Pambano la Anthony Joshua dhidi ya Tyson Fury litakuwa pambano kubwa zaidi- bingwa wa zamani wa uzani wa juu David Haye atangaza.
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu David Haye amesisitiza umuhimu wa pambano kati ya Anthony Joshua na Tyson Fury, akiliita pambano muhimu zaidi,
Uwepo wa pambano hilo ulichochewa zaidi mapema mwezi huu baada ya vigogo hao wawili kurushiana maneno katika Uwanja wa Tottenham Hotspur, Huku mashabiki zao wakihitaji Zaidi pambano hilo.
Akizungumza na Sky Sports, Haye alibainisha kuwa muda huo unaweza kuwanufaisha wapiganaji kifedha, akikiri, "Labda watapata pesa nyingi zaidi sasa kuliko wangepata wakati ulipozungumziwa kwa mara ya kwanza."
You, Mehreen and others


