mimba sio njia inayotegemewa zaidi.

Dalili za siku ya kushika mimba,Zifahamu hapa
0 Comment

Kipindupindu Zimbabwe: Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kuanza rasmiAfyaclass Bongo Social •

Kipindupindu Zimbabwe: Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kuanza rasmi

Nchini Zimbabwe, serikali inazindua kampeni ya chanjo ya kipindupindu kesho, Jumatatu Januari 29, huku maambukizi yakienea kwa kasi na kuibua wasiwasi nchini humo. Zaidi ya watu 20,000 wameugua katika miezi ya hivi karibuni, na vifo 500 vimerekodiwa.

Wagonjwa wa kwanza wa kipindupindu walirekodiwa nchini Zimbabwe chini ya mwaka mmoja uliopita, kama kilomita mia moja kutoka mji mkuu na, kama kila mwaka, idadi ya kesi huongezeka katika msimu huu wa mvua.

Mwaka huu, anaeleza John Roche, mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kwa kanda ya kusini, janga hilo ni kubwa kuliko kawaida, na maambukizi elfu ya ziada kila wiki, hasa katika maeneo ya mijini.

“Harare imeathirika hasa kwasababu kuna msongamano mkubwa wa watu. Mfumo wa usambazaji maji katika mji mkuu uko katika hali mbaya, ukiwa umetunzwa vibaya kwa miaka kadhaa. Katika baadhi ya vitongoji, hata haipo. Kwa hivyo watu hukimbilia kwenye visima ambavyo maji yake mara nyingi huchafuliwa na vinyesi.

“Hofu yetu leo ​​ni kwamba mwanzoni mwa mwaka watu wanasafiri zaidi, wanarudi kutoka kwenye sherehe za familia vijijini mwao, wengine wamesafiri kwenda nchi za mipakani na shule pia zimeanza tena. Haya yote yanahatarisha kuharakisha kuenea kwa janga hili.

“Kampeni hii ya chanjo ni jambo zuri sana, dozi moja inatoa kinga kwa miezi sita. Kwa bahati mbaya, hakuna chanjo za kutosha na ni vigumu kuzipata. Barani Afrika, tuna magonjwa ya kipindupindu kila wakati. Labda tuanze kufikiria mambo kwa njia tofauti, labda tufikirie juu ya kutengeneza chanjo mashinani,”

Kipindupindu Zimbabwe: Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa
kipindupindu kuanza rasmi
0 Comment

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)Afyaclass Bongo Social •

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Pid ni ugonjwa gani?

PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke, yaani pelvic inflammatory disease,

Infection kwenye kizazi ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.

Chanzo cha ugonjwa wa PID

PID husababishwa na nini?chanzo kikuu cha Pid

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza zaidi kuwa chanzo cha Pid kwa wanawake.

Je mwanamke hupataje PID?

Kwa Njia hizi hapa chini ni rahsi sana kwa mwanamke kupata maambukizi katika via vyake vya Uzazi.

(1) Kufanya mapenzi au ngono isiyo salama

(2) Kupata maambukizi katika via vya uzazi mara baada ya mama tu Kujifungua ambapo kitaalam huitwa “POSTPARTUM INFECTION”

(3) Maambukizi ambayo mwanamke huweza kuyapata mara tu baada kutoa mimba kwa Njia zisizo salama kitaalam huitwa Post abortion infection au baada ya mimba kutoka yenyewe ambapo kitaalam huitwa post miscarrage infection

(4) Matumizi ya baadhi ya Njia za Uzazi wa mpango kama lupu au(IUCD)  ambapo mwanamke kuweza kupata PID wakati wa uwekaji n.k

(5) Maambukizi kwa Njia ya damu kutoka kwa Mtu mwenye maambukizi katika via vya Uzazi

Dalili za Ugonjwa wa PID ni zipi?

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni;

  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kutokwa na uchafu sehemu za siri wenye rangi kama njano n.k. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na Pia kutapika

MADHARA YA Ugonjwa wa PID(MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE)

1- Mwanamke kushindwa kabsa kubeba Mimba au Ujauzito,

Mtu mwenye PID anaweza kupata mimba?

Moja ya madhara ya PID ni kuathiri uwezo wa mwanamke kupata Ujauzito

2- Ujauzito kutoka hasa katika miezi 3 ya mwanzoni

3- Kutokwa na uchafu unaombatana na harafu kali hata kukukosesha raha,hasa hasa kama Upo kwenye mahusiano ya kimapenzi

4- Kupata maumivu makali chini ya Kitovu wakati wa Tendo la Ndoa

5- Kupata maumivu wakati wa period huku ikiambatana na damu nyeusi,yenye mabonge mabonge  na wakati mwingine kutoka nyama kama Vipande vya maini.

6-Hali ya kichefuchefu na kutapika kutokea

7-Uke kuwa Mkavu hata kuleta maumivu wakati wa Tendo la Ndoa.

Vipimo vya Ugonjwa wa pid:

Baadhi ya vipimo kwa Mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa PID ni kama ifuatavyo;

➖Kuchunguza mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi. Lakini pia Mkojo huweza kutumiwa kwa kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo maambukizi hayo.

➖Kipimo cha Damu kwa ajili ya kuchunguza vimelea mbali mbali vya Magonjwa ikiwemo PID,ambapo kitaalam kipimo hichi huitwa Full Blood Picture.

➖Uchanguzi wa utando unaozunguka shingo ya uzazi ambapo huweza kutumika vifaaa kama SPECULUM

➖Mwanamke mwenye dalili hizi kufanya kipimo cha ULTRASOUND

TIBA YA UGONJWA WA PID

Kama una tatizo la PId waone wataalamu wa afya au nenda Hospital kwa Ajili ya vipimo na matibabu kamili,Kumbuka ukifika hospital unaweza kufanyiwa vipimo kama ULTRASOUND na kupata matibabu sahihi kwako.

Baada ya Ugonjwa wa PID kugundulika,mgonjwa atapewa  dawa za kutibu ugonjwa huu. Shirika la Afya Duniani (WHO)  limeonyesha baadhi ya miongozo na maelekezo ya kutibu Ugonjwa wa PID.

Baadhi ya dawa zilizoorodheshwa kwa ajili ya matibabu ya maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke(PID) ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.

KINGA DHIDI YA UGONJWA WA PID

✓Kutokufanya ngono zembe kwani hiki ni mojawapo ya Chanzo cha Kupata ugonjwa wa PID

✓Kutokufanya tendo la ndoa mara tu baada Ya kujifungua kwani mlango wa uzazi utakuwa bado haujafunga vizuri na ni rahis kupata maambukizi pia

✓Fanya vipimo vya mara kwa mara hasa ukiwa na dalili kama nilizozitaja hapo juu

✓Muone mtaalam wa afya pale tu unapojihisi tofauti

NB: KAMA UNA TATIZO HILI NA MENGINE TUWASILIANE KUPITIA Namba 0758286584.

 BONUS TIPS:MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika Juu ya Tatizo hili siku hizi.

Wengine Hata kushindwa kabsa Kushiriki Tendo la Ndoa,kwa kuogopa Maumivu ambayo wamekuwa wakiyapata Wakati wa Tendo la Ndoa.

VISABABISHI VYA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA

(1)Kuvimba kwa Kuta za Uke- Na hii huweza kuusababishwa na FANGASI aina ya CANDIDA ALBICANS au BACTERIA

(2)Uvimbe wa Kizazi au Shingo ya Kizazi Huweza kuleta hali hii ya Maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(3)Mirija ya kizazi kuziba-Hali hii inaweza kukuletea maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(4)Saratani ya Shingo ya Kizazi-Mojawapo ya dalili za kansa ya shingo ya kizazi ni mwanamke kupata maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(5)Ukavu wa sehemu za siri-Hali hii huweza kupelekea maumivu makali pamoja na michubuko sehem za Siri wakati wa Tendo la Ndoa

KUMBUKA; JUKUMU LANGU KWAKO,NI KUKUSHAURI,KUKUELIMISHA NA KUKUPA MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA

kwa ushauri/Elimu/Tiba mawasiliano ni +255758286584.

0 Comment

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024Afyaclass Bongo Social •

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024.

Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imeratibiwa Januari 27-31, 2024, katika kaunti za Mandera, Wajir, na Garissa!

Dhamira kubwa ikiwa ni kuwalinda watoto chini ya miaka 5 dhidi ya polio.

Zaidi ya hayo, Wizara ya Afya nchini Kenya inasema hivi;

Lakini subiri, kuna zaidi! Katika Kaunti Ndogo za Fafi na Daadab, zikiwemo kambi za wakimbizi, tunapanua kampeni ili kujumuisha watoto wote walio chini ya umri wa miaka 15.

Haya ni Maelekzo kwenye page ya wizara ya Afya nchini Kenya;

“Round 3 of the Polio Campaign is scheduled for January 27th-31st, 2024, in Mandera, Wajir, and Garissa counties! Our mission? To safeguard children under 5 from polio.

But wait, there’s more! In Fafi and Daadab Sub Counties, including refugee camps, we’re expanding the campaign to include all children under 15 years old”.

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024
0 Comment

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024Afyaclass Bongo Social •

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024.

Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imeratibiwa Januari 27-31, 2024, katika kaunti za Mandera, Wajir, na Garissa!

Dhamira kubwa ikiwa ni kuwalinda watoto chini ya miaka 5 dhidi ya polio.

Zaidi ya hayo, Wizara ya Afya nchini Kenya inasema hivi;

Lakini subiri, kuna zaidi! Katika Kaunti Ndogo za Fafi na Daadab, zikiwemo kambi za wakimbizi, tunapanua kampeni ili kujumuisha watoto wote walio chini ya umri wa miaka 15.

Haya ni Maelekzo kwenye page ya wizara ya Afya nchini Kenya;

“Round 3 of the Polio Campaign is scheduled for January 27th-31st, 2024, in Mandera, Wajir, and Garissa counties! Our mission? To safeguard children under 5 from polio.

But wait, there’s more! In Fafi and Daadab Sub Counties, including refugee camps, we’re expanding the campaign to include all children under 15 years old”.

KENYA: Awamu ya 3 ya Kampeni ya Polio imesharatibiwa Januari 27-31, 2024
0 Comment

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyesAfyaclass Bongo Social •

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyes’

Wataalamu wasema zinachangia kuongeza maumivu, waonya zaweza kusababisha uoni hafifu na upofu.

Wataalamu wa afya na madaktari bingwa wa macho wamesema wanapokea idadi kubwa ya wagonjwa wakiwa katika hali ya ugonjwa mkali, kutokana na matumizi ya njia mbadala kutibu macho, ikiwamo matumizi ya mkojo na chumvi.

Hali hiyo imebainika siku 15 tangu kutangazwa kuibuka ugonjwa huo ujulikanao viral keratoconjunctivitis (red eyes) Januari 13, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Wataalamu waliozungumza na Mwananchi Digital jana Januari 28, 2024 wameeleza wagonjwa wanaotumia chumvi, mkojo, chai ya rangi na kitunguu saumu kama tiba, macho yao huvimba na kuuma zaidi pamoja na kupatwa homa. Athari hasi zaidi zinazotajwa ni kusababisha vidonda kwenye kioo cha jicho.

Tiba hizo mbadala zinaelezwa zinaweza kusababisha kovu kwenye jicho litakalomfanya mgonjwa apate uoni hafifu au kupoteze uwezo wa kuona kabisa.

Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Sarah Mrema ameisema idadi ya wagonjwa wanaohudhuria hospitalini hapo kutibiwa macho imekuwa ikiongezeka na kupungua.

Amesema wamekuwa wakipokea wagonjwa wakiwa tayari walianza kutumia tiba za majani ya chai, vitunguu saumu na chai ya rangi.

“Si kwamba wanapona wakitumia tiba mbadala, maumivu yanazidi, wakija hapa wanakuwa na maumivu makali. Ukihoji anakwambia alitumia mkojo, chumvi na njia nyingine nyingi. Unampa dawa anatumia, kisha anapona,” amesema Dk Sarah.

Kwa mujibu wa Dk Sarah, takwimu za hospitali hiyo zinaonyesha tangu Desemba 22, 2023 wagonjwa 105 walifika kutibiwa na kuna siku orodha ya wagonjwa inapanda na siku nyingine inapungua.

Daktari bingwa wa macho katika Hospitali ya Muhimbili-Upanga, Neema Moshi amesema unapotumia vitu vikali kutibu macho, ni rahisi kuharibu kioo cha mbele cha jicho na maumivu yanayotokea huwa makali.

Amesema wakati mwingine unaweza kupoteza uoni kwa sababu ya kuharibu kioo hicho.

“Tunapokea wagonjwa wengine wana hali mbaya, lakini hawezi kuwa mkweli, unajua mgonjwa hawezi kuja kusema alitumia kitu fulani, mara nyingi wanafichaficha labda tatizo liwe kubwa zaidi ndipo wanasema ukweli,” amesema.

Dk Neema amesema kama mgonjwa ametumia vitu hivyo na hajapata athari hawezi kupata athari baadaye.

“Si kwamba athari hizo zinakuwa za taratibu, kama amepona na haikuonekana kupata shida yoyote haiwezi kutokea tena baadaye,” amesema.

Meneja Mpango wa Taifa wa huduma za macho kutoka Wizara ya Afya, Dk Bernadetha Shilio amesema wapo wagonjwa wanaopata athari, lakini hawana takwimu, akisisitiza ni muhimu wagonjwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

“Taarifa hizi zinatolewa na wataalamu wa afya, yaani madaktari kwenye vituo husika, labda mimi kuna mtu amekuja amefanya hivi na vile lakini kutoa hali ilivyo kwa sasa wangapi wamethirika kwa sasa bado.

“Hata leo nimepewa taarifa kuna mtu anatumia sijui vitu gani, lakini pia kuna taarifa za uvumi kuna mtu katoka huko anashauri wagonjwa wanywe Azuma inatibu, huo ni uongo,” amesema.

Dk Shilio amewataka wagonjwa waepuke kutibu macho kwa kutumia kitunguu saumu kwa kuwa kunaweza kusababisha michubuko kwenye ngozi ya jicho na kioo cha mbele ya jicho, hivyo kuathiri uwezo wa jicho kuona.

“Maji ya chumvi yanaweza kusababisha michubuko au kidonda kwenye kioo cha mbele cha jicho, hivyo kutengeneza kovu litakalopunguza uwezo wa jicho kuona au ulemavu wa kutoona wa kudumu,” amesema.

“Matumizi ya chai ya rangi katika kutibu macho yanaweza kusababisha vidonda kwenye kioo cha jicho na kusababisha kovu kwenye jicho litakalokufanya upate uoni hafifu au upoteze uwezo wa kuona kabisa,” amesema.

Dk Shilio amewataka wagonjwa pia kuepuka kutibu macho kwa mkojo, kwani ni hatari kwa usalama wa macho kwa kuwa mkojo hubeba uchafu na vijidudu vinavyoweza kusababisha maambukizi mengine na kupoteza uwezo wa kuona kabisa.

Amewataka kuzingatia kunawa mikono mara kwa mara na wapatapo ugonjwa huo kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu sahihi na kwa wakati.

Via Mwananchi.

Soma Zaidi hapa Dawa ya Kutibu Ugonjwa wa macho mekundu(Red Eyes)

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyes
0 Comment

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwiAfyaclass Bongo Social •

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi

Kuna njia nyingi ambazo hutumika ili kusaidia kuzuia maambukuzi ya Virusi vya ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kufanya mapenzi,

Kama umepima wewe na mwenza wako,Moja wenu kapata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Hivi ni Vitu vya msingi sana vya Kuzungatia ikiwa mpo kwenye hali kama hii;

1. Hakikisheni mpo kwenye tiba,

Moja ya njia rahisi na inayofanya kazi ni kuhakikisha mwenza wako yupo kwenye matibabu na anafuata kanuni zote za Tiba ya HIV.

hii inasaidia kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine(An undetectable viral load makes HIV untransmittable).

2. Njia nyingine mpya ni kwa mwenza ambaye hana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutumia dawa zinazoitwa PrEP

Kwa mwenza ambaye yupo NEGATIVE Anaweza kutumia PrEP, Hizi ni dawa za kunywa(vidonge) ambavyo husaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kabla ya mtu kuwa kwenye mazingira ya hatari.

Na kwa mujibu wa tafiti mbali mbali PrEP zina uwezo mkubwa wa kufanya hivo.

3. Matumizi Sahihi ya kinga kama kondomu

Matumizi sahihi ya condomu kwa Mwanaume au mwanamke huweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kusambaza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

4. Jikinge na magonjwa mengine ya Zinaa(STI’s),

Ikiwa mwenza wako ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU), kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa mengine ikiwemo ya Zinaa, kwa sababu ya kinga yake ya Mwili kuwa dhaifu Zaidi.

Hii huongeza hatari ya wewe kupata magonjwa mengine zaidi.

5. Mambi haya pia huweza kukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi;

  • Viral Load kuwa juu
  • Muda wa kufanya mapenzi
  • Kufanya mapenzi katika mazingira magumu(roughness of sex), hapa hakuna maandalizi ya kutosha, mnafanya kwa nguvu kama kukomoana, kuchubuana n.k

Moja ya vitu muhimu vya kuchunguza kwa mwenza wako ikiwa ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) ni pamoja na VIRAL LOAD,

Kwa mujibu wa Utafiti mmoja ulionyesha kwa Watu ambao VIRAL LOAD ilikuwa chini uwezekano wa kusambaza maambukizi ulikuwa mdogo sana au sawa na Zero.

Utafiti huo Unasema;

 “The PARTNER study reported zero HIV transmissions after 900 couples had sex more than 58,000 times WITHOUT condoms. In this study undetectable viral load was defined as being less than 200 copies/m”.

Utafiti huu unaendelea kwa kusema; Hatari ya kupenya Virusi kwa Mtu anayefanya mapenzi bila kondomu na mtu ambaye ana kiwango cha juu cha virusi(HIGH VIRAL LOAD) inaweza kuwa juu Zaidi kama 1 kati ya 10 (hatari 10%). Lakini hatari ni sifuri kwa mtu ambaye anatumia matibabu(dawa) na ambaye ana kiwango cha chini sana cha virusi(LOW VIRAL LOAD) au kisichoonekana.

Mambo ya kuzingati wewe na Mwenza wako ikiwa mmoja wenu ana Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

Je, wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua tahadhari gani?

Kuna tahadhari kadhaa ambazo wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua ili kuzuia kuambukizwa au kusambaza VVU kupitia ngono.

(1) Hakikisheni mnatumia njia za kujikinga kama condoms pamoja na njia nyingine

Mbinu za kujikinga kama vile kondomu huweza kusaidia kuzuia michubuko na kugusa maji maji ya mwili wakati wa kujamiiana na mtu anayeishi na VVU.

Vikitumiwa  ipasavyo, vizuizi hivi vinaweza kuzuia uambukizaji wa VVU na magonjwa mengine ya Zinaa.

Kutumia vilainishi au mafuta ya kutosha kunaweza pia kusaidia kupunguza hatari ya VVU, pia – bila kusahau, kufanya ngono kuwa bora zaidi.

(2) Hakikisheni mnatumia dawa muhimu ikiwemo ART, PrEP, na PEP

Kuna dawa chache zinazoweza kusaidia kuzuia maambukizi ya VVU:

ART: Mtu anayeishi na VVU anaweza kutumia dawa zinazojulikana kama ART ili kumsaidia kuwa na afya bora na kuzuia uambukizaji wa VVU.

Watu wengi wanaotumia dawa kama ilivyoagizwa wanaweza kupunguza kiwango chao cha virusi hadi kiwango kisichoonekana.

PrEP: Hii ina maana ya pre-exposure prophylaxis, PrEP ni dawa ambayo mtu asiye na VVU anaweza kutumia kabla ya kuingia kwenye mazingira hatarishi ili kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU kwa asilimia 99.

PEP: Hii ina maana ya Post-exposure Prophylaxis, PEP hutumika baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa,

au PEP, ni regimen ya dawa inayoweza kusaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kuambukizwa inapoanzishwa au kutumika ndani ya saa 72.

(3) Jengeni Utaratibu wa kufanya Vipimo mara kwa mara ikiwemo Vipimo vya magonjwa ya Zinaa(STIs)

Ni muhimu kwako na kwa mwenzi wako kupima magonjwa ya Zinaa mara kwa mara. Utambuzi wa mapema na matibabu ya magonjwa ya zinaa inaweza kupunguza hatari ya matatizo.

Kuwa na magonjwa ya zinaa kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU.

(4) Fahamu Dalili kubwa za Ukimwi na magonjwa mengine ya Zinaa(STIs)

Kufahamu kuhusu dalili za magonjwa ya Zinaa(STI) ni muhimu kwa mtu yeyote anayeshiriki ngono.

Muone mtaalamu wa afya ukigundua mojawapo ya haya:

  • kutokwa na uchafu usio wa kawaida kutoka kwa njia ya haja kubwa, uume au uke
  • kutokwa na damu kusiko kwa kawaida ukeni, kama vile kutokwa na damu baada ya kujamiiana au katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuhisi kuungua au maumivu wakati wa kukojoa
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Kuwa na vidonda au malengelenge kwenye au karibu na sehemu zako za siri,eneo la haja kubwa(mkundu) n.k
  • Kuwa na upele kwenye au karibu na sehemu zako za siri au mkundu
  • kuwashwa sehemu za siri n.k

(5) Hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja kutoka kwa wataalam wa afya.

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi
0 Comment

Uchunguzi wa ugonjwa wa ukoma kuanzia ngazi ya kayaAfyaclass Bongo Social •

UCHUNGUZI WA UGONJWA WA UKOMA KUANZIA NGAZI YA KAYA

Na: WAF -Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, kushirikiana na Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa Ugonjwa wa Ukoma kuanzia ngazi ya kaya ili kupata wagonjwa wapya wa Ukoma na kutoa tiba kinga.

Prof. Nagu amesema hayo wakati akitoa tamko la Siku ya Ukoma Duniani Januari 28, 2024 Jijini Dodoma ambapo amesema
Kila mwanajamii ana wajibu wa kutambua dalili za Ukoma na kuhakikisha wote wenye dalili wanafika katika kituo chochote cha kutolea huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu.

“Nitoe rai kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, kushirikiana na Vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kuhakikisha Kila Halmashauri nchini inafanya juhudi kuibua wagonjwa, inafuatilia mwenendo wa ugonjwa, na kuwa na takwimu sahihi za kufuatilia wagonjwa kulingana na maeneo au vijiji au mitaa wanakopatikana”. Amesema Prof. Nagu

Prof. Nagu ameongeza kuwa Idadi ya wagonjwa wapya imepungua kutoka wagonjwa 2,297 mwaka 2015 hadi wagonjwa 1,309 mwaka 2023 sawa na punguzo la asilimia 57.

“Mwaka 2023 nchi yetu ilikuwa na wagonjwa 3 kwa kila watu 100,000 hivyo, Tanzania imefika kiwango cha awali cha shirika la Afya Duniani cha kutokomeza ugonjwa wa Ukoma yaani chini ya mgonjwa mmoja kati ya watu 10,000 tangu mwaka 2006” Amesema Prof Nagu

Prof. Nagu amesema Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo Thamini Utu; “Tokomeza Unyanyapaa dhidi ya Waathirika wa Ukoma”. Ambapo amesema Kaulimbiu hiyo inachagiza umuhimu wa kila Mtanzania kushiriki katika kutokomeza ugonjwa huo

“Ugonjwa wa Ukoma si ugonjwa wa kulogwa, kurithi, wala laana, ni ugonjwa wa kuambukizwa, unatibika na kupona. Hivyo naisihi jamii kuachana kabisa na dhana hizo potofu na aina zote za unyanyapaa” amesema Prof Nagu.

Uchunguzi wa ugonjwa wa ukoma kuanzia ngazi ya kaya
0 Comment

Ugonjwa wa moyo husababishwa na niniAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?

Hili ni Swali ambalo watu wengi huuliza na wengi wao wanafahamu kama ugonjwa wa moyo ni ugonjwa mmoja, Hapana fahamu hapa…!!!

Ugonjwa wa Moyo;

Ni maneno yanayoelezea magonjwa yote yanayoathiri moyo au kwa kitaalam tunaita heart diseases, hakuna Ugonjwa mmoja wa moyo, ila kuna magonjwa mbali mbali yanayoathiri moyo.

Hivo mtu akikuambia una ugonjwa wa Moyo,muulize ugonjwa upi wa moyo?.

Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;

  • Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
  • Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
  • Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
  • Tatizo la moyo kutanuka
  • Tatizo la Moyo kujaa maji
  • Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
  • Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
  • Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo

Dalili zinategemea na aina ya Ugonjwa wa moyo unaokusumbua kwa wakati huo, Kwa Mfano;

Dalili za Ugonjwa wa Moyo unaoathiri mishipa ya damu(Coronary artery disease) ni pamoja na;

  1. Kupata maumivu ya kifua,kifua kuwa kizito au kubana
  2. Kukosa pumzi au mtu kupumua kwa shida
  3. Kupata maumivu ya shingo,taya, koo,sehemu ya juu ya tumbo au mgongoni
  4. Kuhisi hali ya ganzi kwenye viungo vya mwili,
  5. Viungo kama miguu au mikono kuhisi hali ya kupoa sana(baridi), kuwa dhaifu, au kupata ganzi n.k

Dalili za Ugonjwa wa moyo kutokana na shida ya mapigo ya moyo kutokuelewe irregular heartbeats (heart arrhythmias);

  1. Kupata maumivu ya kifua
  2. Kuhisi hali ya kizunguzungu
  3. Kuzimia
  4. Kuhisi maumivu ya kichwa
  5. Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda mbio zaidi (tachycardia)
  6. Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda taratibu(bradycardia)
  7. Mtu kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na hitilafu uliyozaliwa nayo(congenital heart defects);

  • Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa kijivu au blue (cyanosis)
  • Kuvimba miguu,tumbo au kuzunguka macho
  • Kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k

Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na shida kwenye misuli ya Moyo: heart muscle (cardiomyopathy);

  1. Kupata kizunguzungu
  2. Mwili kuchoka kupita kiasi
  3. Kupumua kwa shida baada ya kufanya kazi kidogo au hata ukiwa umepumzika
  4. Mapigo ya moyo kwenda mbio sana
  5. Kuvimba miguu,mikono n.k

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?

Zipo sababu mbali mbali kulingana na aina ya Ugonjwa wa moyo, na Sababu hizo ni pamoja na;

– Kuwa na makovu kwenye misuli ya Moyo(Heart muscle scarring),

Hii inatokana na Sababu mbali mbali ikiwemo: kuumia/kupata ajali na kuwa na kidonda kwenye moyo n.k

– Kuwa na mafuta yanayosababisha kuziba kwenye mishipa ya damu ndani ya moyo(Coronary artery disease)

– Matatizo ya kurithi(Genetic issues).

– Kuwa na Matatizo kwenye Utendaji kazi wa Figo

– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali, hapa tunazungumzia mtu kushambuliwa na viini mbali mbali vya magonjwa ikiwemo;

  • Bacteria
  • Fangasi
  • Virusi n.k

– Kuwa na matatizo kwenye tezi la Thyroid(Thyroid problems).

– Kuwa na magonjwa kama vile Rheumatic disease.

– Kuumia Sehemu ya moyo

– Kuwa na Shida ya shinikizo la Juu la Damu(High blood pressure)

– Kupata Shida ya Shambulio la Moyo(Heart attacks)

– Matumizi ya baadhi ya Dawa, mfano baadhi ya dawa za chemotherapy n.k

– Kuwa na magonjwa jamii ya Autoimmune diseases. n.k.

Vitu hizi huongeza hatari ya Mtu kupata Ugonjwa wa Moyo?

  • Kuwa Mzee
  • Kuwa na kiwango cha juu cha cholestrol kwenye damu
  • Kuwa na shinikizo la juu la damu
  • Matumizi ya tumbaku au Uvutaji wa Sigara
  • Unywaji wa Pombe
  • Kuwa na Uzito mkubwa wa mwili
  • Kutokufanya Mazoezi
  • Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari
  • Kula vyakula vya mafuta mengi,chumvi nyingi n.k

Vipimo unavyoweza kufanya ili kugundua Ugonjwa wa Moyo ni pamoja na;

– Electrocardiogram (EKG or ECG).

– Ambulatory monitors.

– Echocardiogram (Echo).

– Cardiac computerized tomography (CT).

– Heart magnetic resonance imaging (MRI).

– Vipimo vya Damu(Blood tests) n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo

Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo yanategemea chanzo husika pamoja na aina ya Ugonjwa wa moyo, ila kwa Ujumla kuna;

  • Dawa
  • Upasuaji
  • Pamoja na kubadilisha kabsa mtindo wa maisha

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Bonus Tips; Zingatia Mambo Haya Muhimu;

✓ Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa mwili, na kuwa na Uzito unaotakiwa kiafya

✓ Hakikisha unakula mlo bora kiafya(Healthly diet)

✓ Jitahidi kufanya Mazoezi ya mwili angalau kwa Nusu Saa(dakika 30) kila siku

✓ Epuka Uvutaji wa Sigara au matumizi ya tumbaku au dawa zozote za kulevyia

✓ Epuka Matumizi ya Pombe n.k…!!!!

Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini
0 Comment

Abiria afungua mlango wa ndege na kutembea juu ya bawaAfyaclass Bongo Social •

Abiria afungua mlango wa ndege na kutembea juu ya bawa

Mwanamume mmoja amekamatwa nchini Mexico baada ya kufungua mlango wa dharura wa ndege na kutembea juu ya bawa.

Mwanamume huyo alichukua hatua baada ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Guatemala City kukwama kwa saa nyingi kwenye lami bila kiyoyozi wala maji kwa abiria.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mexico ulisema hakuna madhara yoyote yaliyotokea, lakini abiria huyo amefikishwa kwa polisi.

Abiria wenzake, hata hivyo, wameandika taarifa ya pamoja, wakisema mtu huyo aliungwa mkono na kila mtu.

Tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita, mwendo wa saa 11:30 – takriban saa tatu baada ya ndege ya Aeromexico kupangwa kusafiri kutoka Mexico City.

Ucheleweshaji huo ulisababishwa na suala la matengenezo, ripoti ya tukio ilisema.

Iliendelea kueleza kuwa kubadilishwa kwa ndege kumekuwa muhimu baada ya abiria huyo ambaye hajatambuliwa kuunga mkono kwa kauli moja na wenzake.

Haijabainika iwapo mwanamume huyo atasalia kizuizini – au ni mashtaka gani anaweza kukabiliwa nayo.

Abiria waliokasirika, hata hivyo, walichukulia tukio hilo kwa mtazamo tofauti.

“Abiria wote kwenye ndege kutoka CDMX [Mexico City] kwenda Guatemala [ndege] AM 0672 wanasema kwamba abiria aliyefungua dirisha la dharura alifanya hivyo kwa ajili ya ulinzi wa kila mtu, kwa msaada wa kila mtu, kwa sababu kuchelewa na ukosefu wa hewa ilisababisha hali hatari kwa afya ya abiria,” barua iliyoandikwa kwa mkono na abiria wenzake inasomeka.

“Aliokoa maisha yetu,” waliandika – na kuongeza majina na saini zao kwenye barua iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Abiria afungua mlango wa ndege na kutembea juu ya bawa
0 Comment

Bibi arusi aliye na Saratani afariki wiki kadhaa baada ya kufunga Harusi ya ndoto yakeAfyaclass Bongo Social •

Bibi arusi aliye na Saratani afariki wiki kadhaa baada ya kufunga Harusi ya ndoto yake.

“Kwa kweli alikuwa mwanga chanya unaoangaza”

Katelen Green na mumewe Billy walifunga ndoa yao kwa “muujiza” mnamo Novemba – baada ya ukumbi wao na wasambazaji zaidi ya 30 kuchangia kila kitu bila malipo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24, kutoka Shropshire nchini Uingereza, alikuwa na hatua ya nne ya Hodgkin lymphoma- saratani isiyo ya kawaida ambayo hujitokeza katika mfumo wa lymphatic.

Saratani ilirejea kwa mara ya tatu mwaka jana na madaktari walikuwa wamemwambia hakuna kitu zaidi wangeweza kufanya.

Katelen alitarajia kuchangisha pesa kwa ajili ya majaribio ya kimatibabu ili aweze kuwa na muda zaidi na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, lakini alifariki wiki iliyopita.

Bibi arusi aliye na Saratani afariki wiki kadhaa baada ya kufunga
Harusi ya ndoto yake
0 Comment

Kukosa usingizi husababishwa na nini?Afyaclass Bongo Social •

Kukosa usingizi husababishwa na nini?

Mtu mwenye afya bora hupaswa kupata usingizi wa kutosha ili kuweza kukua katika afya bora,Lakini kwa baadhi ya watu suala la kupata usingizi limekuwa ni tatizo la mda mrefu na lenye kuwatesa sana.

Tatizo hili la kukosa Usingizi kwa kitaalam hujilikana kama “Insomnia”.

Wengi wamekuwa wakikosa usingizi kabsa, na baadhi yao huupata usingizi lakini katikati ya usiku au wakati wakiwa wamelala hushtuka na mala washtukapo hukosa usingizi mpaka kuna kucha.

Matatizo haya hutokana na sababu mbalimbali za kiafya..kiakili..kimwili na hata kwa baadhi ya tabia za mhusika mwenyewe.

Kukosa usingizi husababishwa na nini?

Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia mtu kukosa usingizi kama vile;

  • Msongo wa mawazo/hofu ya jambo fulani
  • Matumizi ya dawa za kulevya,kahawa,nikotini, n.k
  • Mazingira mabovu ya kulala n.k
  • Pamoja na Sababu nyingine nyingi…!!!!

Kwa kawaida mtu mzima mwenye afya bora na asiye na matatizo yoyote hupaswa kupata usingizi kwa mda wa masaa 7-8.

• Soma Zaidi muda Sahihi wa Kulala kiafya(Masaa ya kulala)

Tumezoea mara nyingi kwamba Mtu anapaswa kulala wakati wa Usiku(ni sahihi kabsa na kiafya inashauriwa Zaidi hivi),

ingawa kuna baadhi ya watu hulala mchana tu na usiku hawalali,hali hii kiafya haishauriwi sana kwani hudumaza ubongo na kusababisha msongo wa mawazo.

MADHARA YA KUKOSA USINGIZI

> Kupata msongo wa mawazo na kuwa na hali ya uchovu kila wakati

> Akili kuchoka na kutoweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi

>Kupata maumivu ya mwili na pia mwili kuwa na homa za mara kwa mara

> kuanza kupata shida ya kusahau sahau vitu(Kupoteza kumbukumbu) n.k

TIBA ya Kukosa Usingizi

Mara nyingi tiba ya tatizo hili imekuwa ni Matumizi ya dawa mbali mbali za kuleta usingizi ambazo zimetengenezwa kwa kemikali mbalimbali,

kemikali hizi zimekuwa ni chanzo kingine cha kusababisha magonjwa ya akili na pia matatizo ya ubongo.

Ni muhimu sana kutafta chanzo cha kukosa Usingizi na kutumia njia mbadala za kukusaidia kupata Usingizi.

Fahamu njia/Tiba hizo za Asili za kukusaidia kupata Usingizi, Soma Zaidi hapa(Usingizi tips)

MAMBO 10 YA KUKUSAIDIA KULALA KAMA UNA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI USIKU.

Inawezekana wewe ni moja kati ya ambao wamewahi kuwa na tatizo la kukosa usingizi wakati wa usiku(INSOMNIA),

Hii huwa ni hali ambayo mara nyingi inasumbua na kukera hususani kama mtu umechoka.

MAMBO YA KUZINGATIA kama unatatizo la Kukosa Usingizi

1. Fanya mazoezi wakati wa mchana

2. Kuwa na muda binafsi na tafakari ilivyokuwa siku yako;

Kabla ya kulala pia inashauriwa kupata muda binafsi ili kutafakari yaliyotokea kwa siku hiyo na jinsi siku inayofuata inaweza kuwa nzuri na ya mafanikio.

3. Fanya Sala;

Inashauriwa pia kwa dini na imani yoyote, kufanya ibada au sala kunasaidia akili ku relax na kufanya usingizi uje na unaweza kulala kwa amani.

4. Soma kidogo vitu chanya.

5. Kuwa na ratiba maalumu ya kulala;

Hii pia itasaidia kulala bila shida kwa wakati uliozoea.

6. Chunga tabia yako ya kulala;

Ni muhimu sana kuzingatia, kuachana na vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la kushindwa kulala wakati wa usiku ikiwa ni pamoja na kulala wakati wa jioni jambo linaloweza kukata usingizi pindi muda wa kulala unapofika wakati wa usiku.

7. Acha kuangalia TV nyakati za usiku sana;

Pia ni muhimu kuachana na tabia ya kukaa macho na kuangalia TV nyakati za usiku sana kwani mwili hujijengea kutolala wakati huo unapofika kwani huwa ni muda ambao kwa kawaida unakuwa unaangalia TV.

Soma Zaidi hapa Madhara ya kuangalia TV au kutumia Simu nyakati za usiku sana;

8. Chunga unachokula au kunywa kabla ya kulala;

 Inashauriwa kuepuka kunywa kahawa au pombe kabla ya kwenda kulala kwa sababu ni vitu ambavyo vinachukua muda mrefu kuyeyushwa tumboni.

Vitu hivi pia ni chanzo kikubwa cha Mtu kukosa Usingizi.

9. Andaa mazingira mazuri ya kulala;

Kulala kwenye mazingira mazuri ni muhimu. Inashauriwa kulalia mashuka masafi na mito misafi, huku eneo zima kama chumbani liwe safi lisilo na vumbi wala harufu.

10. Tumia choo kabla hujalala;

Baadhi ya watu hupoteza kabisa usingizi na kushindwa kuupata tena pindi wanapoamka usiku ili kwenda chooni au kwa sababu nyingine zozote. Kwa mantiki hiyo wataalamu wanashauri ni vyema kwenda haja kabla ya kwenda kulala ili kwamba mwili usisumbuliwe wakati umelala.

 FAIDA ZA USINGIZI PAMOJA NA NJIA 13 ZA KUPATA USINGIZI MZURI

Japokuwa kadri umri unavyokuwa Mkubwa ndivo masaa ya kulala hupungua,ila bado umuhimu wa kulala vizuri ni Mkubwa sana, Tafiti Zinaonyesha Mtu anayepata usingizi au anayelala vizuri,Mfano kwa Mtu Mzima wastani wa masaa 8 yanatosha kabsa,Humsaidia sana katika vitu vitu mbali mbali.

SUMMARY:

Katika Sehemu hii tunajadili Faida za kupata Usingizi Mzuri na Njia 13 za kukusaidia wewe mwenye matatizo ya kukosa usingizi kila siku,kutatua tatizo hili kwa haraka sana.Na kuendelea kufurahia Maisha.

Baadhi ya Faida za kupata Usingizi Mzuri ni pamoja na hizi hapa;

✓ Kuimarisha Kinga yako ya Mwili

✓ Kuongeza Uwezo wako wa akili pamoja na uwezo wako wa Kufikiri Vizuri

✓ Huondoa uchovu wa Mwili pamoja na kuupa mwili Nguvu ya Kutosha

✓ Husababisha Ngozi ya mwili kunawiri pamoja na afya ya seli hai za mwili

✓ kuboresha afya ya Ubongo na uwezo wa kukumbuka n.k

NJIA 12 ZA KUKUSAIDIA KUPATA USINGIZI MZURI

Zifuatazo ni Njia ambazo zitakusaidia wewe kwa kiasi kikubwa kupata Usingizi mzuri na kuleta Nguvu na si uchovu katika Mwili wako;

1. Punguza Matumizi ya vitu vyenye mwanga wa Blue wakati wa siku,kama vile kwenye Taa au simu,Tv, Computer n.k.

Tafiti zinaonyesha kwamba mwanga wa Blue hupunguza uzalishaji wa Homoni au kichocheo aina Ya Melatonin ambacho ndyo huhusika na kuleta Usingizi.

2. Kaa kwenye Mwanga wa Kutosha wakati wa Mchana,

Hii husaidia mwili wako kuweza kutofautisha wakati wa usiku ni upi na wakati wa Mchana ni upi,hivo kukusaidia wewe kupata usingizi mzuri wakati wa usku.

3. Epuka Matumizi ya Vinywaji vyenye Caffeine hasa wakati wa Usiku,

kwani vinywaji kama hivi huuchangamsha mwili wako na kukusababishia kukosa Usingizi kabsa wakati wa Usku. Hivo epuka matumizi haya ya Vinywaji vyenye Caffeine wakati wa Usku.

4. Punguza tabia ya kulala wakati wa mchana,hii itakusaidia wewe kulala vizuri wakati wa Usku.

Inashauriwa kwa asilimia kubwa muda wa kulala na kumka kila siku uzingatiwe sana,hali hii huuzoesha mwili kwamba sasa ni wakati wa usku na ni wakati wangu wa kulala.

5. Epuka matumizi ya pombe au kilevi chochote,kwani hivi huathiri uzalishaji wa kichocheo au homoni hii ya Melatonin ambayo inahusika na Usingizi moja kwa moja.

6. Boresha Mazingira yako ya kulala,

Tafiti zinaonyesha watu wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kukosa Usingizi, hulala kwenye vyumba ambavyo si rafiki,

mfano; Chumba ambacho kina mwanga sana,chumba chenye Joto sana,Chumba chenye baridi sana,Chumba ambacho kina makelele ya aina yoyote,mfano Redio au watu.n.k

7. Epuka matumizi au ulaji mwingi wa chakula wakati wa usiku,pia Epuka kula vyakula vizito sana wakati wa Usku.

8. Pumzisha akili yako na iburudishe na vitu  kama Mziki laini n.k kabla Ya kulala na epuka kutazama vitu kama Movies ndefu za kutisha wakati wa usku.

9. Hakikisha umeoga kabla ya kwenda kulala Au kuupumzisha mwili wako kitandani.

10. Tumia godoro zuri na mto safi kama wewe ni mpenzi wa mto wakati wa kulala, Kulala chini au kwenye kamba n.k,ni ngumu sana kupata usingizi mzuri

11. Fanya mazoezi kila siku wakati wa mchana kabla siku yako haijaisha au kabla hujaenda kulala kitandani.

12. Epuka kunywa kwa wingi vimiminika,kwani vitakufanya uanze kuamka amka mara kwa mara wakati wa usku,hivo kupelekea kukosa usingizi mzuri.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Kukosa usingizi husababishwa na nini?
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD