Koo kuwasha husababishwa nini? na Tiba yake

Koo kuwasha husababishwa nini? na Tiba yake

Koo kuwasha huweza kusababishwa na Vitu Vingi ikiwemo; hali ya Mzio(allergies),Maambukizi ya magonjwa n.k, Katika Makala hii tutachambua Sababu hizo kuu ambacho husababisha Koo kuwasha.

Kwanini Koo Linawasha?

Mambo mengi yanaweza kufanya koo lako liwashe au uhisi hali ya Koo kuwasha. Hapa kuna sababu kubwa Zaidi:

1. Mzio au Allergies: Koo lako linaweza kuingiwa na vitu kama vile vumbi, Moshi,ukungu au vyakula fulani ambavyo vikipita hapo hukuletea hali ya kuwashwa sana kooni. 

Mwili wako hutoa kemikali zinazoitwa histamini, ambazo zinaweza kusababisha hisia hiyo ya kuwasha.

2. Maambukizi ya Vimelea vya magonjwa kama Vile Bacteria,Virusi: Virusi kama vile vya Mafua au COVID-19 huweza kusababisha hali ya koo kuwasha. Maambukizi ya Bacteria kama vile Streptococcus pyogenes huweza pia kusababisha koo kuwasha.

Hali hii ya Koo kuwasha huweza kudumu kwa wiki kadhaa baada ya kupata maambukizi haya.

3. Vitu vingine(Irritants) kama: Moshi,Vumbi,baadhi ya Kemikali n.k. huweza kuleta hali hii ya Koo kuwasha.

4. Hewa Kavu pamoja na Upungufu wa Maji mwilini(Dry air/dehydration): Ikiwa hewa ni kavu sana au hunywi maji ya kutosha, koo lako linaweza kukauka na kuhisi kama linakwaruza,kuwasha au hata Kuuma wakati mwingine.

5. Tatizo la Acid reflux: Asidi ya tumbo inaweza kusafiri kwenda kwenye koo lako, na kusababisha muwasho kwenye Koo.

6. Matumizi ya Baadhi ya Dawa: Mfano Dawa jamii ya ACE inhibitors kwa ajili ya Wagonjwa wa Presha,huweza kusababisha hali hii ya Koo kuwasha.

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma pia;

Rejea Link:

https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/itchy-throat

0 Comments