Uliza / Post Makala (New Post)

Preview
Imepokelewa!

Asante sana. Posti yako imetumwa kikamilifu na kwa sasa ipo under review. Itafanyiwa kazi na kuonekana hivi punde.

Matumizi sahihi ya p2

Vidonge vya dharura vya kuzuia mimba (emergency contraceptives), vinavyojulikana pia kama P2, hutumika kusaidia kuzuia ujauzito baada ya kufanya ngono bila kinga au kama kinga imeharibika.

Aina zinazotumika sana zina dawa ya Levonorgestrel.

Matumizi sahihi ya p2

Jinsi ya kutumia kwa Usahihi Vidonge vya P2

-Meza kidonge haraka iwezekanavyo baada ya tendo la ngono bila kinga.

Hufanya kazi vizuri zaidi ndani ya saa 24.

Kinaweza kutumika hadi saa 72 (siku 3), na baadhi ya aina hadi siku 5 lakini ufanisi hupungua kadri muda unavyoongezeka.

Muhimu kufahamu:

-Hakizuizi mimba iliyokwisha kutungwa tayari.

-Si dawa ya kutoa mimba.

-Hakikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa.

-Si vizuri kutumia mara kwa mara kama njia kuu ya uzazi wa mpango; ni kwa dharura.

Madhara yanayoweza kutokea

  • Kichefuchefu
  • Maumivu ya kichwa
  • Uchovu
  • Kutokwa damu kidogo
  • Hedhi kuwahi au kuchelewa kwa siku chache

Wakati wa kufanya kipimo cha mimba

Ikiwa hedhi imechelewa zaidi ya wiki moja baada ya muda uliotarajiwa, ni vizuri kufanya pregnancy test.

Madhara ya p2,haya ni madhara ya matumizi ya Vidonge vya P2


Madhara baada ya kutumia p2,Fahamu hapa

Fahamu P2 ni dawa ya dharura yaani kwa kitaalam hujulikana kama emergency contraceptive pill, dawa hii inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya mapenzi pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya mapenzi au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa.

Ukweli ni kwamba dose ya hormones ndani ya p2 ni kubwa kuliko vidonge vya kawaida vya Uzazi(birth control pills) kitu ambacho kinaifanya isifae kwa Matumizi ya kila siku,

Hii husababisha madhara Zaidi kwa Mtu mwenye mazoea ya kuzitumia mara kwa mara. Na moja ya madhara ni mzunguko wako wa hedhi kuathiriwa sana – Periods yako inaweza isitoke kama kawaida, inaweza kuwa nyingi,zito sana,isiyoeleweka(Irregular bleeding) n.k.

Pia baadhi ya Wanawake huongezeka uzito, Hivo basi P2 haishauriwi kabsa kwa matumizi ya kila siku au kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Madhara baada ya kutumia p2,

Haya ni baadhi ya Madhara au matokeo baada ya kutumia p2(emergency contraceptive pills):

  • Kupata kichefuchefu
  • Kutapika
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kichwa
  • Kupata maunivu ya tumbo
  • Maziwa kuuma au kuvuta zaidi
  • Kubadilika kwa hedhi yako ya kawaida,ikiwemo kuvuja damu nyingi au kwa muda mrefu,au kuvuja katikati ya mzunguko n.k

Kutokwa na Vitone vya damu mara kwa mara(spotting) – Unaweza kupata vitone vya damu ndani ya wiki ijayo baada ya kumeza kidonge cha dharura cha kuzuia mimba yaani P2,

Pia, hedhi yako inayofuata inaweza kuwa nyepesi au nzito, ikawahi kutoka mapema au kuchelewa kuliko kawaida. Hakikisha unapata Msaada wa Tiba ikiwa unakutana na changamoto hizi.

Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida(Irregular menstrual cycle) – Kwa sababu ya tembe za dharura za kuzuia mimba(p2), kipindi chako cha hedhi kinaweza kufika mapema au kuchelewa, jambo ambalo hutokea sana kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi. Hata hivyo, unapaswa kufanya kipimo cha ujauzito ikiwa hupati kipindi chako cha hedhi ndani ya wiki mbili za tarehe inayotarajiwa.

Rejea Zaidi hapa:

...See more

DISCUSSIONS BOX(MAONI)|REPLY

Related Discussions...