Afyaclass Bongo Social Colombia:Mgombea Uraisi apigwa risasi kichwani akiwa kwenye mkutano

Colombia:Mgombea Uraisi apigwa risasi kichwani akiwa kwenye mkutano



Mgombea urais wa Colombia yuko katika hali mbaya baada ya kupigwa risasi tatu, ikiripotiwa mara mbili kichwani, katika hafla ya kampeni katika mji mkuu, Bogotá.

Miguel Uribe Turbay, seneta mwenye umri wa miaka 39, alishambuliwa alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake kwenye bustani siku ya Jumamosi.

Polisi walimkamata mshukiwa mwenye umri wa miaka 15 katika eneo la tukio, ofisi ya mwanasheria mkuu ilisema.

Mkewe Uribe, Maria Claudia Tarazona, alitoa wito kwa taifa kumuombea apone.

“Miguel kwa sasa anapigania maisha yake, tumuombe Mungu aongoze mikono ya madaktari wanaomhudumia,” alisema.

Chama cha Uribe Centro Democratico kimelaani shambulio hilo, na kulitaja kuwa tishio kwa "demokrasia na uhuru nchini Colombia".

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD