Dalili za Gono Sugu kwa Mwanaume (Gonorrhea sugu)
1. Maumivu au Kuwasha Wakati wa Kukojoa
Hili ni mojawapo ya dalili za kwanza. Mwanaume anaweza kuhisi maumivu makali au kuwashwa wakati wa kukojoa. Hii hutokea kwa sababu njia ya mkojo (urethra) imeathiriwa na uvimbe unaosababishwa na bakteria.
2. Kutokwa na Majimaji Yasiyo ya Kawaida au Usaha kwenye Uume
Majimaji haya yanaweza kuwa na rangi ya kijani, njano, au weupe mzito. Kutokwa na majimaji haya au Usaha kwenye Uume ni dalili kuu ya gono kwa wanaume. Mara nyingi, ute huu hutoka asubuhi au baada ya kukojoa.
3. Kuvimba kwa Urethra (Njia ya Mkojo)
Sehemu ya uume inayozunguka tundu la mkojo inaweza kuvimba na kuwa nyekundu. Hii ni kutokana na uchochezi (inflammation) unaosababishwa na maambukizi.
4. Maumivu ya Korodani au Kuvimba kwa Korodani
Korodani moja au zote mbili zinaweza kuvimba na kuwa na maumivu. Gono ikiwa sugu inaweza kusambaa hadi kwenye sehemu ya korodani na kusababisha hali iitwayo epididymitis, ambayo ni hatari na huweza kuathiri uzazi.
5. Maumivu ya Sehemu ya Nyuma (Anus) kwa Wanaume Wanaoingiliana Kinyume na Maumbile
Ikiwa mwanaume anafanya ngono kwa njia ya haja kubwa,kitu ambacho ni hatari sana kwa afya, anaweza kupata dalili kama:
- Kuwashwa au kuchoma sehemu ya haja kubwa.
- Kutokwa damu au ute.
- Maumivu wakati wa haja kubwa.n.k.
6. Maumivu ya Koo
Ikiwa maambukizi yamepatikana kwa njia ya mdomo (oral sex), mwanaume anaweza kupata:
- Maumivu ya koo yasiyoisha.
- Kuvimba kwa tezi za shingo.
- Kukosa hamu ya kula kutokana na maumivu ya kumeza.
Hali ya Kukosa Dalili Kabisa (Asymptomatic)
Baadhi ya wanaume hawataonesha dalili yoyote kwa muda mrefu, lakini bado wataendelea kuwaambukiza wengine. Hii ndiyo sababu ya hatari kubwa ya maambukizi kuenea kwa urahisi bila kutambuliwa mapema.
Dalili za Gono Kuwa Sugu (Antibiotic Resistance)
Wakati gono inapokuwa sugu, dalili zinaweza kudumu muda mrefu hata baada ya kutumia dawa, na zinaweza kuwa:
- Dalili hazipungui baada ya matibabu.
- Maumivu kuongezeka badala ya kupungua.
- Kutokwa na usaha (discharge) unaoendelea hata baada ya kutumia dawa.
- Kuhisi uchovu au homa ya mara kwa mara.n.k.
Madhara ya Gono Sugu kwa Mwanaume
Kama gono sugu haitatibiwa ipasavyo, inaweza kusababisha:
- Ugumba (kutokuwa na uwezo wa kumpatia mwenza mimba).
- Maambukizi sugu kwenye mfumo wa uzazi.
- Maambukizi kusambaa kwenye damu (disseminated gonococcal infection).
- Kuathiri viungo vingine kama macho au viungo vya ndani.n.k.
Hitimisho
Gono sugu kwa mwanaume ni hali hatari inayohitaji uchunguzi wa kitaalamu na matibabu maalum kwa kutumia antibiotiki mpya ambazo bado zinafanya kazi dhidi ya bakteria hawa. Ni muhimu sana kupata Msaada mapema ukiona dalili yoyote au baada ya kufanya ngono isiyo salama. Pia, kuzuia ni bora kuliko tiba – tumia kondomu, epuka wapenzi wengi, na fanya uchunguzi mara kwa mara.
Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code