Uliza / Post Makala (New Post)

Preview
Imepokelewa!

Asante sana. Posti yako imetumwa kikamilifu na kwa sasa ipo under review. Itafanyiwa kazi na kuonekana hivi punde.

Dirisha Muhimu la Kuzuia Hantavirus Lafunguka Duniani 

Wataalamu wa afya duniani wameanza kuwa katika hali ya tahadhari baada ya kugundulika kwa maambukizi ya virusi hatari vya Andes hantavirus ndani ya meli ya kitalii ya MV Hondius, huku mataifa mbalimbali yakichukua hatua tofauti kufuatilia wasafiri waliokuwa ndani ya meli hiyo.

Meli hiyo iliwasili katika bandari ya Rotterdam nchini Uholanzi Jumatatu ikiwa imebeba abiria kutoka zaidi ya mataifa 20 duniani. Tukio hilo limeonekana kuwa jaribio kubwa la kwanza kwa mifumo ya afya duniani tangu kipindi cha janga la Covid-19.

Virusi vya Andes hantavirus vinatajwa kuwa hatari sana kwani takribani asilimia 40 ya wagonjwa wanaopata maambukizi hayo hufariki dunia. Tofauti na aina nyingine za hantavirus, aina ya Andes inaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, jambo linaloongeza hofu ya kuenea kwa maambukizi hayo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza, abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo tangu mwanzoni mwa Mei sasa wanaingia katika kipindi muhimu ambacho dalili zinaweza kuanza kujitokeza.

Hofu hiyo imeongezeka baada ya mamlaka za afya nchini Canada kuthibitisha kuwa mmoja wa abiria aliyekuwa amewekwa karantini alipatikana na maambukizi ya Andes hantavirus baada ya kuanza kuonyesha dalili.

Daktari Isaac Bogoch, ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza na profesa katika Chuo Kikuu cha Toronto, amesema haitakuwa jambo la kushangaza kama kutakuwa na visa vingine vitakavyothibitishwa katika siku zijazo.

Bogoch kwa kushirikiana na Daktari Jason Andrews kutoka Chuo Kikuu cha Stanford wamefanya tafiti kuhusu namna virusi hivyo vinavyoenea kwa kutumia mifano ya milipuko iliyowahi kutokea nchini Argentina mwaka 1996 na 2018.

Tafiti hizo zimeonyesha kuwa kuna “dirisha muhimu” la muda ambalo mamlaka za afya zinaweza kutumia kuwafuatilia watu waliokutana na walioambukizwa ili kuzuia maambukizi yasienee zaidi.

Mataifa mbalimbali sasa yanatumia mbinu tofauti kukabiliana na hali hiyo. Baadhi yanaweka karantini kwa wasafiri waliokutana na wagonjwa huku mengine yakichagua kuwafuatilia kwa karibu bila kuwazuia kusafiri.

Wataalamu wa afya wanaonya kuwa mawasiliano ya wazi kwa umma ni muhimu ili kuondoa hofu na kuzuia kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi kuhusu virusi hivyo.

Hantavirus mara nyingi huanzia kwa dalili zinazofanana na mafua kama homa, maumivu ya mwili, uchovu na matatizo ya kupumua. Katika hali mbaya, ugonjwa unaweza kusababisha kushindwa kwa mapafu kufanya kazi vizuri na hatimaye kusababisha kifo.

Mpaka sasa, mamlaka za afya duniani zinaendelea kufuatilia kwa karibu abiria wote waliokuwa ndani ya MV Hondius huku wiki zijazo zikitarajiwa kuwa muhimu katika kubaini kama kutakuwa na maambukizi zaidi. Via CNN.

...See more

DISCUSSIONS BOX(MAONI)|REPLY

Related Discussions...