Halima Cissé aliweka Rekodi ya Dunia kujifungua watoto 9 mara moja

Halima Cissé aliweka historia kwa kujifungua watoto tisa mara moja—Hii imemfanya kuingia kwenye rekodi ya dunia kupitia Guinness World Records

Watoto hao Walizaliwa kwa njia ya upasuaji(C-section) nchini Morocco, watoto wote tisa—wasichana watano na wavulana wanne—waliingia katika historia ya matibabu Duniani.


Mnamo mwaka 2021, dunia ilishuhudia muujiza wa kipekee: mama Halima Cissé kutoka Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo — wavulana wanne na wasichana watano — tukio ambalo halijawahi kutokea tena kwa mafanikio duniani!



Serikali ya Mali iliwasafirisha yeye na mume wake, Abdelkader Arby, hadi Morocco kwa matibabu ya hali ya juu baada ya kugundua alikuwa na ujauzito wa mapacha 7. Lakini walipofika Morocco, walipokea mshangao mkubwa — walikuwa ni mapacha tisa!

Kutokana na tukio hilo la kipekee, Halima Cissé aliandikishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness (Guinness World Records) kama mwanamke wa kwanza kuwahi kujifungua watoto tisa kwa mpigo na wote wakaishi, jambo lililovutia dunia nzima.

Sasa mapacha hao wametimiza miaka minne, wakiwa na afya njema na furaha kubwa. Wazazi wao hivi karibuni walisherehekea siku hiyo ya kipekee kwa kushiriki picha na kumbukumbu kupitia Instagram, wakikumbuka safari yao ya ajabu ya uzazi.

#afyaclass #worldrecord #news

...See more

DISCUSSIONS BOX(MAONI)|REPLY

Related Discussions...