Kima cha chini cha pensheni ya kila mwezi kuongezwa

Kima cha chini cha pensheni ya kila mwezi kuongezwa

#1

Kima cha chini cha pensheni ya kila mwezi kuongezwa



Katika mwaka 2025/26, Serikali itaongeza kima cha chini cha pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu wanaolipwa na hazina kutoka shs 100,125.9 hadi shs 250,125.9, sawa na ongezeko la asilimia 149.8 na utekelezaji wake utaanza katika pensheni ya Julai 2025.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26.

” Napenda kuwahakikishia watanzania kuwa Serikali inaendelea kusimamia mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuhakikisha inabaki kuwa himilivu na kulipa mafao ya wastaafu wote kwa wakati. Katika kutekeleza azma hiyo, kutoka mwaka 2021 hadi Mei 2025, Serikali imelipa madeni yenye thamani ya shilingi trilioni 2.67,” amesema Waziri Nchemba.

Amesema kati ya kiasi hicho, shs trilioni 2.18 ni madeni ya PSSSF ya waliokuwa wafanyakazi kabla ya mwaka 1999 (Pre-65 99), shs bilioni 433.71 ni madeni ya NSSF ya muda mrefu na shs bilioni 63.52 ni madeni ya Kampuni ya Pension Property Limited (PPL).

REPLY HAPA


image quote pre code