Roho Mtakatifu ni nguvu inayomsaidia Mkristo kufanya yale anayopaswa kufanya katika Imani.
Ujumbe huu uweke Shauku Mpya ndani yako ya kutaka Kujazwa Roho Mtakatifu kwa nguvu zote ili akusaidie.
Kama wewe ni Mkristo na huna Roho Mtakatifu, Ujue huna Nguvu itakayokusaidia kufanya yale unayopaswa kufanya. Huyu ndiye Msaidizi tuliyeachiwa,atatufundisha yote na kutukumbusha yote.
Wanafunzi wa Yesu Kabla ya Kwenda Kufanya kazi ya kuhubiri waliambiwa Wasubiri kwanza wapokee Msaidizi ambaye ndiye Roho Mtakatifu ili awasaidie maana peke yao hawawezi. "Matendo ya Mitume 2:1-4 inaizungumzia Siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Mstari wa 4 "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka". Hapa Ndipo Petro alihubiri wakaokoka watu takribani 3000 Siku hiyo hiyo, baada ya ujazo wa Roho Mtakatifu, Biblia inasema maneno yao yalikuwa yanatoka kwa nguvu kiasi kwamba yalikuwa yanachoma mioyo ya wale waliyokuwa wanayasikia(Nguvu ya Roho Mtakatifu).
Nitakupa Mifano Michache tu,Lakini naamini Mungu atakusaidia kuelewa;
1.Mfano katika Kuomba: Kama Ni Mkristo lazima uwe na Roho Mtakatifu ili akusaidie kuomba jinsi inavyotakiwa; Warumi 8:26 Inasema "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa".
Kama huna Roho Mtakatifu huwezi kufanya maombi kwa Usahihi,Kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo.
2.Mfano katika Kugeuzwa kuwa Mtu mwingine: Ili Ufiti katika Nafasi Uliyopewa Lazima Roho Mtakatifu aje akugeuze kuwa Mtu mwingine ambaye atakaa kwenye nafasi kama inavyotakiwa, Tuangalie habari za Sauli alivyopewa Maelekezo na Samweli baada ya kupakwa mafuta kuwa Mfalme wa Israel;"1 Samweli 10:6 Inasema "na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine".
Lakini pia ili Ubadilike kabsa na kuwa Mtu mwingine tofauti na Kipindi hujaokoka,Lazima nguvu ya Roho Mtakatifu ikusaidie, Nguvu hii itakusaidia Kama Mkristo kufanya unayopaswa kufanya katika Imani.
Kwa Maneno haya Machache,Omba Mungu akupe Roho Mtakatifu,Jaa Roho Mtakatifu,Pata Nguvu itakayokusaidia Kusimama,Peke yako hutaweza.
You, Mehreen and others


.jpeg)