Tatizo la TUMBO kuunguruma chanzo chake nini?
Tatizo la tumbo kuunguruma ni hali ambayo huhusisha sauti za kama kelele au milio kutokea tumboni kutokana na harakati za hewa, maji, au chakula kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Ingawa mara nyingi ni hali ya kawaida, wakati mwingine inaweza kuwa dalili ya tatizo fulani la kiafya.
CHANZO CHA TUMBO KUUNGURUMA
1.Njaa
Mwili huongeza harakati za tumbo na utumbo kama maandalizi ya kula chakula, na hutoa sauti.
2.Tatizo la Hewa Tumboni
Hali hii huhusisha Kumeza hewa kupita kiasi unapokula haraka, kunywa vinywaji vyenye gesi, au kula huku unaongea.
Baadae unaweza kuacha kupata changamoto hii ya TUMBO kuunguruma
3.Mmeng'enyo wa chakula
Harakati za misuli ya utumbo kusukuma chakula wakati wa Umeng'enyaji chakula huweza kusababisha milio tumboni.
4.Chakula fulani au Baadhi ya vyakula ulivyokula
Vyakula vigumu kumeng’enywa (kama maharage, kabeji, maziwa kwa wenye shida ya lactose intolerance) huongeza gesi na kelele.
5.Maambukizi ya njia ya mmeng'enyo (Gastroenteritis)
Husababishwa na bakteria au virusi, huambatana na kuharisha, kichefuchefu, gesi, na sauti tumboni.
6.Irritable Bowel Syndrome (IBS)
Hali sugu inayosababisha tumbo kuunguruma, kujaa gesi, maumivu ya tumbo, na mabadiliko ya choo.
7.Kutokuwepo kwa choo kwa muda mrefu (Constipation)
Chakula hukwama, harakati huzidi bila matokeo, hivyo sauti nyingi huweza kutokea.
8.Tatizo la Hyperacidity
Kuongezeka kwa asidi tumboni huathiri utumbo na kusababisha milio au hata maumivu.
DALILI ZINAZOAMBATANA NA TUMBO KUUNGURUMA
- Tumbo kujaa gesi
- Maumivu ya tumbo
- Kuvimbiwa au kuhara
- Kichefuchefu
- Kupiga kelele wakati wa njaa au baada ya kula
- Kutojisikia vizuri baada ya kula
Je,Una tatizo hili? Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.





Post a Comment
Related Discussions...