Nyota wa Muziki wa Latin kutoka nchini Colombia Shakira amepata ushindi mkubwa wa Kesi ya ukwepaji Kodi
Nyota wa Muziki wa Latin kutoka nchini Colombia Shakira ameibuka na ushindi mkubwa mahakamani baada ya mahakama ya juu nchini Hispania kumaliza rasmi tuhuma za ukwepaji kodi zilizokuwa zikimkabili kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa za uamuzi huo, mahakama imebaini kuwa hakukuwa na msingi wa kutosha wa kumtia hatiani, hivyo kesi iliyokuwa ikiendelea kwa miaka kadhaa imefungwa rasmi.
Kesi hiyo ilikuwa ikihusisha madai ya mamlaka ya kodi ya Hispania kwamba msanii huyo hakutekeleza kikamilifu wajibu wake wa kulipa kodi wakati akiishi nchini humo, jambo lililosababisha uchunguzi mpana wa kifedha dhidi yake.
Baada ya uamuzi huo, mahakama pia imeitaka Hazina ya Serikali ya Hispania kurejesha fedha zilizokuwa zimekusanywa wakati wa uchunguzi, ambazo zinakadiriwa kufikia zaidi ya euro milioni 55 pamoja na riba yake.
Uamuzi huo umehitimisha moja ya kesi zilizodumu kwa muda mrefu zaidi katika maisha ya Shakira, ukiondoa sintofahamu iliyokuwa imezunguka masuala yake ya kodi na kumfungulia ukurasa mpya wa maisha yake ya kitaaluma na binafsi.





Post a Comment
Related Discussions...