Naitwa John Temba kutoka Iringa,Naona Saivi kuna habari zinasambaa kuhusu kitu kinaitwa HantaVirus, ni nini hiki? na pia napenda kujua;

Kuna Tofauti Gani kati ya HantaVirus na Corona Virus?

...See more

1 Comments

  1. Hantavirus ni virusi vinavyoenezwa zaidi na panya kupitia mkojo, kinyesi au mate yao, na vinaweza kusababisha matatizo makubwa ya mapafu au figo.

    COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (SARS-CoV-2), unaoenea kutoka mtu hadi mtu kupitia hewa au matone ya kukohoa na kupumua.

    Tofauti kuu:
    Hantavirus: Chanzo kikuu ni panya.
    Corona Virus: Chanzo kikuu cha maambukizi ni binadamu kwenda binadamu.

    ReplyDelete

Post a Comment

Related Discussions...