Mama Magufuli amefariki kwa Ugonjwa wa Moyo

Wasifu wa Bi. Suzana Ngolo Musa, Mama wa Hayati Rais John Pombe Magufuli umesomwa leo wakati wa ibada ya kumuaga ukieleza historia yake ya maisha, afya na mchango wake katika Jamii.

Akisoma wasifu huo, mdogo wa Hayati Magufuli, Michael Joseph amesema marehemu alikuwa Mtu mwenye upendo, mkarimu na mcha Mungu na aliyeishi kwa kushirikiana na Watu bila ubaguzi wa aina yoyote.

Katika wasifu huo pia imeelezwa kuwa marehemu alipata Kiharusi miaka minane iliyopita kutokana na matatizo ya Moyo yaliyosababisha mapigo ya haraka na yasiyo ya kawaida, sambamba na Shinikizo la Damu na Kisukari.#MillardAyoUPDATES

...See more

Una maoni gani? Changia hapa!

Mijadala Inayoendelea