Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni)

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni)

#1

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni)

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni) mara nyingi huitwa kwa kitaalamu Globus Sensation. Hali hii inaweza kutokea hata kama hakuna kitu halisi kilichokwama.

Sababu zinazoweza kusababisha

  1. Misuli ya koo kukaza–  kwa Sababu mbali mbali ikiwemo Msongo wa mawazo,au wasi wasi n.k
  2. Asidi kupanda kutoka tumboni – hali iitwayo kitaalam Acid Reflux  inaweza kufanya koo lihisi kama kuna kitu.
  3. Maambukizi ya koo – kama yale ambayo husababisha tonsils kuvimba.
  4. Uvimbe wa tezi ya koo
  5. Mate kuwa machache au koo kukauka.
  6. Kuna chakula au kitu kimekwama kweli (hasa kama ulimeza kitu kigumu kama mfupa).

Dalili zinazoambatana na hali hii

  • Kuhisi kama kuna donge kooni
  • Ugumu kidogo wa kumeza
  • Kukohoa mara kwa mara
  • Koo kukauka au kuwaka moto,kuwasha n.k

Ufanye nini kwa haraka

  • Kunywa maji ya uvuguvugu polepole.
  • Jaribu kumeza chakula laini kama uji au ndizi.
  • Epuka vyakula vyenye pilipili nyingi, kahawa na soda kama asidi inahusika.
  • Punguza stress.

Nenda hospitali haraka kama:

  • Unashindwa kumeza kabisa
  • Kuna maumivu makali kooni
  • Unapumua kwa shida
  • Dalili zinaendelea zaidi ya wiki 2
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code