Mama mjamzito kutokwa na damu,chanzo na Tiba

Mama mjamzito kutokwa na damu 


Mama mjamzito kutokwa na Damu Ukeni ni hali ambayo inawapata wanawake wengi wakiwa wajawazito, na Sio mara Zote inamaanisha kuna tatizo kubwa la kiafya. Leo tunachambua Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii ya kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito kwa wakina Mama wengi.


Chanzo cha Mama mjamzito kutokwa na Damu

Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili,Sababu hizo ni pamoja na;

1. Damu Inayotoka wakati wa kiinitete(embro) kujishikiza kwenye Ukuta wa Mji wa Mimba kwa kitaalam hujulikana kama Implantation bleeding

Baada ya Yai kufanikiwa kurutubishwa na Mbegu ya Kiume,ndipo tunasema una mimba na Safari yako huweza kuanzia hapo,

Baada ya Urutubishaji huu,kiinitete kinachokua lazima kijishikize kwenye Ukuta wa mji wa mimba,kwa kitaalam mchakato huu hujulikana kama Implantation.

Katika hatua za awali za ujauzito,unaweza kupata hali ya kutokwa na damu nyepesi isiyo na madhara, inayojulikana kama "Light spotting".  Huu ndio wakati kiinitete kinachokua kinajipandikiza na kujishikiza kwenye ukuta wa tumbo lako la uzazi.

Katika kipindi hiki,baadhi ya Wanawake hutokwa na Damu nyepesi au matone matone ya Damu.

Aina hii ya kutokwa na damu mara nyingi hutokea wakati ule ule wa kipindi cha hedhi yako kutoka Unapofika., Hili sio tatizo bali ni hali ya kawaida kabsa.

2. Mabadiliko kwenye mlango wa kizazi(Cervical changes)

Mimba inaweza kusababisha mabadiliko kwenye mlango wa kizazi au Cervix, na hii inaweza wakati mwingine kusababisha damu kutoka- hasa baada ya tendo la ndoa,


 3. Sababu nyingine ni Kuharibika kwa mimba au mimba kutunga nje ya kizazi(hapa nazungumzia Miscarriage or Ectopic pregnancy)

 Wakati wa wiki 12 za kwanza za ujauzito, kutokwa na damu ukeni kunaweza kuwa ishara ya kuharibika kwa mimba au mimba kutunga nje ya kizazi,

Na Ikiwa unatoka damu katika hatua hii ya ujauzito na mimba ikatoka kwa bahati mbaya, hakuna sababu ya wewe usiendelee kutafuta Ujauzito mwingine kama huna tatizo lolote lingine. Ingawa ni muhimu sana kufahamu chanzo husika cha tatizo lako ili kama linahitaji Tiba upate Tiba mapema na kukaa Sawa kabla ya kutafuta tena ujauzito mwingine.


Mimba kutoka au kutishia kutoka;

Mbali na Damu kutoka Ukeni,Unaweza kupata dalili zingine kama Mimba inatishia kutoka au inatoka, dalili hizo ni kama vile;
  • kupata maumivu makali kwenye tumbo au chini ya kitovu
  •  kutokwa na Uchafu au majimaji ukeni
  •  kutoka kwa tishu au vitu kama nyama Ukeni
  •  kutopata tena dalili za ujauzito
 Ikiwa unavuja damu au unapata dalili zozote kati ya hizi, wasiliana na Wataalam wa afya Mara moja. au Kwa Ushauri Zaidi,elimu na Tiba tuwasiliane hapa hapa afyaclass kupitia namba +255758286584.


Vipi Kwa Upande wa Mimba kutunga Nje ya Kizazi?

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi mara nyingi huanza kuonekana kati ya wiki 6 hadi 8 za ujauzito lakini zinaweza kutokea baadaye pia.

Mbali na Damu kutoka Ukeni,Unaweza kupata dalili zingine kama Mimba imetunga nje ya Kizazi,dalili hizo ni pamoja na;
  • Kupata Maumivu chini ya tumbo ambayo yanaweza kuwa upande mmoja
  •  kutokwa na damu ukeni au kutokwa na maji ya kahawia
  •  Kupata Maumivu katika ncha ya bega lako n.k
4. Tatizo la Placental abruption

Hii ni hali mbaya ambayo placenta au kondo la nyuma huanza kutoka kwenye ukuta wa tumbo la Uzazi.  Kuachia kwa plasenta huweza kusababisha maumivu ya tumbo, na hii inaweza kutokea hata ikiwa hakuna damu.

Lakini pia tatizo hili huweza kusababisha Damu kutoka Ukeni.

5. Tatizo la Low-lying placenta au (placenta praevia)

Hili ni tatizo lingine ambalo huweza kusababisha mama mjamzito kutokwa na damu ukeni,

Huu ndio wakati plasenta inaposhika katika sehemu ya chini ya uterasi, karibu na au kufunika Cervix.  Damu inayotoka kwenye placenta hii iliyoshika sehemu ya chini inaweza kuwa nzito sana, na kukuweka wewe na mtoto wako katika hatari zaidi.


Hitimisho;

Hizo ndyo baadhi ya Sababu ambazo huweza kusababisha Mama mjamzito kutokwa na Damu Ukeni,

Je,Unaona Dalili hii ya kutokwa na Damu ukeni na hujui cha kufanya?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!