Kundi maarufu la watoto wa dansi kutoka Uganda, Ghetto Kids lapata nafasi ya kushiriki kwenye Kombe la Dunia 2026

Kundi maarufu la watoto wa dansi kutoka Uganda, Ghetto Kids, limeendelea kuvuta hisia duniani baada ya kupata nafasi ya kushiriki kwenye halftime show ya fainali ya Kombe la Dunia 2026 kupitia mwaliko maalum kutoka kwa Shakira.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wiki iliyopita, Shakira aliwatangaza rasmi watoto hao kama kundi la kwanza alilolichagua kushiriki naye katika burudani ya fainali ya Kombe la Dunia itakayofanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico msimu huu wa joto. Tangazo hilo limeibua furaha kubwa kwa watoto hao waliotokea mitaa ya Kampala kabla ya kuwa gumzo duniani kupitia vipaji vyao vya kucheza.

Kundi hilo lilianzishwa kama sehemu ya NGO inayosaidia watoto wa mitaani na yatima kupitia sanaa na dansi. Umaarufu wao ulianza kukua kupitia video zao za kucheza zilizosambazwa sana mitandaoni na baadaye kuwafungulia milango ya kushiriki kwenye kipindi maarufu cha America’s Got Talent.

Mmoja wa watoto hao mwenye umri wa miaka minane, Daniella Busingye Josephine, amesema wana hamu kubwa ya kuonyesha dunia kile wanachoweza kufanya kupitia jukwaa hilo kubwa la kimataifa. Kwa upande wake, Ssegirinyi Madwanah mwenye miaka 16 amesema nafasi ya kusafiri nje ya Uganda na kutumbuiza mbele ya mamilioni ya mashabiki ni fursa kubwa inayoweza kubadilisha maisha yao.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha jinsi vipaji vya watoto wa Afrika Mashariki vinavyozidi kupata nafasi kwenye majukwaa makubwa duniani kupitia sanaa, ubunifu na mitandao ya kijamii.

...See more

WEKA COMMENT YAKO HAPA(MAONI)KUHUSU MADA HII

Related Discussions...