Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five 2026
Wanafunzi waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) wanaweza kuangalia shule au chuo walichopangiwa kupitia mfumo wa TAMISEMI mara tu majina yanapotangazwa.
Hatua za kufuata:
-
Fungua tovuti ya Selform ya TAMISEMI:
-
Chagua sehemu ya Form Five Selection.
-
Chagua mwaka 2026/2027.
-
Chagua mkoa uliposoma Kidato cha Nne.
-
Chagua halmashauri (council) yako.
-
Tafuta jina lako kwenye orodha ya waliochaguliwa.
-
Utaona:
- Shule uliyopangiwa
- Combination (PCM, PCB, EGM, HGL n.k.)
- Maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions) kama yapo.
Jinsi ya Kuangalia Selection za Vyuo vya Kati
Kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati (Diploma au Certificate), matokeo hupatikana kupitia taasisi husika na mfumo wa NACTVET.
Tovuti rasmi ya NACTVET:
Hatua za kuangalia:
- Tembelea tovuti ya NACTVET hapo juu.
- Angalia matangazo ya udahili (Admissions).
- Ingia kwenye mfumo au fuatilia maelekezo ya chuo ulichoomba.
- Tumia namba ya simu au taarifa ulizotumia wakati wa maombi ikiwa zinahitajika.
Links Muhimu:
TAMISEMI Selform: https://selform.tamisemi.go.tz/
NACTVET Admissions: https://www.nactvet.go.tz/page/students-admission
Tovuti Kuu ya TAMISEMI: https://www.tamisemi.go.tz/


Post a Comment