Mahakama ya Kenya Yazuia Kujengwa kwa kituo cha Ebola nchini Kenya
Jaji wa mahakama hiyo Patricia Nyaundi, ametoa amri inayoikataza serikali ya Kenya kuchukua hatua yoyote ya kujenga au kuanza shughuli katika kituo hicho kilichopangwa kujengwa mjini Nanyuki hadi kesi hiyo itakapomalizika.
Jaji huyo pia aliamuru serikali kuweka wazi makubaliano yote na taratibu za uendeshaji zinazohusiana na kituo hicho ndani ya siku saba, na akapanga usikilizwaji unaofuata wa kesi hiyo kufanyika June 23.
Afisa mmoja wa utawala wa Marekani, aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wako katika mawasiliano na mamlaka ya Kenya na wana matumaini kwamba wanaweza kutatua pingamizi zilizotolewa. Dw


Post a Comment