Makala hii imeandikwa na Dr.Ombeni Mkumbwa,kwa kuzingatia Uzoefu,Idadi ya Wagonjwa wa UTI wanaoripoti hospital kila mara,historia zao,Tafiti mbali mbali za afya ikiwemo kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO),pamoja na Taasisi zingine za afya kama vile HealthLine,WebMd n.k.
Jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa UTI
Tumia njia hizi kujikinga na Maambukizi ya njia ya Mkojo(UTI), Tips muhimu sana kwako:
1.Epuka tabia ya kubana Mkojo mara kwa mara
Kubana Mkojo mara kwa mara wakati mkojo unatakiwa utoke,huongeza hatari ya Bacteria kukaa kwenye kibofu cha Mkojo na kuzaliana zaidi,
Kama unahisi kukojoa,Please kojoa! hii itakusaidia sana kama ulikuwa hujui.
Hivo Epuka tabia hii ya kubana mkojo mara kwa mara.
2. Hakikisha Unakunywa maji mengi kila Siku
Ingawa maji sio Tiba Kamili ya UTI,Zipo tafiti nyingi huonyesha Mtu anayekunywa maji mengi angalau lita 2 kwa siku hupunguza uwezekano wa kushambuliwa na UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya Asilimia 50%.
3. Usafi binafsi pamoja na Usafi wa Chooni
Moja ya Vitu ambavyo vinaongeza mashambulizi ya bacteria wa UTI(E.coli) ni kutumia vyoo vichafu,
Ndyo maana Watu wanaotumia Vyoo vya Kushare na Watu wengi(public toilets) kama vile Vyoo vya Stendi,Sokoni,Hospitalini Au hata nyumbani, kama havijafanyiwa Usafi vizuri huweza kusababisha hatari zaidi ya maambukizi ya UTI.
Kingine! Epuka tabia ya kutumia maji machafu chooni,tumia maji masafi, Kama maji yamekaa muda mrefu kwenye vyombo kama ndoo za maji,usiongezee masafi juu yake,mwaga, tumia maji Safi,
Maji machafu kwenye ndoo hizi,huongeza hatari ya bacteria wa UTI kukua na kuongezeka zaidi.
4. Epukaa kukaa na nguo za ndani mbichi
Hii si tu inaongeza hatari ya maambukizi haya ya Bacteria kwenye mfumo wa Mkojo,Lakini pia maambukizi kama ya Fangasi n.k....
Tazama Zaidi Video hii:
Rejea Zaidi:



image quote pre code