Tanzania yaibuka kidedea Mashindano ya CAF African Schools U-15

Tanzania yaibuka kidedea Mashindano ya CAF African Schools U-15

#1

Tanzania yaibuka kidedea Mashindano ya CAF African Schools U-15

Timu ya Taifa ya Wasichana U-15 ya Tanzania imeweka rekodi mpya baada ya kutwaa ubingwa wa Mashindano ya CAF African Schools Football Championships – CECAFA Qualifiers 2025 yaliyofanyika nchini Uganda.

Tanzania ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Ethiopia, katika mchezo mkali uliowakutanisha timu hizo mbili zilizong'ara zaidi katika hatua za awali. Matokeo hayo yameifanya Tanzania kuwa mabingwa wa ukanda wa CECAFA kwa mwaka 2025.

Ushindi huu unaibua sura mpya kwa taifa katika soka la shule, na kuitambulisha Tanzania kama moja ya nguvu mpya zinazochipukia katika mpira wa miguu wa wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code