Uume kuvimba husababishwa na Nini?
Uume kuvimba kunaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, kulingana na hali ilivyo. Hizi ndizo Sababu kubwa;
1. Maambukizi ya Vimelea mbali mbali vya magonjwa
-Maambukizi ya bakteria au fangasi (hasa chini ya ngozi ya kichwa cha uume)
-Magonjwa ya zinaa kama
- kisonono,
- klamidia,
- au kaswende
Dalili Zake huambatana na maumivu, usaha, harufu mbaya au kuwashwa
2. Msuguano au jeraha
-Kujamiiana kwa nguvu au muda mrefu bila kuwa na hali ya ulainishi Ukeni au kuwa na Ukavu Ukeni
-Kujikuna au kuumia
Huweza kusababisha uvimbe wa muda na maumivu pia.
3. Tatizo la Allergy / mzio
-Dhidi ya Vitu kama Kondomu (latex)
-Sabuni, mafuta au dawa za kupaka
Huweza kuleta uvimbe pamoja na hali ya kuwashwa kwenye Uume
4. Hali ya Kuziba na maji kujikusanya eneo moja (Edema)
Maji kujikusanya kwenye ngozi ya uume
Mara nyingine huonekana bila maumivu makali,Lakini huweza kusababisha Uume kuvimba
5. Tatizo la Phimosis au Paraphimosis
Hapa Ngozi ya kichwa cha uume hushindwa kurudi kawaida
Hali hii ni hatari ukichelewa kupata Tiba→ huhitaji Matibabu ya haraka sana.
6. Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
Wakati mwingine maambukizi kama ya UTI huweza kusababisha Uume Kuvimba pia pamoja na maumivu wakati wa kukojoa au Hisia ya kuwaka moto wakati wa kukojoa n.k.
MUONE DAKTARI HARAKA KAMA:
-Uume umevimba na una maumivu makali
- Kuna usaha unatoka au damu zinatoka
- Unapata homa
- Uume umevimba sana na ngozi imekaza
Hali imekaa zaidi ya siku 2–3 bila kupungua
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Soma pia hapa:





.jpeg)



image quote pre code