Hasira zaibuka DRC baada ya kijana kufariki kwa EBOLA
Hali ya taharuki imetokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya umati wenye hasira kuvamia na kuchoma sehemu ya hospitali inayowahudumia wagonjwa wa Ebola katika eneo la Rwampara karibu na mji wa Bunia, jimbo la Ituri.
Tukio hilo limetokea baada ya familia na marafiki wa kijana aliyefariki kwa Ebola kuchukua mwili wake kwa nguvu wakitaka kufanya mazishi ya kawaida, jambo lililosababisha vurugu kubwa huku mahema yaliyokuwa yakitumika kuwahifadhi wagonjwa yakichomwa moto.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, miili ya watu waliofariki kwa Ebola huwa na uwezo mkubwa wa kueneza virusi hivyo, ndiyo maana serikali hulazimika kusimamia mazishi maalum yenye usalama mkubwa.
Wahudumu wa afya waliopo hospitalini hapo kwa sasa wanalindwa na jeshi huku polisi wakifanya juhudi za kurejesha hali ya utulivu eneo hilo.
Wananchi wengi katika jamii hiyo bado wanaonekana kutofahamu ukubwa wa hatari ya ugonjwa wa Ebola licha ya tahadhari zinazoendelea kutolewa na mamlaka za afya.
#DRC #Ebola #Bunia #AfricaNews





Post a Comment
Related Discussions...