Jinsi ya Kupika Maandazi ya Nazi kwa Urahisi
Maandazi ya nazi ni moja ya vitafunwa vinavyopendwa sana kutokana na ladha yake tamu na harufu nzuri ya nazi. Unaweza kuyaandaa nyumbani kwa ajili ya familia au hata biashara ndogo ya kuuza vitafunwa. Ukiweka hiriki kidogo kwenye maandazi haya, ladha yake huwa tamu zaidi na huvutia wakati wa kifungua kinywa.
Viungo Vinavyohitajika
- Vikombe 4 vya unga wa ngano
- Kikombe 1 cha tui la nazi
- Vijiko 2 vya sukari
- Kijiko 1 cha hamira
- Kijiko 1 cha baking powder
- Vijiko 2 vya siagi au mafuta
- Mafuta ya kukaangia
- Hiliki kidogo (hiari)
Hatua za Maandalizi
1. Andaa unga
Chekecha unga wa ngano vizuri ili kuondoa uchafu wowote. Weka unga kwenye bakuli kubwa la kukandia.
2. Changanya viungo vikavu
Ongeza sukari, hamira na baking powder kwenye unga kisha changanya vizuri.
3. Weka tui la nazi
Mimina tui la nazi kidogo kidogo huku ukichanganya mpaka unga ushikamane. Unaweza kutumia blenda kuchanganya tui, sukari na hamira kabla ya kuviweka kwenye unga ili kupata mchanganyiko laini zaidi.
4. Kanda unga
Kanda unga kwa dakika 20 au zaidi mpaka uwe laini na usiwe na madonge. Pakaa siagi au mafuta kidogo juu ya unga kisha ufunike ili uumuke.
5. Acha unga uumuke
Acha unga kwa dakika 30 hadi 40 ili uumuke vizuri. Baada ya hapo, kanda tena kidogo kutoa hewa.
6. Kata maumbo ya maandazi
Kata maandazi kwa maumbo unayopenda kama duara, pembe tatu au pembe nne. Hakikisha si makubwa sana ili yaive vizuri.
7. Kaanga
Weka mafuta kwenye kikaango na yapate moto wa wastani. Kaanga maandazi mpaka yawe ya kahawia nzuri. Epuka mafuta kuwa ya moto sana kwani yanaweza kuyachoma nje na kubaki mabichi ndani.
8. Tayarisha kwa kula
Yaache yapoe kidogo kisha yawe tayari kuliwa pamoja na chai, kahawa au kinywaji chochote unachopenda.
Maandazi ya nazi huwa laini, yenye harufu nzuri na ladha tamu inayovutia kila mtu mezani.

.jpeg)



Post a Comment
Related Discussions...