TAHADHARI: Mvua za msimu wa kipupwe kuikabili eneo la Asia Kusini
Jamii katika eneo lote la Himalaya Hindu Kush huko barani Asia wanakabiliwa na hatari inayoongezeka ya janga katika kipindi kijacho cha kipupwe huku nyuzi joto na mvua zikitarajiwa kuvuka viwango vya kawaida.
Haya ni kulingana na wataalam waliotoa onyo hilo Alhamis.
Kituo cha Kimataifa cha Masomo na Kubadilishana Ujuzi ICIMOD, kinasema nyuzi joto zinatarajiwa kuwa juu zaidi ya zile za wastani katika eneo lote hilo, huku utabiri wa hali ya hewa ukionyesha mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha.
"Nyuzi joto zinazopanda na mvua kubwa zinaongeza hatari ya majanga yanayosababishwa na maji kama mafuriko na maporomoko ya ardhi na haya yana athari kubwa kwa barafu ya milimani na hifadhi za barafu," alisema katika taarifa Arun Bakhta Shrestha, mshauri mkuu katika kituo cha ICIMOD.
Msimu wa kipupwe wa majira ya joto ambao huleta kati ya asilimia 70-80 ya mvua ya mwaka katika eneo hilo, ni muhimu kwa kilimo na maisha ya mamilioni ya wakulima na usalama wa chakula katika eneo ambalo ni makao ya karibu watu bilioni 2.
Mvua hizo lakini huleta madhara na uharibifu ikiwemo maporomoko ya ardhi na mafuriko kila mwaka. Barafu ya milimani inayoyeyuka huongeza kiwango cha maji huku ujenzi usiodhibitiwa katika maeneo yaliyo kwenye hatari ya mafuriko ukiongeza zaidi uharibifu.
Mwaka jana msimu wa kipupwe ulisababisha maporomoko mabaya ya ardhi na mafuriko kote kusini mwa Asia na kupelekea vifo vya mamia ya watu wakiwemo zaidi ya watu 300 nchini Nepal.
REPLY HAPA
image quote pre code