Hypersomnia ni nini? Je ni tatizo? Fahamu hapa Leo

Je, umewahi kulala kwa saa nyingi lakini bado ukahisi umechoka na usingizi mwingi mchana? Hali hii inaweza kuwa dalili ya Hypersomnia.

Hypersomnia ni tatizo la mfumo wa fahamu linalosababisha mtu kuwa na usingizi wa kupitiliza mchana hata baada ya kulala kwa muda mrefu usiku. Watu wenye hali hii wanaweza kulala masaa mengi kuliko kawaida lakini bado wakajihisi hawajapata mapumziko ya kutosha.

Dalili zake ni pamoja na:

  • Kusinzia sana mchana
  • Kukosa nguvu mara kwa mara
  • Ugumu wa kuzingatia mambo
  • Kusahau haraka
  • Kuhisi akili nzito au kuchanganyikiwa

Tofauti na uchovu wa kawaida unaotokana na kukosa usingizi, hypersomnia hutokana na matatizo katika jinsi ubongo unavyodhibiti usingizi na hali ya kuamka.

Wataalamu wanaamini kuwa hali hii inaweza kuhusishwa na mabadiliko ya kemikali za ubongo, matatizo ya mzunguko wa usingizi, afya ya akili au magonjwa mengine ya mfumo wa fahamu.

Ikiwa usingizi mwingi unaathiri kazi, masomo au shughuli zako za kila siku, ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi na ushauri wa kitaalamu.

Kumbuka: Kulala muda mrefu si mara zote humaanisha mwili au ubongo wako umepata mapumziko ya kutosha,Wakati mwingine ni tatizo.!!

...See more

Una maoni gani? Changia hapa!

Mijadala Inayoendelea