Afyaclass Ajali ya boti yaua Wahamiaji 7 huko kwenye Kisiwa cha Ugiriki

Ajali ya boti yaua Wahamiaji 7 huko kwenye Kisiwa cha Ugiriki



Vyombo vya habari Ugiriki vinaripoti kuwa takribani wahamiaji 7 wamefariki dunia leo baada ya boti yao kupata ajali katika eneo la kati ya Uturuki na kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos.

Kituo cha Ugiriki cha ERT kimeripoti kuwa watoto wawili ni miongoni mwa waliofariki.

Polisi inasema watu 23 wameopolewa ila manusura wamesema watu 31 walikuwa wamepanda boti hiyo. Utafiti wa awali unaonyesha kuwa wahamiaji hao wametokea Afghanistan na Syria.

Watu wanaofanya biashara ya usafirishaji haramu hujaribu mara kwa mara kuwasafirisha wahamiaji Ulaya kutoka pwani za magharibi mwa Uturuki, Lebanon au Syria.

Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi UNHCR linasema angalau wahamiaji 125 walifariki dunia au walipotea mashariki ya Bahari ya Mediterenia mwaka 2024, ila walinzi wa pwani ya Ugiriki wanashuku idadi ya visa ambavyo havijaripotiwa viko juu zaidi.

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD