Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa TumbakuAfyaclass Bongo Social •

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa Sigara hadharani.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amebainisha hayo leo Aprili 30,2024 Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 215 kutoka kwa Mbunge wa Tumbe, Mhe. Amour Khamis Mbarouk aliyeuliza Je, ni lini Serikali italeta Sheria ya Kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.

Aidha amesema sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.

Vile vile Dkt. Mollel ametoa wito kwa wabunge kuwa mabalozi wa Udhibiti wa Tumbaku katika jamii ili kusaidia wananchi kuepuka magonjwa yasiyoyakuambukiza

Bunge limeendelea ambapo leo ni mkutano wa 15 kikao cha 16.

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria
ya Udhibiti wa Tumbaku
0 Comment

Mhogo Una faida gani kiafya? Soma hapaAfyaclass Bongo Social •

Mhogo Una faida gani kiafya? Soma hapa

Jules Kouassi, Daktari wa Afya ya Umma na mtaalamu wa lishe, kutoka Ivory Coast, anasema muhogo ni chakula muhimu, kwa sababu unaweza kuliwa na kila mtu na kuna njia tofauti za kutayarisha chakula hicho.

Anasisitiza, kwa vyovyote vile unavyotaka kuandaa muhogo, unapaswa kukumbuka muhogo hauliwi mbichi, kwa sababu una kemikali ndani yake.

Anasema unapaswa kuupika muhogo kwa usahihi. Kwani sio tu mizizi yake ndio yenye faida, hata majani ya muhogo pia yana faida.

”Majani na mizizi yana vitamini A, B, C, E kwa wingi – pia hutoa virutubisho vingine kama vile magneshiamu, maadini ya chumvi, chuma na kalshiamu,” anasema Dkt. Kouassi.

“Kuna wanga mwingi kwenye muhogo – ni kama 70% ya muhogo ni wanga, kwa hivyo hufanya mwili kuwa na nguvu za kutosha,” anasema Dkt. Kouassi.

Muhogo una faida sana kwa kwa watu wanaofanya kazi nzito ambayo hutumia nguvu nyingi,” anasema Dkt. Kouassi.

“Muhogo pia husaidia kupambana na shinikizo la damu mwilini na itakusaidia kulala vizuri. Hii ndiyo sababu watu wengi Afrika, wanapomaliza kula muhogo, husema wanataka kulala.”

Kulingana na Dkt. Kouassi, majani ya muhogo yanafaa kusaidia kupambana na upungufu wa damu au ukosefu wa seli nyekundu za damu.

Lakini kwa kuwa kuna mihogo ambayo ina kemikali inayoitwa cyanide ndani yake, ni muhimu kuipika kwa muda mrefu ili kemikali yote itoke.

“Ni lazima uupike vizuri. Na kuumwaga maji,” anasema Dk. Kouassi.

Mhogo Una faida gani kiafya? Soma hapa
0 Comment

Clarithromycin inatibu nini, soma hapa kufahamuAfyaclass Bongo Social •

Clarithromycin inatibu nini

Clarithromycin ni dawa inayotumika kutibu aina nyingi za maambukizi yanayotokana na bacteria(bacterial infections).

Dawa hii pia huweza kutumika pamoja na dawa zingine za vidonda vya tumbo(anti-ulcer medications) kutibu aina kadhaa za vidonda vya tumbo.

Clarithromycin huweza kuzuia aina nyingi za maambukizi ya bacteria, na dawa hii hujulikana kama macrolide antibiotic. Hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bacteria.

Kumbuka; Clarithromycin haitafanya kazi dhidi ya maambukizi yoyote yanayotokana na virusi-viral infections.

Dawa ya Clarithromycin huweza kutumika kutibu maambukizi ya kifua kama vile ya; pneumonia, matatizo ya ngozi kama vile cellulitis, pamoja na maambukizi ya Sikio. Pia  Clarithromycin huweza kutumika kutibu Helicobacter pylori, bacteria anayesababisha vidonda vya Tumbo.

Wakati mwingine Clarithromycin hutumika kwa watu wenye mzio au allergy na dawa jamii ya penicillin au antibiotics zinazofanana na penicillin, kama vile amoxicillin.

Unaweza kupewa Clarithromycin kwa maambukizi ya bacteria kwenye mapafu mfano kwa mgonjwa wa pneumonia, maambukizi kwenye mrija unaolekea kwenye mapafu-bronchitis (infection of the tubes leading to the lungs), maambukizi ya masikio,Ngozi,Koo n.k

Dawa hii ya Clarithromycin huweza kutumika kutibu na kuzuia kusambaza kwa maambukizi ya Mycobacterium avium complex (MAC) [aina ya maambukizi ya mapafu ambayo mara nyingi huathiri watu walio na virusi vya ukimwi (VVU)].

DOSES;

Kwa Upande wa Doses, Lazima ushauriane na wataalam wa afya,kwani itategemea na umri wako,Uzito, tatizo linalokusumbua, hali yako ya kiafya pamoja na uwezo wa mwili wako kujibu matibabu.

Ikiwa unatumia dawa hii kutibu maambukizi, endelea kutumia dawa hii hadi kiasi kamili kilichowekwa kiwe kimekamilika, hata kama dalili zitatoweka baada ya siku chache. Kuacha dawa mapema kunaweza kusababisha kurudi kwa maambukizi. Mwambie daktari wako ikiwa hali yako hudumu au inazidi kuwa mbaya.

Maudhi(Side Effects) ya Clarithromycin

Haya hapa ni maudhi yanayoweza kutokea kwa Mtu anayetumia dawa ya Clarithromycin;

  1. Kuharisha
  2. Kuhisi kichefuchefu
  3. Kutapika
  4. Kupata maumivu ya kichwa
  5. Kubadilika kwa ladha mdomoni n.k

Watu wengi wanaotumia dawa hii hata wakipata baadhi ya Side effects hizi, hawapati kwa kiwango kibaya.

Hakikisha unaongea na wataalam wa afya ili kuacha na kubadilishiwa mara moja dawa hii ya Clarithromycin ikiwa baada ya kutumia;

– Unapata kichefuchefu na kutapika bila kukoma

– Unapoteza uwezo wako wa Kusikia

– Unapata dalili zote za kuchanganyikiwa au matatizo ya akili

– Unapoteza uwezo wa kuona vizuri, unaona marue rue n.k

– Misuli inakuwa Dhaifu

– Unapoteza uwezo wa Kuongea

– Unapata maumivu makali sana ya Tumbo

– Unakojoa Mkojo mweusi

– Ngozi na macho vinabadilika rangi na kuwa manjano.

– Unapata homa ambayo haiishi

– Unavimba lymph node,

– Unaaza kutokwa na vipele kwenye ngozi

– Unakosa pumzi au kupata shida ya kupumua

– Unapata kizunguzungu

– Unaaza kupata muwasho mkali kwenye ngozi,usoni,kwenye Ulimi,kooni n.k.

Rejea Link;

Clarithromycin inatibu nini, soma hapa kufahamu
0 Comment

Gharama za upasuaji wa kurekebisha maumbile zinaanzia Sh15 milioni hadi Sh22.5 milioniAfyaclass Bongo Social •

Gharama za upasuaji wa kurekebisha maumbile zinaanzia Sh15 milioni hadi Sh22.5 milioni.

Wakati Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ikitarajia kufanya upasuaji wa kurekebisha maumbile Mei 2024, imeelezwa wanawake wenye uhitaji wa huduma hiyo ni wengi, lakini wanakwamishwa na kipato.

Daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Erick Muhumba akizungumza na Mwananchi Digital hivi karibuni amesema gharama za upasuaji zinaanzia Sh15 milioni hadi Sh22.5 milioni sawa na Dola za 6,000 za Marekani hadi Dola 9,000 za Marekani.

Upasuaji huo ni pamoja na kuongeza makalio, matiti na kupunguza tumbo.

Dk Muhumba amesema kambi maalumu ya siku tatu kwa ajili ya upasuaji huo inatarajiwa kufanyika Mei 13 hadi 15, 2024.

“Wanaojitokeza na kulipia huduma ni wachache, mpaka sasa kwa kambi ijayo aliyelipia ni mmoja lakini kwa walioonyesha nia ya kulipa ili wapatiwe huduma wapo sita,” amesema Dk Muhumba.

“Wanaoulizia huduma ni wengi, wengine wanakuja wanauliza gharama baada ya kuelezwa wanasema hawana fedha. Tunazungumza nao na tumeshawapatia control number (namba ya malipo) ili wafanye malipo watakapokuwa tayari.”

Dk Muhumba amesema wamesogeza huduma kwa kuwa awali, Watanzania wengi walienda nje ya nchi.

Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

(Imeandikwa na Herieth Makwetta)

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa

Gharama za upasuaji wa kurekebisha maumbile zinaanzia Sh15 milioni hadi
Sh22.5 milioni
0 Comment

Zaidi ya watu 45 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya bwawa kupasua kingoAfyaclass Bongo Social •

Zaidi ya watu 45 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya bwawa kupasua kingo zake kufuatia mvua kubwa na mafuriko, maafisa wamesema.

Watu katika vijiji karibu na Mai Mahiu, yapata kilomita 60 kutoka mji mkuu, Nairobi, walisombwa na maji walipokuwa wamelala.

Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mafuriko ambayo yameharibu sehemu za Kenya katika mwezi uliopita.

Vikosi vya waokoaji vinachimba matope kusaka manusura katika vijiji kadhaa, vikiwemo Kamuchiri na Kianugu kaunti ya Nakuru.

Maelezo ya video,Makumi ya watu wamepoteza maisha baada ya bwawa kuvunja kingo zake nchini Kenya

Kati ya miili 42 iliyopatikana mapema wasubuhi 17 ilikuwa ya watoto, kamanda wa polisi Stephen Kirui alisema, akinukuliwa na shirika la habari la Reuters.

“Maji yalikuja kwa kasi kutoka Bwawa la Old Kijabe na kusomba nyumba na magari mengi. Hatujawahi kuona mafuriko makubwa kama haya tangu tulipozaliwa hapa Mai Mahiu,” David Kamau aliiambia BBC.

Mkazi mwingine, Peter Muhoho, alisema kuwa wengi wa majirani zake walisombwa na maji katika kijiji cha Kianugu chenye takriban nyumba 18.

“Nilikuwa nimelala niliposikia kishindo kikubwa na mayowe. Maji yalikuwa yamefurika eneo hilo. Tulianza kuokoa watu,” Bw Muhoho aliambia BBC.

Akionyesha begi alilokuwa ameshikilia, Bw Muhoho aliongeza: “Mkoba huu ni wa mtoto niliyemfahamu. Alisombwa na maji. Niliupata [mfuko huo] chini ya mkondo.”

Serikali imeahirisha kufunguliwa kwa shule kote nchini Kenya huku mvua zaidi ikitarajiwa kunyesha, kulingana na idara ya utabiri wa hali ya anga .

Zaidi ya watu 130,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko hayo, huku watu wengi wakipata hifadhi shuleni.

Mvua kubwa pia imenyesha katika nchi jirani za Tanzania na Burundi.

Takriban watu 155 wameuawa nchini Tanzania tangu Januari.

Nchini Burundi, karibu watu 100,000 wamekimbia makazi yao.

Idadi ya waliopoteza maisha haijulikani, lakini tovuti inayohusishwa na Umoja wa Mataifa inaripoti kuwa watu 68 waliuawa katika mji mkuu, Bujumbura, tarehe 10 Februari pekee baada ya mvua kubwa kuharibu nyumba 3,500.

Mwandishi wa BBC anayeshughulikia utabiri wa hali ya hewa Chris Fawkes anasema kuwa mojawapo ya vichochezi vikubwa vya mvua ni Dipole ya Bahari ya Hindi (IOD).

IOD – ambayo mara nyingi huitwa “Indian Niño” kwa sababu ya kufanana kwake na sehemu yake ya Pasifiki – inaelezea tofauti ya halijoto ya uso wa bahari katika sehemu tofauti za Bahari ya Hindi.

Wakati wa awamu chanya, maji katika Bahari ya Hindi magharibi yana joto zaidi kuliko kawaida na hii inaweza kuleta mvua kubwa bila kujali El Niño.

Hata hivyo, wakati wote IOD chanya na El Niño hutokea kwa wakati mmoja, kama ilivyokuwa mwaka jana, mvua katika Afrika Mashariki inaweza kuwa kali.

Mojawapo ya mifumo chanya ya IOD kwenye rekodi ililingana na mojawapo ya mifumo thabiti zaidi ya El Niño mwaka wa 1997 na 1998, huku mafuriko makubwa yakiripotiwa. Haya yalisababisha vifo zaidi ya 6,000 katika nchi tano katika eneo hilo.

Mada: Via BBC

Zaidi ya watu 45 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya bwawa kupasua
kingo
0 Comment

Maporomoko ya tope yafunika nyumba 13 MulebaAfyaclass Bongo Social •

Maporomoko ya matope kutoka Mlima Kabumbilo hadi mwalo wa Kabumbilo yalianza kujitokeza Aprili 17, 2024 na awali iliripotiwa kwamba nyumba moja na ekari 10 za mashamba viliathiriwa.

Muleba. Maporomoko ya matope katika Mlima Kabumbilo Kijiji cha Ilemela wilayani Muleba yamefunika nyumba 13 wananchi wakizuiliwa kufika eneo hilo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Aprili 29, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk Abel Nyamahanga amesema nyumba 13 zifunikwa na matope yaliyoporomoka kutoka Mlima Kabumbilo

Mlima huo upo kwenye vitongoji vya Bushabo na Kabumbilo katika Kijiji cha Ilemela, Kata Gwanseli wilayani Muleba Mkoa Kagera.

Dk Nyamahanga amesema mpaka mchana wa leo hakuna majeruhi wala vifo vitokanavyo na maporomoko hayo.

Amesema wananchi wote walishapewa taarifa za kuhama katika eneo hilo na kwa sasa hakuna mtu anayetakiwa kuendelea kuishi au kwenda eneo hilo, maana ni eneo hatarishi.

Mkuu wa wilaya amesema wataalamu wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha madhila hayo.

“Nyumba 13 zimefunikwa na matope, mashamba ya watu yamefunikwa tumetuma Jeshi la Polisi kuzuia eneo hilo, ni marufuku wananchi kwenda huko, wakae mbali na eneo hilo ni hatari. Kuna mambo unaweza kukimbia kuangalia ila huko wasiende,” amesema Dk Nyamahanga

Zainabu Hamza, mkazi wa Bushabo amesema nyumba yake imefunikwa na matope, migomba na mazao mengine pia vimefunikwa na tayari familia yake ameihamisha kutoka eneo hilo.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ilemela, Chirisant Marchades amesema kila wakati kasi ya kasi inaongezeka, yanazidi kufunika makazi na mazao na kwamba kuna hatari ya uharibifu zaidi wa nyumba nyingine kufunikwa.

Amesema Kitongoji cha Kabumbilo kina nyumba 275 na watu 1,225 wanaishi humo na eneo lililoathiriwa lina nyumba 45, kati ya hizo nyumba 13 zimefunikiwa na matope.

Marchades amesema katika kuhakikisha familia zinapata sehemu ya kujihifadhi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba imewapatia mabati 90 ili kuwasaidia waliokumbwa na madhila hayo.

Ameiomba Serikali iendelee kuongeza ulinzi maana watu wanazidi kuwa wengi wanaokwenda kwenye eneo hilo ambalo lina hatari kubwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Kagera, Zabron Muhumha amesema watu wote wanatakiwa kuhama kwenye  mazingira hayo, maana udogo na matope vinazidi kuporomoka.

“Kwa sasa hatakiwi mtu yeyote kuwepo, wasubiri tamko la Serikali,” amesema.

Maporomoko ya tope kutoka Mlima Kabumbilo hadi mwalo wa Kabumbilo yalianza Aprili 17, 2024 ndipo mkuu wa wilaya aliwataka wananchi kuhama eneo hilo, baada kuliripotiwa kwamba nyumba moja na eka 10 za mashamba kuathiriwa.

Maporomoko ya tope yafunika nyumba 13 Muleba
0 Comment

Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na mabaka mabaka ya rangi ya blueAfyaclass Bongo Social •

Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na mabaka mabaka ya rangi ya blue hasa hasa maeneo ya makalioni na mgongoni, mabaka mabaka haya kwa kitaalam hujulikana kama Mongolian spot.

MABAKA MABAKA HAYA HUDUMU KWA MUDA GANI?

Mabaka mabaka(mongolian spot) huweza kupotea yenyewe ndani ya muda mfupi au kudumu  kwa kipindi kirefu hata miaka Minne na kuendelea,

Kwa wengine hupotea yenyewe baada ya mtoto kufikia umri wa kubalehe Na baadhi ya watoto wachache mabaka mabaka haya huendelea kuwepo maisha yao yote.

CHANZO CHA MABAKA MABAKA HAYA NI NINI?

– Chanzo cha mabaka mabaka haya au Mongolian spot, ni kutokana na uwepo mkubwa wa seli hai kwa ajili ya kuleta rangi kwenye ngozi maarufu kama melanocytes hasa hasa maeneo ya makalioni na mgongoni,

ndyo sababu kubwa ya rangi ya ngozi katika maeneo haya kubadilika na kuwa blue kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha Melanocytes ambazo huzalisha melanin(kwa ajli ya kuipa ngozi rangi yake).

MATIBABU YA MONGOLIAN SPOT

– Tatizo hili kwa mtoto huweza kuisha lenyewe wala hakuna matibabu yoyote ambayo hufanyika kwa mtoto mwenye shida hii kwenye ngozi yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na mabaka mabaka ya rangi ya blue
0 Comment

Mwanamtandao maarufu wa TikTok Nchini Iraq auawa kwa RisasiAfyaclass Bongo Social •

Mwanamtandao maarufu wa TikTok Nchini Iraq auawa kwa Risasi

Mwanamtandao maarufu wa TikTok Nchini Iraq aitwaye Ghufran Sawadi maarufu kama Om Fahad, ameuawa kwa risasi nje ya nyumba yake mashariki mwa Mji Mkuu wa Baghdad Ijumaa usiku ambapo camera za usalama zilimnasa Muuaji aliyevalia mavazi meusi akishuka kwenye pikipiki na kumpiga risasi.

Tayari Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq imesema imeunda Timu ya Wataalamu kuchunguza mazingira ya mauaji ya Mwanamtandao huyo aliyekuwa na Wafuasi wanaokaribia nusu milioni pamoja na likes zaidi ya milioni tatu kwenye mtandao wake wa Tiktok ambao aliutumia kuweka video zake akicheza nyimbo mbalimbali, kutoa misaada kwa Watu na kuonesha maisha yake binafsi.

Februari mwaka 2023 Ghufran alihukumiwa kwenda Jela miezi sita kwa kosa ambalo Mahakama ilisema ni la kusambaza video za maongezi machafu ambayo yanadhoofisha adabu na maadili ya Jamii ya Nchi hiyo ambapo Watayarishaji wengine watano wa maudhui mtandaoni walihukumiwa jela hadi miaka miwili kwa makosa mbalimbali katika maudhui yao.

Hii ilikuja baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq mwezi January mwaka 2023 kuzindua Kamati ya kugundua maudhui machafu na yenye kudhalilisha ambayo yamekuwa yakiwekwa mitandaoni na Raia wa Nchi hiyo wenye ushawishi kama Om Fahad ambapo Serikali ilisema wanachokifanya ni kulinda maadili na mila za familia katika Jamii ya Wairaq.

Mwanamtandao maarufu wa TikTok Nchini Iraq auawa kwa Risasi
0 Comment

Ugonjwa unaosababishwa na konokonoAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa Schistosoma.

Konokono wanapoambukizwa na minyoo hawa, wanaweza kueneza ugonjwa huo kwa binadamu wanapokua majini ikiwa wamebeba minyoo hao.

Dalili za schistosomiasis

Dalili za schistosomiasis zinaweza kujumuisha homa, kichefuchefu, kutapika, na kuharisha.

Pia inaweza kusababisha dalili za muda mrefu kama vile kuvimba kwa ini na kibofu cha mkojo, na uharibifu wa viungo vya ndani.

Chanzo cha schistosomiasis

Chanzo cha schistosomiasis ni maambukizi ya minyoo ya Schistosoma, ambayo hupatikana katika maji yenye konokono walioambukizwa. Watu huambukizwa wanapokutana na maji yenye minyoo hiyo, kwa mfano, wanapofanya shughuli kama kuogelea au kunawa.n.k

Tiba ya schistosomiasis

Tiba ya schistosomiasis inahusisha matumizi ya dawa za kupambana na minyoo, kama vile praziquantel. Kuzuia maambukizi ya awali ni muhimu, kwa kuepuka kuingia kwenye maji yenye konokono walioambukizwa na kutumia maji salama kwa kunywa na kujisafisha.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa unaosababishwa na konokono
0 Comment

Serikali kuanzisha taasisi upasuaji ubongoAfyaclass Bongo Social •

Serikali kuanzisha taasisi upasuaji ubongo

Wizara ya Afya imedhamiria kuanzisha taasisi mahususi itakayoshughulikia masuala ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ili kuboresha huduma hizo za ubingwa na kutoa katika Taasisi ya Mifupa Ubongo (MOI) ambapo itabakia na masuala ya upasuaji wa mifupa pekee.

Waziri wa Afya. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Aprili 27, 2024 baada ya uzinduzi wa chama cha madaktari bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu kikiongozwa na Rais wa chama hicho Dk Othmani Kiloloma Jijini Dar Es Salaam.

“Lengo la chama hiki ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora na salama za upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, ikiwemo upatikanaji wa madaktari bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu,” amesema Waziri Ummy.

Amesema Tanzania kuna madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu 25 tu, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inapendekeza angalau katika kila watu 150,000 kuwe na daktari bigwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu mmoja.

“Ukichukua idadi ya madaktari bigwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu 25 tulionao maana yake kwa Tanzania daktari bigwa mmoja anahudumia Watanzania milioni 2,400,000, huduma hizi bado hazijawafikia Watanzania wengi ndio maana chama hiki kimekuja ili pia kujengeana uwezo na kuhamasisha madaktari wengine waweze kusomea fani hiyo ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu”,amesema Waziri Ummy.

Serikali kuanzisha taasisi upasuaji ubongo
0 Comment

Wiki chache zilipita na nilipoenda kwa daktari aliniambia nina ujauzitoAfyaclass Bongo Social •

‘Nilitaka kujiua baada ya kugundua nimepata ujauzito kutokana na ubakaji’

Alienda kuchota maji mtoni kama kila siku. Ghafla, wanaume wawili walimkamata kwa nyuma, wakamwekea kisu kooni, wakampiga na mmoja wao akambaka.

Kwa sababu ya ubakaji huo, Fausia ambalo siyo jina lake la kweli, alipata mimba.

Kuanzia wakati huo, matatizo yalianza ambayo yangebadilisha maisha yake milele.

Wabakaji, ambao aliwafahamu vyema, walitishia kumuua yeye na familia yake yote ikiwa angesema kilichotokea.

Fausia alitaka kutoa mimba hiyo lakini nchini Honduras utoaji mimba ni kinyume cha sheria bila kujali mhusika yuko katika hali gani. Haijalishi ikiwa mwanamke alibakwa, maisha yake yamo hatarini au ikiwa ujauzito una matatizo yoyote.

Pia hakuwa na uwezo wa kupata tembe ya dharura ya kuzuia mimba, ambayo ingemzuia kupata ujauzito, kwa sababu ilikuwa imepigwa marufuku wakati huo.

Yeye ni mwanamke wa kiasili wa Watu wa Nahua na mtetezi wa haki za binadamu katika nchi yake.

Honduras ni mojawapo ya mataifa sita katika Amerika ya Kusini na Caribbean – pamoja na El Salvador, Nicaragua, Jamhuri ya Dominika, Haiti na Suriname – ambapo utoaji mimba ni marufuku kabisa.

Kituo cha Haki za Uzazi na Kituo cha Haki za Wanawake kiliwasilisha kesi mbele ya Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutaka “haki kwa Fausia” na Honduras kurekebisha mfumo wa kisheria ambao unaharamisha kabisa utoaji wa mimba.

BBC Mundo iliwasiliana na serikali ya Honduras ili kujua maoni yake lakini hadi wakati wa kuchapishwa kwa makala haya tulikuwa hatujapata jibu.

Huu ni ushuhuda wa Fausia alioeleza wakati wa mahojiano. Baadhi ya maelezo ya simulizi yake yameachwa ili kulinda utambulisho wake.

“Kwa kuwa nyumbani hatukuwa na huduma ya maji ya kunywa, nilienda mtoni kutafuta maji ili kuandaa chakula cha jioni. Nilipokuwa nikifanya hivyo, wanaume wawili waliokuwa wamejificha kwenye kichaka cha nyasi, walinivamia kwa nyuma. Wakaniwekea kisu kooni kisha wakanishika mikono yangu kwa nyuma.

“Niliwaambia wasinidhuru, waniache tafadhali, kwamba sina pesa, lakini waliniziba mdomo na kunipiga. Mmoja wao alinibaka.”

“Wanaume hawa ni kizazi cha familia iliyonyakua sehemu ya ardhi kutoka kwa baba yangu. Miezi michache kabla, tukio lilikuwa limetokea kuhusu ardhi. Jamaa mmoja wa walionibaka alienda kubomoa uzio wa shamba letu na kuniambia utalipia, nitakutumia genge la watu.”

“Sikuyachukulia maneno yake kwa uzito, lakini baada ya shambulio hilo tuliketi na kutathmini kilichosemwa na kile kilichotokea na tukagundua kwamba yalihusiana na suala la ardhi.”

“Wiki chache zilipita na nilipoenda kwa daktari aliniambia nina ujauzito.

“Ziwezi kueleza nilichohisi wakati huo. Nilijisikia vibaya, nilijiona mchafu, ni jambo ambalo halikuwa katika mipango yangu, ambalo sikutaka, na hasa jinsi lilivyotokea.

“Mwitikio wangu ulikuwa mbaya, ulikuwa kutokubaliana na uhalisia wa mambo, “Sitaki, sitaki, sitaki,” kila wakati nilifikiria hivyo.”

Uavyaji mimba sio tu kwamba hauruhusiwi nchini Honduras, lakini pia umepigwa marufuku na Katiba ya nchi hiyo. Mnamo Januari 2021, Bunge la Kitaifa liliidhinisha katika mjadala, mmoja marekebisho ya katiba ambayo yanapiga marufuku kabisa ya kukatizwa kwa ujauzito.

Kila siku wasichana watatu walio chini ya umri wa miaka 14 hupata mimba kutokana na kubakwa, kulingana na data ya Wizara ya Afya (2022).

Daktari aliniuliza nini kimetokea. “Umewasilisha malalamiko?” aliniuliza, Hapana, nilijibu, kwa sababu walikuwa wamenitishia kuwa wataniua ikiwa nitatoa taarifa.

Alipendekeza nifanye hivyo. Nilienda kwa Wizara ya Umma na daktari wa uchunguzi alinitibu.

Alinichunguza na kusema, “Tunajua tayari una mimba. Ukitoa mimba au tukagundua kuna kitu kimetokea kwenye ujauzito huu, tutakuweka gerezani kwa sababu utoaji wa mimba ni marufuku nchini.”

“Sikutaka kuendelea na ujauzito. Nikawa na uchungu mwingi sana, nikakata tamaa na sikutaka tena kuendelea na mateso hayo.”

“Ilikuwa ni mimba hatari kwangu, kwa miezi tisa nikihisi kichefuchefu, afya yangu ya kimwili ilikuwa mbaya kwa sababu sikuweza kula.”

“Muda ulipita na mara kadhaa nilifikiria kujiua kwa sababu nilijiona sina thamani. Mpaka nilipojaribu kujitoa uhai.”

Nakumbuka kulikuwa na mwembe na kwenye mti huo kulikuwa na chandarua. Mama yangu hakuwepo wakati huo, alikuwa ameenda mtoni kufua nguo na mtoto wangu mdogo.

Nilikuwa peke yangu. Hapo ndipo nilipojaribu kujiua. Kwa sababu sikuwa nala vizuri, nilikuwa dhaifu sana, sikuwa na nguvu. Niliweka kiti, lakini kiti kilianguka na sikufanikiwa kutimiza lengo langu.

Hapo ndipo yule binti yangu aliponiona na kukimbia kumwambia mama yangu kwamba nilikuwa ninaning’inia. Kisha mama yangu akaja kuniokoa. Nadhani nilipoteza fahamu, sikumbuki kilichotokea baada ya hapo.

Nakumbuka tu kwamba niliamka nikiwa kitandani. Binti yangu na mama yangu walikuwa karibu na kitanda. Msichana alisema huku akilia: “Mama, usife, mama, usife.”

Hilo lilikuwa gumu sana kwa sababu nilikuwa na hamu ya kutoroka uhalisia unaonikabili, lakini pia nilitaka kuwa pamoja na watoto wangu. Nilihisi kama nilipaswa kutafuta nguvu ili niweze kusonga mbele na maisha.

Wakati wa kujifungua mambo yalikuwa magumu sana. Siku hiyo nilifika nikiwa na uchungu, waliniambia kuwa njia tayari imeanza kufunguka na kuniingiza kwenye chumba cha upasuaji. Sikuwa tayari kujifungua kwa sababu nilikuwa nimeenda kupangiwa siku ya kufanyiwa upasuaji.

Muda huo daktari alifika akiwa na karatasi na kuniambia nisaini karatasi hiyo, aliniambia kuwa ni lazima nisaini kwa sababu walikuwa wakinifunga mirija ili nisizae tena.

Nilimwambia hapana, kwamba sitaki kusaini, kisha akakasirika sana na kuniambia: “Sawa, usisaini lakini nitakuona hapa baada ya miaka miwili tena kujifungua.”

Nilimsisitiza kuwa sitaki kusaini kwa sababu sikujua inahusu nini, kwa sababu sikuwa nimepewa taarifa kabla. Alitaka nisaini kwa lazima hati hiyo. Alikasirika sana hadi akaanza kunitukana.

Walikuwa wanaenda kunipa dawa ya ganzi na daktari akaniuliza kwa nini nilikuwa nalia. Kisha nikamwambia kuwa mimba hiyo ni matokeo ya kubakwa. Aliniambia: “Tulia na kunipapasa kichwa changu.”

“Baada ya hapo, mtoto wa kike alipozaliwa, muuguzi mmoja aliniambia nimbusu. Nikakataa. Nikamwambia sitaki kumuona, na kwamba amuondoe machoni pangu.”

Kisha wakanihamisha kwenye chumba cha kupona. Wakati ulifika ambapo msichana alipaswa kunyonyeshwa.

Walimleta tena kwangu na kumlaza kwenye kitanda changu ili nimnyonyeshe. Alilia na kulia kwa sababu alikuwa na njaa na sikutaka kumnyonyesha.

Muuguzi alinifokea, na kuniuliza mimi ni mama wa aina gani!, yaani ni mnyama kiasi gani kwa kutotaka kumnyonyesha binti yangu.

“Hawakunikubalia njia mbadala ya kumnyonyesha kwa chupa wakati na mimi naendelea kufikiria kilichokuwa kikitokea.”

Nilikaa hospitalini kwa siku mbili, kisha nikaruhusiwa kurudi nyumbani. Sikurudi kwa jamii yangu kwa sababu tuliondoka nyumbani nikiwa na ujauzito.

Tulihamishwa na vitisho vya kuuawa kutoka kwa wabakaji. Waliniambia kwamba wangeniua, wangeua watoto wangu na familia yangu.

Pia, nyumba yetu iliporwa na kuharibiwa. Na hatukurejea tena huko.

Ubakaji huo ulitokea Novemba 13, 2015. Wabakaji hao walikamatwa mwaka wa 2017 na kupelekwa gerezani kwa miezi 4, na kuachiliwa huru.

Mnamo Juni 2022, kibali cha kuwakamata tena kilitolewa.

Tangu Desemba 2023, mbakaji anatumikia kifungo cha miaka 14 na mshirika wake anatumikia kifungo cha miaka 9.

Hata hivyo, mashirika yanayomwakilisha Fausia yanahofia kwamba upande unaotetea wabakaji hao utakata rufaa siku zijazo ambayo inaweza kubatilisha hukumu hiyo na wakaachiliwa huru.

Miaka minane imepita. Matarajio yangu baada ya niliyopitia, ni serikali kufikiria upya sheria za nchi hii juu ya utoaji wa mimba.

Tunaendelea kuishi katika jamii ambayo imetawaliwa na mfumo dume, utoaji mimba ni mwiko, dunia ambayo dini inawaambia watu kwamba kutoa mimba ni dhambi, ukifanya hivyo unabadilika na kuwa muuaji, kwamba huwezi kupata msamaha wa Mungu.

Natumai mambo yatabadilika kwa sababu niliyopitia yanaweza kutokea kwa mwanamke mwingine yeyote wa Honduras.

Imetafsiriwa na Asha Juma.

Via:BBC

Wiki chache zilipita na nilipoenda kwa daktari aliniambia nina ujauzito
0 Comment

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yakeAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake.

Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu)

Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?

Ugonjwa wa Pink eye ni ugonjwa wa macho pia ingawa ni nadra sana kutokea, ila wapo baadhi ya watu hupatwa na Ugonjwa huu.

Ugonjwa wa Pink eye,huweza kusababisha macho kuwa ya Pink, kuwasha,kuuma,kuhisi hali ya kuungua,kutoa uchafu au kuvimba ndani na kuzunguka jicho au macho.

Ingawa ni nadra sana kutokea ugonjwa huu, ila upo na wapo baadhi ya watu hupata.

Mtu mwenye Pink eye hupata tatizo la Conjunctivitis, au kuvimba kwa conjunctiva —

Pink eye huweza kuambukizwa na mara nyingi huhusishwa na watoto, lakini mtu yeyote anaweza kupata. Matibabu itategemea ikiwa maambukizi kwenye jicho lako yanatokana na virusi, bakteria, mizio, au vitu vya kuwasha jicho.

Pia Ugonjwa wa Pink eye husababisha wekundu kwenye macho, kuwasha, maumivu, kuchoma, kutokwa na uchafu na uvimbe ndani na karibu na macho. Kusababisha tatizo la kuona marue rue, ukungu na kukufanya uhisi mwanga zaisi, lakini bado utaweza kuona.

Pink eye inaweza kutokea kwa mtu yeyote, bila kujali umri, lakini ni kawaida Zaidi kwa watoto. Inaweza kuambukiza sana, kuenea kwa haraka katika shule na vituo vya kulelea watoto wachanga, lakini ugonjwa huu ni mara chache sana kutokea.

Ugonjwa huu Hauwezi kuharibu uwezo wako wa kuona, hasa ikiwa utapata matibabu kwa haraka. Unapotunza, kuzuia kuenea kwake na kufanya kila kitu ambacho daktari wako anapendekeza, jicho la pink husafishwa bila matatizo ya muda mrefu.

Chanzo cha Pink Eye

Je unawezaje kupata Pink Eye?

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu ambazo huongeza hatari ya wewe kupata Ugonjwa wa pink Eye;

1. Maambukizi ya Viruses

2. Maambukizi ya Bacteria

3. Tatizo la Mzio au Allergies dhidi ya vitu mbali mbali kama vile; vumbi,moshi, pollen, n.k

Irritants zingine ni kama vile shampoos, uchafu, moshi na klorini ya bwawa

4. Reactions kwenye baadhi ya dawa za macho yaani eye drops

5. Reactions baada ya kuvaa miwani au contact lens

6. Maambukizi ya Fangasi, amoebas, au parasites.

Ugonjwa huu wa Pink Eyes wakati fulani hutokana na magonjwa ya Zinaa(STDs). Ugonjwa kama Kisonono unaweza kuleta aina hatari ya bakteria ambayo huweza kushambulia macho na kusababisha tatizo la conjunctivitis.

Na Unaweza kusababisha kupotea kwa uwezo wa kuona ikiwa hautatibu. Klamidia inaweza kusababisha conjunctivitis kwa watu wazima. Ikiwa una chlamydia, kisonono, au maambukizi ya bakteria wengine katika mwili wako unapojifungua, unaweza kupitisha tatizo la jicho la pinki(Pink Eye) kwa mtoto wako kupitia njia ya kujifungua(Ukeni).

Pink eye, inayosababishwa na baadhi ya bakteria na virusi, inaweza kuenea haraka kutoka kwa mtu hadi mtu. Lakini sio hatari kubwa kiafya ikiwa itagunduliwa mara moja. Hata hivyo, ikiwa hutokea kwa mtoto mchanga, mwambie daktari mara moja, kwani inaweza kuwa maambukizi ambayo yanaweza kuathiri macho ya mtoto.

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake
0 Comment

MVUA kubwa kwenye Mikoa 16 Tanzania bara,chukua tahadhariAfyaclass Bongo Social •

MVUA kubwa kwenye Mikoa 16 Tanzania bara,chukua tahadhari.

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simivu. Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema baadhi ya maeneo katika mikoa 16 ya Tanzania bara na visiwa na Unguja na Pemba zitashuhudia mvua kubwa leo Ijumaa, Aprili 26, 2024.

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simivu, Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 26, 2024 na TMA huku ikiweka angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili.

Upepo huo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya  Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba).

“Athari zinazoweza kujitokeza, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,” imeelezwa na TMA.

Kwa siku zilizobaki kuanzia Aprili 27 hadi Aprili 30, TMA imetoa tahadhari ya ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mita mbili.

Upepo huo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) na ukanda wa ziwa Nyasa (Mikoa ya Songwe, Njombe na Ruvuma).

Aprili 28, 2024, TMA imesema kutakuwa na upepo mkali unaoziDi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.

“Tahadhari hiyo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikon ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) na ukanda wa ziwa Nyasa (Mikoa ya Songwe, Njombe na Ruvuma,” imeandikwa.

Aprili 29, TMA imesema upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayouzidi mita mbili itakumba baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aprili 30, Upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili pia itashuhudiwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

MVUA kubwa kwenye Mikoa 16 Tanzania bara,chukua tahadhari
0 Comment

Afrika hujumuisha asilimia 95 ya wagonjwa wa malaria duniani;WHOAfyaclass Bongo Social •

Nchi zinazokabiliwa Zaidi na Vifo na milipuko ya ugonjwa wa Malaria kama vile Uganda, zimefaulu angalau kwa kiwango fulani.

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria Tarehe 22.04.2024.

juhudi za mataifa yanayokumbwa zaidi na vifo na milipuko ya ugonjwa huo kama vile Uganda, zimefaulu angalau kwa kiwango fulani.

Uganda ambayo iko katika nafasi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na idadi ya wagonjwa na vifo imewekeza katika mbinu kadhaa kupambana na ugonjwa huo.

Ila baadhi ya jamii bado wanakwamisha juhudi hizo kwa kutumia vibaya vifaa wanavyopewa. Kwa mfano baadhi ya watu hutumia vyandarua vya mbu kuvulia samaki au kuvigeuza kuwa uzio dhidi ya ndege wanaoharibu mashamba yao.

Afrika hujumuisha asilimia 95 ya wagonjwa wa malaria duniani. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO mataifa 10 barani Afrika na nchi ya India ndiyo yalio na idadi kubwa ya vifo na visa vya wagonjwa wa homa ya malaria.

Uganda inashikilia nafasi ya tatu barani Afrika ikiifuata Nigeria. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndiyo inaongoza. Waziri wa Afya dokta Jane Ruth Aceng anathibitisha hali hiyo huku akielezea kuwa vita dhidi ya malaria vinatakiwa kumuhusisha kila mtu katika jamii.

”Hii ina maana kuwa tatizo la malaria Uganda ni la kiwango cha juu, kwa hiyo hata idadi ya vifo ni ya juu. Ndiyo sababu sisi kama Uganda tunatakiwa kushirikiana kama jamii kupambana na tatizo hili la malaria.”

Ijapokuwa idadi ya wagonjwa wa malaria nchini Uganda imeshuka kutoka asilimia 42 ya idadi ya watu mwaka 2009 hadi chini ya aslimia 9 kwa sasa, takwimu za wizara zinaonyesha kuwa  watu 16 hufariki kila siku nchini humo kutokana na ugonjwa huo unaoambukizwa na mbu.

Wizara ya afya ikishirikiana na mashirika mbalimbali ya kimataifa imeendesha shughuli kadhaa za kukabiliana na ugonjwa huo na angalau juhudi hizi zimezaa matunda, kama anavyofafanua zaidi Dokta Jimmy Opigo, kamishna msaidizi anayesimamia shughuli za kukabiliana na homa ya malaria kama alivyozungumza na DW.

”Nchini Uganda kila familia ina chandarua cha mbu, familia pia hujigharamia kupambana na malaria kwa kununua dawa za kupuliza au kujipaka. Tuna viwanda vya vyandarua, vya dawa za malaria na pia vile vinavyotengeneza vifaa vya kupima malaria.”

Hata hivyo, baadhi ya watu hasa kwenye maeneo ya maziwa na mito hutumia vyandarua vya mbu kama nyavu za kuvulia samaki au kuvigeuza uzio dhidi ya ndege wanaoharibu mashamba yao. Dokta Daniel Kyabayinze ni mkurugenzi wa afya ya umma katika wizara hiyo.

”Tunapaswa kuwaambia watu watumie vyandarua kwa njia iliyokusudiwa. Malaria inaweza kuwaua na pesa wanazochuma kwa kutumia vibaya vyandarua hazitayaokoa maisha yao.”

Shirika la WHO linaeleza kuwa duniani, kila dakika moja mtoto mmoja mwenye umri wa chini ya miaka mitano hufariki kutokana na homa ya malaria. Idadi kubwa ya vifo hivyo ni barani Afrika. Katika wiki chache zijazo Uganda itatoa chanjo dhidi ya malaria kwa watoto ikijiunga na mataifa mengine ya Afrika yaliyotangulia kama vile Kenya mwaka 2019. Lakini waziri wa afya Jane Ruth Aceng anatahadharisha kuwa chanjo hiyo haitoi kinga kwa watoto wote wanaoipata.

”Kwa watoto, chanjo hiyo ina kinga ya asilimia 50 tu. Kwa hiyo siyo suluhisho lenye uhakika, suluhisho la uhakika tunalotegemea ni kuzidisha juhudi za kijamii.”

Uganda pia inazingatia kurejelea mpango wa kunyunyiza viwatilifu vya kuangamiza mbu hata kama itakuwa DDT ambayo mataifa ya Ulaya yalitumia kuangamiza malaria.Kamerun yazindua kampeni ya kihistoria ya chanjo ya Malaria Jitihadi za awali za kutumia mbinu hiyo zilipingwa na wanasiasa. Waziri Aceng anadai kuwa wanasiasa hao walichochewa na makampuni yanayouza dawa za kutibu malaria yakihofia kuwa yangepoteza soko la dawa zao.

Afrika hujumuisha asilimia 95 ya wagonjwa wa malaria duniani;WHO
0 Comment

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti kuwa "hayuko sawa" anapopambana na sarataniAfyaclass Bongo Social •

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti kuwa “hayuko sawa” anapopambana na saratani.

Afya ya Mfalme Charles III inasababisha wasiwasi kwa marafiki na ikulu wakati anaendelea kupambana na ugonjwa wa saratani unaomsumbua.

“Tukizungumza na marafiki wa mfalme katika wiki za hivi karibuni kuhusu afya yake, jibu la kawaida ni … ‘Si Nzuri,’” Tom Sykes wa gazeti la Daily Beast aliripoti Alhamisi, Aprili 25.

Rafiki wa mfalme alidai Charles ” kweli hayuko sawa.

Mwandishi wa kifalme Tina Brown pia alidokeza juu ya shida za kiafya za mfalme, akiandika hivi karibuni kwamba saratani ya Charles imewaweka Prince William na Kate Middleton “katika ukaribu wa kutisha wa kupanda kiti cha enzi.

“Matarajio yake, naambiwa, yanawaletea wasiwasi mkubwa.”

Sykes pia aliripoti kwamba mipango ya mazishi ya mfalme, iliyopewa jina la “Operesheni Menai Bridge”, kwa sasa inapitiwa upya.

Hati tofauti ambayo inaelezea kile kilichoenda vizuri katika mazishi ya Malkia Elizabeth Septemba 2022 na kile kinachoweza kufanywa vizuri wakati mfalme mwingine akifa pia inazunguka, kulingana na Daily Beast.

Vyanzo vyote vilisisitiza kuwa mipango ya mazishi ya kifalme inakaguliwa kila wakati. Walakini, mfanyakazi mmoja wa zamani alikubali kwamba shida za kiafya za Charles zimesababisha mipango ya mazishi yake kuwa haraka Zaidi.

“Mipango imefutwa na inaangaliwa kikamilifu,” mfanyakazi huyo wa zamani alielezea.

“Siyo zaidi ya vile unavyotarajia kutokana na kwamba mfalme amegunduliwa na saratani. Lakini mzunguko wao hakika umeelekeza akili.”

Buckingham Palace ilitangaza mnamo Februari kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongezeka kwa tezi dume(benign prostate enlargement) iligunduliwa kuwa mfalme huyo ana saratani.

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti
kuwa "hayuko sawa" anapopambana na saratani
0 Comment

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti kuwa "hayuko sawa" anapopambana na sarataniAfyaclass Bongo Social •

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti kuwa “hayuko sawa” anapopambana na saratani.

Afya ya Mfalme Charles III inasababisha wasiwasi kwa marafiki na ikulu wakati anaendelea kupambana na ugonjwa wa saratani unaomsumbua.

“Tukizungumza na marafiki wa mfalme katika wiki za hivi karibuni kuhusu afya yake, jibu la kawaida ni … ‘Si Nzuri,'” Tom Sykes wa gazeti la Daily Beast aliripoti Alhamisi, Aprili 25.

Rafiki wa mfalme alidai Charles ” kweli hayuko sawa.

Mwandishi wa kifalme Tina Brown pia alidokeza juu ya shida za kiafya za mfalme, akiandika hivi karibuni kwamba saratani ya Charles imewaweka Prince William na Kate Middleton “katika ukaribu wa kutisha wa kupanda kiti cha enzi.

“Matarajio yake, naambiwa, yanawaletea wasiwasi mkubwa.”

Sykes pia aliripoti kwamba mipango ya mazishi ya mfalme, iliyopewa jina la “Operesheni Menai Bridge”, kwa sasa inapitiwa upya.

Hati tofauti ambayo inaelezea kile kilichoenda vizuri katika mazishi ya Malkia Elizabeth Septemba 2022 na kile kinachoweza kufanywa vizuri wakati mfalme mwingine akifa pia inazunguka, kulingana na Daily Beast.

Vyanzo vyote vilisisitiza kuwa mipango ya mazishi ya kifalme inakaguliwa kila wakati. Walakini, mfanyakazi mmoja wa zamani alikubali kwamba shida za kiafya za Charles zimesababisha mipango ya mazishi yake kuwa haraka Zaidi.

“Mipango imefutwa na inaangaliwa kikamilifu,” mfanyakazi huyo wa zamani alielezea.

“Siyo zaidi ya vile unavyotarajia kutokana na kwamba mfalme amegunduliwa na saratani. Lakini mzunguko wao hakika umeelekeza akili.”

Buckingham Palace ilitangaza mnamo Februari kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongezeka kwa tezi dume(benign prostate enlargement) iligunduliwa kuwa mfalme huyo ana saratani.

Mipango ya mazishi ya Mfalme Charles yaharakishwa kufuatia ripoti
kuwa "hayuko sawa" anapopambana na saratani
0 Comment

Mtoto aliyeokolewa kutoka tumboni mwa mamake afarikiAfyaclass Bongo Social •

Mtoto aliyeokolewa kutoka tumboni mwa mamake aliyeuawa Gaza Afariki.

Mtoto aliyeokolewa kutoka tumboni mwa mamake aliyekuwa mahututi baada ya shambulizi la anga la Israel kusini mwa Gaza amefariki, BBC imebaini.

Mtoto Sabreen al-Sakani alizaliwa kupitia upasuaji katika hospitali ya Rafah muda mfupi baada ya saa sita usiku Jumapili.

Hata hivyo alifariki siku ya Alhamisi na amezikwa karibu na mama yake.

Mtoto Sabreen alikuwa miongoni mwa watoto 16 waliouawa katika mashambulizi mawili ya anga huko Rafah wikendi iliyopita.

Wote waliuawa katika shambulio la bomu lililolenga nyumba walimokuwa wakiishi.

Mtoto aliyeokolewa kutoka tumboni mwa mamake afariki
0 Comment

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya kuongeza UsuguAfyaclass Bongo Social •

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya kuongeza Usugu.

Ushahidi mpya uliotolewa na shirika la afya ulimwenguni, WHO unaonesha kuwa wakati wa janga la COVID-19 kulikuweko na matumizi yasiyo ya lazima na ya kupita kiasi ya viuavijasum au antibiotics ambayo huenda yamesababisha kusambaa kwa usugu wa viuavijiumbe maradhi au Antimicrobials.

Taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na WHO inasema ingawa ni asilimia 8 tu ya wagonjwa waliolazwa kwa ajili ya COVID-19 ndio walikuwa na maambukizi yatokanayo na bakteria au vimelea na hivyo kuhitaji viuavijasumu, takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa watatu kati ya wanne sawa na asilimia 75 ya wagonjwa walitibiwa kwa viujavijasumu pengine tu ingaliweza kuwasaidia hata kama haikuwa inahitajika.

Wagonjwa wasio mahututi Afrika walipatiwa viuavijasumu

Matumizi ya viuavijasumu yalikuwa ni kuanzia asilimia 33 kwa wagonjwa ukanda wa Pasifiki Magharibi hadi asilimia 83 ukanda wa Mediteranea Mashariki na Afrika.

Kati ya mwaka 2020 hadi 2022 kitendo cha daktari kuandikia dawa aina ya viuavijasumu kwa wagonjwa kilipungua huko Ulaya na Amerika, ilhali kiliongeza katika nchi za Afrika.

Kwa wastani kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa hizo miongoni mwa wagonjwa wa COVID-19 waliokuwa mahututi kilifikia asilimia 81.

Ingawa hivyo kulikuwa na utofauti mkubwa wa utoaji wa dawa hizo kwa wagonjwa ambao hawakuwa mahututi lakini ukanda wa Afrika uliongoza kwa kupatiwa wagonjwa wa kiwango hicho kwa asilimia 79.

Matumizi holela ya viuavijasumu huweza kusababisha usugu wa dawa

“Pindi mgonjwa anapohitaji viuavijasumu, manufaa yake yanazidi hatari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo au hatari za kuleta usugu hapo baadaye,” ameesma Daktari Silvia Bertagnolio, Mkuu wa kitengo cha Ufuatiliaji, Ushahidi na uimarishaji wa Maabara WHO.

Amesema “hata hivyo pindi viuavijasumu vinapotumika pale isipo lazima, hazina faida yoyote zaidi ya kuongeza hatari na matumzi yake yanaweza kusababisha kuibuka au kusambaa kwa usugu wa dawa hizo kwa vijiumbe maradhi, au microbes.”

Daktari Bertagnolio  amesema takwimu hizi mpya zinataka sasa kuimarisha matumizi sahihi ya viuavijasumu na kupunguza madhara yasiyo ya lazima kwa wagonjwa na jamii.

Kwa ujumla matumizi ya viuavijasumu hayakuimarisha tiba ya wagonjwa wa COVID-19. Badala yake, inaweza kuwa iliongeza hatari kwa watu ambao hawakuwa na maambukizi ya bakteria au vimelea ikilinganishwa na wale ambao hawakupatiwa dawa hizo wakati wanaugua COVID-19.

Utafiti huu kuchangia kwenye mapendekezo yajayo

Uchambuzi zaidi utafanyika wa takwimu hizi mpya ili ziweze kujumuishwa kwenye mapendekezo yajayo ya matumizi ya viujavijasumu kwa wagonjwa wa COVID-19, kama sehemu ya mwongozo wa tiba dhidi ya ugonjwa huo. Mkutano utafanyika Hispania mwezi ujao.

Na baadaye mwezi Septemba mwaka huu, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litakuwa na kikao cha viongozi kukubaliana hatua za kupunguza usugu wa viuavijiumbe maradhi kwa ajili ya afya ya binadamu, Wanyama, na sekta ya kilimo pamoja na mazingira, halikadhalika kusongesha uongozi na ufadhili wa fedha ili kupunguza usugu wa dawa hizo au AMR.

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya
kuongeza Usugu
0 Comment

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Omeprazole inatibu ugonjwa gani

Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi wa @afyaclass, Leo tumeamua kuichambua dawa hii kazi zake kwa faida ya wengi.

Dawa ya Omeprazole:

Omeprazole ni dawa inayotumika kutibu hali kadhaa ambazo huhusiana na Ongezeko la kiwango kikubwa cha Acid tumboni.

Dawa hii huweza kutumika kutibu matatizo kama vile;

GERD; ni tatizo linalohusu acid kurudi kutoka tumboni kwenda kwenye umio au esophagus(acid reflux).

#Soma Zaidi hapa; Tatizo la gastroesophageal reflux disease (GERD).

Pia wakati mwingine omeprazole hutumika ikiwa pamoja na dawa zingine jamii ya antibiotics (mfano, amoxicillin, clarithromycin) kutibu vidonda vya tumbo vinavyotokana na maambukizi ya bacteria aina ya H. pylori bacteria.”

Omeprazole huweza kutumika kutibu tatizo la Zollinger-Ellison syndrome, hali ambayo Tumbo huzalisha kiwango kikubwa sana cha acid.

Pia Omeprazole ni nzuri kwa matibabu ya shida ya dyspepsia, hali inayosababisha tumbo kuwa chungu, kupata kiungulia mara kwa mara, au chakula kutosagwa vizuri.

Usichokifahamu kuhusu dawa ya omeprazole, ni kwamba dawa hii huweza kutumika kuzuia tatizo la kuvuja damu yaani upper gastrointestinal tract bleeding kwa wagonjwa wenye hali mbaya sana.

Ijue Dawa ya Omeprazole:

Omeprazole ni dawa jamii ya proton pump inhibitor (PPI),  inafanya kazi kwa kupunguza kiwango cha Acid kinachozalishwa na Tumbo.

Dawa hii inaweza kutolewa kwa cheti cha daktari au bila cheti cha daktari(This medicine is available both over-the-counter (OTC) and with your doctor’s prescription).

Dawa ya Omeprazole inapatikana kwa forms hizi:

  • Powder for Suspension
  • Tablets
  • Capsules
  • Au Packet

Haya ndyo Maelezo mafupi kuhusu dawa hii jamii ya Omeprazole….

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa
0 Comment

Kuongeza Nguvu Katika Mapambano Dhidi ya MalariaAfyaclass Bongo Social •

LEO ni Siku ya Malaria Duniani ambayo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu ilipoanzishwa na nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2007 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya.

Lengo la kuadhimisha siku hii ni kuweka msisitizo katika mapambano ya ugonjwa huu hatari ambao umegharimu mamilioni ya watu duniani. Mapambano hayo dhidi ya malaria ni kuonyesha umuhimu wa uwekezaji endelevu na utashi wa kisiasa katika kukinga na kudhibiti malaria.

Kaulimbuiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ni “Kuongeza Nguvu Katika Mapambano Dhidi ya Malaria” ikisisitiza jitihada za pamoja kwa mataifa yote duniani katika kuzuia, kupambana na kutokomeza malaria. Kwa Tanzania, maadhimisho yatafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, Tabora na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Wakati maadhimisho hayo yanafanyika pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kwa serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi, takwimu zinaonyesha kuwa bado ni hatari hasa kwa watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano pamoja na wajawazito.  Aidha, nchi za Afrika ikiwamo Tanzania, kwa mujibu wa takwimu, ndizo zinazoathirika zaidi na malaria hivyo jitihada zaidi zinatakiwa katika kupambana na kutokomeza maradhi haya.

Tamwinu za WHO zinabainisha kwamba mwaka 2022, kulikuwa na vifo 608 000 vilivyotokana na malaria na maambukizi mapya ya ugonjwa huo yalikuwa milioni 249. Asilimia 94 ya vifo na maambukizi hayo ilikuwa katika bara la Afrika na kwa mantiki hiyo, jitihada zaidi zinapaswa kufanywa kwa Afrika katika mapambano dhidi ya malaria.

Kutokana na ukweli huo, nchi za Afrika kupitia jumuia za kikanda kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Uchumi kwa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika (AU) zinapaswa kuweka moja ya ajenda za kipaumbele kwenye mikutano yao.

Nchi hizo, ambazo ndizo waathirika wakubwa wa malaria, kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo na mashirika ya kimataifa zinapaswa pia kuweka mikakati thabiti katika kupambana na malaria ili kunusuru nguvu kazi na kuzifanya nchi ziwe na ustawi.

Kuna kampeni mbalimbali na mikakati ambayo imefanyika katika kupambana na malaria katika ngazi mbalimbali lakini bado tatizo ni kubwa, hivyo inahitajika mikakati zaidi katika vita hivyo. Ili kufanikisha hilo, mapambano yanapaswa kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa na si kuachia wataalamu pekee.

Katika kufanya hivyo, kila Mtanzania anapaswa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya yakiwamo kuteketeza mazalia ya mbu katika maeneo ya makazi, kutumia chandarua chenye dawa, kuwakinga watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano pamoja na wajawazito ambao ndio walio katika hatari zaidi ya kupatwa na ugonjwa huo.

Aidha, imekuwa ikisisitizwa kuwa mtu anapoona dalili za malaria, hana budi kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya vipimo na atakapobainika apatiwe matibabu stahiki.

Licha ya maelekezo hayo, idadi kubwa ya Watanzania hawazingatii ndiyo maana ugonjwa huo umekuwa ukizidi kugharimu maisha ya watu huku taifa likiendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kinga na tiba.

Ni dhahiri kwamba iwapo kila mtu atazingatia maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na malaria, kutakuwa na mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo na hatimaye kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi wala vifo vitokanavyo na malaria.

Shime kila Mtanzania asimame katika nafasi yake huku akisema Tanzania, Afrika na dunia bila malaria inawezekana. Hapo ndipo ushindi dhidi ya maradhi haya utakapopatikana na hatimaye maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi kuonekana.

Kuongeza Nguvu Katika Mapambano Dhidi ya Malaria
0 Comment

Bibi apandikizwa figo ya nguruwe pamoja na moyo wa bandiaAfyaclass Bongo Social •

Bibi apandikizwa figo ya nguruwe pamoja na moyo wa bandia

Bibi mmoja mwenye umri wa miaka 54 amefaulu kupokea upandikizaji wa kwanza wa pamoja wa figo ya nguruwe na pampu ya moyo.

Lisa Pisano, mzaliwa wa New Jersey aliye na ugonjwa wa figo ukiwa katika hatua za mwishoni, pamoja na tatizo la kushindwa kwa moyo kufanya kazi(Heart failure),

alikaa kwa muda pasipo upandikizaji wa moyo na figo kutokana na uhaba wa michango ya viungo vya binadamu na hali sugu za kiafya ambazo zilipunguza uwezekano wake wa kupata matokeo mazuri.

Alisema: “Ninachotaka ni fursa ya kuwa na maisha bora.

“Baada ya kutengwa kwa ajili ya upandikizaji huo nilijifunza sikuwa na muda mwingi uliobaki.

“Madaktari wangu walidhani kunaweza kuwa na nafasi ya kuidhinishwa kupokea figo ya nguruwe iliyohaririwa na jeni, kwa hivyo niliijadili na familia yangu na mume wangu. Amekuwa upande wangu katika kipindi chote cha majaribu haya na anataka niwe bora zaidi.”

Madaktari wa upasuaji wa Afya wa NYU Langone walifanya utaratibu wa ubunifu wa hatua mbili mapema mwezi huu huko New York. Mnamo Aprili 4, walipandikiza kwa upasuaji pampu ya moyo inayoitwa kifaa cha usaidizi cha ventrikali ya kushoto (LVAD) kwenye Pisano.

Kisha Aprili 12, walimfanyia upasuaji wa kupandikiza figo ya nguruwe iliyohaririwa na jeni, ambayo Ilijumuisha tezi ya nguruwe ili kusaidia dhidi ya mwili wake kukataa kiungo cha wanyama.

Bibi apandikizwa figo ya nguruwe pamoja na moyo wa bandia
0 Comment

Umri wa mtoto kuota meno pamoja na dalili zake,fahamu Zaidi hapaAfyaclass Bongo Social •

Umri wa mtoto kuota meno pamoja na dalili zake,fahamu Zaidi hapa

Umri wa kuota meno ya kwanza kwa mtoto

Muda wa kuota meno kwa watoto hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine, baadhi ya watoto huzaliwa na meno ya awali na wengine huota meno baada ya miezi 4 hadi mwaka. Hata hivyo tegemea mwanao kupata meno akiwa ndani ya mwaka wake wa kwanza toka amezaliwa. Tafiti zinaonyesha watoto wengi huota meno yao ya kwanza wakiwa na miezi sita. Dalili zifuatazo zinaweza kuwa ishara ya mtoto kuota meno ya kwanza.

Dalili za meno kuota kwa mtoto

Maumivu ya fizi na kubadilika rangi (kuwa na rangi nyekundu wakati meno yanataka kutoka nje)

Shavu moja la mtoto hubadilika rangi

Mtoto huchokonoa masikio(kwa sababu ya miwasho au maumivu)

Kutoa udenda zaidi ya kawaida

Hupenda kutafuna na kusugua fizi zaidi ya kawaida

Mtoto kulialia na kusumbua isivyo kawaida

Kuweka mikono kinywani na kuinyonya

Kung’ata ziwa la mama anapokuwa ananyonya

Kupata homa kiasi

Kuharisha(hii ni baadhi ya dalili ambayo huripotiwa na wazazi)

Pitia makala ya dalili zinazoambatana na kuota meno kwa maelezo zaidi.

Kumbuka endapo mtoto akipata homa halisi yaani joto la mwili kupanda kiasi cha nyuzi joto za centigredi 38, wasiliana na daktari kwa sababu kuota meno huwa hakusababishi kupata hivi kwa joto.

Kwa sababu watoto wengi huota meno kwenye umri wa kuanzia miezi sita, ni vema mzazi ukawa na tabia ya kusafisha meno hayo, tumia mswaki wa watoto kusafisha meno ya mtoto kwa kutumia dawa ya meno yenye fluoride mara mbili kwa siku ili kuimarisha meno yake. Hakikisha mtoto hamezi dawa.

Pia katika kipindi hiki msaidie mtoto kuondoa maumivu ya jino kwa kutumia panado kulingana na dozi uliyoelekezwa na daktari wako. Kanda sehemu jino linapoota ili kuondoa maumivu na kumtuliza mtoto. Tumia vifaa maalumu pia kumwekea kinywani ili mtoto apate kung’ata na kujisikia vema dhidi ya miwasho ya meno kuota. Kuwa makini hata hivyo mtoto asimeze au kupaliwa.

Meno huota kwa mpangilio upi?

Maelezo ya hapa chini yameelezea wastani wa umri wa kuota meno kwa watoto walio wengi, hii ndio maana kuna utofauti wa maelezo haya na picha hapo juu. Ili kufahamu meno yanayozungumziwa ni yapi, tazama picha juu kufananisha.

Meno ya insiza ya chini kwanza

Huanza kuota kwenye umri wa miezi 5 hadi 7

Meno ya insiza ya juu

Huanza kuota kuanzia miezi 6 hadi 8

Meno ya insiza ya pembeni juu

Huanza kuota kuanzia miezi 9 hadi 11

Meno ya insiza ya pembeni chini ya taya

Huanza kuota kuanzia miezi 10 hadi 12

Meno ya kwanza ya mola

Huanza kuota kuanzia miezi 12 hadi 16

Meno ya kanaini

Huanza kuota kati ya miezi 16 hadi 20

Meno ya pili ya mola

Huanza kuota miezi 20 hadi 30

Kwa maelezo zaidi pitia picha hapo juu.

Ni umri gani meno yote ya kwanza huwa yameota?

Watoto wengi huwa wameshaota meno yao yote ya awali mpaka wanapfikia umri wa miaka 2 na nusu

Soma zaidi kuhusu makala zingine kwa kubofya makala zingine zinazohusu:

Chanjo kwa mtoto

Hatua za ukuaji wa mtoto

Namna ya kumfanya mtoto ale chakula zaidi

Namna ya kuandaa lishe ya mtoto

Namna ya kunyonyesha mtoto

Wakati gani maziwa ya mama huanzakutoka baada ya kujifungua?

Utapiamlo

Uandaaji wa lishe ya mtoto

Ukuaji wa mtoto wa kawaida(uzito na urefu

Maendeleo ya mtoto Mwaka 1 hadi 2

Maendeleo ya mtoto Miaka 2 hadi 3

Maendeleo ya mtoto Miaka 3 hadi 5

Umri wa mtoto kuota meno pamoja na dalili zake,fahamu Zaidi hapa
0 Comment

Mloganzila kuanzisha huduma ya upandikizaji wa iniAfyaclass Bongo Social •

Mloganzila kuanzisha huduma ya upandikizaji wa ini

Daktari Bingwa Bobezi wa upasuaji ambaye pia amebobea katika masuala ya upandikizaji wa ini kutoka Hospitali za HGC, Dkt. Basant Mahadevappa

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila itaendelea kujikita katika kuanzisha huduma mpya za ubingwa bobezi hapa nchini ili kuwapunguzia wananchi gharama na usumbufu wa kutafuta huduma hizo nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji, Dkt. Godlove Mfuko alipokuwa akiongea katika kongamano la kitaalam liliondaliwa kwa ushirikiano wa MNH-Mlogazila na Hospitali za HCG za nchini India kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalam kuhusu upasuaji wa upandikizaji wa ini.

Dkt. Mfuko ameongeza kuwa kutokana uwekezaji uliofanywa na Serikali nchini ambao umeleta mapinduzi makubwa katika kutoa huduma za afya, hivyo ni wajibu wa Mloganzila kutoa huduma ambazo hazipatikani nchini na kuimarisha huduma zilizopo kwa kuendelea kuwajengea uwezo wataalam.

“Baada ya uwekezaji uliofanywa na Serikali, sisi kama wataalam kazi yetu ni kujituma na kufikiri kwa namna gani Hospitali ya Taifa inachangia kuanzisha huduma za ubingwa bobezi ikiwemo kupandikiza ini hapa nchini na inawezekana” ameongeza Dkt. Mfuko

Kwa upande wake Daktari Bingwa Bobezi wa upasuaji ambaye pia amebobea katika masuala ya upandikizaji wa ini kutoka Hospitali za HGC, Dkt. Basant Mahadevappa amesema huduma ya upasuaji wa upandikizaji wa ini unahitaji maandalizi muhimu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wa kada mbalimbali.

Huduma ya Upasuaji wa Upandikizaji wa ini inatolewa katika nchi mbili Afrika ambazo ni Misri na Afrika Kusini ambapo kama Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila itaanzisha huduma hii itakuwa  na manufaa kwa watanzania na nchi nyingine Afrika hivyo kuchochea utalii tiba nchini.

Mloganzila kuanzisha huduma ya upandikizaji wa ini
0 Comment

TMA yatoa taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewaAfyaclass Bongo Social •

TMA yatoa taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia Jumatano Aprili 24, 2024 saa 9.30 mchana.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia leo Jumatano Aprili 24, 2024 saa 9.30 mchana.

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Alhamisi Aprili 25, 2024

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Ijumaa Aprili 26, 2024

Mamlaka imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Arusha, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Tabora na Katavi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Jumamosi Aprili 27, 2024

Limetolewa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Jumapili Aprili 28, 2024

TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka imesema uwezekano wa hali hiyo kutokea ni wastani, sawa na kiwango cha athari zinazoweza kutokea.

TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

TMA yatoa taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewa
0 Comment

Mlipuko wa homa ya Nyani watokea tena, Chukua tahadhariAfyaclass Bongo Social •

Mlipuko wa homa ya Nyani watokea tena, Chukua tahadhari

Kufuatia uwepo wa taarifa za visa 19 vilivyothibitishwa katika miji mitano ikiwa ni pamoja na jiji la Brazzaville, Serikali ya Nchi ya Jamhuri ya Kongo imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nyani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Gilbert Mokoki amesema licha ya kutangazwa kwa ugonjwa huo bado hakuna vifo vilivyorekodiwa hadi kufikia sasa, huku akiutaka umma kuchukua tahadhari.

Amesema, watu wanatakiwa kutosogeleana na wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huo na kuepuka kukaribiana na wanyama au kushika nyama za wanyamapori, huku akisema dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa, maumivu na vidonda kwenye ngozi.

Homa ya Nyani, ni ugonjwa ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC mwaka 1970.

Chama afunguka wanayopitia Msimbazi

Tanzania kuwa na uhakika upatikanaji wa Petroli.

>>SOMA ZAIDI kuhusu ugonjwa wa homa ya nyani

Mlipuko wa homa ya Nyani watokea tena, Chukua tahadhari
0 Comment

Wiki ya Kimataifa ya Chanjo yaanza leo 24 hadi 30 ApriliAfyaclass Bongo Social •

Wiki ya Kimataifa ya Chanjo yaanza leo 24 hadi 30 Aprili

Wiki ya Kimataifa ya Chanjo ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.

Shirika la Afya Duniani, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.

Lengo kuu la Wiki ya Kimataifa ya Chanjo ni kwa watu zaidi na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.

WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.

Mwaka huu Wiki ya Kimataifa ya Chanjo inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani.

WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo.

Wiki ya Kimataifa ya Chanjo yaanza leo 24 hadi 30 Aprili
0 Comment

Watoto wa kike milioni 5 nchini Tanzania kupatiwa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi- WHOAfyaclass Bongo Social •

Watoto wa kike milioni 5 nchini Tanzania kupatiwa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi- WHO

#PICHA: Uzinduzi wa kampeni ya siku 5 ya kitaifa ya chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Tanzania uliambatana na wanawake na wanaume kubeba mabango yenye ujumbe kuhusu usalama wa chanjo hiyo.

Nchini Tanzania kampeni ya siku 5 ya chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, au Human Papilloma Virus, (HPV) imeingia siku ya tatu hii leo nchini kote ikilenga zaidi ya watoto wa kike milioni 5 wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 14.

Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni huko jijini Geneva, nchini Uswisi na Mwanza nchini Tanzania inasema kampeni hiyo inaendeshwa kwa ubia kati ya serikali ya Tanzania,  Ubia wa chanjo duniani, GAVI , mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na WHO.

Virusi vya HPV ni sababu kuu ya saratani ya shingo ya kizazi, kwingineko ikijulikana kama mlango wa kizazi au Cervical Cancer kwa lugha ya kiingereza na kampeni itamalizika tarehe 26 mwezi huu wa Aprili.

WHO inasema wakati saratani ya shingo ya kiazi inasalia kuwa moja ya sababu kuu ya vifo miongoni mwa wanawake nchini Tanzania, ambapo mwaka 2022 wagonjwa 6,800 kati ya 10,800 walifariki dunia, bado ugonjwa huo unazuilika kwa chanjo.

“Chanjo ya HPV ni salama na ina ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi,” inasema WHO, ikiongeza kuwa wakati wa kampeni, watoto wa kike wenye umri wa kupatiwa chanjo hiyo watakuwa na fursa ya kupatiwa dozi moja ya chanjo bila gharama yoyote.

Muuguzi nchini Tanzania akimpatia mtoto wa kike chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, au HPV wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 5 ya chanjo hiyo kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Utoaji wa chanjo ya HPV Tanzania umekuwa wa mafanikio

Shirika hilo linaongeza kuwa juhudi za kuongeza upatikanaji wa chanjo hiyo dhidi ya saratani nchini kote Tanzania zimekuwa na mafanikio makubwa.

Mwaka 2018, chanjo hiyo inayotolewa kwa dozi mbili, ilijumuishwa kwenye programu ya chanjo ya kitaifa kwa watoto wote wa kike wenye umri wa miaka 14, ikionesha azma ya serikali ya Tanzania ya kulinda afya na ustawi wa vizazi vijavyo.

Hali leo hii, kwa mujibu wa WHO, ufikiaji wa dozi ya kwanza ya HPV ni asilimia 79, na dozi ya pili asilimia 60.

Ni kwa kuzingatia hilo, WHO inasema juhudi za pamoja zinahitajika kuhakikisha kila mtoto wa kike Tanzania anapata kinga hiyo muhimu dhidi ya ugonjwa huo hatari lakini wenye kinga.

Maendeleo ya Tanzania katika kutoa chanjo ya HPV ni muhimu kama sehemu ya mpango wa kimataifa unaoungwa mkono na Ushirika wa Chanjo ambao umeazimia kutoa fedha zaidi na rasilimali ili kuhakikisha watoto wa kike milioni 86 kote duniani wanakuwa wamepatiwa chanjo hiyo ifikapo mwaka 2025.

Watoto wa kike milioni 5 nchini Tanzania kupatiwa chanjo dhidi ya
saratani ya shingo ya kizazi- WHO
0 Comment

Madaktari waliokuwa wakiendelea na mgomo kusimamishwa kazi kenyaAfyaclass Bongo Social •

#Kenya: Chama cha madaktari na matabibu nchini Kenya, KMPDU kimesema kwamba “hakitalegeza msimamo wake” wala kuridhia kurejea kazini hadi pale hatima ya madaktari wanafunzi itakapojulikana.

Kufuatia kauli hizo, baraza la magavana linatishia kuwaachisha kazi madaktari wanaogoma kwani serikali za kaunti ndiye muajiri wao.

Mwenyekiti wa baraza la magavana, Anne Waiguru, alisisitiza kuwa daktari yeyote ambaye hatarejea kazini haraka iwezekanavyo atachukuliwa hatua za kisheria. Aidha ameongeza masuala waliyowasilisha madaktari yanaanza kufanyiwa kazi.

Madaktari waliokuwa wakiendelea na mgomo kusimamishwa kazi kenya
0 Comment

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa ganiAfyaclass Bongo Social •

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo sababu mbali mbali zinazosababisha tatizo hili ambazo tutazichambua hapa,

Sababu zingine ni za kawaida, na zingine zinahitaji matibabu ya haraka. Tatizo la mate kujaa mdomoni huweza kuwa la muda mfupi au la kudumu.

Chanzo cha tatizo la mate kujaa mdomoni

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za tatizo hili la mate kujaa mdomoni;

– Tatizo la Kuzalishwa kwa mate kupita kiasi Mdomoni, au kwa kitaalam Hypersalivation,

Tatizo hili pia hujulikana kama sialorrhea au ptyalism, Na huhusisha mdomo kuzalisha mate mengi sana kupita kawaida.

Kulingana na sababu, tatizo la hypersalivation linaweza kuwa la mara kwa mara au kwa vipindi. Linaweza pia kuwa la muda mrefu au sugu.

Kwa wastani, mtu mwenye afya njema hutoa kati ya lita 0.75 na 1.5 za mate kila siku. Uzalishaji wa mate huongezeka wakati mtu anakula na huwa chini kabisa wakati wa usingizi.

Mate yakiwa mengi yanaweza kusababisha matatizo ya kuzungumza na kula, pamoja na midomo kupasuka au chapped lips na maambukizi ya ngozi.

Tatizo hili pia linaweza kusababisha wasiwasi kwa mtu,kutokujiamini kwa watu na kupunguza Mtu kujithamini.

– Sababu Zingine ni pamoja na;

(1) Madhara ya kuvaa meno bandia

(2) Matatizo kwenye muundo wa meno au Mdomo

(3) Kushindwa kumeza mate vizuri,au kuondoa mate mdomoni

(4) Kushindwa kuweka mdomo wako ukiwa umefungwa

(5) Hali ya Ujauzito ambayo huweza kusababisha mate kuzalishwa zaidi mdomoni

(6) Kuwa na maambukizi kwenye eneo la mdomo,ulimi au kinywa kwa ujumla,

Maambukizi makali kama ya Kichaa cha mbwa(rabies) au ugonjwa wa TB(tuberculosis)

(7) Tatizo la false teeth

(8) Kuwa na vidonda au Uvimbe mdomoni

(9) kupata matatizo ya Taya, mfano; Taya kuvunjika,kuhama mahali pake n.k

Ukiwa unatatizo hili hakikisha unapata msaada wa matibabu mara moja

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani
0 Comment

Tupunguze matumizi ya pombe isiyozimuliwa ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukizaAfyaclass Bongo Social •

Tupunguze matumizi ya pombe isiyozimuliwa ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Na WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa iwapo jamii itapunguza matumizi ya pombe isiyo zimuliwa yaliyokithiri itasaidia kukabiliana na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.

Waziri Ummy amesema hayo Aprili 23, 2024 Jijini Dar Es Salaam wakati akifungua na kuhutubia Mkutano unaojadili namna ya kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza Barani Afrika, ambapo amesema kiwango cha Matumizi ya pombe kali nchini kimongezeka kutoka Lita 9.1 mpaka Lita 10 .4 kwa Mwaka.

“Tanzania tunaona ongezeko la unyaji Mkubwa wa pimbe wakati tumepunguza watu wanaokunywa pombe, tulikuwa na watu wanaokunywa pombe mwaka 2019 ilikuwa ni kama 26% tumeipunguza mpaka asilimia 20, lakini kiwango cha Pombe kimeongezeka kutoka lita 9.1 kwa mwaka mpaka 10.4 kwa mwaka, tuepuke unywaji wa pombe uliokithiri”

Ameongeza kuwa Tanzania kama Nchii nyingine za Afrika inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza.

“Tunaona ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza hususani shinikizo la juu la damu, kisukari, Saratani lakini pia Selimundu kama nchi tutaendela kuwekeza katika mikakati ya kinga na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata elimu na huduma dhidi ya magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza” amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema Serikali inaendelea na kutoa Chanjo ya kukinga dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

“Tunaweza tukatokomeza Saratani ya Mlango wa Kizazi kama tutawapa watoto wetu chanjo ya dhidi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya Kizazi (HPV) na inatolewa kwa mabinti ambao hawajaanza kujamiiana kwa sababu vile virusi vya HumanPapiloma vinatoka kwa mwanamke, kwahiyo tunaatoa kwa mabinti ya miaka 9 mpaka 14, tunaweza baada ya miaka 10 hadi 20 tukasahau kuhusu saratani ya Mlango wa Kizazi” amsema Waziri Ummy

Tupunguze matumizi ya pombe isiyozimuliwa ili kukabiliana na magonjwa
yasiyoambukiza
0 Comment

Beki wa Super Falcons, Plumptre afanyiwa upasuajiAfyaclass Bongo Social •

Beki wa Super Falcons, Plumptre afanyiwa upasuaji.

Beki wa Super Falcons, Ashleigh Plumptre amefanyiwa upasuaji ambao umeenda kwa mafanikio nchini Saudi Arabia.

Plumptre alipata jeraha hilo akiwa kazini katika klabu ya Saudia, Al Ittihad mwezi uliopita. Jeraha hilo lilimlazimu kukosa mechi ya Nigeria ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya 2024 dhidi ya Banyana Banyana ya Afrika Kusini.

Mchezaji huyo wa zamani wa Leicester City alitumia akaunti yake ya X Jumapili usiku, Aprili 21, kutangaza habari za upasuaji wake na kuwashukuru klabu, timu ya taifa, pamoja na mashabiki wake kwa sapoti yao.

Aliandika: “Asante kwa kila mtu katika @ittiladiesclub na kwa Dk Pieter D’Hooge katika @Aspetar kwa kuniunga mkono kupitia upasuaji wangu wa kwanza.

“Imekuwa muda mrefu kuja kujaribu kupata majibu lakini ninashukuru sana kuwa katika hatua hii.

“Kwa wachezaji wenzangu wa @NGSuper_Falcons na mashabiki wa Nigeria… asante kwa subira na uelewa wenu wakati sijaweza kuwa nanyi. Naweza kusema kwa uaminifu nimepigana kwa bidii na kwa muda mrefu niwezavyo na maumivu haya. Siwezi kusubiri kuwa na afya njema na ninyi nyote.

“Klabu yangu – @ittiladiesclub. Ninashukuru sana kuzungukwa na watu wazuri sana kwenye kilabu hii. Asanteni nyote kwa kunisaidia na kuniunga mkono katika kila hatua ninayopitia.

Beki wa Super Falcons, Plumptre afanyiwa upasuaji
0 Comment

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya machoAfyaclass Bongo Social •

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho

Kuna magonjwa mengi yanayohusiana na macho, mengi yanatibika lakini kuna baadhi ya magonjwa ni vigumu kutibika.

Glaucoma ni ugonjwa ambao unazidi kuenea katika siku za hivi karibuni. Na ni vigumu kupata kuona tena baada ya kupata ugonjwa huu.

Glaucoma ni ugonjwa unaoathiri macho. Ugonjwa huu huathiri mishipa inayounganisha macho na ubongo. Husababishwa na umajimaji unaojikusanya kwenye jicho na kuziharibu mishipa hiyo.

Wagonjwa wa glaucoma huanza kuwa na matatizo ya kuona na isipogunduliwa na kutibiwa mapema, uwezo wa kuona unaweza kupotea kabisa.

Ugonjwa huu huathiri watu wa rika zote, lakini hatari zaidi ipo kwa watu wenye umri wa miaka 70 hadi 80.

Pia unaweza kusoma

Ishara 4 zinazoonyesha kuwa unahitaji miwani mpya kwa matatizo ya macho20 Mei 2023

Mlemavu wa macho aliyenyimwa elimu awa bilionea13 Februari 2022

Dalili za glaucoma ni nini?

Moja ya matatizo yanayohusiana na ugonjwa huu ni kwamba hakuna dalili za wazi katika hatua za mwanzo na njiia pekee nikufaya vipimo hospitali.

Kuna wakati mtu aliyeathiriwa hawezi kuona chochote. Kutoona vizuri au kuona miduara inayofanana na upinde wa mvua karibu na mwanga ni miongoni mwa dalili za glaucoma.

Ingawa ugonjwa unaweza kuathiri macho yote mawili, lakini mara nyingi ni jicho moja tu linaweza kuathiriwa. Baadhi ya dalili ni:

Maumivu makali machoni

Kuhisi kichefuchefu na kutapika

Macho kuwa mekundu

Maumivu ya kichwa

Maumivu pembeni ya macho

Kutoona vizuri

Kwa hiyo, ikiwa unahisi mojawapo ya dalili zilizo hapo juu, usizipuuze na nenda hospitali mara moja kaonane na daktari.

Ni muhimu sana kutambua na kutibu glakoma katika hatua zake za mwanzo, vinginevyo kuna hatari ugonjwa huo kukuwa na kusababisha kutoona.

Waliohatarini kupata ugonjwa

Umri, licha ya ukweli kuwa wapo watu wa miaka 40 hupata. Lakini ugonjwa huu mara nyingi huwaathiri watu wa miaka 70 na 80.

Watu wenye asili ya Kiafrika na Asia wana uwezekano mkubwa wa kupata glukoma.

Kurithi pia ni sababu, ikiwa mmoja wa wazazi au ndugu zako wamekuwa na ugonjwa huo, basi kuna uwezekano mkubwa nawe kupata ugonjwa huo.

Matatizo ya moyo ni hatari nyingine. Watu walio na kisukari au matatizo mengine ya kuona pia wana uwezekano mkubwa wa kupata glakoma.

Matibabu na Kujikinga

Bado haijajulikana kwa uhakika ni ipi njia bora ya kuzuia glaucoma, lakini uchunguzi wa mara kwa mara wa macho unaweza kuzuia ugonjwa huu na unaweza kutibiwa mapema.

Faida ya uchunguzi wa macho mara kwa mara ni kwamba ugonjwa unaweza kugunduliwa hata bila dalili na hivyo inashauriwa kufanya uchunguzi wa macho kila baada ya miaka miwili.

Ikiwa mtu hupoteza maono kutokana na glaukoma, maono yake hayawezi kurejeshwa, lakini ikiwa maono yanaathiriwa kwa kiasi kidogo, matibabu yanaweza kuzuia uharibifu zaidi.

Matibabu ya glakoma hutegemea aina na kwa kawaida huhusisha kutumia matone maalum ili kupunguza athari kwenye jicho.

Kwa kuongezea, mionzi inaweza kutumika kuondoa kizuizi katika mishipa ya kwenye jicho, pamoja na upasuaji.

#SOMA ZAIDI Ugonjwa huu wa glaucoma hapa

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho
0 Comment

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa ganiAfyaclass Bongo Social •

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani.

Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza chanzo chake ni nini?

Maumivu chini ya kitovu yanaweza kuwa dalili za hali kadhaa, kama vile maambukizi ya njia ya mkojo, maumivu ya hedhi, matatizo ya utumbo kama vile kuvimba kwa utumbo, au hata mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Ni muhimu kushauriana na daktari ili kupata uchunguzi sahihi na matibabu sahihi.

Katika Makala hii, nitajadili chanzo cha maumivu chini ya kitovu kwa undani zaidi.

Maumivu chini ya kitovu ni tatizo linaloweza kutokea kwa watu wa umri na jinsia zote, na sababu zake zinaweza kutofautiana kulingana na hali ya mtu binafsi. Hapa nitaelezea baadhi ya sababu za kawaida za maumivu hayo:

1. Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI):

Maambukizi ya njia ya mkojo ni sababu ya kawaida ya maumivu chini ya kitovu, haswa kwa wanawake. Bakteria wanaweza kusababisha maambukizi haya, ambayo huathiri mfumo wa mkojo, kuanzia kwenye kibofu hadi kwenye urethra.

Dalili zinaweza kujumuisha maumivu wakati wa kukojoa, hisia ya kutaka kwenda kukojoa mara kwa mara, na maumivu chini ya kitovu.

>>SOMA Zaidi hapa Kuhusu Maambukizi ya njia ya mkojo(UTI)

2. Matatizo ya Utumbo:

Pia Matatizo kama vile kuvimba kwa utumbo, spastic colon (colon ambayo hufanya kazi ya ziada), au matatizo mengine ya utumbo yanaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu.

Hali kama vile colitis (kuvimba kwa utando wa utumbo mpana) au ileitis (kuvimba kwa sehemu fulani ya utumbo) zinaweza kusababisha dalili kama maumivu, kuharisha, au mabadiliko katika kula.

#SOMA Hapa Zaidi Kuhusu Saratani ya Utumbo mpana(Colon cancer)

3. Matatizo ya Uzazi kwa Wanawake:

Kuvimba kwa mirija ya uzazi au maambukizi kwenye viungo vya uzazi kama vile ovari, kibofu cha uzazi, au mfuko wa uzazi yanaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu kwa wanawake.

Matatizo kama vile endometriosis (ambapo tishu zinazofanana na utando wa ndani wa uterasi hukua nje ya uterasi) au fibroids (uvimbe katika uterasi) ni sababu za kawaida za maumivu haya.

#SOMA Hapa Zaidi Kuhusu PID

4. Matatizo ya Figo:

Matatizo kama vile maambukizi ya figo au mawe ya figo yanaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu. Maumivu yanayohusiana na figo mara nyingi huenda yakawa ya upande mmoja wa mwili, lakini yanaweza kusambaa hadi sehemu ya chini ya tumbo.

5. Matatizo ya Misuli na Viungo:

Maumivu chini ya kitovu yanaweza pia kusababishwa na matatizo ya misuli au viungo katika eneo hilo. Kuvuta misuli, kuharibika kwa tishu, au hata misuli iliyokwama inaweza kusababisha maumivu haya.

Hitimisho

Kumbuka kuwa hizi ni sababu chache tu za maumivu chini ya kitovu, na kila mtu anaweza kuwa na sababu tofauti. Ni muhimu kwa mtu mwenye maumivu haya kutafuta ushauri wa kitaalam ili kupata utambuzi sahihi na matibabu stahiki.

Kwa kujua chanzo cha maumivu, matibabu yanaweza kutolewa ipasavyo ili kupunguza au kutibu kabisa tatizo.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani
0 Comment

Jumla ya watu 391 wamekufa kutokana na Kipindupindu na ugonjwa wa Dengue SUDANAfyaclass Bongo Social •

Jumla ya watu 391 wamekufa kutokana na Kipindupindu na ugonjwa wa Dengue katika mwaka wa vita nchini Sudan, Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza siku ya Alhamisi.

Takriban wagonjwa 11,000 wa Kipindupindu walirekodiwa, vikiwemo vifo 325 katika Wilaya 12, huku wagonjwa wa homa ya Dengue wakifikia 9,000, vikiwemo vifo 66, Waziri wa Afya wa Sudan Haitham Mohamed Ibrahim alisema katika taarifa yake.

Licha ya mzozo huo, uingiliaji kati wa haraka unaofanywa na Wizara ya Afya umesaidia kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko, kilisisitiza chanzo hicho, kikibainisha uagizaji wa vifaa vya matibabu vya haraka vya thamani ya pauni bilioni 19 za Sudan.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Mashariki ya Mediterania, Hanan Hassan Balkhi, alionya kwamba hospitali za Sudan ziko katika hatihati ya kukabiliwa na “uhaba wa dawa” wakati ambapo magonjwa ya milipuko yanaenea nchini humo.

Kati ya 70% na 80 ya hospitali katika Wilaya zilizoathiriwa na mzozo hazifanyi kazi, kutokana na mashambulizi ya muda mrefu, ukosefu wa vifaa vya matibabu, au ukosefu wa wafanyakazi wa afya, alisema.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), mwaka mmoja baada ya kuzuka kwa mzozo kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), mnamo Aprili 15, 2023, Sudan inakabiliwa na moja ya majanga yanayoendelea kwa kasi duniani, yenye mahitaji ambayo hayajawahi kushuhudiwa.

Takriban watu milioni 25, wakiwemo zaidi ya watoto milioni 14, wanahitaji msaada wa kibinadamu na usaidizi, na zaidi ya watu milioni 8.6, sawa na asilimia 16 ya watu wote nchini humo, wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita, inabainisha. OCHA

Jumla ya watu 391 wamekufa kutokana na Kipindupindu na ugonjwa wa
Dengue SUDAN
0 Comment

Mafuriko yaathiri kaya 29,510 watu 125,668, Morogoro kaya 12,824 watu 51,491 na Mbeya kaya 27, 000 watu 96,000.Afyaclass Bongo Social •

SERIKALI imesema wananchi 273,159 hawana makazi kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Kadhalika, viongozi wa dini wataondoka leo na treni ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kwa ajili ya kufanya maombi na dua ya kuliombea taifa kesho.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Mobhare Matinyi, amesema jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alikuwa akizungumzia mafuriko, Muungano na safari ya majaribio ya treni ya kisasa (SGR).

Amesema idadi ya walioathirika kwa Mkoa wa Pwani ni

kaya 29,510 watu 125,668, Morogoro kaya 12,824 watu 51,491 na Mbeya kaya 27, 000 watu 96,000.

Katika maeneo ya Rufiji mafuriko yameanza kupungua kutokana na mvua kupungua katika baadhi ya mikoa ambayo mito yake huingiza maji katika Bonde la Rufiji.

Matinyi amesema kutokana na athari hizo za mvua walianzisha makazi ya muda na hadi sasa kuna kambi sita zenye waathirika 2,883 kwa Mkoa wa Pwani yenye kaya 29,510 zilizoathirika.

Amesema mvua hiyo imeathiri miundombinu ya barabara, vituo vya afya, shule, nyumba, mifumo ya maji na mashamba 152,956. 24 yenye mazao ya chakula.

Aidha, amesema misaada inaendelea kupelekwa katika mikoa ya Pwani, tani 700 za chakula, mafuta ya kula lita 7,880, vyandarua 2,260, mablanketi 1,290 na vifaa vingine ikiwamo mahema 26, magodoro 1,258, mafuta ya petroli lita 3,000 na dizeli 2,900.

Matinyi amesema mahitaji mengine kwa Mkoa wa Pwani ni boti mbili zaidi, umeme wa nguvu za jua, magodoro 2,000, vitanda 150, matangi 50 ya lita 5,000, mahema makubwa manne na madogo 10, mafuta ya petroli lita 100,000 na dizeli 50,000.

“Misaada inaendelea kuja na wahisani wanaombwa kuelekeza misaada Wilaya ya Kibiti ambapo hadi sasa kumekuwa na uhaba wa misaada kutokana na mingi kupelekwa Rufiji,” amesema Matinyi.

Amesema kwa Mkoa wa Morogoro kuna jumla ya kata 50 zilizoathirika na mafuriko na watu 78 waliokolewa na serikali. Sasa kuna kambi sita za waathirika zenye watu 1,500 na Mlimba kuna waathirika 1,365, Ifakara 135 zilizopo halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero.

Alisema watu wote waliopata mafuriko wapo katika makambi wanahudumiwa na serikali kwa kupewa chakula, makazi, tiba, maji na usalama.

Matinyi amesema tathimini ya mafuriko ya mvua inaendelea kufanywa na watatoa taarifa ikiwamo idadi kamili ya vifo vilivyotokana na mafuriko ya mvua.

Aidha, amesema viongozi wa dini, watendaji wa serikali, watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na waandishi wa habari baada ya kumaliza ibada kesho watapanda treni hiyo majira ya saa nane mchana na kuwasili Dar es Salaam majira ya saa moja usiku.

Amesema treni hiyo ipo katika majaribio, na isije kuonekana imetumia muda mrefu kusafiri. “Hizi ni shughuli za majaribio mwendokasi sio kipimo cha kazi haya ni majaribio.”

Amesema hadi sasa wameshapokea mabehewa ya treni ya kisasa 65 na vichwa tisa “kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kimekamilika kwa asilimia 98.9 na kipande cha Morogoro kwenda Dodoma kimekamilika kwa asilimia 96.1.”

Amesema nchi inaadhimisha miaka 60 ya Muungano na kumekuwa na matukio mbalimbali ya kuzindua mradi, tukio kubwa linalofuata Aprili 22, mwaka huu jijini Dodoma ni kuliombea taifa na mgeni rasmi ni Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.

Amesema wananchi wataanza kuingia katika uwanja kuanzia saa 12 asubuhi kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwamo kwaya na shughuli la kuliombea taifa itaongozwa na viongozi wa dini.

Amesema tukio jingine kubwa ni Aprili 24, mwa huu kutakuwa na uzinduzi wa kitabu cha miaka 60 ya historia ya Makamu wa Rais iliyoanzishwa baada ya Muungano kutokea.

Aidha, amesema Aprili 25, majira ya saa tatu Rais Samia Suluhu Hassan, atalihutubia taifa kutoa ujumbe wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano saa sita kamili usiku, mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam, Geita, Mbeya, Mwanza na Zanzibar kutakuwa na urushwaji wa fataki.

Amesema Aprili 26, kilele cha shughuli hizo zitafanyika katika kiwanja cha Uhuru na mgeni rasmi atakuwa Rais Samia.

Taifa linatarajia kuwa na wageni kutoka mataifa ya jirani na marafiki katika siku hiyo.

Mafuriko yaathiri kaya 29,510 watu 125,668, Morogoro kaya 12,824 watu
51,491 na Mbeya kaya 27, 000 watu 96,000.
0 Comment

WATOTO 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wafanyiwa UPASUAJIAfyaclass Bongo Social •

WATOTO 25 WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI WAFANYIWA UPASUAJI AWAMU YA KWANZA YA KAMBI YA MATIBABU MOI

Na Abdallah Nassoro-MOI

Watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji katika awamu ya kwanza ya kambi ya upasuaji inayoendelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), iliyoratibiwa na MOI kwa ushirkiano na chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Tanzania (ASBATH) chini ya ufadhili wa taasisi ya MO Dewji Foundation.

Daktari bingwa wa Mbobezi wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI Dkt. Hamisi Shabani amesema watoto hao ni kati ya 50 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya matatibu.

“Jumla ya watoto wote katika mpango huu ni 50, katika awamu hii ya kwanza ya upasuaji watoto 25 wamefanyiwa upasuaji na Mei, 4, 2024 watoto 25 waliobakia watafanyiwa upasuaji ili kukamilisha malengo ya kambi hii” amesema Dkt. Shabani ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo na kuongeza kuwa

“Watoto hawa wanafanyiwa upasuaji kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya upasuaji wa kutumia matundu, ETV, upasuaji ambao humfanya mgonjwa kuruhusiwa kurudi nyumbani ndani ya siku chache tangu kufanyiwa upasuaji”

Amesema bado tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi ni kubwa hapa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa watoto 7500 wanazaliwa na tatizo hilo ila mwaka.

“Sisi MOI kwa mwaka jana tuliweza kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 800 hii inaonesha bado kuna wimbi kubwa la watoto ambao hawajapata matibabu”

Kwa upande wake Mratibu wa Miradi wa MO Dewji Foundation Amina Ramadhani amesema lengo la msaada huo ni kuwawezesha watoto hao kupata matibabu ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida.

“Maisha ya kila mtu ni muhimu, iwapo kutakuwa na ongezeko la watoto zaidi ya 50 tutaangalia namna ya kuwasaidia ingawa lengo la mwaka huu lilikuwa watoto 50, tunawashukuru MOI na chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH)”

Merina Damon na Mohamed Hamisi ni wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa waliofanyiwa upasuaji wameishukuru MOI, chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH) MO Dewji Foundation kwa msaada wa matibabu hayo.

WATOTO 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wafanyiwa UPASUAJI
0 Comment

Shisha kwa vijana na hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuuAfyaclass Bongo Social •

Shisha kwa vijana na hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu

Ni kawaida siku hizi katika kumbi za starehe mijini kukuta mitungi ya shisha juu ya meza, huku watumiaji wakichangia kilevi hicho. Je, unajua kuna uwezekano mkubwa mtumiaji kupata maambukizi ya Kifua Kikuu (TB)?

Ijapokuwa hakuna utafiti wa moja kwa moja Tanzania unaoonyesha shisha ni chanzo cha TB, nchini Uswizi kupitia utafiti uliofanywa na Dk Anna Marchetti na kuchapishwa katika jarida la afya la ‘European Journal of Case Reports in Internal Medicine’ mwaka 2020 umebainisha kuwa kilevi hicho ni chanzo cha ugonjwa huo unaoshambulia mapafu.

Katika utafiti huo, baada ya mgonjwa mwenye umri wa miaka 20 aliyekuwa na kikohozi kikali kwa miezi mitatu, kupimwa na kubainika kuwa na TB, uchunguzi uliofanywa uligundua kuwa chanzo chake ni shisha.

Katika utafiti huo unaoitwa ‘Uvutaji wa shisha kama sababu ya hatari ya kusambaza kifua kikuu,’ uchunguzi wa X-ray na CT Scan wa kifua, sampuli za makohozi, uwapo wa mycobacteria kwa mgonjwa huyo vilibainisha maambukizi katika mapafu na kifua kikuu na kwamba mgonjwa huyo alikuwa mtumiaji wa shisha mara kwa mara.

Dk Marchetti anamalizia katika utafiti wake kwa kutoa ushauri kuwa uvutaji wa shisha ni sababu inayoweza kueneza ugonjwa wa kifua kikuu kutokana na tumbaku iliyomo au kuchangia bomba moja la kuvutia.

“Madaktari lazima waulize wagonjwa kuhusu uvutaji wa shisha ikiwa anashukiwa kuwa na TB. Iwapo mgonjwa mtumiaji wa kilevi hicho atathibitishwa kuwa na TB, watu wote walioshiriki naye kutumia shisha watafutwe na mtungi husika usitumike tena,” alipendekeza Dk Marchetti.

Makala hii imechunguza ulevi wa shisha katika muktadha wa hatari ya kusababisha maambukizi ya Kifua Kikuu, hasa kwa kundi la vijana ambao ndio watumiaji wakuu katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Dodoma na Tabora.

Katika kumbi za starehe jijini Dar es Salaam, shisha inavutwa kwa kutumia mrija maalumu (filta) ambao kila mtumiaji huwa na wake, hivyo hupokezana kuivuta.

Gazeti hili limegundua hali tofauti ya uvutaji wa shisha mikoani.

Tabora katika moja ya klabu za usiku iliyopo mjini maeneo ya Isevya, shisha huvutwa bila kuwapo ‘filta’ hivyo kusababisha watumiaji kuchangia bomba moja.

Janeth Marwa, mtumiaji wa kilevi hicho mkoani Tabora anasema hapendi kutumia filta kwa sababu inamchelewesha kupata ‘stimu’.

“Nilikuwa natumia filta nilivyokuwa Dar, ila nimekuja huku nimezoea bila filta naona kama nikiitumia sitapata stimu ninazozitaka,” anasema.

Hata hivyo, mwandishi alipomtafuta meneja wa klabu hiyo kwa masharti ya kutotajwa jina lake na la ukumbi huo wa starehe alisema filta zipo ila hutolewa kwa anayezihitaji.

Kauli ya Serikali

Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP), Dk Peter Neema alipoulizwa kuhusu hatari ya watumiaji wa shisha kupata TB alisema uwezekano wa kupata maambukizi upo endapo kuna mtu aliyeathiriwa na ugonjwa huo kati ya wanaochangia au uvutaji kupindukia utakaoharibu mapafu.

“Ugonjwa wa Kifua Kikuu unaambukizwa kwa njia ya hewa pale mtu mwenye vimelea vya TB anapokohoa au kupiga chafya.

“Matumizi ya shisha yanahusisha uvutaji na upulizaji wa moshi ambao kwa namna moja au nyingine huwa na uwezekano wa kuchochea mtu kupata vimelea iwapo mmoja kati ya wavutao atakuwa na vimelea hivi na hajaanza matibabu,” alisema Dk Peter.

Alisema bado hakuna utafiti wa moja kwa moja kubaini ongezeko la wagonjwa wa TB unaosababishwa na uvutaji wa shisha.

“Hata hivyo, kwa namna nyingine uvutaji wa shisha kwa kipindi cha muda mrefu unaweza kuathiri mapafu na hivyo mtu kuwa na uwezekano sawa na mvutaji wa sigara katika kupata TB,” alifafanua.

Serikali katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 imepitisha ushuru wa asilimia 30 wa bidhaa hiyo, huku ikitaja lengo la kufanya hivyo ni kujumuisha bidhaa mpya zinazotumika kama mbadala wa tumbaku ambazo pia zina athari sawa na tumbaku kwa ajili ya udhibiti.

“Kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 30 kwenye sigara na bidhaa za aina hiyo zinazotumia mbadala wa tumbaku zinazotambulika kwa Hs code 2402.90.00; tumbaku inayovutwa kwa kutumia bomba la maji inayotambulika kwa Hs code 2403.11.00; na sigara za kielektroniki, shisha na bidhaa za aina hiyo zinazotambulika kwa Hs codes 8543.40.10, 8543.40.90 na 9614.00.00,” inaeleza Bajeti Kuu ya Serikali 2023/2024.

Watengenezaji shisha hatarini zaidi

Edwin Jacob (19), maarufu ‘Dogo Ed’ ni mtengenezaji wa shisha katika kumbi moja ya starehe iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam, anasema kwa siku moja mwishoni mwa juma anatengeneza wastani wa shisha 17 hadi 25 za ladha tofauti, huku zote akilazimika kuzijaribu (kuvuta) kabla hazijaenda kwa mteja.

“Siku za wikiendi wateja wanakuwa wengi, unaweza kuuza mitungi 17, 20 au siku nyingine hata 25. Kuhusu kuijaribu kama ladha imekolea vizuri lazima nivute kwenye bomba ili nijue na wakati mwingine ili moto ukolee,” anasema.

Edwin anasema changamoto anazokutana nazo ni kukaa karibu na moto muda mrefu ambao anautumia kuandaa kilevi hicho ambacho anasema kinapendwa, zaidi  na vijana.

“Mimi sioni shida katika kuvuta (wakati wa kujaribu) ila naumia zaidi na moto ninaoutumia muda wote maana unaunguza kweli,” anasema.

Dk Zainabu Hussein kutoka Kituo cha Afya cha Shirika la Reli Tanzania (TRC) kilichopo Dodoma, anasema watengenezaji wa shisha wapo hatarini kupata maambukizi ya TB kwa sababu wanazijaribu kupitia bomba la shisha ambalo kuna baadhi ya wateja wao wanalitumia wakati wa kuvuta.

Anasema kama watengenezaji wa kilevi hicho ni zaidi ya mmoja, hatari ni kubwa zaidi.

“Hatari inakuwapo zaidi kama ukumbi wa starehe utakuwa na watengeneza shisha zaidi ya mmoja kwa sababu watachangia bomba la mtungi wa shisha katika kutengeneza, jambo ambalo linasababisha maambukizi ya TB kama mmoja wao ana vimelea hivyo,” anasema.

Bei ya shisha

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala haya umebaini bei za shisha hutofautiana kulingana na hadhi ya eneo husika, ikianzia Sh10,000 hadi Sh30,000.

Katika maeneo ya Mwenge, Tabata na Sinza jijini Dar es Salaam kilevi hicho kinauzwa Sh15,000, lakini katika kumbi za starehe za Mikocheni, Masaki na Oysterbay kinauzwa Sh20,000 hadi Sh30,000.

Mwandishi pia alibaini kuwa shisha huwekwa ladha kadhaa kama vile vanila, strawberry, mint, chocolate au kahawa, ili kuwavutia wavutaji. Ladha hizo zinatajwa kuwa kivutio cha mabinti ambao wameingia kwa kasi kwenye uvutaji huo.

Wanachuo vinara

Katika uchunguzi wa mwandishi wa makala haya, umebaini katika majiji ya Dodoma na Dar es Salaam wateja wakubwa ni wanachuo ambao hutumia fedha za kujikimu kuvuta shisha.

Magdalena John (si jina halisi), mwanafunzi wa chuo jijini Dodoma anasema haiwezi kupita wiki moja bila kuvuta shisha kutokana na hamu anayoihisi endapo hajavuta.

“Kila wikiendi mimi na rafiki zangu tunachanga fedha kwa ajili ya kwenda kuvuta shisha (anataja eneo maarufu jijini hapo), tunaipenda ladha ya mint na ‘stimu’ yake inakuwa nzuri,” anasema Magdalena.

Alipoulizwa anapata wapi fedha ya kununua kilevi hicho, Magdalena anasema katika fedha za boom (fedha za kujikimu zinazotolewa na Serikali) lazima watenge kiasi kwa ajili ya starehe hiyo.

Hali ni tofauti kwa wanafunzi wa vyuo jijini Dar es Salaam, ambao wameenda mbali na baadhi yao hununua mtungi wa shisha na kukaa nao vyumbani (ghetto).

“Baada ya kuona nyumba hii tumepanga wanachuo wanne na wote tunapenda shisha tulikubaliana tuchangishane na tununue mtungi wetu,” anasema kijana aliyejitambulisha kwa jina moja la Brighton, mkazi wa Mwenge Mpakani.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini mitungi ya shisha inauzwa kuanzia Sh70,000, huku biashara hiyo ikitangazwa zaidi katika mitandao ya kijamii, hususan Twitter.

“Shisha Pipes (mabomba) mawili kwa Sh70,000, vifaa vya mitungi ya shisha vipo, Vapes na Flavour (ladha) tofauti  zinapatikana kwa mawasiliano zaidi Karibu DM (uwanja wa meseji wa Twitter na Instagram). Mikoani tunatuma,” ni tangazo lililokutwa katika moja ya ukurasa za Twitter wa wauzaji wa shisha.

Akizungumzia ununuzi wa shisha na kuvuta pamoja nyumbani, Dk Zainabu anasema hilo ni hatari zaidi kwa kuwa vifaa vya kuvutia (filta) zikiwaishia watalazimika kutumia bomba moja ambalo linaweza kuambukiza maradhi hayo.

“Hao walionunua wapo hatarini kwa sababu filta zikiisha watatumia vivyo hivyo au watakuwa wanavuta kwa kiwango kikubwa kwa sababu ipo nyumbani muda wote. Hatari kwa mapafu kuathirika ni kubwa,” anasema Dk Zainabu.

Athari nyingine za shisha

Utafiti uliofanywa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) nchini Marekani mwaka 2021, ulioitwa ‘uvutaji na matumizi ya tumbaku’ umetaja athari zinazoweza kusababishwa na uvutaji shisha ambao kwa majina mengine hujulikana kama narghile, argileh, hookah, hubble-bubble na goza.

Maradhi ya kuambukiza; Uvutaji wa shisha hutumia bomba ambalo watu kadhaa hushirikiana. Hali hii husababisha maradhi ya kuambukiza ya Hepatitis B (homa ya ini).

Saratani; Shisha ina wingi wa nikotini, kiwango cha kemikali za tar, carbon monoxide, metali za kiwango cha juu kama cobalt na lead ambavyo ni visababishi vya saratani.

Uraibu; Uvutaji wa shisha husababisha kutengenezwa kwa kiwango kikubwa cha nikotini kwenye damu, hivyo mtu akishazoea kuvuta hawezi kuacha kwa kuwa kilichomo kwenye shisha huvutwa kwenye neva za fahamu na kusababisha mishipa hiyo kwenye ubongo kuhisi kupata faraja na raha ya kipekee.

Takwimu athari za shisha

Takwimu za Shirikisho la Madaktari wa Mapafu Marekani (ALA) zinaonyesha mtu anayevuta shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara 100 katika kiwango cha moshi na sumu ya nikotini anayoivuta mtumiaji husika.

ALA walifanya utafiti kubaini sababu za vijana kuvuta shisha na kubaini wengi hudhani haina madhara ikilinganishwa na sigara.

“Wanaovuta kwa sababu ya rafiki zao (asilimia 25), wanaodhani haina madhara (asilimia 21), kupumzika na kufurahia (asilimia 31) na wanaovuta kujaribu kilevi kipya (asilimia 11),” imesema ripoti hiyo.

Imeandikwa kwa udhamini wa Bill & Melinda Gates Foundation

Shisha kwa vijana na hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD