King Charles III Amtumia Pope Leo XIV Ujumbe wa Pongezi
Mfalme wa Uingereza Charles III ametuma ujumbe maalum wa pongezi kwa Pope Leo XIV katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake kuongoza Kanisa Katoliki duniani.
Katika ujumbe huo, King Charles III alieleza umuhimu wa matumaini, hekima ya dini pamoja na matumizi ya maarifa ya sayansi kama nyenzo muhimu katika kusaidia dunia kujenga amani ya kudumu na kuleta maendeleo yenye manufaa kwa watu wote duniani.
Mfalme huyo alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, wataalamu wa sayansi pamoja na jamii mbalimbali unaweza kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa, ikiwemo migogoro, umasikini na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ujumbe huo umeonekana kama ishara ya mshikamano, heshima na uhusiano mzuri kati ya viongozi hao wawili wakubwa duniani, huku ukionyesha dhamira ya pamoja ya kuhimiza maadili, amani na maendeleo ya binadamu.
Hatua hiyo pia imepokelewa vyema na waumini pamoja na wadau mbalimbali duniani walioeleza kuwa viongozi wa dunia wanapaswa kuendelea kushirikiana katika kujenga mustakabali bora kwa vizazi vijavyo.





Post a Comment
"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".