Afyaclass Bongo Social Afungwa maisha kwa kumuuza Mtoto wake huko Afrika Kusini

Afungwa maisha kwa kumuuza Mtoto wake huko Afrika Kusini



Mtoto huyo wa kike Joshlin Smith, aliye na miaka 6 aliripotiwa kutoweka mwezi Februari mwaka jana katika eneo la Saldanha Bay, Afrika Kusini. 

Mama yake Racquel "Kelly" Smith, alipatikana na hatia ya kumteka nyara na kumuuza mtoto wake kwa dola 1,100 za kimarekani. Jaji Nathan Erasmus alitoa hukumu kwamba Racquel aliye na miaka 35, na mpenzi wake aliyeshitakiwa nae pamoja na rafiki yao watumikie kifungo cha maisha kwa kufanya biashara haramu ya kuuza watu. 

Jaji aliyetoa hukumu hiyo alisema mama huyo wa watoto watatu hakuonesha dalili yoyote ya kujitia matendo yake. 

Kesi hiyo imegusa hisia za wengi nchini humo, huku picha za mtoto Joshlin zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na ahadi ya zawadi ya randi milioni 1 kwa atakayemrudisha salama. Polisi bado inaendelea na uchunguzi ndani na nje ya Afrika kusini.

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD