Napenda Kufahamu Dalili kuu za Ugonjwa huu wa Ebola,maana nasikia sana saivi unasumbua Congo, Lakini pia unasambaaje?
...See more
Napenda Kufahamu Dalili kuu za Ugonjwa huu wa Ebola,maana nasikia sana saivi unasumbua Congo, Lakini pia unasambaaje?
Ugonjwa wa Ebola husababishwa na Virusi ambao wanapatikana kwenye genus ya Orthoebolavirus ndani ya famili ya filoviridae. Aina sita za Orthoebolavirus zimetambuliwa hadi sasa, huku tatu zikijulikana kusababisha milipuko mikubwa:
ReplyDeleteEbola virus (EBOV) causing Ebola virus disease (EVD)
Sudan virus (SUDV) causing Sudan virus disease (SVD)
Bundibugyo virus (BDBV) causing Bundibugyo virus disease (BVD).
Ugonjwa huu huathiri binadamu pamoja na baadhi ya wanyama kama nyani na sokwe. Ebola huenea kwa kasi kupitia kugusana moja kwa moja na damu, mate, jasho, matapishi, mkojo au majimaji mengine ya mwili wa mtu aliyeambukizwa.
Dalili za Ebola huanza kuonekana kati ya siku 2 hadi 21 baada ya maambukizi. Mwanzoni mgonjwa anaweza kupata:
ReplyDeleteHoma kali
Maumivu ya kichwa
Uchovu mkubwa
Maumivu ya misuli na viungo
Koo kuwasha au kuuma
Baadaye dalili huwa kali zaidi na zinaweza kujumuisha:
• Kutapika
• Kuharisha
• Maumivu ya tumbo
• Upele mwilini
• Kutokwa damu puani, mdomoni,Masikioni au kwenye njia ya haja kubwa na ndogo kwa baadhi ya wagonjwa(muhimu).
Post a Comment
Related Discussions...