Baltasar ahakumiwa miaka 8 gerezani kwa kosa la ubadhirifu wa Fedha za Umma
Mahakama ya Mkoa wa Bioko nchini Equatorial Guinea imemhukumu Baltasar Ebang Engonga, Mkuu wa zamani wa Shirika la Taifa la Upelelezi wa Masuala ya Kifedha (NFIA), kifungo cha miaka Minane Jela kwa kosa la ubadhirifu wa Fedha za Umma na kujipatia mali kinyume cha sheria.
Engonga, pamoja na Maafisa wengine Watano waandamizi, walipatikana na hatia ya kuiba mamia ya maelfu ya dola kutoka hazina ya taifa na kutumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi.
Mahakama pia imewaamuru kulipa faini kubwa. Engonga atakuwa na faini ya dola 220,000, wakati maafisa wengine walioshitakiwa kama washirika walipata kifungo cha miaka mitatu.
Baltasar Ebang Engonga ni Mpwa wa Rais Teodoro Obiang Nguema, ambaye amekaa madarakani tangu 1979 na ana umri wa miaka 82, Engonga alikuwa mmoja wa wale wanaodhaniwa kuwa na nafasi ya kurithi madaraka ya Rais.
Hukumu hii inaashiria changamoto kubwa za uwajibikaji wa viongozi serikalini, hasa katika nchi yenye utajiri wa mafuta lakini pia changamoto za ubadhirifu wa kifedha.
Mbali na mashtaka ya kifedha, Engonga amejipatia umaarufu wa aibu baada ya video kadhaa za ngono kuenea mitandaoni, Video hizo zinamhusisha akiwa na wake wa maafisa wengine wa serikali.
image quote pre code