Head

Mahakama ya Afrika Kusini yaamuru Zambia irudishe mwili wa rais wa zamani Edgar Lungu

Edgar Lungu alisema hakutaka mrithi wake kuwepo kwenye mazishi yake au "mahali popote karibu" na mwili wake

Saa chache tu baada ya serikali ya Zambia kusema imechukua mwili wa Rais wa zamani Edgar Lungu, mahakama nchini Afrika Kusini -imeamuru mwili huo urudishwe.

Ni mabadiliko ya hivi punde katika sakata ya miezi 10 kuhusu kile kinachopaswa kutokea kwa mabaki yake kufuatia ugomvi wa muda mrefu kati ya Lungu na mrithi wake, Rais Hakainde Hichilema.

Serikali imesisitiza kwa muda mrefu kwamba, kama mkuu wa zamani wa nchi, Lungu anapaswa kuheshimiwa nchini na kuzikwa pamoja na watangulizi wake katika eneo maalum la mazishi ya rais katika mji mkuu, Lusaka.

Lakini familia ya Lungu ilitaka mazishi ya faragha baada ya mazungumzo na serikali kuhusu mipango ya mazishi kuvunjika.

Agosti iliyopita, mahakama kuu ya Afrika Kusini huko Pretoria ilitoa uamuzi kwamba serikali ya Zambia inaweza kurudisha mwili huo na kumpa mazishi ya kitaifa - matokeo ambayo yaliwaacha jamaa za Lungu wakiwa wamechanganyikiwa waziwazi mahakamani.

#Reply

#5Replies