Tukio,Kimbunga Kalmaegi chasababisha maafa makubwa Vietnam

Tukio,Kimbunga Kalmaegi chasababisha maafa makubwa Vietnam

#1

Kimbunga Kalmaegi kimesababisha upepo mkali na mvua kubwa huko Vietnam. Watu watano wameuwawa wakati kimbunga hicho kilipopiga eneo hilo, kutokea Ufulipino ambako huko idadi ya waliouwawa wamefikia 188.

Nchini Ufilipino katika eneo la Cebu watu 188 waliuawa wengi wao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyotokana na kimbunga Kalmaegi. Watu katika eneo hilo walikusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa waliouawa.

Eneo kubwa la kufanyia mazoezi, ndilo lililogeuzwa sehemu ya kuiaga miili ya walioangamia. Vilio vilisikika huko wakati masanduku meupe ya kubebea maiti, yaliyokuwa na picha za walioaga, yakibebwa na kuanza safari ya kuzikwa. Dharura ya Kitaifa iliyotangazwa na rais Ferdinand Marcos Jr. bado ilikuwa inaendelea Ufilipino wakati nchi hiyo ikijitayarisha kwa kimbunga kingine kinachopewa jina la Uwan.

Kulingana na mamlaka ya hali ya hewa ya Vietnam, kimbunga Kalmaegi kilichoambatana na upepo mkali kimeyang'oa mapaa ya nyumba na kimesomba miti na kuangusha minara ya mawasiliano.

Viwanja vya ndege vimefungwa 

Kutokana na janga hilo viwanja sita vya ndege vimefungwa wakati serikali ikisema watu 260,000 wamehamishwa kutoka mkoani Gia Lai na kupelekwa maeneo salama. Serikali imeongeza kuwa wanajeshi 268,000 wamewekwa tayaei kwa ajili ya operesheni za uokoaji na kuwatafuta waathiriwa wa kimbunga hicho.

Baada ya kimbunga Kalmaegi, kupiga maeneo hayo mawili, kazi ya uokoaji ilianza katika miji na vijiji vilivyoathiriwa katika nchi zote mbili Ufilipino na Vietnam barabi Asia. Watu walianza polepole kuondoa vifusi vya majengo yaliyoanguka na na kurekebisha paa za nyumba zao.

Jimmy Abatayo, aliye na miaka 53 na aliyempoteza mke wake na jamaa tisa wa karibu baada ya kimbunga kusababisha mafuriko katika jimbo la kati la Ufilipino la Cebu, alizidiwa na huzuni alipokuwa anapitisha mikono yake katika jeneza la mke wake.

"Nilifanikiwa kuogelea na kujiokoa, niliiambia familia yangu pia wajaribu kuogelea, kwamba waendelee kuogelea na wataokolewa, lakini hawakunisikiliza, kwahiyo sitowaona tena," alisema kwa majonzi makubwa huku akibubujikwa na machozi.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code
مشاركة: