Mmoja afariki dunia, wengine tisa wamejeruhiwa baada ya tanki kubwa lililokuwa na kemikali hatari kupasuka Washington Marekani
Mtu mmoja amefariki dunia, wengine tisa wamejeruhiwa huku wafanyakazi tisa wakitajwa kutoweka baada ya tanki kubwa lililokuwa na kemikali hatari kupasuka katika kiwanda cha karatasi na vifungashio kilichopo jimbo la Washington nchini Marekani.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi kwa saa za eneo hilo katika kiwanda cha Nippon Dynawave Packaging Co. kilichopo Longview, Washington. Kwa mujibu wa maafisa wa zimamoto, tanki hilo lilikuwa limehifadhi kemikali inayojulikana kama “white liquor”, mchanganyiko wa kemikali unaotumika katika mchakato wa utengenezaji wa karatasi.
Awali maafisa walieleza kuwa tanki hilo lilikuwa limeporomoka kwa ndani (implosion), lakini baadaye ikathibitishwa kuwa lilipasuka na kusababisha madhara makubwa katika eneo hilo.
Idara ya Zimamoto ya Longview ilisema hakuna tishio kwa wananchi wanaoishi maeneo ya jirani, ingawa watu wametakiwa kuepuka eneo hilo wakati operesheni za uokoaji na kudhibiti hali zikiendelea.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto cha Cowlitz 2 Fire Rescue, Scott Goldstein alisema juhudi za uokoaji na kuimarisha usalama eneo la tukio bado ni ngumu sana kutokana na hatari zinazoendelea kuwepo kutoka kwenye kemikali na miundombinu ya kiwanda hicho.





Post a Comment
Related Discussions...