Showing posts with label Mwl Ombeni Mkumbwa. Show all posts
Showing posts with label Mwl Ombeni Mkumbwa. Show all posts

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutokaAfyaclass Forum •

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutoka

Mtu anayemtafuta Mungu ndye mwenye akili kuliko wote, Lakini Shetani hupofusha Fikra za Watu kwa nguvu Zote ili waone kumtafuta Mungu ni kupoteza muda,Kukosa cha kufanya,Kuwa Maskini n.k..

"Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu(Zaburi 14:2)".

Fikra Zako zifunguke Katika Jina la Yesu,Uuone Ukuu wa MUNGU kuliko ngome za mawazo anazojenga adui kwenye fikra zako, angusha ngome hizo,Na Mungu aweke Kiu ndani yako ya kumtafuta kwenye Kila Jambo.

Aweke Kiu kama ya Daudi,anasema katika Zaburi 27:4 "Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake".

0 Comment

Tambua Rehema na Neema za Mungu kwako,UtamshukuruAfyaclass Forum •

Tambua Rehema na Neema za Mungu kwako,Utamshukuru

Rehema ni pale ambapo Mungu hakutuadhibu kwa Dhambi tulizostahili adhabu,

Neema ni pale ambapo Mungu anatubariki wakati hatukustahili.

Toba ya Kweli kutoka Moyoni huturidisha Kwa Mungu,

Yoeli 2:13 inasema "rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya".

Kama Mungu hajakuadhibu Kwa Kosa Ulilostahili adhabu, tena kukubariki wakati hukustahili(Fikiria kwa Kina Utaona UPENDO mkuu wa MUNGU kwako,Nawe UTAMSHUKURU siku Zote).

0 Comment

Usikate Tamaa ya Kuomba,Omba mpaka LitokeeAfyaclass Forum •

Usikate Tamaa ya Kuomba,Omba mpaka Litokee

Hata kama Lipo jambo ambalo umeliombea Muda Mrefu na bado hujapata Majibu,Ujumbe wa Leo kwako; Usikate Tamaa ya Kuomba, Omba mpaka litokee. (Jifunze hapa Kwa Eliya alipokuwa anaomba Mungu ili mvua inyeshe katika Nchi). Mara ya kwanza,hakuna kitu,akaendelea;baadae(mara ya 7) mazingira yakaanza kubadilika na MVUA ikanyesha Nyingi.

Eliya alipopanda juu mpaka kilele cha Mlima Karmeli; alisujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.

Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba.

Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.

Ikawa, muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli.(1 Wafalme 18-42-45).

0 Comment

Mkabidhi BWANA maisha yako ili akusaidie, peke yako hutawezaAfyaclass Forum •

Kumkabidhi BWANA maisha yako;ni kumpa BWANA au MUNGU nafasi ya kuwa Mwamuzi na Kiongozi wa Kila Kitu kwenye maisha yako.

Hii ina maana huwezi kufanya kitu chochote pasipo kutaka uongozi kutoka kwa Mungu, bila kujali una uzoefu kiasi gani,Elimu kiwango gani,Kipato kiwango gani, au akili kiwango gani... Mungu anaamua na kukuongoza kwa kila kitu.

Zaburi 37:5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.

Mithali 3:5-6Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

0 Comment

Tafuta Kibali kwa Mungu,atakupa kibali kwa WanadamuAfyaclass Forum •

Tafuta Kibali kwa Mungu,atakupa kibali kwa Wanadamu

Fahamu Ukipata Kibali kwa Mungu ndipo anakupa Kibali na Kwa Wanadamu. Ukikosa Kibali kwa Mungu unakosa na kibali kwa Wanadamu.

Daudi mtoto wa Yese alipata Kibali kwa Mungu,Mungu akampa kibali na kwa Mfalme Sauli.

"1 Samweli 16:22 Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu".

Unaweza Kupata Kibali kwa Mungu kwa kutenda vyema(jinsi Mungu anavyotaka),Mungu anamuambia Kaini Kama Ukitenda Vyema hutapata Kibali? Maana yake;Kibali cha Mungu kinaweza kupatikana kwa njia ya Kutenda vyema au kutenda kwa jinsi Mungu anavyotaka......

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD