Dawa ya Kutibu Kisonono Kabsa,Wengi Mnaita GonoAfyaclass Bongo Social •

Dawa ya Kutibu Kisonono Kabsa,Wengi Mnaita Gono

Je, ni Ipi dawa sahihi ya kutibu Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?

Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,

Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;

Dalili za Ugonjwa wa Kisonono au Gono

Kwa Wanawake:

1. Kutokwa na Usaha au uchafu usio wa kawaida kwenye uke (unaoweza kuwa na rangi ya njano au kijani).

2. Kupata Maumivu au kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa.

3. Kupata Maumivu chini ya tumbo

4. Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi au baada ya tendo la ndoa.

5. Kupata Maumivu kwenye sehemu ya haja kubwa (ikiwa eneo hilo limeathiriwa). n.k

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

- Kutokwa na usaha kwenye Uume

- Uchafu wa majimaji meupe, ya njano, au ya kijani kutoka kwenye uume.

- Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

- Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

- Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

- Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

- Kupata maumivu kwenye korodani.

- Kupata Maumivu au uvimbe katika sehemu ya haja kubwa (ikiwa maambukizi yameathiri eneo hilo).

- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa n.k.

Dawa ya Kutibu Kisonono

Dawa za kisonono au Gono huweza kutibu kabsa tatizo hili likaisha ikiwa umepata tiba Sahihi na hujakutana na mazingira hatarishi ya kupata maambukizi haya tena baada ya Tiba.

Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati wa Kutumia Dawa za kutibu kisonono kwani badala ya kutibu Kisonono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”

Kwa hivi Sasa,Ukinzani huu kwenye Ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio Ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Ngumu kuipata.

Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kugundulika una ugonjwa wa Kisonono, hakikisha unapata dawa ya Kisonono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.

Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Kisonono – ufuatiliaji wa dawa ya Kisonono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.

Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,

Kuhusu Kipindi cha Matibabu:

Wagonjwa wanaotibiwa maambukizi ya koo wanashauriwa kufanyiwa kipimo cha uhakiki wa tiba (test of cure) siku 7–14 baada ya matibabu, kwa sababu koo ni eneo gumu zaidi kuponya maambukizi.

Kwa wagonjwa wengine (wasio na maambukizi ya koo), matibabu kwa dozi moja ya sindano mara nyingi hutosha, na hakuna haja ya kipimo cha uhakiki wa tiba isipokuwa dalili zitaendelea au maambukizi yawe sugu.

wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.

Dawa ya gono;

Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”

Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ambapo huweza kutumika ni pamoja na;

  • Sindano
  • Na Vidonge

Ingawa dawa hizi Zitazuia maambukizi ya Gono hazitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.

NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dalili za ukimwi huchukua muda gani kuonekanaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za ukimwi huchukua muda gani kuonekana

Ukimwi ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya HIV. Kwa bahati mbaya, ugonjwa huu umekuwa kwa muda mrefu sasa na bado hauna tiba.

Ili kujikinga na ugonjwa huu, ni muhimu kufahamu dalili zake na hatua za kujikinga.

Katika makala hii, tutajifunza kuhusu dalili za ukimwi, muda unaohitajika kwa dalili hizo kujitokeza, na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu hatari.

Kwa mujibu wa vituo vya Udhibiti na Kuzuia Magonjwa yaani centers for diseases control and Prevention-CDC

“Watu wengi huanza kupata Dalili za kama mafua(flu-like symptoms) ndani ya muda wa wiki 2 mpaka 4 toka kupata maambukizi”

Dalili hizi huweza kudumu kwa muda wa siku chache au wiki kadhaa,

Hata hivo dalili hii pekee haitoshi kukufanya uwe na wasiwasi juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,

Dalili za Ukimwi Huchukua Muda Gani Kujitokeza?

HIV ni virusi ambavyo hushambulia seli za kinga mwili. Baada ya kuambukizwa virusi hivyo, mtu huanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo baada ya muda fulani.

Hata hivyo, muda ambao mtu anaweza kuonyesha dalili hizo hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Kwa kawaida, inachukua kati ya wiki mbili hadi miezi michache kwa dalili za ukimwi kujitokeza baada ya kuambukizwa virusi vya HIV.

Kwa hiyo, inaweza kuchukua muda wa miezi michache hadi miaka kadhaa kwa mtu kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

Dalili za Ukimwi

Kuna dalili kadhaa za ukimwi ambazo zinaweza kujitokeza katika hatua tofauti za ugonjwa huo. Baadhi ya dalili hizo ni pamoja na:

  1. Homa
  2. Kichefuchefu na kutapika
  3. Kutokwa na jasho usiku
  4. Kupoteza hamu ya kula
  5. Kuharisha mara kwa mara
  6. Maumivu ya kichwa
  7. Kukosa usingizi
  8. Kupungua kwa uzito kwa sababu ya kupoteza hamu ya kula n.k

Hatua za Kujikinga na Ukimwi

Hatua za kujikinga na ukimwi ni pamoja na:

  • Kutumia kinga wakati wa kujamiiana
  • Kufanyiwa vipimo vya ukimwi mara kwa mara
  • Kuepuka kushirikiana vitu vya ncha kali kama sindano zilizotumiwa na mtu mwingine,nyembe,pin n.k
  • Kuepuka kushirikiana vifaa vya upasuaji, kama vile sindano na visu
  • Kuepuka kuwa na wapenzi wengi
  • kuepuka kushiriki tendo kinyume na maumbile n.k

Jinsi ya Kupata Vipimo vya Ukimwi

Ni muhimu kufanya vipimo vya ukimwi mara kwa mara ili kubaini kama una virusi hivyo au la.

Kuna njia mbalimbali za kupata vipimo hivyo ikiwa ni pamoja na hospitali, vituo vya afya, na mashirika ya kijamii yanayotoa huduma za vipimo vya ukimwi.

Jinsi ya Kujikinga na Ukimwi

Kujikinga na ukimwi ni muhimu na inawezekana kwa kufuata njia za kujikinga ambazo zimeelezwa hapo juu.

Ni muhimu pia kuelimisha jamii kuhusu ukimwi na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu hatari. Elimu hii inaweza kusaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV na kuokoa maisha ya watu wengi.

Hitimisho

Kwa kuhitimisha, dalili za ukimwi zinaweza kuchukua muda tofauti kujitokeza kwa kila mtu. Ni muhimu kujifunza kuhusu dalili hizo, kufanya vipimo vya ukimwi mara kwa mara, na kuzingatia njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari.

Kumbuka, ukimwi unaweza kuepukika, na tunaweza kushirikiana kama jamii ili kujikinga na kusambaza elimu zaidi kuhusu ugonjwa huu.

JE INACHUKUA MUDA GANI UGONJWA WA UKIMWI KUANZA KUONYESHA DALILI?

Hapa tunazungumzia baada ya mtu kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi itachukua muda gani kuanza kupata dalili za ugonjwa huu wa ukimwi,

Hili ni swali ambalo watu wengi hujiuliza na wanapenda kujua,hivi baada ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi dalili huchukua muda gani kuanza kuonekana.

MAJIBU; Dalili za awali kabsa  baada ya mtu kuambukizwa virusi vya ukimwi huanza kuonekana baada ya Wiki 2 mpaka 4, na mara nyingi dalili hizo ni kama vile;

✓ Mtu kuanza kupata homa za mara kwa mara

✓ Mtu kupata maumivu makali ya misuli ya mwili

✓ Mtu kuanza kuvimba tezi mbali mbali za mwili wake kama vile; tezi za shingoni n.k

✓ Mtu kuanza kupata rashes kwenye ngozi

✓ Mtu kuhisi baridi kali mwilini pasipo kujua chanzo (chills)

✓ Mwili kuchoka kupita kawaida

✓ Kuhisi hali ya madonda kooni, na wengine ngozi ya ndani ya mdomo kwa juu huanza kuona hali ya kubabuka au vidonda vidonda

✓ Kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

n.k

Kwa baadhi ya watu ugonjwa huu wa ukimwi hauonyeshi dalili kabsa ukiwa katika hatua za mwanzoni

– Baadae mtu huanza kupata dalili mbali mbali kama vile;

• Kuanza kukohoa sana

• Kupata shida sana ya upumuaji

• Uzito wa mwili kushuka kwa kasi na mtu kuanza kukonda sana

• Kupatwa na homa kali

• Mtu kuchoka sana kupita kawaida

• Kuharisha sana mara kwa mara

n.k

SUMMARY;

– Dalili za mwanzo au awali za maambukizi ya virusi vya ukimwi huweza kuonekana baada ya wiki 2-4

– Sio kila mtu huweza kuonyesha dalili hizi za awali kwenye kipindi hiki

– Asilimia 98% ya maambukizi ya Virusi vya ukimwi huchukua kipindi cha Miezi 3 toka siku ya kuambukizwa, ili kuonekana kwenye kipimo cha ukimwi

– Rudia kupima baada ya miezi 3 kupata majibu sahihi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dalili za magonjwa hatari sehemu za siriAfyaclass Bongo Social •

Dalili za magonjwa hatari sehemu za siri

Dalili za magonjwa hatari sehemu za siri zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa. Hapa kuna dalili ambazo hujitokeza Zaidi zinazoweza kuonyesha uwepo wa magonjwa ya zinaa au maambukizi mengine sehemu za siri:

1. Vidonda pamoja na Maumivu

Vidonda visivyo vya kawaida sehemu za siri, mdomoni, au kwenye njia ya haja kubwa huweza kuwa Ishara ya magonjwa.

Kupata Maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa huweza kuwa kiashiria kingine cha magonjwa haya.

2. Kutokwa na Uchafu Sehemu Za Siri

Kutokwa na Uchafu au majimaji yenye harufu mbaya au rangi isiyo ya kawaida (kama kijani, njano, au kahawia).

Kutokwa na damu isiyo ya kawaida (kwa wanawake) ambayo haiko kwenye kipindi cha hedhi.

Kutokwa na maji maji au Usaha Kwenye Uume n.k, Zote hizi huweza kuwa dalili za magonjwa ya Zinaa Sehemu Za Siri.

3. Kuwa na Uvimbe au Malengelenge

Malengelenge yanayojitokeza kama vipele vidogo vinavyoweza kupasuka na kusababisha vidonda.

Uvimbaji wa tezi za kinena (lymph nodes) karibu na sehemu za siri.

Vyote hivi huweza kuwa dalili za magonjwa sehemu za Siri.

4. Maumivu ya Tumbo

Maumivu ya chini ya tumbo, hasa kwa wanawake, yanaweza kuashiria maambukizi kwenye mfumo wa uzazi kama PID (Pelvic Inflammatory Disease).n.k.

5. Kuwashwa na Kubadilika kwa Ngozi

Kuwashwa au kuhisi hali ya kuungua sehemu za siri.

Mabadiliko ya rangi au uwepo wa vipele sehemu hizo, hizi pia huweza kuwa dalili za baadhi ya magonjwa Sehemu za Siri.

6. Kupata Homa

Kupata homa,Kutoa jasho sana usiku au kujisikia mchovu kupita kiasi. Huweza kuwa Dalili za uwepo wa maambukizi mwilini mwako.

Magonjwa Hatari Yanayoweza Kusababisha Dalili Hizi:

Kwa Ujumla Baadhi ya Magonjwa ambayo huweza Kusababisha dalili hizi ni pamoja na;

  • Kaswende (Syphilis): Mfano vipele au Vidonda visivyo na maumivu katika hatua ya awali
  • Kisonono (Gonorrhea): Maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu mzito, Usaha n.k
  • Klamidia (Chlamydia): Mara nyingi haina dalili mwanzoni lakini baadae zinaweza kuonekana
  • Herpes Simplex Virus (HSV): Malengelenge au vidonda vinavyojirudia mara kwa mara
  • Virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus (HPV): Vinaweza kusababisha masundosundo(warts),Vipele au vinundu, vingine husababisha saratani ya kizazi au sehemu za siri.
  • Ukimwi (HIV/AIDS): Dalili za upungufu wa kinga ya mwili pamoja na magonjwa nyemelezi huweza kujitokeza pia

Unapaswa Kufanya Nini?

Tafuta Matibabu Haraka: Unapoona dalili yoyote isiyo ya kawaida, hakikisha unakutana na wataalam wa afya kwa Msaada wa haraka, au Kwa Ushauri zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass,kupitia kwenye namba +255758286584.

Epuka Kujitibu Bila Ushauri wa Daktari: Tiba isiyo sahihi inaweza kuzidisha tatizo.

Zuia Maambukizi: Tumia kinga kama kondomu, kuwa mwaminifu kwa mwenza mmoja, au punguza idadi ya wapenzi.n.k.

Ukiona dalili yoyote, usisite kutafuta ushauri wa kitaalamu kwa sababu magonjwa haya yanaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa hayatatibiwa kwa wakati.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mtoto Mchanga Kukosa Choo,Sababu Au ChanzoAfyaclass Bongo Social •

Mtoto Mchanga Kukosa Choo,Sababu Au Chanzo

Kama huoni mtoto wako akijisaidia kabsa,hiki ndyo chanzo cha Mtoto mchanga kukosa choo.

Chanzo cha tatizo la Mtoto mchanga Kukosa Choo na Tiba Yake

Baada ya  mtoto kuzaliwa huanza kunyonya maziwa ya mama yake, na baada ya muda huanza kujisaidia haja ndogo na haja kubwa pia. Lakini kukaa kwa muda mrefu bila mtoto kupata choo huweza kuleta mashaka hata kwa mama wa mtoto pia.

Swala la mtoto kukosa choo kwa muda mrefu huweza kusababisha mtoto kulia lia mara kwa mara, Mtoto kupata maumivu ya tumbo,tumbo kujaa n.k

CHANZO CHA TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA WATOTO

Wengine tatizo la kukosa choo kabsa, huanza na haja kubwa kuwa ngumu sana wakati wa kujisaidia, Kujisaidia kinyesi kama cha mbuzi na baadae hali ya kukosa choo kabsa hujitokeza.

Watoto wadogo sana huweza kupatwa na shida hii, Watoto ambao ni kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano pia huweza kusumbuliwa na shida hii.

Maziwa ya mama yanavirutubisho vingi zaidi(So nutritious), hali ambayo huweza kupelekea muda mwingine mwili wa mtoto kufyonza Kila kitu na kuacha kiasi kidogo sana kupita kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula,

Hii pia huweza kusababisha mtoto wako kukosa Choo,

Pia wakati mwingine hunyonyeshi mtoto vizuri akashiba, hawezi kujisaidia maana hana cha kutoa Nje.

Lakini pia Wakati mwingine inaweza kuwa tatizo kubwa kama kuziba Njia ya haja kubwa,ambayo hii huweza kutokea toka mtoto anazaliwa hapati choo, kuambatana na tumbo la mtoto kuvimba n.k

Sababu Za Mtoto Mchanga kukosa Choo

Mtoto mchanga kutokujisaidia inaweza kutokea kutokana na sababu kadhaa, Zipo Sababu za Kawaida kabsa,ila Wakati mwingine hutokana na Sababu za kiafya.

Sababu za Kawaida:

Sababu hizi hazihitaji wewe kuchukua hatua yoyote. Sababu za kawaida zinazoweza kusababisha Mtoto mchanga kukosa choo ni pamoja na;

1. Unyonyeshaji kwa Mtoto: 

Ni kawaida kwa watoto wanaonyonyeshwa kukaa kwa siku kadhaa bila kupata choo kwasababu maziwa ya mama humeng’enywa kwa urahisi na kwa kiwango kikubwa, hali ambayo hupelekea kinachobaki kama uchafu kuwa kidogo sana,

Maziwa ya mama yanavirutubisho vingi zaidi(So nutritious), hali ambayo huweza kupelekea muda mwingine mwili wa mtoto kufyonza Kila kitu na kuacha kiasi kidogo sana kupita kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula.

2. Hatua za Ukuaji Kwa Mtoto(Developmental Stage): 

Mifumo ya mmeng'enyo wa chakula kwa watoto wachanga bado inakua, haijakomaa bado, hali ambayo inaweza kusababisha kutokuwa na Mfululizo unaoleweka wa Mtoto kujisaidia haja kubwa kila siku.

Sababu za Kiafya:

Sababu hizi huashiria hali isiyoyakawaida na wakati mwingine huhitaji Matibabu kwa Mtoto. Sababu hizo ni pamoja na;

1. Tatizo la choo kigumu au Constipation:

Hali hii Ni nadra kutokea kwa watoto wachanga lakini inawezekana, haswa kwa watoto wanaolishwa Maziwa ya Kopo.  Vinyesi vinaweza kuwa vigumu, vikavu sana, au hata kuwa vigumu kinyesi kupita pia.

2. Tatizo la Maji ya mwili kupungua(Dehydration): 

Kwa Mtoto mwenye hali hii ya hatari anaweza asipate choo mara kwa mara, pamoja na dalili zingine kama vile kutokukojoa mara kwa mara,mdomo kukauka sana n.k

3. Tatizo la Ulaji(Feeding Issues):

Mtoto Mchanga kukosa choo inaweza kuwa kutokana na kutonyonyeshwa akashiba vizuri au kutokula vizuri akashiba.

Hivo basi,endapo Mtoto wako hali akashiba mbali na kukosa virutubisho vingine muhimu mwilini,anaweza kupata tatizo la kukosa choo pia.

4. Tatizo la Mzio au Milk Allergy/Intolerance: 

Mzio wa protini ya maziwa ya ng'ombe,maziwa ya kopo au kupitia maziwa ya mama unaweza kusababisha matatizo ya usagaji chakula, ikiwa ni pamoja na tatizo hili la Mtoto mchanga kukosa Choo.

5. Tatizo la kuziba njia ya haja kubwa-Blocked Anus (Imperforated Anus): 

Wakati mwingine mtoto hukosa choo kwa Sababu njia ya haja kubwa imeziba. Hali hii ni nadra kutokea lakini ni hatari, na huweza kutokea ikiwa njia ya haja kubwa haijaundwa vizuri wakati wa Ukuaji wa Mtoto tumboni.

Hakikisha Unatafuta Msaada wa Kitaalam ikiwa;

- Mtoto wako kakosa Choo Zaidi ya Siku 7 na anaonekana hayupo sawa

- Mtoto anaonyesha dalili za tumbo kuuma

- Mtoto anatapika,hasa matapishi ya kijani au Njano

- Mtoto anajisaidia Damu au kinyesi kilichochanganyika na Damu. n.k.

NJIA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO

- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutatua tatizo hili kulingana na Umri wa mtoto, Mfano;

Kwa watoto ambao tayari wanakula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama pekee, hushauriwa ;

• kula matunda ambayo yana nyuzi nyuzi kama maembe,machungwa na matunda yenye kiwango kikubwa cha maji kama matikiti maji,

• Watoto kunywa kiwango kikubwa cha maji kwa siku

• Watoto kuepuka kubana kinyesi kila mara wanapohisi haja kubwa

• Lakini pia kuna njia ya kumassage tumbo la mtoto, hali ambayo itamsaidia mtoto kujisaidia kwa haraka zaidi.

Kama Mtoto hapatu choo Kabsa unaweza kuonana na wataalam wa afya hasa wa mambo ya Watoto kwa ajili ya Msaada zaidi.

#SOMA PIA; Kuhusu tatizo la Mtoto kutokupata Choo

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

kisonono husababishwa na nini,Dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

kisonono husababishwa na nini(Chanzo)

UGONJWA WA KISONONO

Ugonjwa wa Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na Bacteria ambaye kwa kitaalam hujulikana kama Neisseria gonorrhoeae na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Maeneo ambayo Ugonjwa wa Kisonono huathiri

Ugonjwa huu wa zinaa hushambulia na kuathiri zaidi maeneo ya mwili yenye joto Pamoja na Unyevu unyevu kama vile;

  •  Kwenye urethra au mrija ambao huvuta mkojo kutoka kwenye kibofu
  • Kwenye macho
  •  Eneo la Kooni
  • Ukeni
  • kwenye Uume
  •  Kwenye njia ya haja kubwa(anus)
  • Kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke ikiwemo Kwenye Kizazi,Mirija ya Uzazi, Pamoja na Mlango wa kizazi yaani cervix n.k

UGONJWA WA KISONONO HUSAMBAAJE AU KUAMBUKIZWA?

Ugonjwa huu husambazwa kwa Njia ya Kujamiiana,

Kufanya Mapenzi kwa njia ya Mdomo,Sehemu ya haja kubwa au Ukeni yaani oral, anal, or vaginal sex.

Kutumia kondomu au njia nyingine ya kizuizi unaposhiriki tendo la ndoa kunaweza kusaidia sana kupunguza uwezekano wako wa kusambaza au kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono,

Kumbuka tu matumizi ya njia hizi hayataondoa kabisa hatari ya wewe kupata magonjwa kama haya, hasa ikiwa hutumii kwa Usahihi,

Unaweza kutumia Njia kama Condom na bado ukapata Kisonono(Gono) endapo hukutumia kwa Usahihi wake.

Dalili za Ugonjwa wa Kisonono

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO;

Kumbuka; Ugonjwa huu wa kisonono kwa asilimia kubwa ni vigumu mwanamke kuonyesha dalili za moja kwa moja hata kama ameambukizwa. Lakini kama akionyesha dalili basi baadhi ya dalili kama hizi hapa chini huweza kutokea.

MIONGONI MWA DALILI AMBAZO HUWEZA KUJIONYESHA KWA MWANAMKE NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kupatwa na tatizo la maumivu makali wakati wa kufanya mapenzi

- Mwanamke kutokwa na maji maji ukeni ambayo yana harufu sana

- Mwanamke kutokwa na ute ute ambayo umechanganyika na usaha ukeni

- Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa

- Kupatwa na shida ya blid mara mbili ndani ya mwezi mmoja

- Kupatwa na maumivu makali ya tumbo

- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa

- Kuvimba kwenye eneo la mashavu ya uke 

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

- Kutokwa na usaha sehemu za Siri

- Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

- Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

- Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

- Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa

MADHARA YA UGONJWA WA KISONONO

je kisonono kinaweza kusababisha matatizo gani?

(1) Ikiwa wewe ni Mwanamke, una nafasi kubwa ya kukumbwa na matatizo ya muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kisonono kama hukupata Tiba ukapona,

Magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama vile kisonono na Chlamydia yanaweza kuleta athari kwenye njia ya uzazi na kuathiri maeneo mbali mbali ikiwemo Kizazi chenyewe(Uterus), mirija ya uzazi Pamoja na ovaries.

Hii inaweza kusababisha matatizo mengine kama vile maambukizi ya bacteria kwenye via vya Uzazi vya Mwanamke yaani pelvic inflammatory (PID),

PID inaweza kusababisha maumivu makali, ya muda mrefu na uharibifu wa viungo vya uzazi.

- Kuziba au kupata kovu kwenye mirija ya uzazi,

Na hii huweza kuleta madhara mengine kama vile;

  • kufanya iwe vigumu zaidi Kwa mwanamke kupata mimba
  • kusababisha tatizo la mimba kutunga nje ya Kizazi yaani ectopic pregnancy,
  • Kisonono kinaweza pia kusababisha shida ya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wa kujifungua(Njiti/premature)

(2) Ikiwa wewe ni Mwanaume,Kisonono kinaweza kusababisha:

  • kovu kwenye urethra
  •  Kupata jipu ndani ya uume wako, ambalo linaweza kuathiri uwezo wako wa kutungisha Mimba
  • Kupata tatizo la Epididymitis, au kuvimba kwa mirija ya kubebea shahawa karibu na korodani zako
  • Maambukizi ambayo hayajatibiwa yanaweza pia kuenea kwenye mfumo wako wa damu, ambapo yanaweza kusababisha matatizo adimu kutokea lakini makubwa kama vile ugonjwa wa baridi yabisi(arthritis) pamoja na uharibifu wa valve ndani ya moyo.

MATIBABU YA UGONJWA WA KISONONO

Ni vizuri kwenda hospital kufanyiwa vipimo kwanza kabla ya dawa, Na baada ya hapo kama utagundulika una tatizo hili basi utapata matibabu sahihi kulingana na ugonjwa wako pamoja na hatua ulipofikia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

ENDELEA ZAIDI KUSOMA HAPA CHINI...

MAENEO MENGINE AMBAYO HUSHAMBULIWA ZAIDI NA UGONJWA WA KISONONO PAMOJA NA DALILI ZAKE

Ugonjwa wa Ugonjwa wa Kisonono huathiri Maeneo Yapi? Fahamu Zaidi hapa kwa Kina

Ugonjwa huu wa zinaa hushambulia na kuathiri zaidi maeneo ya mwili yenye joto Pamoja na Unyevu unyevu kama vile;

  •  Kwenye urethra au mrija ambao huvuta mkojo kutoka kwenye kibofu
  • Kwenye macho
  •  Eneo la Kooni
  • Ukeni
  • kwenye Uume
  •  Kwenye njia ya haja kubwa(anus)
  • Kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke ikiwemo Kwenye Kizazi,Mirija ya Uzazi, Pamoja na Mlango wa kizazi yaani cervix n.k

(1) kwenye eneo la Haja kubwa au Rectum. 

Dalili za Ugonjwa wa gono hapa ni Pamoja na;

  • Kuhisi hali ya muwasho kwenye eneo la haja kubwa
  • Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa 
  • Kutokwa na vidamu kwenye eneo la haja kubwa
  • Kupata hali ya mkazo na maumivu eneo hili la Rectum n.k.

(2) Kwenye Macho.

Dalili za Ugonjwa wa Gono hapa ni pamoja na;

  • Macho kuwasha sana
  • Hali ya macho kuogopa mwanga
  • Macho kuuma
  • Kutokwa na Usaha machoni n.k

(3) Kwenye eneo la Kooni au Throat. 

Dalili za Ugonjwa wa gono hapa ni pamoja na;

  • Kuvimba kwa tezi za shingoni yaani swollen lymph nodes
  • Kuhisi hali ya vidonda kooni
  • Koo kuuma n.k

(4) Kwenye Joints.

Dalili za Ugonjwa wa Gono hapa ni pamoja na;

  • Kuhisi hali ya Joto kwenye joints
  • Joints kuvimba
  • Kuhisi maumivu makali kwenye joints hasa wakati wa kutembea,hali hii kwa kitaalam hujulikana kama Septic arthritis.

Muone Daktari Wako Ikiwa;

Ukiona dalili Zozote kama vile kuungua unapokojoa au kutokwa na usaha kwenye uume, uke au Sehemu ya Haja kubwa.

 Pia weka miadi ikiwa mwenzi wako amegunduliwa na ugonjwa wa kisonono.  Huenda usiwe na dalili, lakini ikiwa una maambukizi, unaweza kumwambukiza mpenzi wako tena hata baada ya mpenzi wako kutibiwa kisonono.

Chanzo cha Ugonjwa wa Gono

Kisonono husababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae.  Bakteria hawa wa kisonono mara nyingi hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine wakati wa kujamiiana, ikiwa ni pamoja na kujamiiana kwa njia ya mdomo, mkundu au uke

Sababu Ambazo huongeza hatari ya Kupata Ugonjwa wa Kisonono

1. Wanawake wanaofanya ngono chini ya miaka 25 na wanaume wanaojamiiana na wanaume wako kwenye hatari kubwa ya kupata Ugonjwa wa kisonono.

2. Mambo mengine ambayo yanaweza kuongeza hatari ya Kupata Ugonjwa wa Gono ni pamoja na:

  •  Kuwa na mwenzi mpya ambaye hujui hali yake ya kiafya.
  •  Kuwa na mwenzi ambaye ana wapenzi wengine.
  •  Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja.
  •  Kuwa na Ugonjwa wa kisonono hapo nyuma au maambukizi mengine ya zinaa. n.k

 Madhara ya Ugonjwa wa Kisonono

Ugonjwa wa Kisonono isiotibiwa unaweza kusababisha matatizo makubwa, kama vile:

1. Ugumba kwa wanawake.

 Kisonono kinaweza kusambaa hadi kwenye mfuko wa uzazi na mirija ya uzazi, hivyo kusababisha ugonjwa wa maambukizi ya Bacteria kwenye Via vya uzazi vya mwanamke(PID).  PID inaweza kusababisha makovu kwenye mirija, hatari kubwa ya matatizo ya ujauzito na ugumba.  PID inahitaji matibabu ya haraka. SOMA Zaidi hapa Ugonjwa wa Gono

2. Ugumba kwa wanaume. 

 Kisonono kinaweza kusababisha uvimbe kwenye epididymis, mrija uliojikunja juu na nyuma ya korodani unaohifadhi na kusafirisha manii.  Ugonjwa huu wa kuvimba hujulikana kama epididymitis na bila matibabu unaweza kusababisha utasa.

3. Maambukizi ambayo huenea kwenye viungo na maeneo mengine ya mwili. 

 Bakteria wanaosababisha Ugonjwa wa gono au kisonono wanaweza kuenea kwa njia ya damu na kuambukiza sehemu nyingine za mwili, ikiwa ni pamoja na viungo,joints n.k  Homa, upele, vidonda vya ngozi, maumivu ya pamoja, uvimbe na ugumu ni matokeo yanayoweza kutokea.

 4. Kuongezeka kwa hatari ya kupata VVU/UKIMWI. 

 Kuwa na kisonono kunakufanya uwe rahisi kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU), virusi vinavyoongoza kwa UKIMWI.  Watu ambao wana kisonono na VVU wanaweza kupitisha magonjwa yote kwa wenzi wao kwa urahisi zaidi.

 5. Matatizo kwa watoto wachanga. 

 Watoto wanaopata Ugonjwa wa kisonono wakati wa kuzaliwa wanaweza kupata upofu, vidonda kwenye ngozi ya kichwa na maambukizi mengine kwa Urahisi Zaidi.

 Jinsi ya Kuzuia Ugonjwa wa Kisonono

 Ili kupunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa kisonono,Fanya haya;

 ✓ Tumia kondomu ikiwa unafanya Tendo la Ndoa.

 ✓ Kutokufanya ngono na kuepuka shughuli za ngono ni njia ya uhakika ya kuzuia Ugonjwa wa kisonono. 

 Lakini ukiamua kufanya ngono, tumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa aina yoyote.

 ✓ Epuka tabia ya kuwa na Wapenzi wengi,  Kuwa katika uhusiano na mke mmoja ambapo hakuna mwenzi anafanya ngono na mtu mwingine yeyote kunaweza kupunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa Gono.

✓ Hakikisha wewe na mwenzi wako mmepimwa magonjwa ya zinaa.  Kabla ya kujamiiana,

 ✓ Usifanye ngono na mtu ambaye anaonekana kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kabla ya kutibiwa. Ikiwa mtu ana dalili za maambukizo ya zinaa, kama vile kuungua wakati wa kukojoa au upele au kidonda sehemu za siri, usifanye ngono na mtu huyo.

 ✓ Fikiria uchunguzi wa mara kwa mara dhidi ya Ugonjwa wa kisonono na magonjwa mengine ikiwemo ya Zinaa.

  Uchunguzi wa kila mwaka unapendekezwa kwa wanawake wanaofanya ngono chini ya miaka 25 na kwa wanawake wakubwa walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa.  Hii ni pamoja na wanawake walio na wapenzi wapya, zaidi ya mwenzi mmoja au wenzi ambao wana magonjwa ya zinaa.

 Uchunguzi wa mara kwa mara pia unapendekezwa kwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume.  Washirika wao pia wanapaswa kupimwa.

KWA USHAURI ZAIDI NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mama mjamzito anatakiwa alale vipiAfyaclass Bongo Social •

Mama mjamzito anatakiwa alale vipi

Staili za kulala kwa mama mjamzito,Soma hapa kufahamu

Inaweza isiwe mara ya kwanza kwako kusikia kwamba,si kila staili ya kulala ni nzuri kwa mama mjamzito,

huenda ukawa umesikia mama mjamzito akilala sana chali atagandamiza mshipa mkubwa wa damu uonapita eneo la mgongoni na kusababisha mzunguko mbaya wa damu, mtoto kukosa hewa,chakula na hata kupoteza maisha.

Ni kweli kabsa sio kila staili ya kulala ni nzuri na salama kwa mama mjamzito, na Leo tunakuchambulia baadhi ya staili za kulala kwa mama mjamzito;

Staili za kulala kwa mama mjamzito

✓ Ulale ubavu wa Kushoto Au Kulia?

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.

Ukweli ni kwamba, Kulala upande wa kushoto wakati wa ujauzito huwezesha mtiririko mzuri wa damu na kuhakikisha kwamba viungo muhimu na mtoto hupokea virutubisho na oksijeni.

Sleeping on the left side during pregnancy facilitates blood flow, ensuring that vital organs and the baby receive the nutrients and oxygen. 

Pengine wajiuliza namna gani sahihi ya kulala kwa mjamzito? Wakati wa ujauzito madaktari wanapendekeza zaidi ulae kwa ubavu hasa kama mimba yako imeshakuwa kubwa. Hii ni kwasababu ya kuepuka kubonyeza mshipa mkubwa wa damu na kuzuia mtiririko mzuri wa damu inayozunguka kuelekea kwenye kizazi.

Kulala Kwa Ubavu wa Kushoto

Kulala kwa ubavu wa kushoto ni mkao sahihi zaidi kwa mama mjamzito ikilinganishwa na staili zingine za kulala kwa mjamzito. Kwasababu mkao huu unaruhusu mzunguko mzuri wa damu kutoka kwenye moyo wa mama kuelekea kwa mtoto.

Kulala kwa ubavu wa kushoto pia kunapunguza mgandamizo kwenye ini na figo. Hii itasaidia kupunguza kuvimba kwa vidole vya mikono , miguu na kwenye enka.

Je ni kweli Kulala Upande flani Ni kigezo cha Jinsia ya Mtoto?

Unaweza kuwa umesikia tetesi kwamba mwanamke akipenda kulalia upande flani basi ni jinsia fulani ya mtoto. Hii ni tetesi tu haina ukweli wowote. Hakuna utafiti wowote unaoonesha ukweli wa jambo hili.

Miezi Mitatu Ya Kwanza Ya Ujauzito(First Trimester)

Kipindi hiki unaruhusiwa kulala kwa namna yoyote, aidha kwa ubavu wa kushoto, kulia, kulalia tumbo au hata mgongo. Lakini kama unataka kujizoesha mapema kwa ajili ya baadae basi anza kulala kwa kuweka mto katikati ya miguu yako. Hii itakusaidia ufurahie usingizi na usipate kashkashi zozote.

Miezi Mitatu Ya katikati ya ujauzito(Second trimester)

Kadiri tumbo linavoongezeka utahitaji kupata godoro imara ambalo halibonyei sana kujizuia mgongo kujikunja sana unapolala. Endelea kutumia mto katikati ya miguu.

Miezi mitatu ya mwisho(Third trimester)

Endelea kutumia mto kukupa sapoti katika miezi hii ya mwisho kuelekea kujifungua. Katika kipindi hiki pendelea zaidi kulala kwa ubavu wa kushoto. Na mara chache lala kwa ubavu wa kulia, hakikisha pia unaweka mto mwingine eneo la kichwa liwe juu kidogo.

✓ Kulala Chali je ni Sahihi na Salama?

Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi. Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.

Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao hufariki dunia. Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto kufariki wanaozaliwa katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

✓ Kulala kwa Tumbo ni Salama?

Pengine umekuwa ukijiuliza vipi naweza kulala kwa tumbo nikiwa na mimba na isilete madhara yoyote? Jibu ni ndio unaweza kulala kwa tumbo kwa week 16 za kwanza za mimba. Kadiri mimba inavokuwa kubwa wewe mwenyewe itakushinda kulala na tumbo na itabidi ubadili mkao.

Usiwe na hofu kwamba mimba itaharibika pengine ikitokea kwa bahati mbaya umelala na tumbo. Mtoto analindwa na majimaji ya amniotic fluid kwenye chupa yake.

✓ Kulala kwa Mgongo

Kulala kwa mgongo ni salama ukiwa kwenye miezi mitatu ya mwanzo. Baada ya hapo kulala kwa mgongo itakuwa siyo salama kwani itasababisha upate matatizo ya maumivu chini ya mgongo, bawasili, matatizo ya tumbo na pia damu kutozunguka vizuri inavotakiwa.

Ikitokea mara chache usiku ukajisahau na kulala kwa mgongo basi usiwe na hofu badilisha tu mkao na maisha yaendelee vizuri mpaka ukishajifungua.

Ni matumaini yangu umejifunza na kuelewa vizuri kuhusu Staili za kulala kwa mama mjamzito.... Mungu akujalie Uzazi Salama, na Ujifungue salama katika Safari hii....!!!!!!!

1 Comment

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na nini,Chanzo,Aina,Dalili pamoja na TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na nini,Chanzo,Aina,Dalili pamoja na Tiba

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao huhusisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko kawaida au kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari kwenye damu kuliko kawaida.

Hivo hapa tunapata aina mbili za kisukari;

(i) Kisukari cha kupanda au kwa kitaalam tunaita Hyperglycemia

(ii) Na kisukari cha kushuka au kwa kitaalam tunaita Hypoglycemia

Katika Makala hii tutazungumzia zaidi kuhusu kisukari cha kupanda,hivo kila tutakapozungumzia Ugonjwa wa Kisukari kwenye Makala hii tunazungumzia Sukari ya kupanda.

Ugonjwa wa Kisukari

Ugonjwa wa kisukari- huu ni ugonjwa ambao hutokea wakati sukari yako kwenye damu (glucose) iko juu sana.  Na mara nyingi hutokea wakati;
  1. kongosho lako likishindwa kutengeneza insulini ya kutosha
  2.  au Kongosho kutokutengeneza Insulini kabisa,
  3.  au hutokea wakati mwili wako haujibu matokeo ya utendaji kazi wa Insulini ipasavyo. 
Ugonjwa wa kisukari huathiri watu wa umri wowote.  Aina nyingi za ugonjwa wa kisukari ni sugu, na aina zote zinaweza kudhibitiwa kwa dawa pamoja na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Fahamu Kwa Asilimia kubwa Glukosi (sukari) hasa hutoka kwenye wanga au carbohydrates katika vyakula unavyokula na vinywaji unavyokunywa.  Ni chanzo cha nishati kwa mwili wako.  Damu yako hubeba glukosi hadi kwenye seli zote za mwili wako ili kutumia kwa ajili ya nishati.

Glucose inapokuwa kwenye mfumo wako wa damu, inahitaji usaidizi "au ufunguo" - ili kufikia lengo la mwisho.  Ufunguo huu ni insulini (homoni).  Ikiwa kongosho yako haitengenezi insulini ya kutosha au mwili wako hauitumii ipasavyo, glukosi hujilimbikiza kwenye damu yako, na kusababisha sukari kuwa juu kwenye damu (hyperglycemia).

Baada ya Muda, kuwa na kiwango cha juu cha Sukari kwenye damu mfululizo kunaweza kusababisha shida za kiafya, kama vile ugonjwa wa moyo, uharibifu wa neva na shida za macho.


Aina za Ugonjwa wa Kisukari

Kuna aina kadhaa za Ugonjwa wa kisukari. Tunapozungumzia Sukari ya kupanda kuna aina kadhaa ikiwemo:
  1. Kisukari aina ya kwanza(Type 1 diabetes)
  2. Kisukari aina ya Pili(Type 2 diabetes)
  3. Kisukari cha Mimba(Gestational diabetes)
  4. Pamoja na aina Zingine kadhaa ambazo watu wengi hawazizungumzii kabsa ila zipo,mfano; Tuna; Type 3 diabetes,Latent autoimmune diabetes in adults (LADA),Maturity-onset diabetes,Neonatal diabetes n.k

1. Kisukari aina ya Kwanza(Type 1 diabetes)

Aina hii ya Ugonjwa huhusisha kongosho au Pancrease kutokuzalisha na kutoa Insulin kabisa.
Hapa kongosho haitengenezi Insulini kabsa, kwa sababu mfumo wa kinga ya mwili hushambulia seli za kongosho zinazotengeneza insulini.

Aina hii ya 1 ya kisukari kwa Kawaida hugunduliwa kwa watoto na vijana, lakini inaweza kutokea katika umri wowote pia.


2. Kisukari Aina ya Pili(Type 2 diabetes)

Kwa aina hii, mwili wako hautengenezi insulini ya kutosha au seli za mwili wako hazitumii vizuri ipasavyo insulini iliyopo.  Hii ndiyo aina ya Ugonjwa wa kisukari ambao huwapata Watu Wengi Zaidi. Na  Inaathiri zaidi watu wazima, lakini watoto wanaweza kuwa nayo pia.

Katika aina ya 2 ya kisukari, kongosho hutengeneza insulini kidogo kuliko ilivyokuwa hapo awali, na mwili wako unatengeneza ukinzani dhidi ya insulini ndogo iliyopo.

3. Kisukari cha Mimba(Gestational diabetes): 

Aina hii ya kisukari inatokea wakati wa ujauzito, na kawaida hupotea baada ya ujauzito au baada ya kujifungua.  Ingawa baadhi ya tafiti zinaonyesha ikiwa una kisukari wakati wa ujauzito, uko katika hatari kubwa ya kupata kisukari cha Aina ya 2 baadaye maishani.

Dalili Za Ugonjwa wa kisukari

Ukali wa dalili unaweza kutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa wa kisukari uliyo nao.  Dalili hizi kawaida huwa kali zaidi katika aina ya 1 ya kisukari kuliko kisukari cha Aina ya 2.

 Dalili za kisukari kwa Ujumla ni zipi?

 Dalili za ugonjwa wa kisukari ni pamoja na:
  • Kuongezeka kwa kiu na kinywa kuwa kikavu zaidi.
  • Kukojoa mara kwa mara.
  • Kupata sana Uchovu wa mwili
  • Macho kutokuona vizuri au kuona marue rue
  • Kupunguza Uzito kwa kasi bila Sababu inayoeleweka, 
  • Mtu kukonda
  • Kupata Ganzi au hali ya kuchoma choma katika mikono au miguu yako.
  • Vidonda kuponya polepole au kuchelewa zaidi kupona
  • Kuwa kwenye hatari ya kupata Maambukizi ya mara kwa mara ya ngozi, Maambukizi ya Fangasi ukeni n.k
 Ni muhimu kuzungumza na mtoa huduma wako wa afya ikiwa wewe au mtoto wako ana dalili hizi. 

Ugonjwa wa Kisukari husababishwa na nini?

Uwepo wa Glucose nyingi inayozunguka katika mfumo wako wa damu husababisha ugonjwa wa kisukari, bila kujali aina.  Ingawa, sababu kwa nini viwango vya sukari kwenye damu yako ni vikubwa hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa wa kisukari. 

Hizi hapa ni Sababu mbali mbali zinazochangia hali hiyo:

- Tatizo la Insulin resistance: 

Aina ya 2 ya kisukari hutokana hasa na ukinzani wa insulini.  Ukinzani huu wa insulini hutokea wakati seli kwenye misuli, mafuta na ini hazitoi matokeo inavyopaswa dhidi ya insulini. 

Sababu na hali kadhaa huchangia viwango tofauti vya ukinzani wa insulini, Sababu hizo ni pamoja na;
  • Uzito mkubwa au kunenepa kupita kiasi, 
  • Kutokufanya Mazoezi ya mwili
  • Mabadiliko ya Vichocheo au homoni mwilini
  • Swala la kimaumbile au Genetics factor
  • Matumizi ya baadhi ya dawa fulani.n.k
- Tatizo kwenye Mfumo wa kinga mwili(Autoimmune disease):

Kisukari aina ya kwanza(Type 1 diabetes) pamoja na Latent autoimmune diabetes in adults (LADA) ambapo nilitaja aina hii hapo awali, hutokea wakati mfumo wako wa kinga unaposhambulia seli zinazozalisha insulini kwenye kongosho lako.

- Tatizo la Hormonal imbalances:

Wakati wa Ujauzito, placenta huweza kutoa homoni zinazosababisha ukinzani wa insulini.  Unaweza kupata kisukari wakati wa ujauzito ikiwa kongosho yako haiwezi kutoa insulini ya kutosha kushinda ukinzani wa insulini uliojitokeza.  Hali nyingine zinazohusiana na homoni kama vile tatizo la akromegali pia zinaweza kusababisha kisukari cha Aina ya 2.

- Uharibifu wa kongosho(Pancreatic damage): 

Uharibifu wa kongosho lako - kutokana na hali kama vile ajali, upasuaji au jeraha - unaweza kuathiri uwezo wake wa kutengeneza insulini, na kusababisha ugonjwa wa kisukari hasa Aina ya 3 ya kisukari(Type 3 diabetes).

- Matatizo ya kimaumbile au kigenetic(Genetic mutations):

Mabadiliko fulani ya kijenetic yanaweza kusababisha Ugonjwa wa kisukari hasa kuanzia kwa watoto wachanga,aina hii ya kisukari hufahamika kama neonatal diabetes.

- Utumiaji wa muda mrefu wa baadhi ya dawa:

Unachotakiwa kufahamu matumizi pia ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu sana yanaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari hasa Aina ya 2, Dawa hizo ni pamoja na dawa jamii ya corticosteroids..n.k.

Madhara ya Ugonjwa wa Kisukari

Yapo madhara mbali mbali ambayo unaweza kuyapata hasa ikiwa Ugonjwa huu wa kisukari umekuwa wa muda mrefu, Madhara hayo ni pamoja na; 
  • Kupata tatizo la Macho kutokuona 
  • Kupata Magonjwa au matatizo mbali mbali ya moyo kama vile;Coronary artery disease,Shambilio la moyo(Heart attack),kiharusi au Stroke.n.k.
  • Kupata Uharibifu wa Neva,Nerve damage au neuropathy ambapo matokeo yake huleta dalili kama vile, kupata ganzi,kuhisi hali ya kuchoma choma mwilini,maumivu n.k
  • Kukatwa viungo mbali mbali vya mwili kama vile Miguu,vidole n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

Kutokwa na uchafu wa njano ukeni,chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Kutokwa na uchafu wa njano ukeni,chanzo na Tiba

Si kila Wakati kutokwa na Uchafu wa Njano ukeni ni tatizo,


Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni wakati mwingine inaweza kuwa ishara kwamba hedhi yako inakuja au kuashiria ujauzito katika hatua za mwanzo kabsa.  Pia hali hii inaweza kutokea kutokana na kazi za asili za Ukeni. 

KUMBUKA; Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni ni kawaida ikiwa Uchafu huo ni mweupe, mwepesi, na hauna harufu yoyote. Ingawa pia unaweza kuanza kutoka ukiwa mzito na kubadilika kuwa mwepesi kadri siku zinavyoenda. Pia unaweza kuwa na rangi ya manjano nyepesi na bado ukuwa wa kawaida kabisa.


Kwanini Aina hii ya Uchafu huweza kutoka Ukeni ukiwa karibu na Period yako au Ukiwa na Mimba?

Kipindi cha Hedhi;

Kutokwa na uchafu ukeni kunaweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya homoni. Katika sehemu ya katikati ya mzunguko wako wa hedhi, ujazo wa majimaji ya ukeni utaongezeka na kuwa mithili ya Ute kama wa yai.  Hata hivyo, uchafu huo unapogusana na hewa, unaweza kupitia mchakato unaoitwa oxidation unaosababisha kugeuka rangi ya krimu, mawingu au njano hafifu, Rangi hizi zote ni za kawaida kabisa. 

Kipindi cha Mwanzo wa Ujauzito;

Kuongezeka kwa Uchafu kutoka ukeni inaweza kuwa ishara ya mapema ya ujauzito.  Wakati wa ujauzito, mwili hujiandaa kwa kulainisha shingo ya kizazi au Cervix pamoja na kuta za uke.  Ili kuzuia maambukizo kufika kwenye uterasi, mwili hutoa uchafu mwingi zaidi.

 Utoaji huu wa Uchafu ni wa kawaida na Mara nyingi huwa na rangi nyeupe.  Hata hivyo, Unaweza pia kugeuka kuwa njano unapogusana na hewa, kama vile unapobakia katika nguo ya ndani kwa muda mrefu.

Kutokwa na Uchafu wa Njano Ukeni kama kiashiria cha Ugonjwa

Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni kunaweza kuonyesha kuwa una maambukizi ya magonjwa ya zinaa-Sexual transimmited diseases (STDs) au hali zingine zinazohitaji matibabu.  Hii ni kweli hasa ikiwa Uchafu huu unatoka ukiwa na rangi nyeusi,kijani kibichi, au njano pamoja na harufu mbaya.

 Ni muhimu kuonana na mhudumu wa afya kwa kutokwa na uchafu wowote usio wa kawaida ukeni.  Mbali na kuwa ishara kwamba unaweza kuhitaji huduma ya matibabu, unaweza kuwa katika hatari ya kupitisha maambukizi kwa mpenzi wako ikiwa mtafanya tendo, na hivo nyinyi wawili mnaweza kuhitaji matibabu.


Uchafu wa njano Usio wakawaida(Abnormal Yellow Discharge)

Kuna hali nyingine ambapo kutokwa na Uchfu ukeni wa njano sio kawaida.  Katika hali kama hizi, mabadiliko ya rangi mara nyingi yatakuwa ya kina zaidi, na kunaweza pia kuwa na hali Zingine zisizo zakawaida kama vile kuwa na harufu mbaya n.k. 

Unaweza kupata dalili zingine ikiwa kutokwa na Uchafu huu ni Ishara ya shida ya kiafya.

Chanzo cha Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni

Haya ni Baadhi ya Magonjwa Pamoja na Hali za kiafya ambazo huweza kusababisha tatizo la Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni;

1. Tatizo la Vaginitis

"Vaginitis" ni neno linalotumiwa kuelezea idadi ya hali ambazo zinaweza kusababisha kuvimba katika uke.  Hali Hizi zinaweza kujumuisha maambukizi yanayotokana na bakteria, virusi, au Fangasi.

Katika baadhi ya matukio, tatizo hili linaweza kusababishwa na athari ya mzio kwa bidhaa kama vile dawa za kupuliza ukeni, douchi, dawa za kuua manii, baadhi ya sabuni n.k

Matumizi ya baadhi ya dawa fulani pia yanaweza kusababisha tatizo la vaginitis. dawa hizi ni pamoja na baadhi ya dawa jamii ya antibiotics na corticosteroids.

Dalili za tatizo hili la Vaginitis ni pamoja na;

  • Kutokwa na UChafu usio wa kawaida Ukeni ambao unaweza kuwa wa rangi ya njano au kijani
  •  Kutokwa na UChafu usio wa kawaida ambao una harufu mbaya
  •  Kupata Maumivu wakati wa kujamiiana
  •  Kuhisi hali ya Kuungua ukeni au wakati wa kukojoa
  •  Kupata Muwasho ukeni
  •  Kutokwa na damu ukeni wakati au baada ya kujamiiana
  •  Kuwasha nje ya uke n.k

2. Tatizo la Trichomoniasis

Trichomoniasis ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na vimelea au parasite.  Ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyo ya virusi yanayoenea zaidi duniani. 

Ugonjwa huu wa Trikomoniasis hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS

 Unaweza kuwa na trichomoniasis bila kujua kwa sababu maambukizi hayasababishi dalili kila wakati.

 Ila Wakati kuna dalili, trichomoniasis inaweza kusababisha kutokwa na Uchafu ukeni ambayo ni:
  • Mwepesi
  • Kama povu
  • Mweupe,chanjo au kijani
  • Wenye harufu mbaya n.k


3. Magonjwa mengine ya Zinaa ni Chlamydia pamoja na Kisonono

Klamidia na kisonono ni magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na bakteria tofauti.

Magonjwa haya mawili ya zinaa yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni ambayo ni:
  • Mweupe, njano au kijani
  • Wenye harufu mbaya
  •  Unaweza pia kupata maumivu chini ya tumbo au kitovu 
  • na maumivu au hali ya kuhisi kuungua wakati wa kukojoa.
 Klamidia na kisonono vote hutibiwa kwa dawa jamii ya antibiotics. 


4. Ugonjwa wa PID-Pelvic Inflammatory Disease

Pelvic inflammatory disease (PID) ni maambukizi ya bacteria kwenye via vya Uzazi vya Mwanamke, 
Via hizo vya Uzazi ni pamoja na;Kizazi chenyewe(uterus),mirija ya uzazi yaani fallopian tubes pamoja na vifuko vya mayai au ovaries.

Dalili za Ugonjwa wa PID ni pamoja na;

  • Kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya kijani,njano n.k
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu mbaya
  • Kupata Homa
  • Kupata Maumivu ya chini ya tumbo
  • Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi
  •  Kuhisi hali ya Kuungua wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana
  • Kupata Maumivu wakati wa tendo n.k

5. Tatizo la kuvimba Mlango wa kizazi-Cervicitis

Cervicitis ni tatizo la kuvimba kwa mlango wa kizazi au Cervix.  Hali hii Inaweza kusababishwa na maambukizi kama vile ya chlamydia, kisonono, pamoja na genital herpes. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ni matokeo ya sababu zisizo za kuambukiza kama vile ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya kingamwili, na vifaa vinavyowekwa ndani ya uke kama vile IUDs n.k

Mara nyingi tatizo hili halisababishi dalili yoyote wakati wote kwa Nje.  Ila Inapotokea, kunaweza kuwa na kutokwa kwa uchafu unaoendelea, usio wa kawaida ambao ni:
  • Mweupe,Njano au kijani
  • Wenye harufu mbaya n.k

6. Tatizo la Bacterial Vaginosis

Bacterial Vaginosis ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria ukeni, na kwa asilimia kubwa hutokana na kuongezeka kwa bakteria wa kawaida kwenye uke(overgrowth) ambao huvuruga usawa wa asili Ukeni au kukosekana kwa uwiano kati ya bacteria wabaya na wale bacteria wazuri waliopo ukeni.

Tatizo hili linaweza kusababisha kutokwa na majimaji ya njano ukeni na dalili zingine zinazohusiana na kutokwa na uchafu usio wa kawaida kama vile:
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu kali kama shombo la Samaki
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wa rangi ya kijani, n.k
Hizo ni baadhi ya Sababu za Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni.


Bonus Tips; Nikupe Vidokezo Muhimu juu ya Vitu vya kuzingatia ili kujikinga na Tatizo hili la kutokwa na Uchafu wa njano Ukeni;

- Jikinge na Magonjwa yote ya Zinaa

- Epuka matumizi ya vifaa vya kuingiza ukeni maarufu kama douchi

- Epuka kutumia dawa za kuua Manii

- Hakikisha Usafi mzuri wa Sehemu zako za Siri ikiwa ni pamoja na nguo zako za ndani,kubadilisha PEDI kwa wakati kama upo kwenye hedhi n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

Mama mjamzito kutokwa na damu,chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Mama mjamzito kutokwa na damu 


Mama mjamzito kutokwa na Damu Ukeni ni hali ambayo inawapata wanawake wengi wakiwa wajawazito, na Sio mara Zote inamaanisha kuna tatizo kubwa la kiafya. Leo tunachambua Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii ya kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito kwa wakina Mama wengi.


Chanzo cha Mama mjamzito kutokwa na Damu

Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili,Sababu hizo ni pamoja na;

1. Damu Inayotoka wakati wa kiinitete(embro) kujishikiza kwenye Ukuta wa Mji wa Mimba kwa kitaalam hujulikana kama Implantation bleeding

Baada ya Yai kufanikiwa kurutubishwa na Mbegu ya Kiume,ndipo tunasema una mimba na Safari yako huweza kuanzia hapo,

Baada ya Urutubishaji huu,kiinitete kinachokua lazima kijishikize kwenye Ukuta wa mji wa mimba,kwa kitaalam mchakato huu hujulikana kama Implantation.

Katika hatua za awali za ujauzito,unaweza kupata hali ya kutokwa na damu nyepesi isiyo na madhara, inayojulikana kama "Light spotting".  Huu ndio wakati kiinitete kinachokua kinajipandikiza na kujishikiza kwenye ukuta wa tumbo lako la uzazi.

Katika kipindi hiki,baadhi ya Wanawake hutokwa na Damu nyepesi au matone matone ya Damu.

Aina hii ya kutokwa na damu mara nyingi hutokea wakati ule ule wa kipindi cha hedhi yako kutoka Unapofika., Hili sio tatizo bali ni hali ya kawaida kabsa.

2. Mabadiliko kwenye mlango wa kizazi(Cervical changes)

Mimba inaweza kusababisha mabadiliko kwenye mlango wa kizazi au Cervix, na hii inaweza wakati mwingine kusababisha damu kutoka- hasa baada ya tendo la ndoa,


 3. Sababu nyingine ni Kuharibika kwa mimba au mimba kutunga nje ya kizazi(hapa nazungumzia Miscarriage or Ectopic pregnancy)

 Wakati wa wiki 12 za kwanza za ujauzito, kutokwa na damu ukeni kunaweza kuwa ishara ya kuharibika kwa mimba au mimba kutunga nje ya kizazi,

Na Ikiwa unatoka damu katika hatua hii ya ujauzito na mimba ikatoka kwa bahati mbaya, hakuna sababu ya wewe usiendelee kutafuta Ujauzito mwingine kama huna tatizo lolote lingine. Ingawa ni muhimu sana kufahamu chanzo husika cha tatizo lako ili kama linahitaji Tiba upate Tiba mapema na kukaa Sawa kabla ya kutafuta tena ujauzito mwingine.


Mimba kutoka au kutishia kutoka;

Mbali na Damu kutoka Ukeni,Unaweza kupata dalili zingine kama Mimba inatishia kutoka au inatoka, dalili hizo ni kama vile;
  • kupata maumivu makali kwenye tumbo au chini ya kitovu
  •  kutokwa na Uchafu au majimaji ukeni
  •  kutoka kwa tishu au vitu kama nyama Ukeni
  •  kutopata tena dalili za ujauzito
 Ikiwa unavuja damu au unapata dalili zozote kati ya hizi, wasiliana na Wataalam wa afya Mara moja. au Kwa Ushauri Zaidi,elimu na Tiba tuwasiliane hapa hapa afyaclass kupitia namba +255758286584.


Vipi Kwa Upande wa Mimba kutunga Nje ya Kizazi?

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi mara nyingi huanza kuonekana kati ya wiki 6 hadi 8 za ujauzito lakini zinaweza kutokea baadaye pia.

Mbali na Damu kutoka Ukeni,Unaweza kupata dalili zingine kama Mimba imetunga nje ya Kizazi,dalili hizo ni pamoja na;
  • Kupata Maumivu chini ya tumbo ambayo yanaweza kuwa upande mmoja
  •  kutokwa na damu ukeni au kutokwa na maji ya kahawia
  •  Kupata Maumivu katika ncha ya bega lako n.k
4. Tatizo la Placental abruption

Hii ni hali mbaya ambayo placenta au kondo la nyuma huanza kutoka kwenye ukuta wa tumbo la Uzazi.  Kuachia kwa plasenta huweza kusababisha maumivu ya tumbo, na hii inaweza kutokea hata ikiwa hakuna damu.

Lakini pia tatizo hili huweza kusababisha Damu kutoka Ukeni.

5. Tatizo la Low-lying placenta au (placenta praevia)

Hili ni tatizo lingine ambalo huweza kusababisha mama mjamzito kutokwa na damu ukeni,

Huu ndio wakati plasenta inaposhika katika sehemu ya chini ya uterasi, karibu na au kufunika Cervix.  Damu inayotoka kwenye placenta hii iliyoshika sehemu ya chini inaweza kuwa nzito sana, na kukuweka wewe na mtoto wako katika hatari zaidi.


Hitimisho;

Hizo ndyo baadhi ya Sababu ambazo huweza kusababisha Mama mjamzito kutokwa na Damu Ukeni,

Je,Unaona Dalili hii ya kutokwa na Damu ukeni na hujui cha kufanya?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

Tatizo la Fibroids,Chanzo,Dalili na Tiba YakeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la Fibroids,Chanzo,Dalili na Tiba Yake

Fibroids ni ugonjwa gani

Fibroids, ambapo pia huitwa myoma, ni uvimbe usio wa saratani (benign) unaokua katika au kwenye kuta za kizazi (uterus) cha mwanamke,

Hivo basi, Fibroids ni uvimbe unaoweza kutokea kwenye Kizazi lakini sio Saratani.

Uvimbe huu unaweza kuwa wa ukubwa tofauti, kutoka kwa udogo usioonekana kwa macho hadi kwa ukubwa unaoweza kusababisha kizazi kubadilika umbo na ukubwa.

Chanzo cha Fibroids

Chanzo halisi cha fibroids hakijulikani, lakini kuna visababishi kadhaa vinavyohusishwa na ukuaji wa fibroids, ikiwa ni pamoja na:

– Mabadiliko ya homoni:

Homoni za estrogen na progesterone, zinazochochea ukuta wa kizazi kukua kila mwezi kama sehemu ya mzunguko wa hedhi, pia zinaaminika kuchochea ukuaji wa fibroids.

– Sababu za kijenetiki:

Fibroids inaweza kurithiwa katika familia.

– Sababu zingine:

Kama vile uzito wa mwili ulio juu(kuwa na uzito mkubwa/overweight), upungufu wa vitamini D, na matumizi ya pombe, pia yamehusishwa na ukuaji wa fibroids.

Dalili za Fibroids

Baadhi ya wanawake wenye fibroids hawapati dalili zozote, huku wengine wakikumbwa na dalili zifuatazo:

  • Kupata Menstruation au damu ya hedhi nzito au kwa muda mrefu zaidi ya kawaida
  • Kupata Maumivu,shinikizo au hali ya mkazo katika pelvis
  • Kupata Maumivu wakati wa kujamiiana
  • Kukojoa Mara kwa mara au kupata hisia za haraka za kukojoa
  • Kupata choo kigumu au kukosa choo Constipation
  • Kupata Maumivu ya miguu
  • au kupata maumivu chini ya mgongo n.k

Hakikisha unawahi hospital ikiwa unapata dalili hizi;(See your doctor if you have:)

1. Maumivu ya Pelvic hayaishi licha ya kutumia dawa za kuyatuliza

2. Unapata damu ya Hedhi nzito au maumivu makali ambayo hukusababisha hata ushindwe kufanya chochote

3. Unapata damu vitone vitone kila mara au unapata hedhi katikati ya mwezi

4. Ukikojoa mkojo haushi

5. Unapata uchovu ambao hauishi, na mwili kuwa dhaifu au kukosa nguvu kabsa,

dalili hizi huweza kuashiria pia tatizo lingine la Upungufu wa damu(anemia) ambalo unaweza kuwa nalo kutokana na kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu.


Madhara ya Fibroids(Complications)

Mara nyingi Tatizo la Uterine fibroids sio hatari sana kwa afya yako. Ingawa huweza kuleta maumivu na kusababisha madhara zaidi hasa usipopata matibabu.

Moja ya madhara ni kusababisha shida ya kushuka kwa seli nyekundu za damu(Red blood cells-RBCs) au kusababisha tatizo la Upungufu wa damu(anemia)

Hali hiyo inaweza kusababisha uchovu kutokana na kupoteza damu nyingi. Ikiwa unavuja damu nyingi wakati wa kipindi chako cha Hedhi, daktari wako anaweza kukuambia kuhusu kupata zaidi madini chuma(iron supplement) ili kuzuia au kusaidia kudhibiti upungufu wa damu mwilini. Wakati mwingine, mtu mwenye upungufu wa damu anahitaji kupewa damu kutoka kwa watu wengine(Blood transfusion), kutokana na kupoteza damu nyingi.

Utambuzi wa Fibroids

Fibroids mara nyingi hugundulika wakati wa uchunguzi wa kawaida wa pelvic. Vipimo vya ziada kama ultrasound ya pelvic, MRI, na aina nyingine za uchunguzi zinaweza kufanywa kuthibitisha uwepo na ukubwa wa fibroids.

Matibabu ya Fibroids

Matibabu ya fibroids hutegemea ukubwa wa fibroids, dalili, umri, afya ya jumla ya mwanamke, na kama anataka kuzaa siku za usoni.n.k

Matibabu yanaweza kujumuisha:

✓ Udhibiti wa dalili: Dawa za kutuliza maumivu na dawa za homoni kudhibiti dalili zingine huweza kutumika

✓ Njia za upasuaji: Kama vile myomectomy kwa kuondoa fibroids, au hysterectomy kwa kuondoa kizazi kizima (chaguo la mwisho, hasa kwa wanawake ambao hawataki kuzaa tena).

✓ Tiba zisizo za upasuaji: Kama vile utaratibu wa embolization ya artery ndani ya kizazi au uterine, ambayo inapunguza damu inayotiririka kwenye fibroid, na kusababisha ipungue ukubwa.n.k

Kwa wanawake wengi, fibroids si hatari na zinaweza kudhibitiwa na matibabu yanayolenga kupunguza dalili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Fibroids ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi , kwa lugha ya kawaida, Fibroids maana yake ni uvimbe wa msuli wa kifuko cha uzazi. Uvimbe huu unaweza kuwa na ukubwa tofauti kuanzia kama punje ya harage mpaka ukubwa wa nazi. Wakati mwingine unaweza kudhani ni ujauzito!

Sio kila mwenye fibroids anakuwa na matatizo kiafya. Zinaweza kuwepo miaka mingi bila matatizo yoyote. Hata hivyo inashauriwa kila mwenye fibroids awe anapimwa na daktari angalau mara moja kwa mwaka ili kuona jinsi zinavyoendelea na kuhakikisha kuwa hazikui kwa kasi au kuhatarisha kuwa kansa.

Kwa wale zinaowaletea matatizo, fibroids husababisha kutokwa na damu nyingi za hedhi, maumivu ya tumbo, mimba kuharibika zikiwa changa, kuzaa watoto njiti na fibroid kukandamiza viungo vingine kama kibofu cha mkojo na kusababisha kukojoa mara kwa mara au matatizo ya haja kubwa.

Njia ya kugundua uwepo wa fibroid ni kupimwa na daktari na kufanyiwa ultrasound.

Matibabu yake yapo ya aina kuu tatu:

1. Kunywa dawa. Hata hivyo dawa zilizopo sasa hazina matokeo mazuri kuondoa fibroids ila husaidia kupunguza ukuaji wake.

2. Kuiondoa fibroid kwa operation. Ziko aina nyingi za operation kupitia kwenye tumbo au kupitia ndani ya kifuko cha uzazi. Aina ya operation hutegemea mahali ilipo fibroid.

3. Kuondoa kifuko cha uzazi. Njia hii huwafaa wale ambao hawana mpango wa kupata mtoto.

Kuna nadharia mbalimbali juu ya vitu vinavyosababisha fibroids lakini hakuna kitu kilichothibitika moja kwa moja kuwa chanzo cha fibroids. Kwa wale wenye uzito mkubwa inashauriwa kupunguza mwili kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata fibroids.

Zipo tafiti zinazoonyesha kuwa matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango vinapunguza uwezekano wa kupata fibroids.

0 Comment

Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania aitwae Grace Mapunda amefariki dunia Afyaclass Bongo Social •

Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania aitwae Grace Mapunda amefariki dunia 

Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania aitwae Grace Mapunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Aziz Ahmed ambaye ni Muongozaji wa Tamthilia ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu kwa muda mrefu “Ni kweli amefariki usiku wa kuamkia leo Mwananyamala Hospitali, alikuwa anasumbuliwa na nimonia”

“Hajaumwa muda mrefu aliletwa Hospitali juzi kisha jana tukaja kumuona ila usiku wa kuamkia leo ndio hivyo tena, msiba upo nyumbani kwake Sinza Vatcan” —— #MillardAyoUPDATES #RIPGraceMapunda #TutaonanaBaadae

Tasnia ya Uigizaji nchini imepata pigo kubwa baada Muigizaji mashuhuri na mkongwe Tanzania @grace_mapundal  kufariki Dunia asubuhi ya kuamkia leo.

Grace atakumbukwa kutokana na uhodari wake katika sanaa ya Uigizaji kwa kuuvaa uhusika katika filamu zake nyingi alizowahi kucheza na katika miaka ya hivi karibuni alipata kuigiza kama "Tessa" kwenye tamthilia ya 'Huba' 

GRACE MAPUNDA NI NANI?

Grace Mapunda (maarufu kama Mama Kawele) ni mwigizaji wa filamu za Tanzania (Swahiliwood), anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza filamu za hisia na hii ni kutokana na kuwa makini katika kuwakilisha uhusika halisi japo anaonekana kuzipatia filamu za aina hiyo.[1]

Grace Mapunda amebarikiwa kuwa na watoto wawili (Happiness pamoja na Ritha) ambao baba yao alifariki siku za nyuma. Happiness huiigiza na kuimba, aliwahi kuigiza na mama yake katika filamu ya Fake Smile. Ritha naye ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.[2]

Filamu alizoigiza ni pamoja na House of death, hard price, nilindiwe, Kichupa, Majuto, Mwaka wa Hasara, chloroquine love, Chungu ya Nafsi, poor Minds, Jibu la ndoto, Back to life na zingine nyingi[3]

Via;Wikipedia; https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Grace_Mapunda#:~:text=Grace%20Mapunda%20(maarufu%20kama%20Mama,kuzipatia%20filamu%20za%20aina%20hiyo.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD