Ajali yaua Watu 28 Mbeya,Homera atoa agizo

Ajali yaua Watu 28 Mbeya,Homera atoa agizo

#1

Ajali yaua Watu 28 Mbeya,Homera atoa agizo



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt.Juma Zuberi Homera amewaagiza TANROADS kutengeneza kwa Haraka Barabara ya Mchepuo Kutoka Mbalizi mpaka Iyunga ili itumike kwaajiri ya Magari Makubwa huku Magari Madogo yakielekezwa kutumia Barabara kuu ili Kupunguza Ajali zitokanazo na msongamano wa Magari.

Homera ameyasema hayo Leo juni 08,2025 mara baada ya kufika eneo la Ajali iliyotikea jana saa mbilu usiku katima Mlima Iwambi ambambo ajali hiyo imeua Watu 28 na kujeruhi tisa mara baada ya Gari kubwa aina ya Lori(T.830 EDP,T.148 CTD)) kufeli Break na kugonga Magari Mawili ikiwemo Gari Dogo la abiria(Daladala na Gari Dogo aina ya Kirikuu).





“Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania anatoa Maelekezo kwa TANROADS kuhakikisha wanaitengeneza hiyo Barabara ya Mchepuo ili Magari Makubwa yapite kule hapa pabaki kwaajiri ya Magari madogo tuu” Amesema Dkt. Homera

Aidha Dkt.Homera amesema Serikali itagharamia Matibabu kwa Majeruhi wa Ajali hiyo ambao wamelazwa Hospitali teule ya Ifisi, itatoa Mkono wa Pole Laki Tano kwa Kila familia iliyofikwa na Msiba na Matengenezo ya Majeneza kwa miili yote 28.

Pia amefika Hospitali teule ya Ifisi kwaajiri ya kuwatembelea Majeruhi wa Ajali hiyo na wafiwa waliofika kwaajiri ya utambuzi wa Ndugu zao na amewaomba wawe na subira na Amani kwakuwa Serikali Iko Pamoja nao na itahakikisha inashughurikia kila jambo 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa SACP Benjamin Kuzaga amethibitisha Kutokea kwa Ajali hiyo na Kutaja chanzo Cha Ajali kuwa ni uzembe wa Dereva wa Lori na licha ya kujeruhiwa naye lakini pia anashikiliwa kwaajiri ya Mahojiano zaidi.

Hata hivyo SACP Kuzaga ametoa wito kwa Madereva kufata Sheria za Barabarani ili kujiepusha na Ajali zisizo na ulazima zinazopelekea kupoteza Maisha ya Watu.

REPLY HAPA


image quote pre code