Muigizaji wa Kijapani Tagawa Afariki Dunia,akiwa na miaka 75

Muigizaji wa Kijapani Tagawa Afariki Dunia,akiwa na miaka 75

#1

Muigizaji wa Kijapani Tagawa Afariki Dunia,akiwa na miaka 75

Muigizaji wa Kijapani Cary-Hiroyuki Tagawa, maarufu kwa nafasi yake ya Shang Tsung kwenye 'Mortal Kombat', amefariki dunia akiwa na miaka 75 kutokana na matatizo ya kiharusi.

Kwa mujibu wa taarifa za mwakilishi wake, Tagawa alifariki Alhamisi mjini Santa Barbara akiwa na familia yake.

Tagawa alijulikana kwa zaidi ya miongo minne katika filamu za Hollywood, akionekana kwenye filamu zaidi ya 30. Filamu maarufu alizocheza ni pamoja na:

Mortal Kombat (1995)

The Last Emperor (1987)

License to Kill (1989)

Rising Sun (1993)

Pearl Harbor (2001)

Alipata pia umaarufu  kupitia nafasi ya Nobusuke Tagomi kwenye mfululizo wa "The Man in the High Castle."

Tagawa anakumbukwa kama msanii mwenye ushawishi, mwalimu wa martial arts na mlezi wa waigizaji chipukizi. Ameacha watoto wake watatu na wajukuu wawili.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code